Dk Margaret Chan, Mkurugenzi mkuu wa WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Margaret Chan, atawasili nchini kesho kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lei, akiwa nchini, Mkurugenzi huyo atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mjini Dodoma, ambapo atafanya mazungumzo naye.

Baada ya kutoka Dodoma, Dkt. Margaret Chan, atatembelea maeneo mbalimbali ili kuona shughuli zinazofanywa na Sekta ya Afya, katika kupambana na ugonjwa wa malaria nchini.

Pia, anatarajia kutembelea hospitali ya Amana, ambapo atapokea taarifa ya kazi zinazofanywa katika hospitali hiyo, hususan za kupambana na ugonjwa wa malaria nchini.

Mkurugenzi huyo, akiwa nchini, pamoja na mambo mengine, atatembelea Kituo cha Taasisi ya Afya Ifakara, kilichopo katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ili kuona mpango wa chanjo ya malaria, pamoja na maendeleo ya utoaji wa huduma za afya kwa akina mama na watoto.

Mambo mengine atakayoyafanya, ni pamoja na kuzungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, ambapo pia, atatoa ufafanuzi kuhusu ziara yake, akiwa na mwenyeji wake, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Prof. David Mwakyusa.

Wakati wa kuhitimisha ziara yake hapa nchini, Mkurugenzi huyo atakwenda Zanzibar, ambapo atakutana na Rais Aman Abeid Karume. Akiwa Zanzibar, atapokea taarifa kutoka kwa wataalam wa afya, kuhusu ugonjwa wa malaria na harakati zinazoendelea, za kuutokomeza ugonjwa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. We michuzi usichafue hali ya hewa ni rais Abeid Aman Karume au Aman Abeid Karume? tafadhali wewee kama umekosea badilisha, kama mie nimekosea niwie radhi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...