Boston Bongo Rangers
Bongo Stars united wakiwa kambini
Bongo Stars United

Lile pambano la soka linalosubiriwa na wengi wa washabiki wa mjini Boston na vitongoji vyote vya Massachusetts linakaribia na homa yazidi kupamba.
wachezaji wa Boston Rangers,japo wao wanadai hawapo kambini lakini habari za radio mbao zilizotufukia ni kwamba wameamua kuunganisha wachezaji wa state yote ya Massachusetts kwa mpambano huo hio siku ya jumamosi August 8 utakao chezewa mjini Boston,timu hiyo ikiwa na wachezaji wengi wazoefu akiwemo Francis Makala aliyewahi kuichezea Simba,wameahidi ushindi kwa mashabiki wao.
katika kambi ya Bongo stars united(kandanda safi kiwango cha TBS) wao wanasema hawana wasi wasi wowote na timu ya Boston tunajua wanavyocheza kwani tulituma muakilishi aliyetuletea mkanda wa video katika mechi yao walipo cheza na Wakenya wa huko Boston.
Katika homa nyingine ya mpambano huo wa jumamosi ni mchezaji Tifu (NJ) kila timu ikidai ni mchezaji wake.
Tifu huchezea Bongo Stars katika mechi zake nyingi na Boston Rangers hua wanamwalika katika mechi zake za huko kama mchazaji mualikwa. Bongo stars imesema wao ndio watakae msafirisha Boston na kama Boston bado wataendelea kudai ni mchezaji wao Bongo Stars haitambui hilo.
kambi za timu zote ni shwari. Bongo Stars itaondokea DC ijumaa Usiku kupitia New Jersey na New York itapiga kambi mji wa Leominster uliopo miles chache nje ya Boston.
Wachezaji wawili Libe Mwang'ombe(DC) na Mody Majaliwa(Seattle) wao wataingia Boston ijumaa asubuhi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wadau Tunaomba mechi ya kirafiki kati yenu na sisi wadau wa UK. Wasiliana na bw Sweet kwnye E-mail ifuatayo: sweety_s_2007_@hotmail.com mjichague mastaa wote marekani nzima. Tupo pamoja wadau.

    ReplyDelete
  2. Nassoro nakusubiri nikuone

    ReplyDelete
  3. Hapo nia yenu ni kutuonyesha na kututambishia jezi, maana sisi wapinzani wenu wa jadi majuzi tulikuwa hatuna hata jezi moja..hahaha, hongereni lakini

    ReplyDelete
  4. Hii organization nzuri sana,kwa mazingira ya USA (ukubwa)na ughali wa maisha mnaweza kukusanya wachezaji kutoka Seattle(Washington),Washington(Dc),New Jersey,New York etc.
    Basi next time itabidi ivuke bahari na kupambana na Sweden,Finland etc.

    ReplyDelete
  5. sasa jamani hii mechi inachezwa wapi?? mbona boston wabongo tuko kibao lakini hata hatujaalikwa kujiunga au kujifua na timu hii? Kiongozi ni nani atupe info.?

    ReplyDelete
  6. Humphrey, Innocent, Simon wa NC hamjambo?

    ReplyDelete
  7. MBONA CHELSEA KIT!

    ReplyDelete
  8. mipango iko mbioni kuvuka bahari mwakani mwezi wa saba hasa Sweden tulichagua Sweden kwasababu tunamchezaji wetu mmoja huko anaitwa Richard,lakini kama kuna timu yoyote inatuhitaji tuje sisi tupo tayari kuna vipaji vingi hapa Marekani na kama tukiweka nguvu pamoja hakuna timu yoyote itakayo tia mguu,kila kitu ni mipango mail yetu ljoe_oo@hotmail.com tufanye mawasiliano mapema kuleta timu si tatizo,asante

    ReplyDelete
  9. Baba UbayaAugust 04, 2009

    hizo jezi za Chelsea nadhani Abramovich atakuwa amewakodishia kiaina.na hizo za Cuba huenda washakabiziwa uridhi na Kikongwe Castro..teh teh

    ReplyDelete
  10. Baba UbayaAugust 04, 2009

    itakuwa full shangwe kama watu wa UK mkachagua mastaa wenu na USA wakachagua mastaa wao alafu mtanange mkaja kuupigia huku Bongo.nitawapatia udhamini wa jezi na usafiri kwa muda mtakaokuwa hapa.pia baada ya pambano lenu,mtachagua mastaa toka pande zote mbili na kuwapatieni gemu na timu ya taifa ya vijana.

    ReplyDelete
  11. Baba Ubaya tunashukuru. Kama upo serious e-mail za pande zote mbili unazo. Kazi kwako.

    Mdau wa marekani e-mail yako nimeipata tutawasiliana. Sweden ikawa Via Uk kwa siku kazaa mkala dozi si mbaya. Na sisi tutafanya safari kuja baadae kuwapatia fursa ya kulipiza kisasi.
    Ta mate.

    ReplyDelete
  12. kwenye team ya Boston namwona mshkaji wangu - Siraji M. Tumesoma naye Azania sec. safi sana wazee kwa kuendeleza hoby ya michezo!? F. Tall.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...