Kibajaji ikiwa kichwa chini miguu juu
Habari wana jamii,
Kuna ajali imetokea leo maeneo ya makumbusho Millenium tower muda wasaa saba na nusu hivi baada ya kibajaji hicho kugongwa na dala dala yamwenge posta na kukimbia, Kibajaji hiki kilijaribu kukimbia bara baraya pili bila mafanikio na kujikuta kikidumbukia moja kwa moja.Hakuna aliyedhurika

Mdau Francis, M.
KIT & Communication Consultant
Also Master of Ceremony (MC)
P. O. Box 106055
Cell : +255 713 55 40 55 :
+255 786 55 40 55
Dereva wa Kibajaji wa pili akihojiwa na Polisi wa usalama bara barani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bajaj ni brand kama zilivyo Honda, Toyota, Kilimanjaro etc. Ni kosa kuviita hivi vyombo kibajaj, tunawapa wahindi wa Bajaj free advertising.

    Jina sahihi ni "Tuk Tuk", hebu imagine miongoni mwa Tuk Tuk ikiwemo aina ya Piagio utaiita bado ni kibajaj?

    Tuk Tuk imepata ajali, achana na kibajaj.

    ReplyDelete
  2. Michuzi kupitia globu hii ya jamii ningeomba kuwafikishia taarifa wanausalama watusaidie kuhakikisha bajaji zote zinawekewa mikanda kama ilivyokwenye taksi

    ReplyDelete
  3. NINAOMBA UFAFANUZI, HIKI KILIGONGWA AU KILITUMBUKIA KWENYE MTARO? MWANDISHI KWANZA ANASEMA KILIGONGWA NA DALADALA LAKINI HUYOHUYO ANASEMA TENA KUWA KILIKUWA KIKIENDA UPANDE WA PILI WA BARABARA KIKAJIKUTA KIKITUMBUKIA MTARONI, HATA HIVYO KWA WAANDISHI WA TANZANIA HII NI KAWAIDA.

    ReplyDelete
  4. Wanausalama mna kazi ya ziada kuhusu waendesha vibajaji hawafuati taratibu za usalama barabarani wana overtake wanavyojisikia wao unaweza ukakuta wanaovertake upande wa kushoto kitu ambacho sio sawa vilevile wanapenda sana kuchomekea kila siku nina ona haya. Kwanza nina wasiwasi hata kama madereva wake wana leseni au anajifunza jinsi ya kuendesha bajaji na kuingia barabarani. Wanausalama barabarani tunaomba waangalie jinsi ya kutatua jambo hili

    ReplyDelete
  5. bajaj za india zina ngao, mziki mkubwa. enyi vibajaj mtaweka lini angalau mziki tukikaa humo nasie tujisikie tumo tumo na uendeshaji wenu wa kuuaua?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...