JK akikagua kivuko katika mto Lituhi, wilayani Mbinga kinachotoa huduma kati ya Wilaya ya Mbinga na Ludewa,mkoani Iringa. Wananchi na viongozi wa wilaya hizo walimweleza kuwa kivuko hicho hakijatatua kero ya usafiri kaztika eneo hilo kwa kuwa hufanya kazi miezi michache sana kutokana na kuzidiwa nguvu wakati wa mvua nyingi na kutatizwa na mchanga wakati wa kiangazi. Viongozi wa eneo hilo waliiomba serikali kujenga daraja kama ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo. JK, ambaye yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua shughuli za maendeleo ikiwemo kufungua miradi mbalimbali na kuongea na wananchi, ameahidi kulitafutia ufumbuzi swala hilo.
JK akimjulia hali Bi.Martha Mahundi na motto wake mchanga aliyejifungua kwa upasuaji katika kituo cha Afya Lituhi,wilayani Mbinga,Mkoani Ruvuma, jana.Wa pili kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mbinga Dr.Emmanuel Mapunda na kushoto ni mganga mkuu wa kituo hicho Martin Ndunguru. JK alikitembelea kituo hicho cha Afya ambapo Askofu Mapunda aliomba kituo hicho kupandishwa hadhi na kuwa hospitali kamili.

Mama Salma Kikwete akimtwika maji Bi Magrethi Kayombo wa kijiji cha Litumba Lihamba muda mfupi baada ya JK kuzindua mradi wa maji kijijini hapo, huku JK na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Mh. John Komba wakishuhudia




JK akiwasalimu baadhi ya wanafunzi wakati aliposimama kwa muda katika kijiji cha Ruanda wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma jana. JK alikuwa anaelekea kijiji cha Lituhi ambapo alizindua mradi wa maji, kutembelea kituo cha afya na kuzungumza na wananchi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Komba kweli limekuwa komba, sijui limejiachia na nene kama Tembo. Komba punguza kula.

    ReplyDelete
  2. I SECOND annoy hapo juu...huyu KOMBA asipoangalia ata drop dead kwa heart attack...Please please lose some few lbs

    ReplyDelete
  3. Ndugu zang kufa ni mapenzi yamungu wangapi wamekufa wakati wanaafya njema kabisa,kuwa mnene sio lazima ni ugonjwa wenginendio maumbile yao.Heart attack anapata hata mtu mwembamba.Wengapi tumewaona wamekufa na wanamuacha Komba kama alivyo.

    Kabla ujamjudge mwenzako jiangalia wewe afya yako kwanza.Na sidhani hapa swala zima lilikuwa ni kujadili afya ya Komba.

    MJusi

    ReplyDelete
  4. we annoy wa kwanza umenivunja mabvu kwa kucheka yani acha tu blog hii kiboko lazima utacheka tu lol ila jamani komba mazoezi ni muhimu saana huo sasa ni ugonjwa ndo mana ze comedy hasa mpoki wanakufanya kichekesho mie huwa tumbo linauma kwa kucheka fanyeni mazoeziiiii sio muda woote kwenye malandkruza tuuuu hata mkiwa dodoma badala ya kwenda nyama choma fanyeni jogging raisi wa ufaransa ni mfano wa kuigwa anakula tizi hasa jogging kwa sana tuu ......VITAMBI NI JANGA LA TAIFA.......

    ReplyDelete
  5. we mama nanihii kwa nini hiyo ndoo ya maji usijitwike mwenyewe....hivi mnaona ndio maendeleo watz kuendelea kubeba ndoo za maji?

    ReplyDelete
  6. jamani ni macho yangu au hiyo picha ya kwanza huyo mama aliyelala kitandani na mwanae hakufunikwa vizuri wakati rais anaenda kumsalimia.naona kama kifua kiko nje?? nisaidieni wadau manake macho saa nyingine yanaona double double..

    ReplyDelete
  7. Michuzi nadhani mto ni Ruhuhu na si Lituhi kama ulivyoandika hapo juu.

    ReplyDelete
  8. Hatimaye JK amesikia kilio chetu na kuanza kufanya vekesheni za ndani.

    ReplyDelete
  9. Anon wa 4:11pm ni kweli hakufunikwa vizuri i was asking the same question naona ni cultural tena!

    ReplyDelete
  10. duu hata mimi nimemshangaa huyo mama alivyoachia kifua wazi, ingawaje amefanyiwa operation lakini asingeshidwa kuvuta hicho kitenge chake akajifunika especially akijua kuna ugeni mzito around the hospital.

    ReplyDelete
  11. Anon 04.11 huyo mama kama angekuwa hana maumivu makali angeweza kuvuta hio nguo na kujifunika mwenyewe tu. Lakini ndugu yangu mama huyo amefanyiwa upasuaji na inawezekana ganzi aliowekewa imeshatoka anamaumivu makali sana tumboni huyo mama hapo alipo ndio maana hata kulala amelala hivyo unavyomuona hapo.

    ReplyDelete
  12. Wewe Tarehe Wed Aug 12, 04:11:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
    Wazazi Bongo ni kawaid kuwa na matiti nje ili kunyonyesha mtoto. Sio kama ughaibuni lazima ujifunike

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...