Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Mohamed Aboud akimpongeza Vodacom Miss Lake zone 2009 Miriam Gerald baada ya mchuani uliofanyika Ijumaa usiku Yatch Club jijini Mwanza
Hatimae Miriam Gerald mrembo kutoka mkoa mwanza amenyakua taji la vodacom miss lake zone. kulia kwake ni mrembo Mary Charles Alieshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikirudi hukohuko mara kwa mrembo Sabina Budodi,namba nne ikishikiliwa na Glory Innocent mrembo kutoka Shinyanga,na namba tano alichukua mrembo Emaculata Alphonce kutoka Kagera.

Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa ushirikiano Afrika mashariki,MOHAMED ABOUD.Ambae aliwakabidhi washindi zawadi zao,namba moja alipewa fedha taslim sh. laki sita, huku aliechukua nafasi ya pili akiondoka na kitita cha laki nne, na mshindi wa tatu sh, laki tatu, namba nne na tano walipewa sh laki moja na nusu.

warembo wote walipewa zawadi zao isipokuwa mrembo namba tano Emakulata Alphonce kutoka kagera alipatwa na mshtuko na kupoteza faham aliposomwa na jaji mkuu kwamba ameshika namba tano,hivyo hakuweza kufika mbele kwani alikuwa amepelekwa hosipitali ya rufaa bugando,tunamshukuru mungu kwani kwa sasa anaendelea vizuri.

Kwa picha zaidi naomba waingie
florasalon.blogspot.com.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...