John akiwa na Yatima Mbalagala
John katika wodi za watoto Shirati, wodi zote zililipiwa gharama za matibabu. hapa baadhi yao wanapokea nauli za kurudi makwao
Wazee na wajane wenye shida wakipokea vyakula rorya
Na wazee wa Kituo cha Fungafunga, Morogoro
Baadhi y Vijana waliopokea baiskeli na fedha za mtaji huko rorya

KONGAMANO LA TUWAJALI WENZETU

The John Mashaka Foundation, wakishirikiana na Zain Corporation na wanahabari wa kujitolea, wanawataarifu wanajamii kupitia vyombo vya habari kwamba kutakuwepo na tamasha katika viwanja vya Biafra Kinondoni siku ya Jumamozi tarehe 29 Agosti kuanzia saa saba mchana.
Lengo la Tamasha hilo ni:
1. Kupinga na kulaani mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino inayoendelea nchini Tanzania na hata katika baadhi ya nchi jirani
2. Kuhamasisha wanajamii kuwa na upendo kwa watu wengine walio katika mazingira magumu, kama vile walemavu, watoto yatima, wazee nk.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo atakuwa Mh. Waziri wa Afya Prof. David Mwakyusa. Wasanii kama G-Solo, Mrisho Mpoto, Mkoloni, Soggy Doggy na wengine wengi watapamba tamasha hilo.

John Mashaka kupitia asasi yake isiyo ya kiserikali, la The John Mashaka Foundation, ametembelea na kutoa misaada mbalimbali katika vituo kadhaa nchini kama vile Tanzania Mitindo House, Kituo Cha Wazee cha FungaFunga, Wazee na Wajane huko Wilayani Rorya.
Kadhalika ametoa mabaiskeli na mitaji kwa vijana huko Rorya. John ametembelea na kutoa misaada katika vituo vya kulelea mayatima ya Msimbazi Center, na Chamazi kule Mbagala.

Kadhalika ametoa misaada mbalimbali kwa maalbino. John amejitolea kuwasomesha maalbino wawili ambao pia ni mayatima kwa gharama ya millioni moja. Tayari John anasomesha mayatima wengine 6 katika shule za sekondari nchini.
Misaada mingine ni pamoja ni mitambo yenye gharama kubwa kwa ajili ya kusukuma maji kusaidia vijiji kadhaa huko wilayani Rorya mkoani mara. Shuguli yote imegharimu kiasi cha Sh. Million 18.6.

Shukrani zetu za dhati zinafikishwa kwa WOTE waliotusaidia kwa namna moja ama nyingine wakiwemo Business Times, na Clouds FM
WITO: WATU WOTE MNAKARIBISHWA KATIKA TAMASHA HILO HAKUNA KIINGILIO CHOCHOTE
Karibuni Sana







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 66 mpaka sasa

  1. Mwaka ujao lazima John Mashaka awe mbunge wa Rorya...naona ameanza kampeni mapeam sana na kwa nguvu zote...you are smart john.

    ReplyDelete
  2. Tatizo letu watanzania mtu anayefanya mambo mema huwa hatuthamini mazuri yake, lakini kusema kweli kijana ameonyesha mfano mzuri kwa jamii yetu, kwa kweli mungu akulinde nauendelee namoyo huo wa kuwasaidia hawa ndugu zetu wasio jiweza,mungu akubariki

    ReplyDelete
  3. Mbona sisi tunasaidia kama hivyo lakini kelele na mashairi kama haya hatupati???

    ReplyDelete
  4. wazungu wanaita "photo opportunity" hiyo.

    ReplyDelete
  5. tamasha litakuwa kwa kingereza?kwani John mashaka anajua kiswahili?wengi wetu hatujui kingereza itakuwaje kwenye Tamasha.
    pia kuwa na Foundation isiwe sababu ya mtu kwenda kuchukua pesa kwa wafadhili Marekani.
    Bakhressa anatoa misaada hana Foundation yake.
    misaada na picha nyingi inatisha sana.

    ReplyDelete
  6. Bila ya kuangalia mtizamo wangu juu ya makala za John Mashaka, ningependa kumpongeza John kwa kitu hiki anachokifanya. Jambo hili ni mfano wa kuigwa kwa Watanzania wote. Fikiria kama wabeba box wote wangekuwa wanasaidia yatima mmoja kila mmoja,..badala ya kukaa kusifia tu ulaya tambarare na kauli zao za " sirudi tena bongo". Fikiria kama Michuzi naye angekuwa na Michuzi Foundation, akatumia uwezo wake na influence aliyonayo kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wazee,yatima,walemavu n.k.Na wewe unayetumbulia macho comment hii na huku moyoni unasema hauna hela kiiivyo..ungekuwa kwa mwezi unatenga hata elfu 30 kwa ajili ya wasiojiweza ungesaidia maisha ya wengi sana, .. Hiyo ni mifano, lakini nachomaanisha kwamba iwapo kila mtu kulingana na uwezo wake angefanya kitu kwa ajili ya ndugu zetu wasiojiweza; tungeweza kuifanya Tanzania boro zaidi.John umeonyesha njia na uzalendo. Umenigusa, na kunifanya kufikiria suala hili na kulifanyia kazi,kuanzia sasa...

    ReplyDelete
  7. Kumbe kuandika kote huko anataka madaraka duhh mi nilikuwa najua tumepata mkombozi kumbe ana yake jamani

    ReplyDelete
  8. Jamani mshaurini huyu bwana kwamba sisi si wapiga kura hivyo anapoteza muda wake kujiuza kwetu..
    Yaani kutoka kote Marekani unakwenda Bongo kutoa misaada umeambiwa Tanzania ni Masikini?? Hii ni sawa tu na Vodacom wanazunguka huku na huko kugawa vimisaada kama pipi.
    Huyu bwana ananikumbusha Maneno ya Nyerere kuwa ukiona mtu anakimbilia sana Ikulu(Ubunge pia) ushtuke!!!
    Watanzania tunachohitaji ni mawazo na mbinu mbalimbali na bora za kuboresha kazi zetu za uzalishaji. Maana hawa watu wanaopewa nauli hakuwakuta wanakufa wana afya zao na wana shughuli zao za kila siku. Na tena ukiongea nao watakuambia vizuri vikwazo vyao. Sasa msaada wa kweli na kudumu ni kuwaimarisha katika kile wanachokifanya sio kuwadanganya na pipi.
    Hii tabia ya kupenda misaada ndio inayotumaliza ....Kwa nini hatuwi kama yule mchagga aliyeenda Mombassa mara ya kwanza?? Yeye kila aina yeyote ya msaada aliishuku na sisi pia.Kama unavyojua tena mambo ya huko.
    Hakuna anaeipenda Tanzania ili aipe vitu bure malipo tunalipa tena sana.
    MASHAKA LETA MAWAZO NA MBINU ZA KISASA TATIZO LETU NI UMASIKINI WA FIKRA, NYENZO ZA KISASA, TIJA YETU IKO CHINI, NK... SIO VIJISENTI!!!!!
    Mzawa!

    ReplyDelete
  9. Namsifu sana John, na Mungu amzidishie, but lazini akumbuke kwamba give a man a fish, and he will eat for a day, teach a man how to fish and he will eat for the rest of his life, sasa akiwapa chakula cha wiki, what about next weeks!! akitoa pesa what about pesa ikiisha!! kwanini asianzishe mradi na kuwapa ajira hao!! na vile vile akumbuke kitoacho mkono wa kulia, basi wa kushoto usijue, he can do all these out of publicity, Mungu anamuona, and thats all what matter!!
    nana

    ReplyDelete
  10. mashaka kumbe tozi nae, mikiki mikiki ya 2010 hiyo, kama unania ya kweli ya kupambana na wahusika sikushauri upitie chama fulani

    ReplyDelete
  11. hata ukiwa fisadi sio mbaya sababu unaonyesha mambo uliyo yafanya japo hayatoshi ungesaidia sana kuweka lami katika barabara ndogo za jiji kupunguza foleni.halafu ungetununulia treni iendayo kasi kwakutumia umeme kwa watu wa kigoma kusaidia watu wanao teseka na usafiri wa treni.hapo bila kupinga ungepita ubunge hatimae uwaziri.tunahitaji watu wakufanya vitu hivyo hatuwapati.

    ReplyDelete
  12. Umefanya vema Mashaka ila kumbuka Mwenyezi Mungu analaani tabia ya kuwatumia wenye shida kwa malengo binafsi, kama siasa, umaarufu na kadhalika.

    ReplyDelete
  13. HUYU JOHN LAZIMA AWE SMART BILA HIVYO ATAKULAJE JAMANI HEBU MUACHENI JAMANI SASA HIVI MSTOE UKWELI MANAKE ZINABANWA KURUSHWA HEWANI WEWE OGOPA KIJANA 97% YA MISAADA YAKE NI KWA MKOA WA DAR PEKE ALAFU KUGAWA FEDHA KAMA NAULI NA KUGAWA MOVIE CAMERA KWA MITINDO HOUSE AIDAIDII KIVIILE AWAJENGEE VIJANA CHUO KIDOGO CHA UFUNDI ILI HATA WALEMAVU WAJISAIDIENI MBELENI ALAFU SI LAZIMA UJITANGAZE KWA SANA UNAWEA PIGA MOTO UNDERGROUND NA WATU WAKAKUKUBALI VILE VILE ILA ILE CAMERA UMETOA DEMU WAKO WA KIZUNGU SIJUI UTAKWENDA MWAMBIAJE MANAKE NDIO ALIKUNUNULIA SHAURI YAKO? WAKUMBUKE KWA MISAADA KIJIJINI KWENU BASI JAMANI
    MDAU STIVE
    POLAND

    ReplyDelete
  14. Nisaidieni kuelewa jamani: Ni lazima ukisaidia ujitangaze?

    Tanga kuna mama mmoja Mtanzania yuko huko huko Marekani huwa anasaidia lakini hajitangazi, je, anakosea?

    New York yuko mshikaji, (simtaji), anakusanya vifaa vya hospitali na kusaidia Tanzania, lakini hajitangazi. Je, anakosea?

    ReplyDelete
  15. great job... Congrats John

    ReplyDelete
  16. Kutoa ni moyo jamani si utajiri, hongera kaka na mungu akuzidishie pale pote ulipotoa kwa ajiri ya kusaidia dungu zetu wahitaji. Na siku zote mwenye moyo wa kutoa huongezewa, nami nawish siku moja nitafanya kama wewe naomba mungu anipe uzima ili nifikie malengo yangu.

    ReplyDelete
  17. DU! Mh John Mashaka, mashauzi yote ayo kumbe unataka uingie mjengoni??? ahahaaa...ok mkubwa, nakutakia kila la kheri japo ungefanya jambo la mbolea ungepitia hapa SAIGONi upate baraka zetu sie wanazuoni.

    ReplyDelete
  18. Mdau Kilo unayoyasema ni kweli kabisa ila sasa kwa gear aliyoingilia hatampata mtu unless otherwise uchaguzi wa 2010 iwe kama test kwake ya kujipanga vizuri mwaka 2015

    Na kama ndio anapiga picha ili kuanzisha project za kizushi ajue tunamwangalia tuuuu

    ReplyDelete
  19. Mtanzania mwingine anayesaidia ni huyu hapa........

    http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1608

    ReplyDelete
  20. PETER NALITOLELAAugust 28, 2009

    BARUA YA WAZI KWA JOHN MASHAKA...
    HAWEZI KUPATA CHOCHOTE HUYO JOHN MASHAKA ATABAKIA KUTOA MIHADHALA YA KINGEREZA KIGUMU CHA KUKALILI HUMU HUMU KWENYE BULOGU WAKATI MAFISADI YANAPETA. UNADHANI MAFISADI YAKITAKA KUSOMESHA ZERUZERU NA VIWETE SIYATAWAPELEKA MPAKA HUKO ULAYA KWA OBAMA? MICHUZI MWAMBIYE RAFIKI YAKO HIZO PESA AJIDUNDULIZIYE ANUNUE KIWANJA SOMEWHERE ATAZIPOTEZA ZOTE TANZANIA HAIHONGEKI KIRAHISI HIVYO MWAMBIYE KWANZA ASAIDIYE NDUGU ZAKE HUKO AMERICA HATUJAWAONA NYUMBALI MIAKA MINGI LABDA NI NAURI INAWASUMBUA KURUDI KUSAIDIA KWAO. NATOA USHAURI MASHAKA RUDI ULAYA UTAPOTEZA FWEZA NA HATA UDIWANI USIPATE ANIULIZE MIMI NIMEJALIBU NA KULIWA FWEZA YOTE NA BADO HAKUNA NILICHO PATA TENA WEWE MASHAKA HATA KISWAHILI HUJUI WATU WATAFIKIRI NI MJALUO WA KENYA AMA UGANDA HUWEZI HATA KUONGEA KISWAHILI UNATUMIA MISAMIATI YA KIZUNGU KUONGEA NA JAMII HATA HUMU KWA MICHUZI BABA RUDI KWENU AMERICA USIJE KUFANYIWA MCHEZO MBAYA KIPAPAI...HII NI BONGO SIYO AMERICA!!!

    ReplyDelete
  21. All the best john, umeonyesha moyo wa upendo sio kama mafisadi wanaokula mpaka chakula cha mgonjwa. mungu akubariki akupe nguvu uendelee kusaidia na kusaidiwa

    ReplyDelete
  22. WAKAMSOGELEA KISHA WAKAMUULIZA "RABI(MWALIMU)NI SADAKA IPI BASI ILIO KUU KULIKO ZOTE??Ndipo mwana wa Adam akanena"UNAPOTOA SADAKA KWA MKONO WAKO WA KUUME BASI MKONO WAKO WA KUSHOTO USIJUE MKONO WAKO WA KUUME UNAFANYA KITENDO GANI"naam SADAKA iliobora kabisa na iliotukuka na kumpendeza bwana ni ile ITOLEWAYO SIRINI NA BABA YNG ATAIFURAHIA SADAKA HIO. kisha bwana akaendelea na wala MSIWE WENYE KUPAYUKA PAYUKA MBELE ZA WATU WA MATAIFA NA PIA MNAPOSALI MSIPENDE KUSALI SALI NDEEEFU,MNAPOSALI BABA YENU ALIE SIRINI Atazisikia sala zenu na kuzipokea

    ReplyDelete
  23. samahani kaka michuzi sijui ni mimi tu ama hata wewe na wana jamii wengine wamestukia huyu jamaa kakaa kitaperi taperi anaonekana ni uchu tu wa madaraka kama si uchaguzi umekaribia huyu babu angetokea kusaidia kweli? mimi naogopa michuzi namwogopa huyu babu naogopa mpaka misaada yake sijui wee umefanyaje hata kumweka humu namwogopa sana

    ReplyDelete
  24. m.K.a.T.o.L.i.k.iAugust 28, 2009

    Ningependa kusema kwamba ingawa huyu Mashaka anaonekana kufanya mambo mema, JE KUNA ULAZIMA WOWOTE WA KUTUONYESHA PICHA ZA JINSI ANAYOTOA HIYO MISAADA? MIMI NINAJUA WANTANZANIA WENGI TU AMBAO WANAJITOLEA MAMILIONI KUSAIDIA YATIMA NA WAZEE LAKINI HAWATAKI HATA MAJINA YAO YAFAHAMIKE KWAMBA WAMESAIDIA. WATU HAWA WEMA HUFUATA MANENO YA BIBLIA KWAMBA "UTOAPO SADAKA KWA MKONO WA KULIA, BASI HATA MKONO WA KUSHOTO USIJUE".

    SASA KAMA MASHAKA ANA NIA NJEMA YA KUSAIDIA, KWANI NI LAZIMA KUJIONESHA KWENYE BLOG ZA JAMII.

    NDUGU YANGU MICHUZI, NITAELEWA KAMA UTABANIA HII COMMENT, MAANA YAWEZEKANA BWANA MASHAKA AMESHAKUWEKA "SAWA"

    AMANI!

    ReplyDelete
  25. HAPO JOHN NAKUPA 2000000 percent! KWANI UMEONYESHA WEWE NI TOFAUTI NA WATU KAMA DR SHAYO WANAOKWENDA BONGO KUONANA NA RIZIWANI NA KUTUAMBIA KWAMBA BONGO KUNA OPPORTUNITIES KIBAO!!HYPOCRITIC MAN!!ETI BAADA YA MIEZI SITA TUSISHANGAE KUWAONA WAKO BONGO!! TOA DETAILS ZA FOUNDATION YAKO JOHN NIWEZE KUCHANGIA CHOCHOTE!!

    ReplyDelete
  26. Im so interested na accountablity thing! have to look were you got the money to give out! isije ikawa unachangisha watu huko then ukiwa reader unapaswa kuwalipa fadhila......si unajua chips zinaleta mimba kwa watoto wa kike....ngoja vijana wa kazi wanakuanagalia lengo lako....

    ReplyDelete
  27. John Mashaka

    Achana na waosha vyinywa ni kawaida yetu. Endeleza juhudi za kuwasaidia watanzania wenzetu. Japo Material this are only temporary relief lakini ni bora.

    Kaka Michuzi HAPPY BIRTHDAY TO YOU....

    Stay Blessed, Ramadhan Kareem

    ReplyDelete
  28. huu ndio mfano wa kuigwa,sio maneno tuuuuu!!,ONYESHA KWELI UNAJALI kwa vitendo na sio blah blah,kudos mzee.

    ReplyDelete
  29. Tamasha la mauaji ya albino unafanyia dar? wewe vipi bana? maalbino wanauawa huko Shinyanga , mwanza Nk. umewahi kusikia albino kauawa Dar?

    ReplyDelete
  30. HUYU KWELI NI KAKA MASHAKA YULE WA MAREKANI????MBONA KACHOKA SANA HUYU MJOMBA.

    ReplyDelete
  31. POLITICS BWANA, WATU WANAANZA MAPEMA KUTOA MICHELE!!!!

    ReplyDelete
  32. Ikiwa nia hasa ni kusaidia, Hongera sana na Mungu awajaalie zaidi. Walakini ikiwa nia ni kujichotea umaarufu na kuwatumia mafukara kwa manufaa binafsi, Mungu anawaona pia. Kutoa ambako ni lazima kuamabatana na vyombo vya habari kuna tia mashaka!!

    ReplyDelete
  33. Naizimia roho yake hata kama ni kampeni maana wengine wangewekeza kwa wenye roho za kifisadi tu. watu wa Rorya kama huyu atagombea mumpe kura za ndiyo na atawaletea maendeleo ya kweli kwani atamjali kila mtu.
    Achaneni na watu wanaowanunua kwa pombe na vitu visivyo hata na maendeleo kuwaghilibu tu.

    GJK

    ReplyDelete
  34. Mashaka hajasema kwamba anataka ubunge.
    Kwa upande mwingine kama akija kuwa mbunge tunaweza kusema globu ya jamii imemjenga mpaka akawa mbunge.

    ReplyDelete
  35. Anafaha kabisa kwanza sio mvivu wa KILINGLISH kwahilo mikataba atakua akihisoma,Sio kama wengi wa viongozi wetu wavivu wa kinglishi kama MIMI ubaki ubishi wakutetea UJINGA WAO. MASHAKA KWA PRESIDENT

    ReplyDelete
  36. WEWE BWANA MICHUZI NA MASHAKA KAMPENI ZENU TUMEISHA ZISHITUKIA, HUYO MASHAKA KUTOA HIO MISAADA NI STAIL ZA ZAMANI KUPATA UONGOZI KATIKA HIZO SEHEMU COS CAMPENI ZIKIANZA WABUNGE WOTE WANAO GOMBEA HUA WANATOA HIVYO VIJIHONGO ILI WAPATE KURA SO HAPO HAKUNA JIPYA MASHAKA WENZIO WALIISHA FANYA SO INAONYESHA NI JINSI GANI NA WEWE UNAFATA NYAYO ZAO NA HIO NDIO ITAKUA HADI KWENYE UONGOZI WAKO KAMA MISAADA UNAMAANANISHA HAINA HAJA YA KUJITANGAZA UNAMTAFUTA MICHUZI AKUWEKE HUKU WATU WAKUONE HIO SIO MISAADA YA MOYONI ILA NI SHOO OOFUUUU WENYEWE WANASEMA
    NYANGAU WEWE

    ReplyDelete
  37. Duh, MWANAKIJIJI hio babu kubwa. Hizo ‘comments’ zako zinazoirushia ngwala ‘Charlie Rose Show’ jamaa hata hajui ‘what is hitting his business’. Mchezo wako ndio ule ule wa mtu mmoja na majina yako kibao, ati hiyo ndio ‘forum’ ya watu wengi.

    ‘power’ yako ndio hiyo hiyo ya ‘lies and deception’. Ukiwa‘trick’ hao hosts wa hizo ‘shows’ za ughaibu na kuingia hizo news media za ‘television, radio, and movie industry’ za marekani, kumbuka unauwakilisha uhuni wako, umalaya wako, na wewe mwenyewe tu. Tanzania has more than 40 million people.
    =====
    =====
    A conversation with author Jim Collins
    in Business, Books

    Comments
    #
    =====
    A conversation with author Robert Wright
    in Books

    Comments
    #
    .
    .
    .

    ReplyDelete
  38. Mtoa maoni wa 1 (Kilo) naomba uwe unatafakari kwanza kuhusu mada husika kabla ya kutoa maoni.Umefika wakati sasa watanzania tubadilike,tuondokane na fikra za kizamani.Kusaidiana ni jambo MUHIMU SANA katika jamii.Hata wewe usingesaidiwa usingejua hata kufungua blogu hii.Wenzetu hapa Ulaya na hata Amerika walianza zamani kusaidiana katika shida mbalimbali,na moyo huo umeendelea hadi sasa hata wewe unanufaika na misaada Tanzania inayosaidiwa ktk bajeti na kutoka nchi tajiri.Nia aibu sana jamani..tubadilike,hao wasiokuwa na kitu na wenye shida mbalimbali hawakupenda kuwa hivyo,na wewe pia zinaweza kukufika kama wao siku moja(hujafa hujaumbika).John wala sio tajiri,ni mtu mwenye utashi unaostahili anayeona ukweli.Wapo matajiri wengi Tanzania na hasa hapo Dar lkn ukienda kijijini kwao na hata ukionyeshwa ndugu zao hali zao zilivyo unaweza kulia..Ndugu zangu Watanzania tuepukane na mawazo ya kikoloni yenye ushindani usio na maana..Kujalliana na kusaidiana ndio njia pekee ya kujikwamua jamii nzima.
    Mungu zibariki kazi za John Mashaka na wote wenye moyo kama huo,na Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  39. John M. ni mfano wa kuigwa.

    John Mashaka ni maendeleo!

    ReplyDelete
  40. wizi mtupu!

    ReplyDelete
  41. Kwani hauwezi kusaidia bila ya kujitangaza????????????????????????

    Wale wote wanaojitangaza kamwe wana lao jambo!!!!!!!!!! Nyie subirini tu muone!

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  42. TUWAOGOPE SANA WATU WANAOTUMIA UMASKINI WA WATU KUJITENGENEZEA MAJINA!!
    WANATOA VIGUNIA VIWILI VYA MCHELE NA SHILINGI KUMI KUJITANGAZA!!MJUE SHILINGI NGUMI AMIYOITOA NA KUPIGA KELELE TANZANIA NZIMA IKAJUA ITAKUJA KUMZALISHIA MABILIONI.
    TUWE MAKINI NA WATU WANAOTOA KIGUNIA CHA MCHELE KWA MILUZI.
    MICHUZI NA HII BINYA TUNAJUA NAWEWE UMESHAPEWA SHILINGI KUMI.

    ReplyDelete
  43. kazi nzuri bwana mashaka...hongera sana,TX vipi?

    ReplyDelete
  44. achia comments hizo usizibanie banie sio ushuzi huo kama zitanuka vibaya ndio maana mnatokwa na vitambi kumbe tabia zenu za kubaniabania hizo.

    ReplyDelete
  45. TVZ KicartoonAugust 29, 2009

    U.S BLOGGER, Hatutaki malumbano ya hoja tunataka malumbano ya vitendo, JIBU sasa!
    Pchsss!

    ReplyDelete
  46. Hongera ndugu John kwa kazi nzuri unayofanya. Tungekuwa wengi wenye moyo huo, TZ ingekuwa mbali! Jamani hata kama tunadhani motives ni zingine, tupeane support ya kazi nzuri inayofanyika.

    ReplyDelete
  47. Happy birthday to youuuu happy bithday to youuuuuu, happy birthday dear issa michuzi, happy birthday to you...how old r u now? how old r u now.
    - Mdau Virginia Beach

    ReplyDelete
  48. to much publicity sio nzuri sana , unafanya watu tuwe na question why and what the reason behind? mbona kuna watu wengi wanatoa misaada na hakuna matangazo ? oh million moja ,laki tano..... keep it for you and your god.otherwise kama kuna reason behind

    ReplyDelete
  49. Kwenye jimbo la Rorya ni kama hivi, kulia kuna prof. Sarungi na kushoto kuna Mabere marando na katikati ni John mashaka mbona patakuwa hapakaliki lakini mashaka ukishindwa usife moyo jaribu hata upinzani ama special seat za wanawake all the best and good lucky ila punguza mbwembwe na kizungu you might be able to bounce back year 2015

    ReplyDelete
  50. Na kwa kupitia CHADEMA ofcourse kwa vile ndo chama cha vijana kilichobaki! Misupu usitie kijiba huu ujumbe

    ReplyDelete
  51. DA MICHUZI LEO ULICHOKA NINI? NAONA UJACHUJA KABISA,SAFISANA.

    ReplyDelete
  52. Mashaka ahsante sana kwa kusaidia watu nyumbani. Hila utaendelea kutoa vyakula, pesa,etc mpaka lini????? Wabongo umaskini wetu mkubwa ni MAWAZO kama mmoja alivyosema hapo juu. SAIDIA WATU WAWEZE KUEPUKANA NA UMASKINI NA SIO KUWAPA KITU CHA SIKU MOJA, ukiondoka shida zinarudi pale pale!!! Wape mbinu za kuondokana na umaskini ili miaka ijayo wasizidi kuendelea kuwa watu wa kusubiri Mashaka!

    ReplyDelete
  53. JOHN MASHAKA I COMMEND FOR YOUR GREAT WORK MAY YOU BE BLESSED ABUNDANTLY SO YOU CAN BE ABLE TO REACH MANY WHO NEED HELP AND MAY OUR COUNTRY AND PEOPLE BE BLESSED SO WE CAN BE ENCOURAGEMENT AND NOT DISCOURAGING TO THOSE WHO HAVE THE KIND OF COURAGE YOU HAVE. YOU ARE A TRUE GENTLEMAN AND I WISH YOU ALL THE BEST (YOU ARE GOING TO MAKE SOMEONE A VERY LUCKY GIRL SOMEDAY IF YOU HAVE NOT ALREADY)

    ReplyDelete
  54. Nisaidieni jamani, mbona Mrembo anayetoa zawadi simuoni, namuona huyu jamaa tu mwenye kepu? Si ni warembo ndio huwa wanatoa misaada, nisaidieni wachafua vinywa.

    ReplyDelete
  55. Siwaelewi hao waoshwa vinywa wanaoponda kuwa John angewapa miradi badala ya chakula, jamani hamjasoma maelezo, au nyie mkiona tu mada ya John Mashaka mnaanza kuponda, mbona katika maelezo ya picha John kafanya hivo!!!

    Picha ya kwanza
    John yuko na yatima kambeba. Je ni kipi anachohitaji mtoto yatima kama sio UPENDO ili naye ajisikie mapenzi kama watoto wengine? Je anahitaji hiyo miradi za vitendea kazi kazi?
    Picha ya Pili
    John katika wodi ya watoto. Ni kipi zaidi wanachohitaji watoto na wazazi wao wakiwa hospitali kama sio upendo na malipo ya gharama za hospitali?

    Picha ya Tatu
    John akigawa chakula kwa wazee. Jamani wazee kama bibi unayemuona katika picha, kweli wanahitaji mtaji au mradi au ufundi? Mzee kama huyo anahiyaji nini zaidi ya chakula na malazi na kuoneshwa kwamba unamjali?

    Picha ya Mwisho kabisa
    BAADHI YA VIJANA WA RORYA WALIOPOKEA MTAJI, NARUDIA TENA MTAJIIIII!!! NA BAISKELI KWA AJILI KUJIENDELEZA KUTOKA KWA JOHN MASHAKA.

    Jamani acheni hizo!! Give the credit where it's due, sio kila wakati kutoa kasoro tu. Wewe unayetoa kasoro na John Mashaka hivi ni nani amefanya la maana kusaidia WaTZ,bila kuangalia kwa kiasi gani?? Kwa hili namuunga mkono John na Mungu ambariki, ingawa sio wakati wote huwa nakubaliana naye

    ReplyDelete
  56. ACHENI CHUKI,
    HUYU JAMAA KAONYESHA MFANO WA KUIGWA.
    MSIFUNI KWA ANACHOKIFANYA SWALA LA UBUNGE HALIJATAJWA.
    ETI AKASAIDIE WABEBA BOX WENZAKE!!HII INAKUJAJE? MALIMBUKENI WAKUBWA.
    JE NYINYI HAMTAKI KUWA WABUNGE? KAONGENI BASI NA NYINYI.

    HONGERA SANA JMASHAKA,
    ENDELEA NA MOYO HUO.
    KAMA UNANIA YA KUWA MBUNGE BASI USIISHIE TU KWENYE UBUNGE MPAKA URAIS.
    UMESHAONYESHA MFANO .ENDELEA NA MOYO HUOHUO KWANI UTAKUWA NI KIONGOZI UNAEJALI WATU WAKO NA SIO HAO MAFISADI.
    NIPE DETAILS ZA FOUNDATION YAKO TUWASAIDIE WAHITAJI.

    alexiano2000@yahoo.com

    ReplyDelete
  57. MTANZANIA NDIO KIUMBE CHA AJABU DUNIANI SIJAWAHI KUONA.HUYU ANAYESAIDIA WATU ANALALAMIKIWA KWAMBA ANATAKA UBUNGE NDIO MAANA ANAFANYA HIVYO,WALE AMBAO WANATAKA UBUNGE WANAPEWA BILA WASI WASI NA BILA KUTOA MISAADA KWENYE MAJIMBO YAO.JAMAA HUYO HIO FOUNDATION HELA NI ZA MICHANGO AMEKUSANYA NA AMEFANYA WEMA KUWAFIKIA WALENGWA,ACHENI WIVU WAAJABU MKAANZA KUMTAFUTA MCHAWI NANI BILA SABABU.WEWE KAMA HUNA SHIDA BASI UJUE KUNA MTU MWENYE SHIDA.WEWE KAMA UNATOA MISAADA KWA SIRI NI VIZURI LAKINI YEYE PIA KAFANYA VIZURI KUWEKA WAZI KWANI INASAIDIA WATU WENGINE KUPATA MOYO.ndugu zangu watanzania sio kila sehemu lazima tuoneshe au tuhakikishe kwamba sisi ni vichwa vya wendawazimu.swala dogo sana hili halina haja ya kuwa na roho za korosho bado vijana sisi na tukiwa na wivu wa ajabu ajabu hatutafika popote.
    mdau msema kweli.

    ReplyDelete
  58. Dr shayo unaona mwenzio anavyojipanga? Kumbuka kule jimboni kwako kuna Kimaro, agustino Lyatonga Mrema, Kuna Felex Mosha, Kuna Minja na wote hawa watambana na wewe.

    Nilikuwa jimboni hivi majuzi nikagundua kuwa na wewe umetembelea mashule na kugawa vitabu na misaada mbali mbali. Hii ilikuwa ni mwezi wa tano mwaka huu je picha ziko wapi au wewe unastail yako ya kipekeee?

    Wewe mashaka na shayo, kumbukeni ubunge siyo lelemama. Takrima hizo hazisaidii.

    Kazi kwenye, ila ningekuwa mimi ndiyo nyie siasa sintaingia kabisa, ni uwanja mchafu sana

    ReplyDelete
  59. kweli wabongo nuksi!! hamuachiiii hiyo yooote ni jelaz

    ReplyDelete
  60. mwacheni mbona watoa misaada wengine wana jitangaza ...wanatoa gunia la mchele kwa watoto yatima wanabandika picha humu ..endelea na kazi mzuri kaka usijali na wapinga maendeleo

    ReplyDelete
  61. mambo ya kutend wema n kungoja shukurani hayo

    ReplyDelete
  62. sasa mzee john mashaka kilichobaki ni kutafuta my wife wako..yule hakufai anapenda kuuza sura tu

    ReplyDelete
  63. wabongo tumezidi wivu, mtu akitoa misaada watu wanaona nongwa, tabia mbovu hiyo. hongera sana brother kwa kuwasaidia hao watu, endelea na moyo huo wala usife moyo, hao wote wanaokupinga mbona hatuwaoni wakitoa misaada? ops samahani hawana makaratasi ya kurudi bingo, wanakalia kubeba mabox na kulea wazee mahospitarini huku....tunajua story zote.

    ReplyDelete
  64. HIVI WABONGO TUMEROGWA???TUMEZOEA MAJUTO???MTU AKIWA MWAEUPEE MPE NCHI HANDSOME,AKIANDIKA ARTICLES VIZURI,MPE NCHI AWE RAHISI?KIDOGO TUU HE IS THE NEXT PRESIDENT.HIVI NIKIWAULIZA WHAT IS SOO SPECIAL WITH HUYO JOHN MASHAKA HADI MNAMPA UNABII WA KUWA RAHISI,MBONA SHAKESPEAR KABAKI NA SIFA ZAKE ZA UANDISHI TU,SHAABAN ROBERT NA WENGINE.UONGOZI AU IKULU HAUPIMWI KWA KUANDIKA MAKALA JAMANI.WATANZANIA LETS TRY TO THINK OUT OF THE BOX.DUH I HATE BEING IN THIS GENERATION,NAJUA NITAWAKERA WENGI ILA WENYE AKILI WATANIELEWA.WATANABAHU

    ReplyDelete
  65. mh wabongo balaa tupu lol!

    mtu akitoa kitu mnasema anataka ubunge akila peke yake ana roho mbaya lol acheni hizo, kama mtu hana uwezo wa kutoa sio kusema mbovu sio fresh jamani.

    big up sana John Mashaka umeonyesha njia kaka vijana lazima tujue kusaidiana.

    ReplyDelete
  66. We need his credit history and tax return for the past three years 2006-2008 to make sure he does not provide happiness from illegal means.Anyway is everything is okay then Godbless him and increase his rate of return by 200%.
    Kalumanzila

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...