Niruhusu niweke hili nione wadau wanamchango gani hapa.
Kuna vitu vingi sana vya hatari katika barabara za nyumbani, lakini mojawapo ya vitu vinavyonitisha nikiendesha kwenye barabara za nyumbani ni hizi alama wanazoweka wenzetu wa magari makubwa pale wakiharibikiwa.
Kama sikosei, nafikiri kukiwa na dharura inatakiwa kuwekwe kitu kinaitwa "triangle". Lakini mara nyingi madreva wetu, hasa kwa wenzetu wenye magari makubwa, wanapenda sana kuweka matawi ya miti, au mida mingine miti mizima-mizima (kama kwenye picha hii) au wengine mawe makubwa, na kuongezea na tairi pembeni.
Hapo, kaka Michuzi kama umenielewa, kuna hatari kubwa sana kwa mtu mwenye gari dogo kama akitokea kulivaa hilo tawi, na hatari inakuwa kubwa zaidi nyakati za usiku maana hata uwezi kuliona hilo tawi toka mbali (kama ambavyo ungeweza kuiona triangle). Na cha kushangaza, hawa jamaa wakisha tengeneza magari yao wala hawakumbuki kutoa hiyo miti na mawe, wanachokumbuka ni matairi yao tu.
Wapi traffic police? Kwa kweli wapo na wanafanyakazi yao. Mimi mara nyingi, nikiwa katika barabara ya Dar- Moro, nimeshimamishwa na traffic police. Na mara zote wanauliza leseni, kadi ya gari, triangle, fire extinguisher nk, na hata ukiwaambia triangle ninayo lakini iko nyuma ya buti wanakuambia shuka itoe tuione. Sasa najiuliza kama hayo ndio maswali ya askari wetu (ambayo ni muhimu sana kwa kweli), sasa inakuwaje hao madreva wa magari makubwa wakiharibikiwa wanakosa hizo triangle na mwisho wanaishia kuweka matawi? Au wanajibu nini pale askari akiuliza triangle? najiuliza wanaonyesha nini hasa pale askari akitaka aione hiyo triangle?
Najua wadau watakuwa na maoni tofauti na pengine kuna wengine wataona hii hoja ni upuuzi. Lakini nahisi kuna ajali nyingi tu zinatokea au zinasubiri kutokea kutokana na hii miti, mawe na matairi ya hawa jamaa wa magari makubwa. "Mungu apishilie mbali", lakini ebu fikiri ukumbane na huo mti usiku kwenye kona (mfano za Iyovi kwa wale wanaozijua) na mbele linakuja gari ingine (mfano mfuso na fujo zao) na limewasha taa utadhani wanawinda mbugani!!
Mimi naona kama tunataka kupunguza ajali ni lazima kuwe na umakini sehemu fulani. Unajua sheria Tanzania zipo na tena ni nzuri sana. Ndio maana askari wanapata hata nguvu ya kuuliza triangle, kadi ya gari, leseni nk, nguvu ya kuuliza hivyo vitu inatoka kwenye sheria. Lakini sheria bila "enforcement" ni bure! Ukifanya kosa (liwe la barabarani au vingenevyo) askari inatakiwa atafanya vile sheria inasema. Kama ni faini basi toa faini, kama ni kufikishwa kituoni basi twende kituoni. Lakini kama hawa madreva wetu wakiwa na mindset ya kwamba hata ukiwa na kosa kubwa kuna uwezekano wa kumpooza askari, basi hata siku moja hawataweza timiza sheria za barabarani, na tutaendelea kuuana tu.
Kusema kweli, hizo triangle ni bei rahisi mno pengine kuliko hata hizo rushwa wanazotoa kwa askari. Mimi naona gharama ya kosa la barabarani isiwe katika ile faini ya Tshs.20,000 au hongo kwa askari tu, bali gharama iangaliwe zaidi kwa ule uthamani wa maisha yako dreva, maisha ya wengine,na pia mali (gari, mizigo nk) vinavyoweza potea kwa ajali itakayotokea kwa kuvunja hiyo sheria.
Asante sana kwa kunipa nafasi hii!
Mdau Amsterdam
Retarded and insane tanzanians!!
ReplyDeletewe mdau wa iyovi hiyo miti imesaidia sana kupunguza ajali
ReplyDeleteAfandhali ulivae hilo gogo kuliko Lori mdau! Ukiwa kwenye hizo barabara uwe mpole tu na jiendee zako taratibu. Ukiweka hizo Tariangle hata kama ni porini kiasi gani, utashangaa zinapotea within Minutes!!
ReplyDeleteHuo ni ubunifu mpya kwa tanzania ili kuepusha ajali. maana madereva wa tanzania ukiwawekea trigle zako ni kama unajisumbua watazigonga na kukugonga. ila miti kama hiyo ndio dawa yake maana watasimama ama watapunguza mwendo. ni kweli miti hiyo inachafua barabara kwa kuzagaa hovyo, lakini ni ukweli pia kuwa inasaidia kuzuia ajali kwa madereva kuwa makini baada ya kuiona. ni ubunifu mzuri.
ReplyDelete