Moracka na Lucka
Hemed na Ben

Abba na Mwinyi Modo
Kama kawaida Dar yetu haikosi vitu HOT HOT kila siku, shindano hili la kumsaka mvulana mwenye mvuto limefikia Finally.

Waliobahatika kuingia ni Hemed, Ben(Phot Point), Abba Seduu, Mwinyi Model, Moracka na Luca(Bongo5.com) kama unavyowaona hapo chini.Shindano hili linaloendeshwa na mtangazaji kutoka Clouds FM akijulikana kwa jina la Loveness Love au ukipenda DIVA.
Mwanadada huyu mwenye sauti nzuri yakuvutia akiwa hewani majira ya 3:30 mpaka saa 6:00 usiku kwenye kipindi chake kinachoitwa ALA ZA ROHO.

Jinsi yakushiriki kumpigia kura mshiriki unayempenda ili awe Sexiest Man In Dar, unaingia kwenye blog ya Diva inayoitwa


halafu hapo utaona sehemu ya ku vote mshiriki unayempenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2009

    We woman we are very attracted to powerful men. Sexiest men ,to me should have a carrier,educated, and good looking (is not that important).

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2009

    ujinga mwengine bwana!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2009

    Jamani kila jamii ina tamaduni zake. Haya mambo ya kukopi yatakuja kuingiza vizazi vyetu hko mbeleni kwenye mashimo mabaya, na watashindwa kutoka. Hakuna jamii inayopotoka kwa siku moja, inachukua muda. na nchi za magharibi wameanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja siku hizi. lakini kilicho wafikisha hapo wanakijua. TUSIPO ANGALIA TUTAANZA KUFUNGISHA NDOA ZA WATOTO WAKIUME HADHANI. TUIOKOE JAMII TUKEMEE UJINGA KAMA HUU.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2009

    Duh! ngoja nifunge mdomo wangu watu wasije kusema nasukutua baada ya kubeba ze boxiiiiiiiiiiiiiiiis!

    ReplyDelete
  5. Sexiestman-my-behindJuly 15, 2009

    Tanzania watu wapuuzi kweli. Sasa huu ndo ujinga gani? watu wanaangaika kutafuta tiba ya UKIMWI mengine yanauza Sura. Tumelaaniwa, na tutanizi kulaaniwa, ila naomba kama huu ndo mtindo basi na niombe;
    Kidumu chama cha Mafisadi
    Kidumu kwa sababu vijana wanafanya upumbavu, hakuna hata mmoja anayejali kwamba nchi yao inakwidhaje au iliuzwa vipi. Mbele na ujinga wenu heti Sexieti man???? Hebo !!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2009

    sasa huyo ben mbona kofia tena? avue nimuone vizuri niweze kujichagulia ka serengeti boy

    ReplyDelete
  7. Mimi nadhani waandaaji wa shindano wangesema "shindano la kumtafuta mvulana mwenye sura ya kike"...unapomtafuta sexiest man . sioni hata mmoja hapo mwenye sifa hizo mie nawaona hapo machotara. waarabu na wapemba ambao siku zote wataonekana warembo sababu ya kuchanganya damu.tafuteni dume la nguvu .

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 15, 2009

    Ina maana kwa Bongo kuwa mweupe ndio uzuri? acheni kuchemsha.

    ReplyDelete
  9. Umm would like to see a chocolate dark skinned brother in there! HELLOOO!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 15, 2009

    Black is whack....lol
    Looks like them light skin brothers are getting ol the honnies!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2009

    sexy men vitandani or sexy men alimradi tu wanavaa suruali. to me sexy man ni yule anayeyapiga mapigo ya sita kwa sita kisawasawa, maana hao nawaona hapo kama chakula. my sexy man is hot dark chocolate!! who cares about the look wakati hakuna cha mapigo makali na mifuko yao ukute imetoboka

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2009

    Ndio tulipofikia hapo!!! Subirini mahakama ya Kadhi. Na wenyewe wametega sura kabisa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 16, 2009

    Tuwe na mipaka vitu vya kushabikia
    tusishabikie kila kitu ni upumbavu
    Huu ujinga kesho na keshokutwa wanadakwa na Uwazi hawa weshakuwa maarufu mifuko haina kitu sio kila kitu cha ulaya mnaiga wallah mtabashiwa sexy anakuwa mwanamke mwanaume anasifiwa kwa kutafuta pesa ukiwa na pesa huuzi sura wekundu wa msimbazi tuu. Kila mwanaume ni mzuri mbele ya pesa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 16, 2009

    Mdau wa kwanza: you mean CAREER sio CARRIER. Bora uandike kwa Kiswahili kama hukiwezi kimombo.

    Pili, hamna handsome boy wala nini. PESA ndio inayoongea. Mimi kibonge wa nguvu, sina misuli wala nini ila kitambi cha nguvu. Lakini napata wanawake chungu mzima kwa kuwa nina pesa ya kuwahudumia mahitaji yao yote. Kama una hela, utapata mademu mpaka utachoka wewe. Na sio Bongo tu, nikienda likizo ulaya au Marekani, pesa pia inaongea lugha yake, na siongelei sijui wanawake wahuni hapa, ila wajanja tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 16, 2009

    ninaunga mkono hoja ya kwamba tuige lakini tuchuje. lakini lawama ya kuiga bila kuchuja ni wamiliki au mawakala wa wamiliki wa kampuni za luninga na kampuni za simu ambazo zinamilikiwa na wazungu wa south africa. hawa wa south africa wanatuona tulivyo malimbukeni na wanatumia udhaifu wetu huo kutengeneza mabilioni ya pesa na kutuletea ya kwa o ya kutaka kila cha mzungu kuabudiwe. basi wanakuta na vijana wetu ndio malimbukeni ya kutupa pamoja na ukata, habari ndio hiyo. twafwa!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 16, 2009

    akuna lolote hapo yao ni wauza sura tu.

    ReplyDelete
  17. Wivu tundouna wasumbua kuwa pondea wenzenu sio fresh sio siri ur all looking good nawafagilia sana now tuna kwenda na wakati jamani tuacheni ushamba looo wanume sikuzote hamsifiani but ukweli ndo huo wenzenu ni wazuri sana tuuuuuuu wivu achen tena mzuri sana hapo ni Moracka.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 16, 2009

    People let us be a little carefull on this, because for this type of competition one has to have a certain background that is appealing to the general society.It is my hope that participants goals and future plans, locally and .... are also under consideration. Because once the person wins, the young generation will look at that person as a roll model.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 16, 2009

    Hii ndio dunia bwana kila fani ipo! Unajua nilijaribu kufuatilia haya mashindano ya `Miss' na kuchokonoa kumbukumbu mbalimbali, zikanipeleka enzi za Warumi na Wayunani. Mabwana walianzisha michezo kama miereka kwa watumwa ili kujiburudisha, na warembo (watumwa wa kike) walipitishwa nusu uchi ili kuwaburudisha hao mabwana na mwishowe wanachukuliwa waliopendeza kwa wanawake na midume ilipewa unyapara.
    Sasa hali hii ikaendelea na kuboreshwa hadi kufikia sasa ambapo inafanywa kitaalamu, lakini ukiangalia kiundani yote haya ni kuwaburudisha `watu'
    Sasa nikajaribu kudadisi hili la wanaume warembo limetoka wapi. Nikakumbuka kuwa kuna enzi za wanawake walikuwa ndio watawala, kwa baadhi ya maeneo, nikaunganisha na hilo la warumi, na wayunani mmmh, lakini bado nikaona ulakini, labda mnisaidie kwa hili.
    Anyway, cha msingi hapa ni wewe kujiuliza unamchagua mwanaume mwenzako kuwa ni `sex' ili iweje. Kwa mantiki hii, hili swali linawafaa akina dada ndio wamchague mwanaume `sex' AU?.
    M3

    ReplyDelete
  20. Tatizo letu wabongo kila kitu lazima tuongee shit!!ww kama unaona ili jambo baya kwako,kaa kimya.....kwani unaumia nn/hayo ni mashindano tu,na burudani!km nyingine.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 16, 2009

    Hivi huyo aliyeanzisha haya mambo aliwachagua hawa kwa yy kuwaona wanamvuto au?koz hawa hamna mwenye mvuto hata mmoja ni mahandsome.na kuna tofauti kati ya handsome na mtu mwenye mvuto.angesema shindano la handsome kweli ila si wenye mvuto.msiwe mnafanya mambo bila kujua na akina Tyson Beckford, wasemeje kama hawa wanamvuto

    ReplyDelete
  22. Ili mwanaume uwe sexy kuna vitu vingi. Bode liwe lenye misuli ya kiume, Sauti yenye mkazo, mikunjo ya kutosha bedi, sio hii mnatuwekea hawa wauza sura, wenye sura laini za kidem na vipodozi kibwena eti ndo ma sexy men. Nadani mnatafsiri direct toka kwa madem, kuwa dem sexy awe laini!
    Hao mngesema mnatafuta wachumba wa kuoa hapo sawa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 16, 2009

    ABBA is so SEXYYYYYYYYYYYYYYY

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 16, 2009

    Mmmmm, Fruitcakes.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 16, 2009

    Ushamba wa Wa Tanzania Mtu ukiwa mweupe mwarabu au watasema Mpemba au wamerukakidogo mchaga wacheni ushamba

    Ila mwanaume ni yule jeusi kama Iddi Amin mbona hamuwaweki. Kwanza Wapemba wengi wanatoka Pemba sio Unguja, Unguja sio Pemba, Pemba kuna weusiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!! labda wapemba machotara wa kirabu ndio weupe. Weupe.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 16, 2009

    WIVU BWANA TUMEULIZWA SIO WAKIKE NA SIO WAKIKE NDIO TUMEWAPENDA SASA NYIE WANAUME WAZIMA MNAANZA KUWATIZAMA NYOO MMEWAPENDA EH MMEKAA NA NYIE MNA VOTE. VOTE WA KIKE NYIE.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 16, 2009

    Abba very Sex, cute and Handsome!!!!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 16, 2009

    It's better to start a talent show angalau watoto hawa watajiendeleza na kutengeneza pesa. I mean we TAnzanians are intelligent enough for this rubbish! Who cares kama ni handsome? Kinachomatter ni unatumiaje ubongo wako kwenda na wakati. Watoto hawa wanvipaji fulani, kuimba ku-dance, sarakasi anything at least they can do something to better their lives than kuja kupose kwa uzuri wa sura, na mtoto wa kiume anapojigamba anasura au umbo zuri KUNA MUSHKELI!!!!!!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 16, 2009

    Eeeenh! Na bado tutayaona mengi zaidi ya hayo ndugu zangu kazi kwenu!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 16, 2009

    sawa veery sexy... but what do they do katika maisha yao????????????????????????????????????
    youn be sexy but kama auna maendeleo them thats not sexy

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 16, 2009

    Hala hala wanaume

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 16, 2009

    yale yale!!! ya viazi na kuku kutolewa kuleee bondeni kuja kutafutiwa soko bongo,wakati viazi vya mbeya na kuku wa segerea vinakosa soko. mmmmhhhh msishangae baadaye kusikia ndoa kati ya vidume,yote huanza taratiiiib!!!
    haya jamani yangu macho tu,but if u r smart enough in your calvary u can't do dat bddy!!!just take a time as a man n think a little bit before u start doing what u r doing!!i bet u you won't dare dat!!

    ReplyDelete
  33. Taifa LetuJuly 16, 2009

    Few years ago, Cosmopolitan, a popular magazine in the United States, surveyed women and asked them what attracts them in men. Three things stood out...in this particular order:-

    1. Power
    2. Fame
    3. Intelligence
    4. Height (being tall)

    When they went into names, Nelson Mandela - of all people - came on top, because he had all those.

    At the same time, I would not want to trash this competition. I take it as an interesting way to study our society, the things we value and the influence of global media in the convergence of acceptable forms of arts, and beauty.

    ReplyDelete
  34. It disturbs me that we don'tsee any really dark skinned fellows up there. Hebu tukubaliane waTanzania na waafrika wengi ni weusi hasa. Mbona hawajawa represented? Tusiige mila ya kizungu kuwa eti 'weupe' ndo uzuri. Hata hivyo nawatakia hao vijana mafanikio mema.

    ReplyDelete
  35. hey guys,hamna aliewalazimisha ku vote coz kama ni utamaduni hata nyie mmeuharibu kwa kwenda kujenga nchi za wenzenu na kuacha nchi yenu huku..sasa si mmeondoka huku basi mmeacha sisi tukiwa tunaendesha nchi katika swala la burudani ambayo ni jadi yetu na nia na dhumuni letu ni kupitia burudani na ni clouds fm babes..Hata Raisi alisema KULA ULIWE ..maana yake ifikirie,hakumaanisha vingine ila alimaanisha jambo la busara kabisa..lol!!
    siwezi amini kama u live in uk or us or whatever and una crush wenzio ambao ni watanzania..tukija huko mnakoishi mnatembea uchi na kujifanya mnajua kila kitu na kuna wengine wanafikia hatua ya kujifanya hamjui hata kiswahili wakati nyinyi ni watanzania asilia..
    wengine mnalowea huko na kusahau mpaka familia zenu huku bila kujali watakula nini then eti una crush the sexiest man..why dont u crush yourself kwa kujiona msafi wakati una matatizo yako ambayo unayaweka moyoni kila kukicha na kutabasamu kwa uongo na kweli..wengi wenu mnauza unga tu na kuuza miili yenu..na kuwatuma wenzenu wawafanyie biashara chafu..hizo hamuoni mnaona the sexiest man huh??
    Come on guys kwa nini mnakuwa wagumu kukubali analofanya mwenzio na lazima um let down in one way or another??
    Your talking about money and woman and sex in bed .. kama kweli unajali why dont u go and offer an help kwa orphans..wengi wenu mmebakia kula starehe na kupiga picha za utupu kila kukicha na wengine tukiwa tunawajua na tunawakaushia tu mbona hakuna aliekuja kukwambia what ur doing is not right-
    we live to learn and not to bring others down because we have money..money is not everthing brothers and sisters..
    LOVE is everything and if u have that luv inside of u huwezi kaa na ku crush anachofanya mwengine na uta support coz u luv that person..when u luv u support jamani kama hu support ur an evil.
    hakuna ujinga katika maisha whatever happens kuna reasons za hicho kutokea..usiseme ni ujinga..kama ni ujinga ni wa kujiita anonymous wakati wazazi wako wamekupa jina..wewe ni muoga na hujiamini katika mambo yako ndo maana wajiita huna jina kwa kiswahili..au hufahamiki..amazing!!
    Learn to support and not to crush things..besides,your not God to judge wengine..u will judged the same way u judge others..
    otherwise the competion is fair and ni moja kati ya kuendeleza burudani kama unaona ni kinyume na utamaduni kuna vingi ambavyo ni kinyume na utamaduni ambavyo wengi wanafanya na vinafanywa ila sijaona cha ajabu hapo coz hakuna alie kaa uchi na hakuna mtu anaeuza sura hapo..wauze sura zao wao wabaki na nini??..
    Swala la upemba na uarabu analijua mwalimu nyerere na mzee wetu karume waliotuunganisha kwa kuchanganya nchi zetu mbili kwa kuchanganya mchanga na kuifanya iwe Tanzania..we are all Tanzanians na twaishi kwa amani tu na upendo bila kashkash zozote..
    wewe unae crush na kusema vibaya ungejitahidi na kuzuia utandawazi ungefanya la maana sana kwani huo utandawazi ndo umeleta yote haya na hiyo ni moja kati ya nchi kuendelea,ndo maana Tanzania ulioiacha wakati unaenda huko kwa wazungu ni sawa na huko uishio tofauti majengo tu ambayo moja lipo linaitwa benjamini mkapa tower na ndio maana tuna redio na television na simu za mkononi na hivyo vizungusha tobo..
    ndio maana tunavaa suruali na sisi wanawake,changes ndo zimemfanya Obama kawa President wa dunia ..
    Next time learn tu support wengine wanapofanya jambo na sio kulipinga na maneno makali sana..
    Karibia dunia nzima imejaa mashoga..why we dont kill them kama ni kulinda utamaduni??
    its because wana haki ya kuishi kama wengine na ni binadamu kama wengine cha kufanya ni kuwaombea wabadilike na si vinginevyo..
    who are u to judge others??
    Your nobody..God is there up above and he is the only one who can decide which is good and which is bad..Sikiliza Man in the Mirror ya Michael Jackson..be blcd and thanks kwa support ya wachache..Mungu awabariki sana..
    Am Out- SEXIEST MAN OYEEE????
    jibu ''oyee''

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 16, 2009

    sex man ni mrefu mweusi tiii na misuli huyo ndio mwanamme mzuri wa kiafrica,sio kuweka nywele dawa kama mwanamke..pia mwanamme mzuri awe na elimu na kazi ya maana sio kukaa saluni tuu na kupiga muziki chumbani,,,,hakuna mwamme mzuri hapo hata mmoja

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 16, 2009

    From ma point of view hawa wote ni ma dwarf coz kwenye uzuri wa mwanaume cha kwanza ni Height ma super model wote wanaume na wanaume wanaonekana wazuri na wanaweke wanawafagilia na kuwatamani(Tyson Beckford,Will Smith,Moris Chestnut,Boris Kodjoe just to name a few) ni warefu atleat 6ft and above and vifua vyao ni vipana and on top of that wako inteligent sasa hapa wote ni mazero(not to be offensive but sioni hata mmmoja wao mwenye carrier hapa wote ni mabitozi wasio na mpango)
    Na mpaka wamepata muda wa kujoin hii nonsense inaonyesha ni jinsi gani ni wapuuzi.
    Hamnaga contest ya sexy men watu huwa wanakua named by survey sio mijiwanaume mizima kutembea cat walk ili wawejudged
    Shame on us Tanzanians
    Gob bless Tz and it's people
    Misupuu ukinibania una chuki binafsi

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 16, 2009

    kaka michuzi mimi nahisi neno SEXIEST lisingetafsiriwa kuwa mwenye mvuto bali ALIYEMNGONO ZAIDI. Kwa sababu neno sex tafsiri yake ni ngono. Mwenye mvuto ni attractive.
    mdau XYZ

    ReplyDelete
  39. POT - usaJuly 17, 2009

    Wewe DIVI ,,acha matusi nyie watu wa clouds dream zenu wote ni America , mnajifanya wamarekani wa bongo hata kuongea .. mnajifanya hamjui kiswahili vizuri...acha kukandia. wakati tukija huko Bongo unatusumbua tukutafutie mipango ya visa..

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 17, 2009

    Namshngaa huyo anayejiita sijui DIVA or something like that, kwani ameambiwa watu wanatoa maoni ni wanaoishi tu UK, USA or kwingineko, yeye kama point yake ni kuwa watu wawa-support hao mahandsome feki, he should stick to the point, but he has to know kila mtu anauhuru wakufanya anachota kwa hiyo asitulazimishe hapa kuvotia watu ambayo hata hawana sifa zozote, tafadhali msitupozee muda wetu hapa.

    ReplyDelete
  41. tatizo la tanzania ni sisi wenyewe ukiangalia huu upuuzi eti shindano la sexiest ni aibu kwetu watz una mambo mengi ambayo tunahitaji tuyawekee mkazo na sio mambo yasiyo na umuhimu kwa taifa

    mimi ningemuona diva ni makini kama angeanza na shindano la kusaka vipaji vya kiakili mashuleni na kutoa mapesa kupitia kipindi chake.

    jamani sio kila kitu tunaiga toka majuu na ku paste kama lilivyo,hili shindano nafananisha kama na ujio wa zeutamu blog halina maana zaidi ya kutudhalilisha machoni mwa dunia.

    Wenzetu wakenya wana kitu inaitwa HARAMBEE hata familia yako maskini inapigwa harambee mtoto anakwenda shule.Sisi eti tunaandaa ashindano la kutafuta kisura wa kiume wa dar aibu

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 17, 2009

    hivi wewe dada unaejiiita diva ukaumia muda wako wote kuandika huko kujitea kwako cjui ndo kutuvutia na hiyo idea yako ambayo haina kichwa wala miguu maskin pole sana kwa sababu utavote wewe na hao wenzio wa clouds au labda ujichagulie mwenyewe mshindi aliyekuvutia bure kabisa umeandika pumba na usubiri majibu zaid maana umelianzisha utajuta kwanin ulijibu bora ungekaa kimya,na nyie wanaume msione kupapatikiwa na wanawake ndo mkajiona mmemaliza na kukaa hapo kujiuzisha sura tu, anony tupo na tutaendelea kuwepo.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 17, 2009

    Sexiest man wangu nilishamchagua mapema ananituliza siwezi kumchangua mwingine. Sioni zaidi yake.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 17, 2009

    bora hata wangemuweka Michuzi hapo ningechagua. Lakini haooo watoto wa mama hao hata hawafai.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 18, 2009

    Diva Nilikwambia hiyo Idea Yako Famba We ukawa mbishi mwenye akili hawezi kukubari upumbavu wako nadhani mwenyewe umeona mwenyewe!
    Pili usione wanaopitia mtandao wapo US na Uk,wapo Dunia Nzima Na Kwa Maoni yangu hakuna hata m1 aliekusapoti na pumba zako! Me kila siku nakwambia dada kwa hilo shindano umechemsha nenda school ukajifunze ujasiliamali vizuri..Nashukuru Wadau Duniani Kote Kwa Kumfahamisha huyu dada(DIVA) vizuri maana ni mbishi kweli me nilimwambia mara nyingi sana na hata nikatumia redio yao(clouds) Kumueleza io ishu lkn alipaniki balaa! Thanx Wadau Duniani

    Bob Sambeke
    TANZANIA.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 18, 2009

    kaka michuzi japo maoniyangu hukuyaweka ila nasisitiza kua mtoto wakiume unajitoa mbele ya wanaume wenzio eti wakuangalie na kukuchagua jinsi ulivyomzuri lazma kutakua na wlakin,wazazi msiwakomalie tu watoto wenu wakike na wakiume pia na haya maendeleo,mnajikrim,mnachonga nyusi,mnapaka poda na kuweka kalikiti mbwembwe then mwanaume mwenzio akupigie kura ka nyi watoto huu si utamaduni wa mbongo,naona mwende mombasa,kama swala la mvuto wa mtoto wakiume si kupaka poda n kuchonga nyusi no,nikupiga tizi havi,kusaka mshiko kwa nguvu,ni hayo tu MDAU GREECE

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 18, 2009

    AMA KWELI NI WAREMBO HAWA MMMMMMMMMM NAWATAMANI MIMI JAMAN
    JOSE

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 18, 2009

    Nilkuwa najiuliza huyu DIVA ni mtu wa aina gani kwani wala haelwi anachokisema. Analaumu Wadau walioko nje na kujisifu yuko Tanzania anaendeleza utamaduni. Kama inavyoonekana kwenye comments zake

    “hey guys,hamna aliewalazimisha ku vote coz kama ni utamaduni hata nyie mmeuharibu kwa kwenda kujenga nchi za wenzenu na kuacha nchi yenu huku..sasa si mmeondoka huku basi mmeacha sisi tukiwa tunaendesha nchi katika swala la burudani ambayo ni jadi yetu na nia na dhumuni letu ni kupitia burudani na ni clouds fm babes”

    Haya mashindano uliyoandaa sio jadi ya hata kabila moja la TZ kama ulivyodai hapo juu. Huu ni upumbavu ambao hauna uhusiano wala mashiko katika jamii yetu lengo lake ni kulemaza vijana wawe wanajiuza kwa uzuri. Au ndio unafanya intoxication kwa Watanzania kama vile ulivyojielza katika blog yako kuwa utawa intoxicate watu na tabia zako. Kwa taarifa yako utapata wachache ambao nao watakukimbia baada ya kuona maoni ya Wungwana wa blog ya jamii

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 19, 2009

    Jamani swali limeulizwa, kinachotakiwa ni jibu la aina yake. Hayo majibu mengine ya nini? Haijalishi ni muarabu au muafrika Cha muhimu ni nani anayekuvutia?
    Sikujua hata wanaume wanaoneana wivu!!Au mabasha?
    Waachieni wenye majibu yao wayatoe, kwani uzuri wa kitu uko kwenye macho ya mtazamaji

    GJK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...