

Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Bw. Henry Tzamburakis akimkabidhi mshindi hundi yake leo
Vodacom Tanzania kupitia programu yake ya Uaminifu ya Tuzo Droo Loyalty leo imekabidhi zawadi yake ya kwanza ya mwezi ya promosheni inayoendelea ya Tuzo Droo kwa 2009/10.
Mshindi wa Julai 2009, Bi. Agnes Aaron Sabiti anayetokea KIA –Kilimanjaro -, alikabidhiwa kitita chake cha Tsh 40m/- pale Vodashop Moshi.
Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Bw. Henry Tzamburakis aliiwakilisha kampuni ya Vodacom kwenye sherehe hiyo ya kukabidhi zawadi.
Bi. Sabiti, alisindikizwa na familia yake pamoja na wanachama wa kanisani kwake, aliisifu Vodacom Tanzania kwa moyo wao wa kujali na kurudisha kile kidogo wanachokipata kutoka kwa wateja wao.
Aliwaomba wananchi kujiunga na kutumia mtandao wa Vodacom na aliwahakikishia watanzania kwamba Tuzo Droo hii ni huru nay a haki kwa wateja wote wa Vodacom.
JAMANI HUYU SI MDOGO WAKE KINJE AU?
ReplyDeleteHILO JINA LAKE LA PILI LINAONEKANA KAMA SIO LA KIRAIA AU NDIO UZUNGU WENYEWE!!
HIVI TANZANIA NANI RAIA HALISI!!
ndiyo huyo ni mdogo wake kinje
ReplyDeletehuyo siyo mdogo wake kinje huyo anaitwa henry george hilo jina la mbele sijui kalitoa wapi ila huyo jamaa ana undugu na kinje nadhani kwa upande wa mama huko ,jamaa mbabe sana huyu sijui kama siku hizi amepunguza utoto maana ngumi mkononi huyo anyway umri umeshaenda na majukumu pia naona sasa ametulia ,safi sana mkuu henry piga kazi mwana tusonge mbele
ReplyDelete