hapa ndipo ZIZINI RESTAURANT iliyomo katika jengo la Benjamin Mkapa Towers (zamani Mafuta House) kona ya Barabara za MAKTABA na JAMHURI STREET jijini Dar katika ghorofa ya awali (mezzanine) usoni na Patco Supermarket. Yaani ukimaliza ngazi tu pinda kulia....
Wadau wanaohangaika kupata msosi wa kimatumbi asubuhi, mchana na jioni ZIZINI RESTAURANT ndiyo jawabu. Hapa asubuhi kuna mtori, supu aina zote, vitumbua, maandazi, haf-keki, chapati maji, bajia nk. Mchana kuna misosi kama vile ubwabwa (mchele wa kyela), ugali, maharage ya mbeya, kisamvu cha msangangongele, dagaa wa kigoma, samaki aina kibao pamoja na Zizini Spesho . Meneja wa Zizi hili anko Allan Shaidi anasema wadau msikonde wala nini. Dina la mchana pamoja na lanchi ya usiku pamoja na vilaji vya moto na baridi vinapatikana kwa bei ya kiwandani....
Vilaji moto na baridi vipo, mandhari na samani vya kisasa pamoja na wahudumu walioenda shule pia ni alama ya ongeza hapo Zizini Restaurant.
Usafi na vifaa vya kisasa
kila kona kuna skrini za TV na upande mmoja kuna hili boti maalumu na projekta kwa siku za matukio makubwa kama vile ligi ya uingereza na michezo yote katika SuperSport. kwa sasa Zizi liko wazi toka saa moja asubuhi hadi saa mbili usiku. bei ya vilaji na vitafunwa ni ya kawaida wala usihofu kitu
Pia unaweza kutoa oda ya staftahi
ukaletewa ofisini kwa bei poa. Buku bee umeshiba...
Kwa maelezo zaidi:
ZIZINI RESTAURANT
BENJAMIN MKAPA TOWERS
MAKTABA STREET
MEZZANINE FLOOR
TEL: 0717 964 215
0788 723 802




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Panavutia sana na hiyo menu imetulia sana,naombeni mnisaidie hicho kisamvu cha msangangongele ndio kisamvu gani au kinatoka wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2009

    safi sana. ukizoea hizi menu unaepukana na ile Rashidi kafunga goli moja kachoka wapinzani wanashambulia ye hawezi tena kushambulia na kuongeza mabao kama afanyavyo Fenando Torres wa liva. nadhani hapa hakuna mambo ya kentuky fried chicken (KFC) au macdonalds burgers manake zile ishu ni kurostishana kusiko na mpango. Hongereni sana tena sana wazee kwa kujitahidi kutusaidia kutunza ile naturality. african man masti bi strong as he was naturaly meant to be. ahsante sana kwa taarifa bro michuzi.
    hivi vyakula vya kienyeji ndo tunakiwa tule jamani hizi chipsi zinatuua hasa kwa watoto wetu tusiziendekeze

    ReplyDelete
  3. Parking magari tunapark wapi? huko huko juu au? Usije ukapark chini unamaliza kujilamba na wewe unakuta UMELAMBWA Sait Mira zote!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2009

    Well done Allan. Safi sana!

    Hongera ndugu yangu, sifia pale panapostahili. Nitafika kuonja mtori na thupu ya thamaki

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2009

    annons #2 na mlevi...acheni mbavu zangu

    asante kwa taarifa yenye akili,tutakuja sana tu apo

    bei ziwe pia za kimatumbi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2009

    haya ndo mambo..clean place, nice menu..just perfect!keep it up

    ReplyDelete
  7. Mwakipesile/silver springJuly 15, 2009

    Restaurant ni biashara ambazo zina kufa haraka sana, gharama za uedeshaji wake ziko juu sana na unapo kosa watu wenye utaalam hasa mameneja katika field yenyewe ni kosa kubwa. kumbuka kwamba malighafi inayotoa faida ni chakula,ok na vinywaji na faida ni lazima ianzie kwenye sahani moja inayouuzwa ndiyo uhesabu sahani zote ulizo uza, sasa kufanya ile costing ya sahani moja hapo ndipo watu wengi wana shindwa. Tuna mtakia mafanikio Allan na ajaribu kuangalia sana wastage na wizi vina uwa sana restaurant siyo nyumbani tu hata na hapa USA.Baada ya miaka miwili nyingi zinakufaaaa..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 15, 2009

    Restaurant iko sehemu nzuri.

    Ila mimi naona jina la restaurant"ZIZINI" kama halijakaa vizuri. Nadhani watu wa marketing watatusaidia hapa. Kila mtu anajua kwenye zizi ndipo utakapokuta uchafu uchafu. Sasa kama sehemu ya chakula mmiliki unapaita ZIZINI sijui ndiyo vipi tena.

    Ninamaanisha kuna majina Trade names zimekaa kweli kibiashara na pia kuna trade names ambazo hazijakaa kibiashara.

    Mfano kuna siku nikiwa na demu wangu ambae baadae alikuja kuwa mke wangu hadi hivi leo tulikwenda nae guest house. Tulipofika tukakuta guest imeangikwa "MAMA MZAZI GUEST HOUSE"

    Nilijisikia vibaya kwenda kustarehe na demu wangu katika guest house hiyo sababu ikiwa ni hilo jina tu. Nikaahirisha zoezi mahali hapo.

    Ni maoni yangu tu.

    Mie Scallywag

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 15, 2009

    ni kweli hapo zizini msosi wa nguvu,tena pembeni yake kuna boutique za nguvu kuna pamba kali sana na bei nafuu, kweli Benjamin Mkapa panapendeza ni mahala pa kutembelea, utapata pamba safi za kuvaa tangu casualwear,outing wear na nguo za sendoff na harusi. ukichoka shopping unaingia zizini kupata msosi na snacks za nguvu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 15, 2009

    Michu!!! Allan hakuishia hapo tuu, labda wadau wangepenad kujua kwamba kwa taaluma huyu Bwana Allan ni Hotelier tena mtu wa jikoni. Kama mtakumbuka pale Chuo cha Utalii Kivukoni, huyu bwana ndipo alipokuwa akitoa dozi kama mkufunzi enzi hizo.. anaendeleza libeneke vile vile kwenye http://www.zizini.com .... BIG FIVE Allan (dRU)

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2009

    aya na wewe annon "Scallywag"

    umebanwa au???

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2009

    Anony "Scallywag",umeniua kweli ni hiyo ya mama mzazi...tehehehe.yenyewe mimi nilidhani wanaadvertise mbolea.

    ReplyDelete
  13. Mi ningependa kujua moja. Hii hoteli yaelekea safi tena bab kubwa; jikoni, sehemu za kukaa, nk. Tena...ukweli baadhi ya hoteli zetu siku hizi safi ndiyo.
    Je, inawezekana kupiga pia picha vyoo maana popote duniani ukienda Waafrika tunazo hoteli na baa nzuri nzuri, magari mazuri mazuri, nyumba nzuri nzuri zenye makochi na masuti... lakini nenda sehemu za kujisaidia (msalani) utakuta mambo tofauti kabisa...
    (Ni kama ule wimbo wa zamani wa masuti njiani kumbe nyumbani kunguni tele...!)
    Kama hii hoteli itatunza pia mazingira hayo basi itabidi pia tuelezwe kusudi liwe jambo la mfano; la kuigwa na wengine.
    Nimeliongelea kidogo pia hapa :
    http://www.kitoto.wordpress.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...