Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Waaaaaaaaaaaaapi, Baba kupaaa kunahitaji mabawa!

    ReplyDelete
  2. yaani leo naona wanaipiga vita TCRA, TCAA na TMA, last week ilikuwa TRA na TPDC. Kama karafuu tu ambayo haiko chini ya muungano imewashinda hayo mafuta si yatamilikiwa na familia moja tu?

    ReplyDelete
  3. Mara nyingi anayechekwa ndiye mwenye kupata mafanikio. Muhimu ni kuwa kinachosababisha kuchekwa akiwekee imani ya kuwa ni haki na anaouwezo wa kukitekeleza.
    Ndugu mwandishi nyimbo hii nafikiri sio kama zile tulizozizoweya SIKU HIZI ambazo mara nyingi hukosa vina na sifa ya kuwa nyimbo bora. Kwa mtazamo wangu naamini nyimbo hii imejaa vina na maudhui yake ni MAZURI SANA. Ninaweza kusema kuwa nyimbo hii inafana sana nyimbo zile za zamani zilizokuwa zikiimbwa na bendi kama VIJANA JAZZ na kadhalika. Namuomba mungu anipe maisha marefu yenye amani ili nione ndege huyu anavyopaa. Naamini atapaa. Naamini huyu sio ndege wakawaida na kupaa kwake anaweza kuwashinda ndege wakubwa kama vile MWEWE. JAMBO LA MSINGI asiwekwe tunduni bali arejeshwe porini kwani ndiko kwenye asili yake na huko aonyeshe uwezo wake wa kupaa. Ninayo imani kubwa juu ya ndege huyu. Nahisi anaweza kuisaidia dunia katika kufikisha mwasiliano sehemu ambapo hayafiki, kwani anauwezo mkubwa wa kupaa juu.
    MUACHIENI APAE, MSIMFUNGE KAMBA.
    NITUMIE, MANENO MAZURI YA MHESHIMIWA KIONGOZI WETU WA PILI kutoka juu KWA WADHIFA,hapa TANZANIA "HEBU JARIBUNI MUONE"

    MDAU, CHINA

    ReplyDelete
  4. Watu wanaofikiri Zanzibar ikijitenga itapata matatizo, visiwa vingapi vidogo duniani zaidi ya Zanzibar na watu wake kidogo vinajiendesha wenyewe bila ya kuungana na nchi yoyote, kwanini Tanganyika mnag'an'gania muugano? si muwawache si wakipata tabu na matatizo si ndio watapata fundisho. wapeni uhuru wao watu wacheni kulazimishana katika miasha, mtoto akilila wembe mpe, mnajua kama Zanzibar itaendelea ndio maana roho zenu mbovu hamtaki wajitenge.

    ReplyDelete
  5. Yes U can fulai, fulai to the DITCH!

    ReplyDelete
  6. NautiakasiAugust 03, 2009

    Naam naungana na anon aug 03,01:01pm (china)

    Hata mimi nna imani kubwa tu, kwamba huyu ndege ataruka, muhimu nikurejeshewa uhuru wake wa asili,
    kwani raha ya ndege kichaka si tunduni asilani. Mtoeni tunduni, mfungueni kamba ya mguu mwacheni muone..! Wadhaniao kuruka ni kuwa mbawa na manyoya mengi wamekosea, wapo wenye mbawa na hawaruki, kama ingekuwa manyoya na mbawa angeruka kuku mwenye manyoya mengi, lakini shani ya mungu anaruka "penguin" mwenye vipapatio tu!

    ReplyDelete
  7. What is the message KP is trying to deliver here? Does ZNZ's existence depend on the policies drawn in Dodoma? Or is it some fish up a tree? Both ways are disrespectful of a nation (semi-nation, region, or any other name) which has sacrificed so much for the purpose of the union. I would rather see a cartoon of top politicians seeking advice from the unifiers of Germany on how to sort out sensitive issues. Having said that, I must concur with the contributor above who is worried about ZNZ resources being dominated by a single or couple of families. Hang on a minute, but isn't that what is also happening on the mainland? The difference being that on the mainland, due to the geographical spread and population size, the behaviour is more widely spread and hence less visible.

    ReplyDelete
  8. Bwana Masoud, nafikiri hii picha ungeichora kama huyu ndege amfungwa mabawa yake na ndiyo maana hawezi kuruka.

    Siyo lazima nchi iwe na madini au manufacturing Industry ( viwanda) ndiyo iweze kujiendesha. Nchi ndogo kama Zanzibar kiuchumi ni rahisi sana kuanzisha kitu kinachoitwa "Service Industry" na ikafanikiwa.

    Pili kama Muungano ulikuwa wa hiari , kwa nini muwalazimishe ??

    ReplyDelete
  9. Kabla ya kujitenga inabidi ukumbuke historia.

    Mipaka imewekwa tu na watu tena wasijuwa historia ya Afrika.


    Wazanzibari ni Wanganyika kidamu tena ni asili ya makabili ya Kinyamwezi n.k alafu changanya na Wageni (wakoloni)sasa mtoto ni wa nani?
    Mtoto ajitengi na wazazi bwana :)
    Anayeng`ang`ania kujitenga mchawi tena afai kwa manufaa ya Tanzania hii ya sasa.

    Watu wanataka kuizuru nchi yetu na kwa kutumia majungu ndiyo wanadhani watafanikiwa:(

    MUUNGANO UDUMU MILELE NA MDA SI MREFU TUNAHITAJI MUUNGANO WA AFRIKA yaani USA mpya United States of Africa :)

    Mungu ibariki Zanzibar Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  10. MUUNGANO UDUMU NA UDUGU WETU UENDELEE DAIMAAA LAKINI MIMI NAAMINI KITU KIMOJA KAMAHUYU NDEGE MWILINI KWAKE ANAYOMAFUTA MENGI NACHANZO KIKUBWA CHA ENERGY NI MAFUTA BASI HUENDA AKARUKA JAPO KIBUBUTU(HANA MABAWA MENGI)

    ReplyDelete
  11. Akitoka kifungoni, naamini mabawa yataota na kuruka ataruka! Tena mtakuja kushangaa ndege mdogo kawezaje kuruka mito na milima mikubwa. Just let him get out of the cage!

    ReplyDelete
  12. Kumradhi, samahanini lakini naongea kweli. Hawa wazaliwa wenyewe wa visiwani wengi wao wapo mdebwedo bado wanataka watengane na bara je hiyo Zanzibar si watanyang'anywa na Waarabu???? Elimu yenyewe wengi wa wavisiwani hawajasoma, wengi hawapendi kusoma, Kulalaaa kulala na wao na kuuza maduka ya vyakula. Hebu waondoe Miujinga ya kutaka kuvunja muungano watakufaa.

    Na endapo wakivunja muungano Wapemba wote hatutaki kuwaona huku bara warudi kwao wakale shida za huko kwao Pemba vitu viwadodee madukani wakaone joto.

    ReplyDelete
  13. Hawa wanalilia uwembe utawakata vibaya ile mbaya. Wao wawasikilize hao viongozi wao wenye uchu wa madaraka then waje waone joto.

    Hiyo sera ya kuvunjika kwa muungano ni Uchu wa madaraka wa baadhi ya viongozi. Sioni kiongozi yeyote anayefaa hapo.

    Ulishaonaga wapi kiongozi yupo yupo tuu akiongea mate mdomoni yanamtokatoka pembeni ya mdomo yani hajielewi then umchague ndio aje awe kiongozi???? Loooh.

    Kwa fedha gani alizo nazo hadi asiibe, Uwezo gani hasaaa??? Yeye mwenyewe hana uwezo anahitaji madaraka ili aweze fanikiwa kimaisha ndio awafikirie wananchi??? Yani Watu mnadanganyikaaaa kinoma kama mambumbumbu.

    Kiongozi kama kiongozi anatakiwa angalao awe pesa zishamzoea ndio hatakuwa na tamaa za ovyo ovyo.

    Angalia vaa ya viongozi wanaogombea kwanza ndio ucheke...T he t he t he mimi sisemi naishia hapa nisije lipuliwa bomu.

    ReplyDelete
  14. Jamani kwani Zenji kuna mafuta?

    ReplyDelete
  15. Hii itakuwa ni uchochezi tuu wa baadhi ya watu wasiokuwa na akili. Eti kuvunja muungano. Waarabu wanataka kupata mafuta watawajia kwa ujanja waibiwa hadi wakome.

    Ikiwa kama nchi na Amerika ziliweza kuungana kwanini Afrika isiungane?? Ni kwanini tukubali wachochezi wasiopenda maendeleo yetu??? Ni kwanini kukubali nchi zilizo ungana zivunje muungano wake wakati ndo chanzo cha kuungana na kupelekea Afrika nzima.

    Kwakweli mimi sipendi, tutamani siku moja Afrika ije iwe United state of Afrika. Tusikubali wachache wenye tamaa za kupata madaraka. Hao ni wale waliliao madaraka wahisi mtu ukiwa madarakani unafaidi saaana.

    ReplyDelete
  16. naona wenzetu wa Tz bara wamesahau zanzibar ilitoka wapi, hebu na tuangalie znz ya 1963 iliyokua na kiti cha umoja wa mataifa, sambamba na hilo iliweza kujiendesha kiuchumi. sasa hichi kiherehere cha kuona zanzibar haiwezi kuishi bila ya muungano kimeanzia wapi? pilipili usoila inakuashia nini? kama zanzibar ni ya wazanzibar ikijiweza kiuchumi na kisiasa ama isijiweze nyie msio wazanzibar mnakerwa na nini...

    ReplyDelete
  17. Wee Anon uliyesema Mtoto akililia wembe mpe, ujue kuna msemo mwingine usemao Umoja ni Nguvu na utengano ni Dhaifu.

    Ukiangalia watanganyika na Unguja ni watu wamoja, baadaye utasikia kisiwa cha Mafia nacho kinataka kujitenga oooh hoooo Pemba nayo itasema nasi twataka kujitenga yakheee vipi tena.

    Mi nafikiri watu wanang'ang'ania madaraka, na ambao hawajapa wanapiga mahesabu tukijitenga tu, unajua mimi naweza nikawa raisi, wewe utakuwa balozi

    ni hayo tu

    P.E.D

    ReplyDelete
  18. Zanzibar does not need the Union.

    As a matter of fact the Union has brought nothing but trouble for Zanzibaris.

    Zanzibar does not need crazy taxes. All major corruption scandals have happened in Tanganyika and money stolen at BOT also belongs to Zanzibaris.

    It is better for Zanzibar to claim autonomy because Tanganyikans swallow it and turn it into a region.

    Pinda ameshaanza campaign za kumeza Zanzibar, wazenji musikubali.

    Nchi ya watu 1 million mutaweza tu kuijenga hasa ukizingatia nyinyi ni wachapa kazi na muna wasomi wazuri.

    Mukijitenga mutaendelea sana.

    All u need with Tanganyika ni ushirikiaono kama ushirikiano kati ya nchi na nchi lakini Muungano hauna faida nanyi.

    Kwanza waluoomba Muungano sio wazenji.

    ReplyDelete
  19. mimi ni shabiki mkubwa wa katuni za kp na nimenufaika nazo katika kuona mwenendo wa mambo ya bongo, lakini ninafikiri katika katuni hii kp hakufanya utafiti wa kutosha. badala yake amafuata mkumbo wa wakereketwa ambao ni wa kijazba zaidi kuliko mantiki na busara. muundo wa muungano unahitaji mageuzi makubwa ili uweze kuwa na tija vinginevyo ung'ang'anizi wa nambari wani utakuja kusababisha rabsha. kama mkuu wa nambari 1 angekuwa anaona mbali angetumia nafasi hii kuandika sura (chapter)yake ya pekee katika historia ya bongo. kwa bahati mbaya haoni!!!!

    ReplyDelete
  20. HAKUNA CHA MAANA HAPA INAPANDIKIZWA CHUKI TU,KWA MAISHA YANANAVYO KWENDA NAONA BORA MUUNGANO UFE KABISA HAUNA MAANA HAUNA CHOCHOTE,HATA WATU WA PANDE MBILI ZANZIBAR NA BARA WAKIPIGA KURA 95% HAWAUTAKI NI BORA TUKAUVUNJA WANASIASA HASA CCM SIONI KWA NINI WANAUNG'ANG'ANIA

    ReplyDelete
  21. mdau uliyesema wazanzibari wote ni mdebwedo kazi yao kulala tunaomba ututake radhi kwanza. Pili kukaa na kuuza maduka ndio maendeleo yenyewe yanakoanzia na kama hujui huko bara basi asilimia kubwa ya hayo maduka basi ni ya wanzanzibari, kama si kuuza na nyinyi mkanunua mngeishi vipi. Tumia kigezo chengine katika mada hii na sio hoja hiyo.

    ReplyDelete
  22. Nilikuwa sijui kuwa tanganyika inailea zenji mbawa zake zikuwe iruke yenyewe.

    tg yenyewe haina mbawa.
    lni mbawa za zj zitakuwa?

    ReplyDelete
  23. Nami ni mmoja wa washabiki wakubwa wa katuni za Masoud Kipanya lakini katika hili amekosea.

    Muono kama huu anaojenga katika picha hii ni moja ya sababu kubwa inayowafanya wazanzibari kujenga dhana ya kudharauliwa,kudharauliwa na kuwafanya kujenga siasa kali za Uzanzibari miongoni mwao ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa cha maelewano na kuaminiana kati yao na wenzao wa Tanganyika.

    Alichokifanya Masoud hapa ni kuwapa silaha wale maadui wa kweli wa muungano miongoni mwa wazanzibari. Na haswa wakati kama huu ambao tayari tumeshaona siasa hovyohovyo(irresponsible politics), kilaghai(manipulative) na za kiujanjaujana (unreliable) zikishika mwendo kasi katika kisiwa cha unguja kwa minajili ya kura za uchaguzi ujao.

    Naamini Kipanya ni muungwana na anaweza kumuiga Pinda kuomba radhi kwa kupotoka ama kupotoshwa.

    omarilyas

    ReplyDelete
  24. KP nimelazwa KCMC kwa hiyo picha!! I believe I can touch the sky!!! haaahha let him go please hahhaah He may fly who knows

    ReplyDelete
  25. Mafuta yenyewe hayajapatikana watu wameishaanza kutoleana maneno ya vitisho,na ya kipatikana je?isitakuwa balaa nyingine na kubwa.kama Darfur,South Sudan nk.ukiangalia na ukienda kwenye ukweli ninachoshangaa hapa Zanzibar kwa mfano wakazi wengi hawana ajira,umasikini upo katika kiwango cha juu na cha kutisha,hawajishughulishi kabisa.hapa suala la elimu lipo chini kabisa ndiyo maana mahotel mengi yamejengwa lakini wafanyakazi asilimia kubwa ni wageni toka bara na Kenya.Zanzibar wenyewe wamelala maana elimu hawana watafanya kazi zipi???wavivu sana hapa tena sana.

    ReplyDelete
  26. Ningependa kutanguliza shukrani zangu za dhati kwako mchoraji KP.

    Nafurahi mno ninapoona jitihada zako za kuwaamsha wazanzibari kupitia katuni zako hasa wakati huu ambao kero za muungano zimekuwa zikiumisha vichwa watu wa pande hizi mbili za ZANZIBAR NA Tanganyika.

    Ndugu mchoraji KP,Wazanzibari wengi bado hawajapata bahati ya kufahamu mafunzo adhimu unayowapa kuhusu muungano kupitia michoro yako.wengi wao wamekuwa wakiifahamu vibaya michoro hiyo wakidhani kuwa unaidogosha na kuidharau ZANZIBAR.
    iwapo Wazanzibari hawa wakipata fursa ya kufahamu maudhui unayowapelekea kuhusiana na hatma ya taifa lao la ZANZIBAR basi naamini watabadilisha msimamo wao dhidi yako na badala yake wataanza kukupa heshima na hadhi unayostahili mbele yao ambayo si nyengine zaidi ya kuwa wewe ni SHUJAA WA ZANZIBAR.
    Ninaamini kuwa kwa kulinda maslahi yako ya kikazi na usalama wa maisha yako huna uwezo wa kuwafahamisha wazanzibari kwa uwazi zaidi kuliko ulivyokwishafanya.
    Katika hali hiyo,ndugu yangu KP naomba kutumia fursa hii kuwafahamisha wazanzibari maana halisi iliyoikusudia hapa juu.

    ENYI WA ZANZIBARI,
    KP katuchorea ndege ambaye kamwita jina la Zanzibar.ndege huyu anaonekana bado ana afya nzuri tu.kitu kikubwa kinachomtaabisha ndege huyu hata akawa amejawa na wasiwasi na kutapatapa ni kuwa huu mti alioukalia,mti ambao unaoonekana kuwa hauna rutba hata kidogo na dakika yeyote mti huu unaweza kuanguka chini.KP anazidi kutuonyesha ushujaa wa huyu ndege maana licha ya udogo aliokuwa nao anajitutumua kukimbia hatari ya kuja kuangua na huu mti mbovu.jambo ambalo linaweza kupelekea kupoteza uhai wake.

    Wazanzibari naamini mmeanza kupata picha KP aliyoikusudia.

    NDEGE: KP anaashiria ni taifa la ZANZIBAR
    MTI MBOVU USIO NA JANI HATA MOJA:KP anaaishiria uchakavu wa muungano tuliokuwa nao hivi sasa muungano ambao hauna rutba na hata kama huyu ndege hajauvunja basi utavunjika wenyewe maana hauna tena dalili za uhai.anamaanisha muungano uliokwisha filisika na kukosa muelekeo.
    KUTETEMEKA KWA NDEGE: KP anaashiria hali halisi ya ZANZIBAR katika muungano huo kuwa ni hali iliyojawa na wasiwasi na hofu.KP hapa anazidi kuashiria kuwa hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa na ZANZIBAR ili kujinusuru na kifo.anaashiria kuwa Zanzibar ni lazima ijitowe kwenye muungano ili kulinda heshima na ustawi wake.

    MTI KUGAWIKA MAPANDE MATATU:KP anaashiria mambo mawili hapa

    KWANZA: KP anataka kuwepo na serikali tatu.serikali ya ZANZIBAR,TANGANYIKA NA SERIKALI YA MUUNGANO.hii ndio suluhisho pekee analoliona litakaloweza kuleta hali ya kuelewana baina ya pande mbili hizi za muungano.

    PILI: KP anatuambia kuwa tanganyika na muungano wanaoushikilia kuwa umefilisika.maana hivi sasa kilichopo hapa tanganyika ni matawi matatu tu ambayo ni UDINI,UKABILA na UFISADI.

    Kwa kuyazingatia haya machache tu kijana huyu aliyotueleza kupitia hiki kikatuni chake kidogo ni wazi kuwa yupo pamoja na wazanzibari na anapendelea maslahi na hatma njema ya zanzibar.
    na kwa upande wa pili anawakejeli watanganyika kwa kuwapiga mafumbo ambayo yatawachukuwa karne bila ya kufahamu anachowakejelia.poleni watanganyika.

    Hongera ,hongera na hongera KP

    IDUMU JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  27. Hivi sisi Wa TZ tunapata nini hasa kutoka ZNZ? Mbona hata sioni hasaaa. Umeme wenyewe wanachukua kutoka TZ. Kama ni utalii hata sisi tunao kibao Bagamoyo, Mbuga za wanyama, Mlima etc.

    Wavunje huo muungano waone, mafuta yenyewe hawajakuwa na uhakika yatapatikana kiasi gani wameshaanza kuleta kimdomo sijui yakipatikana mengi itakuwaje.

    Tuwaachia nchi yao. Maisha yenyewe ya huko yako juu kila leo Wazanzibari wanakimbilia huku, biashara ukifanya haitoki.

    Huyo anon aliosema Wazenj ndio wenye maduka mengi Bara hebu hao wazenj warudi Zenj na maduka yao waone kama biashara itatoka. Wanakimbilia huku kwasababu wanajua biashara ipo, wanunuzi bara wapo kibao. Zenj mtu akipata sh 5000 hela ya kula tuu amesharidhika na maisha angoja kesho yake ni tofauti na Bara.

    Hebu wasinitie kichefuchefu mie.

    ReplyDelete
  28. Kwakweli mimi napenda kuwaasa wenzetu wanzanzibari kuwa wasipende kuwakumbatia hao viongozi wenye kupenda madaraka. Hao ni wale viongozi wanaotamani kupata vyeo nao kwa sasa hawana ndio wanaoleta hayo yote wakihisi watapata vyeo na kuwa katika hali nzuri ya maisha.

    Wazanzibari watizame maendeleo, Waache ukabila, udini hauna maana. Hao viongozi wanawachochea then wakianza kupigana sio wao wanaumia wala familia za hao viongozi . Wao wanauwezo wa kwenda nchi nyingine kutulia wananchi ndio watakaoteseka kuuana, njaa hasa watoto na wamama na kama ilivyo wazanzibari wengi ni wazaaji sana.

    Naombeni mufikirie kwa kina kuvunjika kwa muungano, na hao viongozi wanaogombea je wanaweza kuwaongoza. Wako fiti kielimu, Mawazo yao ya busara, na jee wanamapenzi ya kweli na Wananchi au ni danganya toto? Msiwe wakupelekwa pelekwa mtauziwa mbuzi katika gunia.

    Hao viongozi wanaong'gang'ania kuja pata madaraka je wameshawafanyia nini tangu waanze kuwa katika vyama vyao? Kwani naamini hata kama haupo katika uongozi unauwezo wa kutoa mchango wa maendeleo katika nchi yako japo kuonyesha mfano jinsi utakavyo kuja kuwa baadae. Je wao mfano Maalim Seif nk wameshafanya nini cha maendeleo?

    ReplyDelete
  29. Hivi chama cha CUF kimewafanyia nini hasa Wananchi wa Zanzibari? Yaani kimaendeleo yoyote..Japo hakija pata madaraka labda kimetumia hela zao wenyewe kutoka mifukoni?

    Hebu tujulisheni kwanza ndipo tupate kuwasaport au kuwapinga kuhusu muungano.

    Nasema hivi kwasababu wazi kabisa Chama hiki ndio chachu ya kuvunjika kwa muungano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar)

    ReplyDelete
  30. Hao wazanzibari hawawezi kujitegemea kwanza ni wavivu sana kupita kiasi hawana wasomi wa kutosha wakijitegea nchi itauzwa kwa waarabu au wazungu.

    ReplyDelete
  31. NDUGU ZANGU MUUNGANO UTADUMUTU, HATA IKIBIDI TUMWAGE DAMU MAANA MUUNGANO HUU TAYRI UNAYO MISHIPA DAMU BARA NA VISIWANI-ZAID NDUGU ZANGU NYINYI WA BARA TABIA ZETU WATU WA VISIWANI 9PSYCHOLOGICAL PATTERNS) NIKUTILIA MASHAKA WAGENI NA PIA KUONA KAMA MNAONEWA KWA VILE KAMBA YA MAJI INAYOTUZUNGUNKA UTUFANYA TUWE WATU WA MASHAKA NA MUKHARI.
    INGEKUWA VYEMA KAMA SISI WATU WA HAPA VISIWANI TUNGENGALIA KWANZA HALI YA WATU WETU, JE NI KWELI MATATIZO YETU YOTE YANATOKANA NA MUUNGANO? JE, TUKIFUNJA MUUNGANO NDO MAMBO YATAKUWA SHWARI? JE, KABLA YA MUUNGANOA HALI YETU ILIKUWA VPI? JE, SISI TUNAWEZA KUPUNGUZA HADHA KAMA ZILE ZA WAKINA MAMA WANAOLIMA MWANI? JE, KIWANGO CHA ELIMU KUWA DUNI NI KWA SASA YA MUUNGANO?

    ReplyDelete
  32. Namuunga mkono annony wa Tue Aug 04, 03:53:00 PM.

    ReplyDelete
  33. Kwa wale wote wanaodai kuwa Taifa la zanzibar litakapopewa uhuru wake litajiuza kwa waarabu na wazungu.
    Binafsi baada ya kuongea na wazanzibari wengi wameonekana kupendelea kuliegemeza Taifa lao la ZANZIBAR kwa waarabu .ifahamike kuwa mataifa kadhaa ya kiarabu yanataka kuiinua ZANZIBAR kiuchumi lakini hawako tayari kufanya hivyo wakijuwa kuwa ZANZIBAR bado iko mikononi mwa Tanganyika.

    Aidha wazanzibari hao nilio ongea nao hawakuliona na ubaya wowote ule suala la Zanzibar kujiegemeza kwa waaarabu ambao wana kila aina ya nguvu na neema zitakazo ineemesha ZANZIBAR kiuchumi na kijamii.

    Pia wazanzibari hao waliendelea kuhoji kuwa Tanganyika tayari imejisalimisha kwa VATIKAN na maendeleo yake yanaonekana.mfano ni huu waraka wa kanisa uliotolewa majuzi tu.hii ni neema ya Tanganyika kujiegemeza na kufaata maamuzi yanayotolewa na VATICANA na sio CCM.

    Kwa upande wao wazanzibari
    hawa wanaziona faida nyingi tu zitakazopatikana kutokana na kuiiegemeza Zanzibar kwa waarabu,kitu ambacho wanataka kitokezee kwa haraka zaidi.ili na wao waweze kutowa waraka wao pamoja na neema nyengine.

    IDUMU JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...