Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia)akijifunza jinsi ya kutumia tovuti ya wananchi kujibu kero ya wananchi wakati wa mafunzo ya maafisa habari na mawasiliano kutoka Wizara , Idara zinazojitegemea na Taasisi mbalimbali za Serikali leo mjini Morogoro. Wa kwanza kulia ni Afisa HabariMwandamizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Joseph Ishengoma akimfundisha Mkuu huyojinsi ya kutumia tovuti ya wananchi kujibu kero mbalimbali za wananchi kwenyeUkumbi wa Manispaa hiyo.
Picha na na Aziza Msuya wa Maelezo Morogoro.
tovuti hiyo ni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sasa Mkuu si ungetuwekea anuani ya hiyo tovuti basi tuifahamu..!!!

    ReplyDelete
  2. Mdau Aster kutoka jinsia na kids mbona sikuoni???

    ReplyDelete
  3. Tatizo la hawa Wazee, ni conservative. Yaani hawaki kabisa kujifunza kompyuta. Ilimradi secretary anataipu barua zake basi. Hapa labda JK kawatishiwa kuwafukuza kazi. Tubadilike tuanze kuendesha nchi kwa ufanisi.

    ReplyDelete
  4. - kwa mwenye kufahamu je 'wavuti' ni neno rasmi la kiswahili?. Na je ni nini tofauti ya 'tovuti' na 'wavuti'?

    ReplyDelete
  5. Toka nitume swali kwao umepita mwaka sasa sijajibiwa. Wizi mtupu!

    ReplyDelete
  6. Kiongozi yoyote ku embresi tekinolojia sio lazima ajue yeye binafsi kuitumia, Kiongozi anatakiwa kutoa vision afu wachapakazi waifanyie kazi kuifanikisha.

    kwa mfano kwenye kutumia PC hao wakuu wa mikoa sio lazima wajibu maswali kwenye computer wao wenyewe isipokuwa kinachotakiwa ni wasaidizi wao kujibu maswali lakini hao viongozi lazima wathibitishe majibu hayo ni ya ukweli ndio mana wana wasaidizi na masekretari.

    Kwa mana ingine ili hio tovuti na madhumuni yake yafanikiwe sio lazima viongozi hasa wazee wetu wajue kutumia PC, kama wakijifunza ni vizuri lakini sio lazima cha muimu ni wajue hiyo nyenzo ipo na inaweza kuwa saidia kusaidia wananchi wanaowaongoza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...