WAFANYAKAZI YA KUBEBA MIZIGO KATIKA KAMPUNI YA S.S. BAKHRESSA YA AZAM WAMEGOMA, KWA MUJIBU WA HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI.
CHANZO CHA MGOMO HUO INASEMEKANA NI KUSHINIKIZA KUPATIWA MASLAHI MAZURI YA KAZI, IKIWA NI PAMOJA NA AJIRA YA KUDUMU PAMOJA NA UTARATIBU UNAOKUBALIKA NA PANDE ZOTE MBILI ZA KUINGIA NA KUTOKA VIWANDANI. INASEMEKANA HIVI SANA KUNATAKA KUJA UTARATIBU WA VITAMBULISHO VYA MUDA AMBAPO MWISHO WA SIKU MFANYAKAZI ANATAKIWA KUVIREJESHA MARA BAADA YA KUMALIZA KAZI, TOFAUTI NA AWALI AMBAPO KULIKUWA NA VITAMBULISHO VYA KUDUMU.
HABARI HIZO ZINAONGEZEA KWAMBA WALIOGOMA NI WABEBA MIZIGO KATIKA VIWANDA VYA KUSAGIA UNGA A NGANO VYA MZIZIMA NA TAZARA NA SEHEMU NYINGINE NA KWAMBA MAJIDILIANO YANAENDLEA KUTAFUTA MUAFAKA KWA NJIA YA AMANI NA MAELEWANO.
AFISA WA KAMPUNI HIYO AMETHIBITISHA HILO ILA AMESHANGAA KWA HATUA YA WAFANYAKAZI HAO KUGOMA LEO, AKIDAI KUWA NI KINYUME NA MWENENDO WA KESI WALIYOFUNGUA KUDAI HAYO WANAYODAI KATIKA MAHAKAMA KUU KITENGO CHA KAZI AMBAPO KESI HIYO INASIKILIZWA KESHO.
HABARI ZAIDI BAADAYE


Uongozi pale sio mzuri kabisa, ndugu yangu alifanya hapo kazi ilikuwa ni unyanyasaji mtupu
ReplyDeleteBakhresa vumilia uchaguzi 2010..CCM wanataka uchangie nyingi mwaka huu...toa tuu hutasikia matatizo ya wafanyakazi!!
ReplyDeleteHaya yote ni matokeo mabaya ya ubepari. Bepari siku zote yeye anatafuta njia ambazo zitamwezesha kuwanyonya wafuja jasho zaidi.
ReplyDeleteHali inakuwa mbaya zaidi pale wafuja jasho wanakosa wa kuwatetea. Katika nchi ambayo watawala wanakumbatia zaidi wenye mali hali ya maisha ya wafuja jasho ndiyo inakuwa mbaya kabisa.
Wema Huanzia Nyumbani.Inakuwaje anatoa misaada mingi kwa watu Back lakini wanaomzalishia hawathamini?
ReplyDeleteHivi kwanini nchi yetu haingilii kiundani haki za wafanyakazi, kwani mambo yanayotendeka kwenye haya makampuni binfsi ni unyoinyaji,ukandamizaji dhuluma tupu.
ReplyDeleteMakampuni haya yanawalipa wafanyakazi wao pesa kiduchu, lakini cha ajabu wanaweza wakaajiri wafanyakazi toka nje wakawalipa hela nyingi ajabu(kazi hizohizo), je hii ni kusema nini,kuwa Watanzania wao ni `wafanyakazi rahisi'
Jamani hata nyie wazawa ambao mumejaliwa hamuwapendi Watanzania wenzenu,mnataka wawe masikini mpaka lini. Cha ajabu wakisikia mtoto/watoto fulani wanashida,watajifanya wakwanza kusaidia,kwa kujitangaza, wakati watoto kama hawo wapo kwenye watoto wa wafanyakazi wao. Huu unaitwa nini wajameni
M3
kazi kama hizo huku mamtoni ndo zinzliliwa. sema bongo hazilipi ndo tatizo, lakini kazi hizo za kubeba mizigo viwandani ndo hat sisi tulioko mamtoni tunazifanya tena ukiipata kama hiyo unashukuru na unalilia upewe masaa mengi
ReplyDeleteMIMI NAFANYA KAZI HAPA KWA BAKHELSA!!SIO SIRI SISI TULIOAJIRIWA TUNALIPWA VIZURI SANA UKILINGANISHA NA WATU WANAOFANYA KAZI SEHEMU NYENGINE.
ReplyDeleteTATIZO LIPO KWA HAWA MADEI WAKA WAOSIO KAMA SISI SASANAO WANATAKA MSHAHARA MZURI KAMA SISI
NIMESHAWAHI KUFANYA KAZI KWA MENGI HAPO MWANZONI NIKAKIMBIA KWA UNYONYAJI ULIOKITHIRI HUKU LEO NACHUKUA MSHAHARA MARA TATU YA KULE.
MWISHO NASAPOTI HAWA WENZETU WADAIHAKI YAO ILINAO WANUFAIKE
kweli mnaibiwa yaani jamaa kiwanda kizima wanaajiri kama wewe ni hasara tupu sema tu kwavile bongo hawajali ubora wa bidhaa hamuwezi kuwa wazalishaji bora kama mnaandika kwa shida kama wewe but "VERY CHEAP"ndio maana mabosi mengi na bakheresa wanakugombea mzalishaji wao.GOBACK2SCHOOL
ReplyDeleteNachukia sana kwa matajili wa kitanzania kupenda kuwanyonya wafanyakazi wao. huu ni mfano mmoja lakini wapo wengi tu. wanajifanya kutoa misaada kibao na kuimbiwa nyimbo za kusifiwa lakini kiwandani kwao ni hovyo kabisa.
ReplyDeletebadilikeni matajili wa kitanzania waimueni na masikini japo wapate kitu kidogo.