Nyota wa mpira wa kikapu anayechezea ligi ya NBA na timu ya Grizzlies, akiwa amepozi na mama yake mzazi na mdogo wake aitwaye Akbar mara huko marekani.
Hasheem ameiambia globu ya jamii kwa simu muda mfupi uliopita kwamba anajiandaa kuja vekesheni fupi nyumbani, na anafurahi kwamba atapata nafasi ya kuwashukuru wadau kwa kumuombea mema kwenye maisha yake ya baskteball ya kulipwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Big up Thabit, Lakini kiukweli huyu jamaa kaenda hewani, yaani amekaa kwenye kiti amelingana na mama yake! Utafika mbali sana Thabit, Mungu akutangulie kwenye mambo yako yote hasa mambo ya mira wa wavu.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Thabeet , ukija nadhani wapambe watafanya party ya kukukaribisha na kiingilia sh 20,000 , ni kutengeneza hela nyingi kwa mgongo wako ..Martin uko hapo?.

    Haya tukija kw aurefu wa huyu Thabeet , jamani nataka kujua huo urefu ni genetic au ni ile disoder ya mifupa? maana naona kwenye fammilia sioni mwingine mrefu hapo inakuwaje ? hope sio kama ni tatizo ni kwamba urefu wa asili toka kwnye fammilia

    Hongera sana Thabeet , nita kuwa na vaa tshirt imeandikwa Hasheem Thabeet!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana. Upo juu na ongeza bidii, usione hapo pametosha. Hongera sana pia Mama Thabeet. Mwenyezi Mungu amlinde mwanetu na wabaya. Amina.

    ReplyDelete
  4. Hongera Thabeet, ila kitu kimoja mwanangu unacho nikera unapo ongea kiswahili unajifanya kama vile hukijui mwanangu!wakati we ni mbongo pure na kuna watu wamekaa nje ya nchi miaka na miaka lakini wakiongea kiswahili ni saafi na mpaka lugha za kabila zao wanabonga, wewe mwanangu unabana pua kama sio mbongo vile - hiyo ni noma mkataa kwao ni mtumwa - jivunie uafrika na utanzania bila kusahau lugha yako!

    ReplyDelete
  5. JAMAA MPAKA LEO ANASHINDWA KUWEKA SAWA DRESS CODE SUTI NA KAPELO WAPI NA WAPI HAYA NDO MATATIZO YETU PAMBA HAZIKAI SAWA .
    MUANAGALIE DOGO WAKE ALIVYOKUA MAKINI PAMOJA NA MAMA PEMBENI.

    ReplyDelete
  6. mbeba-box mzalendoAugust 11, 2009

    Acheni ku-hate nyie wabeba mabox mlioishiwa fikra. Kwanza kuhusu urefu wa Hashim, inawezekana kabisa kwamba amerithi toka kwa baba yake na huyo mdogo wake amerithi toka kwa mama yake. Kama ulisoma Biology in Form 3/4 utaelewa kwamba genes za Baba na Mama ndio zinampa mtoto genes zake.

    Na kuhusu dress code, mbona huwa tunaona professional ballers wengine wa kimarekani pia wanavaa suits na kapelo. Au kwa kuwa wao ni wamarekani basi sio noma ila akifanya hivyo mmatumbi mwenzetu Hashim basi inakuwa noma. Acheni hizo kasumba nyie waumia migongo.

    La tatu ambalo ni la kweli ni kuhusu watu huko bongo kutaka kutengeneza fedha kwa mgongo wa Thabit. Hiyo ni kweli na inasikitisha sana.Sidhani kama uongozi wa basketball in Tanzania au in Dar-es-salaam walifanya kitu chochote ili kumuwezesha huyu dogo kwenda marekani. Lakini cha ajabu ni pale wanapochukulia mafanikio yake kwamba yametokana na wao. Hivi ni lini TBF ime-organize mafunzo kwa vijana wa mashule? Ni lini TBF wamefanya scouting ya vipaji vya vijana ili kuwa - groom for NBA.

    ReplyDelete
  7. Wazazi wengine muige tabia ya mama yake Thabit, unatakiwa umsaidie mtoto wako katika kile anachoamini na anachoweza, sio kumlazimisha vile uonavyo wewe ni sawa, Kama mtoto anauwezo katika fani fulani wewe kama mzazi usimwangushe wewe muunge mkono na umwambie unaweza na hakika atafanya makubwa. Nawakilisha

    ReplyDelete
  8. Duh hawa jamaa wana hate vibaya kweli, kama mtu unafuatilia Basketball utajua kwa nini ka vaa suti na kofia, basi ni hivi katika siku ya draft lazima uwe presentable to the media na timu ambayo itakuchukua,ni common sense pia uwe smart, na wakitangazza timu gani utaenda,unakuwa presented na kofia kama ukaribisho, thats why kavaa kofia na suti..sio mnaongea tuu pumba
    Mdau Birmingham

    ReplyDelete
  9. Hashim tulikuwa naye pale sinza tukamshauri ajifunze basketi balli kwani hakuweza kucheza nasi alituzidi kimo kinoma, asisahau kutembelea kiwanja cha kipori

    ReplyDelete
  10. we unayeuliza kapelo, hii ilikuwa siku alipoteuliwa na Memphis na baada ya uteuzi wake walimpa kofia ya timu yao avae. Sio yeye peke yake, wachezaji wapya wote walivaa kapelo za timu zilizowateua. Kuvaa kapelo na suti ni kawaida timu zinaposhinda ubingwa wa ukanda wa mashariki/magharibi au zikishinda ubingwa wa taifa wa NBA; au mchzaji anapohamia timu mpya; au wachezaji wapya kuteuliwa.

    Acha ushamba!!

    ReplyDelete
  11. Umetoa pointi nzito sana mdau wa Tue Aug 11, 03:47:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous.
    -Mdau aliyenyooshwa na bakora.

    ReplyDelete
  12. Hongera Hasheem ila watu wanocomment vitu bila kujua maana yake wanaboa sana.
    eTI hasheen hajui kuvaa kavaa kapelo na suti.FYI hiyo kofia ni ya team na haihusiani na outfit .you have to wear and represent a team unayochezea hata other NBA players wengine huvaa za team zao na suti lol...jamani kama kitu hujui uliza sio unmshambulia kaka wa watu. we ndo mshamba kwa kuona kama mwenzio kavaa kutaka kumatisha lol

    ReplyDelete
  13. aliyecomment kuhusu kiswahili cha Hasheem me naomba nimtetee. He did some speech class ambazo proffesionals wengi wanafanya na nia yao ni kumuwezesha mtu awa na American accent .sasa matamshi unakuta mtu anafundishwa kubit tongue wakati anaongea so hata akiongea lugha yake unakuta anatamka vitu the same
    but overall the guy is still humble
    si afadhali yeye hata kiwanja amekaa. wanaoniusgi ni masista du na mabrothermen wa hapo Bongo hata hawajawahi kupanda ndege lakini wanajifanya wanaongea kidhungu halafu kiswahili hawajui.
    it sucks lol

    ReplyDelete
  14. Big Up Hasheem! Nilifurahi kukuona umekuja kwenye soccer match/barbeque ya Wabongo DC metropolitan area, ulionyesha uzalendo.
    Kapelo na suti ni kawaida jamani kutokana na tukio; sportsman wanalazimika kuvaa hizo hats/caps kutangaza timu zao katika ocassions hata kama wamevaa suti.

    Kuhusu kuongea kiswahili with an accent, hapo inabidi kijana akubali kujirekebisha. Hii ni common kwa watu wakikaa nje kidogo tu wnajikuta wakitaka kuonyesha eti hawawezi kuongea lugha yetu bia accent! Kishanglish tukiruhusu lakini jamani maana English ni lugha ya pili na ina more accurate words.

    yes, inasikitisha kuona TBF na watu kadhaa watatumia jina la jamaa kwa manufaa yao. Nilishangaa kumuona Bibo, mwenyekeiti wa TBF mapicha kibao eti kja U.S kuhudhuria NBA draft!! I hope alijilipia nauli.

    Piga tizi mtu wangu ugangamale NBA inahitaji msuli. Ongeza pace unapokuwa court.

    ReplyDelete
  15. nyinyi mnajifanya kutaka kuchuma noti kwa mgongo wa hasheem ebu mwanangu wadis waambie sitaki hiyo mambo jiparty liwe la kawaida tu bila kiingilio au toeni kadi za mialiko za buree na mgawe bila upendeleo acheni kuchuna watu kimtindo alah!!

    ReplyDelete
  16. Jamani kuna raha yake kutamka maneno kwa accent ya Kiamrekani, nime kaa USA nikajikuta siwezi ongea Kingereza bila kuonge kwa accent ya kimarekani tena tatizo nikajikuta nikiongea kwa accent ya ki ghetto ndio nawezea zaidi , ni aaibu ila sina jinsi.

    Nakumbuka pia nime kaa Kenya nikajikuta naonega kama wao , mbaka siku niko USA nikakutana na mbongo akawa ana dhani mimi Mkenya , jamani haya mambo yanatokea bila kutegemea.

    ReplyDelete
  17. Babu usitusahamu,nigee mtaji kaa dola elfu kumi hivi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...