Mkurugenzi mtendaji wa Benchmark Production Madame Ritah Paulsen(kushoto) na Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kulia)akiongea na wanahabari wakati walipotangaza kumi bora ya washiriki wa Bongo Star Search 2009.Vodacom Tanzania ni wadhamini wakuu wa shindano hilo
Washiriki wa Bongo Star Search 2009 wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Benchmark Production Ritah Paulsen ambae ni muandaaji wa shindano hilo yakidhaminiwa na Vodacom Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Madame? Neno lina utata hilo.

    ReplyDelete
  2. hata mie naungana na mdau hapo juu, hiyo title ya madame ina utata. siju kwa bongo ila kwa UK kuitwa madam (Dame) before your name lazima u-earn hiyo title.sio tu unaamka na kujiamulia kujiita madam..
    nway, kama kaka michuzi anavyotuhabarisha kuwa bongo tambarare, kila kitu chawezekana pia...

    ReplyDelete
  3. Kuna uvundo wa hisia za BSS 3 kumuandaa kelvin kuwa mshindi wa mwaka huu. judgement zao zinamproject waziwazi. hata kama wanataka ashinde basi wasionyeshe wazi wazi. we know it is business lakini kuna kaharufu ka upendeleo wanapojaji.

    ReplyDelete
  4. nyie hapo juu sio mnashoboka tuuu madam rita hakujipa hiyo a.k.a ni hao hao washindani wake wa bongo star ndo walombatiza madam rita tena wale wa kwanza wakati hii kitu ndo inaanza walianza ka masihara ndo ikakolea mbona kuna mdada hapo dar anajiita pussy???

    ReplyDelete
  5. Nakuunga mkono Anon 12:06 kuhusu maandalizi ya Kelvin kuwa mshindi. Kwanini wasiache watazamaji waamue nani mshindi. Kwanini kutuongoza kwenye kuchagua nani mshindi kwenye haya mambo ya kuigiza kuimba?

    ReplyDelete
  6. Kweli kabisa kelvin mbati keshaandalia kuchukua gari wengine ni wasindikizaji tu. upendeleo unaonekana wazi, mtu huitaji kuwa mganga wa kienyeji (kupiga ramli)kuliona hili. kuna kijana (simsemi) kamfunika kelvin lakini kelvini anaonekana nyota yake imewaka. hongera zake kelvin.

    ReplyDelete
  7. Jamani tuache ubishi ni kweli Kevin Mbati ataimba vizuri na anajua anachokifanya. Hakuna kusema majudge wanamfagilia wala nini waulize watanzania watawajibu.

    pale mtu anapokuwa anatenda mambo mazuri jamani tumsifie sio kumasaga.

    Kweli watanzania hapo tunashangaza sana sana!

    ReplyDelete
  8. Maeneo ya Las Vegas madame ni mama mwenye danguro au mmiliki wa biashara ya ukahaba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...