
Na Mohammed Mhina,
na
HassaN Juma
wa Jeshi la Polisi- Tarime
Makacherowa Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini kwa kushirikiana na na Askari waOpereshen Maalum, wamefanikiwa kukamata zaidi ya magari kumi yakiwemo ya kifahari ambayo yameingizwa nchini nchini kinyemela.
Katika Operesheni hiyo, zaidi yamagari 350 yaliyopo katika mikoa ya Mara na mkoa mpya wa Kipolisi wa Tarime Rorya, yalikaguliwa kwa kutumia mitambo maalumu iliounganishwa na mtandao wakimataifa wa kusaidia kugundua magari yaliyoripotiwa kuibwa kutoka mataifambalimbali.
Wakati wa zoezi hilo, baadhi ya magari yalibainika kughushiwa namba za chasis na injini zake na mengine kubainika kuibwa kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosaya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, amesema kuwa ofiisi yake inafanya mawasiliano na nchi husika yalikoibwa magari hayo ili kuja kwa utambuzi zaidiili sheria ichukue mkondo wake.
Pamoja na kukamatwa kwa magarihayo, Polisi hao pia wameweza kufyeka zaiidi ya ekari 30 za mashamba ya bangiiliyolimwa katika mashamba ya vijiji mbalimbali vya wilaya za Tarime na Roryawilaya ambazo zinaunda mkoa mpya wa Kipolisi wa Tarimerorya.
Hata hivyo Kamishna Manumbaamesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa magari hayo, Polisi pia imefanikiwakukamata silaha kadhaa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya kihalifuyakiwemo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika wilaya za mkoa huo mpya wa Kipolisi.
haya magari yatolewe tu misaada mahospitalini jamani au hivi sasa yatapelekwa wapi?
ReplyDeletetantarantaaaaaaaaaaaa za mwizi arbaini
ReplyDelete---oya babu mbona unanichanganya mikoa wa mara na mkoa mpya kipolisi tarime rorya ndio nini? kwani sikuhizi kuna mikoa ya kipolisi ama? mkuu wake wa mkoa ni nani? tueleweshane mie sijamsoma kabisa huyo hassan juma na mohamed mhina misupu
ReplyDeleteSasa gari mfano wa hili [kwa sababu najua hili silo mojawapo,background inasema yote]linashushwa Mara jamani,hata fala atalishtukia limetoka wapi.bora Dar kidogo laweza kujichanganya na mengine,namuunga mkono aliyesema yatolewe mahospitalini kutransport wagonjwa [toa viti vyoote vya abiria].
ReplyDeleteunamanisha nini unapo sema TarimeRorya??..maana naelewa tarime ni wilaya, na Rorya pia ni wilaya!! fafanua pls!
ReplyDeletemkoa wa kipolisi ina maana
ReplyDeletekwa jinsi vita na kuuana na kupiga wawekezaji wa dhahabu visivyoisha polisi wameweka area maalumu "green zone" ili wawe karibu na kuzuia balaa izo za watu wa eneo hilo,maana imeshindikana kwa mazungumzo..
siku izi shemu iloshindikana kwa aina yoyote ya kuvuja amani wanaweka "mkoa wa kipolisi"
ila sijaelewa kwanini BADO ng'ombe wanaibwa sana kupelekwa kwa majirani zetu?????