mojawapo ya mabasi ya kwenda mikoani likiondoka stendi ya ubungo milango ya saa nne hivi baada ya mgomo kumalizika
basi likisubiri kubembea kuelekea tanga

hali imerejea kama kawaida stendi ya ubungo

MADEREVA WA MABASI WALIOKUWA WAMELETA MGOMO WA KUSAFIRISHA ABIRIA KWA SIKU YA LEO STENDI KUU YA MABASI UBUNGO HATIMAE WAMEMALIZA MGOMO WAO HUO NA KUENDELEA NA SAFARI ZA KWENDA MIKOANI KAMA KAWAIDA.


UAMUZI HUO WA KUMALIZIKA KWA MGOMO HUO UMEKUJA MARA BAADA MAZUNGUMZO NA MAKUBALIANO YALIYOFANYIKA BAINA YA KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR AFANDE SULEIMAN KOVA NA SUMATRA WALIPOKUTANA NA UONGOZI WA MADEREVA WA MABASI HAYO STENDI KUU YA MABASI UBUNGO.

HIVI SASA MABASI YOOTE YAMEANZA KUTOKA STENDI HAPO NA KUENDELEA NA SAFARI ZAO ZA KWENDA MIKOANI NA NCHI JIRANI KAMA KAWAIDA.
MADAI YAO MAKUU NI KWAMBA ASKARI WA USALAMA BARABANI KATIKA NJIA KUU WAMEKUWA NA TABIA YA KUWANYANYASA KWA KUWAPIGA BAO NA TOCHI ZAO ZA KUGUNDUA MWENDO WA KASI, WAKIDAI JAMAA WAMEKUWA WANANUKA RUSHWA KWENYE KAZI HIYO NA HAKUNA DALILI ZA KUKOMA.
MADAI YAO MENGINE NI KULALAMA JUU YA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA DEREVA MWENZI WAO, WAKIDAI KWAMBA ENDAPO WAHUSIKA WA KILA UPANDE WANGEKUWA MAKINI MATATIZO KAMA HAYO YASINGETOKEA.
VIONGOZI HAO WANAKUTANA LEO SAA KUMI JIONI KUUNDA KAMATI ITAYOKUTANA NA UPANDE WA SERIKALI JUMATATU ILI KUJADILI NJIA MUAFAKA WA KUTATUA MATATIZO YAO NA YA USALAMA BARABARANI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. yatimanimwanao.blogspot.comAugust 14, 2009

    mi naona wazidi kugoma tu, make serikali imezidi na rushwa kwani wakati ajali inatokea dereva alikataaga kuendesha gari baada ya kuona gari halina usalama, lakini akatokea dereva mwenye kiherehere akaliendesha ndo akaua hao watu na yeye mwenyewe. sasa wamemuhukumu huyu bila hatia kwani yeye alishaona noma akakataa kuendesha gari.

    ndivyo magazeti yalivyosema sasa mwenzetu alikamatwa kuisaidia pilisi leo wanamhumu miaka 30 jamani haki ziko wapi??

    jamani tanzania na rushwa tunakwisha maskini.

    wagome mpaka adhabu hiyo ifutwe kwani mwenzao hana hatia.

    ReplyDelete
  2. Miaka 30 haitoshi kwa wauaji hawa. Wanyongwe. Wanaovateki kwenye vilima. Wanaovateki kwenye daraja. Wanaendesha kwa mwendo kasi. Wanafanya mambo ya ajabu sana barabarani halafu wanasema ajali ni bahati mbaya.

    Serikali tafadhali usibadilishe msimamo wako. Maisha ya watu yana thamani.

    ReplyDelete
  3. Madereva wengi wa safari za mikoani wanaendesha magari katika hali inayoatarisha usalama kwa kiasi kikubwa sana. Hivyo inabidi wadhibitiwe sana la sivyo ajali zitazidi kuongezeka.

    Trafiki nao wanapenda sana rushwa hivyo nao wanachangia ajali. Hawa wakishachukuwa pesa kwa dereva basi wanaruhusu gari liendelee na safari ingawa lina makosa. Hivyo mwisho wake inakuwa ni ajali tu mbele ya safari.

    Kama hawa madereva wanagoma kwa sababu ya maamuzi ya mahamaka basi inaelekea wana tatizo la kuelewa sheria. Inaonekana wanatumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja. Hii ina maana gani? Kama mtu hakubalini na uamuzi wa mahakama anatakiwa akate rufaa mahakama ya juu zaidi na sio kugoma. Waacha kufanya mambo kienyeji.

    Serikali isikubali kuendeshwa na hao wadereva na wenye basi. Hatua kali lazima zichukuliwe kulinda usalama wa wasafiri barabarani.

    Rais JK alisema hivi karibu vile vile kwamba serikali itachukua hatua kali kupanda na uongezeko la ajali za barabarani.

    Ajali zimezidi jamani. Wakati mwingine mtu akifikiria kusafiri inakuwa kama vile walivyokuwa wanafanya wanasayansi wa America wakati walipokuwa wanataka kwenda mwezini kwani hawakuwa na uhakika kama wengefika na kurudi salama kwani probability ilikuwa 1/3 tu.

    Tofauti na wanaanga wale waliokuwa wanakwenda anga za mbali, mabasi yanapita barabarani hivyo yasiwe na ajali za kutisha

    ReplyDelete
  4. Baada ya kuchelewa kuondoka DSM mabasi yanayokwenda mbali yasingeruhusiwa kuondoka hadi kesho maana huko barabarani itakuwa ni msemo wa "kichaa kapewa rungu" tunaweza kusikia ajali nyingine za kutisha.

    ReplyDelete
  5. basi inamaana hao walioko safari wakipata ajli labda tairi imechomoka,sterling imegoma auchochote wajue ni miaka 30.na hapo ukumbuke kwamba jela mwaka1au2,3 sio kitu kidogo.na anae ku anapenda watu wafungwe miaka yote hiyo hajawahi kukaa hata loocap ajaribu aone inauma kiasi gani,na walio wengi bongo au hatakokote hawajawahi kuendesha ndio maana wanaropoka afungwe miaka yote hiyo,sio kuweni na huruma.

    ReplyDelete
  6. Hapo kazi ipo kwa sisi walalahoi tunaotumia huo usafiri kila mara.

    Eti tukiwa ubungo trafic anakagua gari akiwa nje eti anamwambia dereva kata kushoto, kulia, njoo mbele anza kuondoka, hivi ndo kakagua nini? huwa naangalia sipati jibu. Hata kabla yakufika Kimara gari linabuma.

    Na madereva wengi ni kama vichaa, wachafu + lugha zao chafu na makonda wao na wale wanaotusumbua milangoni, na hawaheshim kazi yao. Hawana ustarabu kabisa, ukiona umefika uendako basi unamtaja mungu.

    ReplyDelete
  7. Nitakacho kujua mimi ni nini wamekubaliana juu ya dereva mwenzao waliokuwa wakimlilia aliefungwa miaka thalathini. jee wamekubali kuwa anastahiki kifungo alichopewa au wameahidiwa atafunguliwa?

    ReplyDelete
  8. Anon 05:10 hakuna anaependa mtu asie na makosa aende jela. Kama tairi limechomoka bahati mbaya uchunguzi utaonyesha tu. Lakini ukweli ni kuwa madereva wasio faa wanatakiwa kujirekebisha na trafik wanatakiwa wakomeshwe kwenye swala la rushwa ili kukomesha ajali. Sijui wewe labda ni mmoja wa hao madereva kama unaendesha vizuri na kwa usalama basi ni vema. Lakini hizo njia za bara kuna madereva wanaendesha vibaya sana kiasi kinacho hatarisha sana maisha ya watu. Ni kweli kuna madereva wazuri na wengine hufanya hata watu wachague kupanda mabasi wanayoendesha. Lakini wasio faa ni muhimu kuchukuliwa hatua swala la huruma kwenye makosa na uhai wa watu halina msingi. Kama mtu hataki kukaa jela basi aendeshe kwa usalama. Wewe je huoni huruma watu wanakufa na kuacha watoto wadogo hata hawana msingi, watoto hao wanateseka kwa makosa ambayo yangepukika.

    ReplyDelete
  9. Thank God hadi muda huu nakwenda mitamboni hakuna ajali iliyoripotiwa kutokea kwani ile fungulia mbwa pale ubungo mida ile ya saa nne nne duh ilikua balaa! Maana jamaa yangu m1 kanipigia simu anasema kuna basi moja maarufu kama OBAMA lilitinga Mbeya mida ya saa 12 jioni!

    ReplyDelete
  10. Nji hii kushney kabisa!!!!! sheria zipo kwa ajili ya watu fulani wengine hapana. Hii ajali imetokea hivi karibuni ndani ya mwezi mmoja mtu ameshahukumiwa miaka 30! Ni sawa kama sheria zingekuwa hazibagui. Mzee wa vijisenti yukAndrew Chenge ameua watu wawili tena kwa ulevi yuko nje anadunda na ati jalada limepelekwa kwa DPP. Uozo mtupu hii nji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...