hapa ni katika makutano ya barabara za nyerere, posta na nkrumah roads jijini mwanza ambapo pameingia kwenye vitabu vya historia kama mahala pa kwanza kuwekwa taa za barabarani katika jiji hili. ni miezi kadhaa imepita toka ziwekwe na inasemekana kuna wajanja waliiba paneli za solar ambazo taa hizi zinatumia. zikaletwa nyingine






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. mwanza kumekucha kweli, ila walioiba hizo solar panels sii wajanja ni wajinga!
    kelvin, uk!

    ReplyDelete
  2. AAAAAAAAAA Bwana Nanihii hapo umekosea sana hao walioiba wana ujanja gani wa kujiibia wenyewe??? Hao ni wapumbavu kwa maneno mwingine.
    Mzawa

    ReplyDelete
  3. Sio wapumbavu bali ni wajanja,,kuliko wabomoe majumba ya watu! nafuu waibie serikali .Kwasababu hata ndani ya serikali yenyewe ufisadi umezidi.

    ReplyDelete
  4. Michuzi hayo ndio maneni jiji linapendeza lete mengi mapya

    Mkulima

    ReplyDelete
  5. MICHUZI UNATUMIA LUGHA YA KUHAMASISHA NA KUDUMISHA UJAMBAZI..HUWEZI SEMA WAJANJA AU VIJANA WA KAZI.TUNGEWAITA WEZI WAPUMBAVU INGEKUWA INALETA MAANA.TUNAENDELEA KUZUBAA TU MWISHO WATAIBA IKULU NASI TUTAENDELEA KUSHANGILIA NA KUWASIFIA!

    ReplyDelete
  6. MAFUNDI WALIOZIWEKA NDIO HAOHAO WALIOZIIBA KWANI WAO NDIO WALIOZIFUNGA KIUJANJAUJANJA ILI IWE RAHISI KUZIFUNGUA.

    ReplyDelete
  7. walioiba ni watoka Dar tafadharini polepole huko ndiyo kila aina ya uchavuzi wa khali ya hewa umejaa,we anonymous wa kwanza nyie ndiyo mnazomeshwa bure kwa hongo be careful vitu gani unaandika na kushangilia bila sababu je kama ndiyo ndugu zenu wameiba.
    grolia padmore,the colony texas

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli huyu anaesema ni bora kuiibia serikali sijui ni mfananishe na nini.. Hii ni sawa na Kumuibia mkeo ukaenda kununua pombe au kupeleka chakula nyumba ndogo maana watoto wako ndio watakao kufa njaa...
    Serikali haipati hela kwa Mungu bali kutoka kwako wewe na mimi na wananchi wote.Hivyo kuiibia ni sawa na kujiibia mwenyewe....na pengine ndugu yako ANAWEZA KUGONGWA HAPO HAPO NA WEWE TAA UMEIBA SASA UTAMLAUMU NANI???
    KWELI KUSOMA SI KUELIMIKA!
    Mzawa!!

    ReplyDelete
  9. Nakumbuka sana miaka ya 80s and Pamba ikishinda basi wachezaji maarufu watajiania hii sehemu
    well Mwanza --- Mwanza naona picha pamebadilika sana == I love MZA

    mimi RR

    ReplyDelete
  10. Wenzetu wanasema kuwa moja ya vipimo vya nchi masikini ni uwepo wa taa za barabarani. cc tunashangilia.

    Miji iliyopangwa vema huwa haitumii teknolojia ya kale ya mataa. Inabidi kuwe na tunnels yaani handakis, sana sana roundabouts. Mambo ya mataa yamepitwa na wakati, kwani husababisha magari kusimama na mafoleni yasiyo na mpango. Wajameni tuache huu upwefu na kufungua macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...