Habari za kazi kaka michuzi,
naomba msaada uniwekee hii shida yangu kwenye blog yetu ya jamii natafuta ushauri.
Nilipata udaku toka kwa watu kwamba mume wangu anauhusiano na dada mmoja nikapeleleza nikajua na mpaka nikamjua huyo msichana. sasa nikamjulisha mumewangu kwa upole tu kuwa najua unauhusiano na msichana furani na wanafanya kazi karibu.
akanijibu ndio sasa wewe unataka nini na kuanzia leo kila mmoja alale kitanda chake tuwasiliane kuhusu watoto tu na sio mambo ya mapenzi.
hivi nnavyoongea tumeanza kulala kila mtu kitanda chake leo kama wiki imepita. naomba ushauri je nifanyeje bado nampenda mume wangu lakini kuhuliza kwangu kumenisababishia hayo naomba ushauri wenu wadau. usitoe email yangu pls
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. Kwanza pole kwa matatizo,tena matatizo makubwa sana.Kwa taarifa yako moto ndio unafutuka kinachoonekana sasa ni moshi,moshi ndani ya fukuto zito,fukuto libebalo kishido cha moto.

    Sikuwa na nia ya kukutisha au kukukatisha tamaa, nilikuwa najaribu kukuhabarisha uzito wa tatizo lako na umuhimu wa kulitatua sasa na si kesho(self realization).

    Huyo mume wako mapenzi yake kwako yamepungua,tena sana.na inawezekana imechangiwa na huyo mbaya wako,huyo mwizi wa mali yako au wewe, jaribu kujiangalia pia.

    Nakushauri tafuta muda muhafaka,kwa utaratibu kabisa,bila hasira,ndani ya busara tele, jaribu kumueleza mwenzi wako jinsi unavyoumia na kukwazika kwa kitendo chake,mkumbushie ahadi alizokuwa akizitoa kwako,mkumbushie kwamba nyie ni wazazi tayari mna majukumu ya kulea na kupanga mipango yenu ya kesho,mkumbushie janga la ukimwi na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa, kwani yeye anaporudi nyumbani yule binti naye anakwenda kwa mabwana zake wa permanent au temporary na hao mabwana zake wana wenzao wa permanent au temporary na chain inaendelea.

    Ikishindikana kabisa itabidi uwahusishe washenga, nao ikishindika nenda kwa wazazi, na ikishindikana basi nenda kwa wachungaji wenu au mashehe waliosimika ndoa yenu.Hapo lazima kieleweke la sivyo itabidi kuamua kusuka au kunyoa.

    Hilo ni tatizo kubwa sana, na likiendelea laweza zaa tatizo lingine la maradhi,ni bora huyo bwana aende zake kwa huyo malaya kuliko kuwatengenezea njia ya kaburini wewe na mtoto.

    ReplyDelete
  2. Dada pole sana!! hili tatizo sio dogo, bora tuwe wakweli ni zito sana. Mimi nasema hivi kwa sababu hata mimi ndoa yangu imavunjika, tunajipa moyo tu kwamba ni kawaida ila inaumiza hasa pale utakapojikuta huna tabia ya vinjari na waume za watu, MIMI NAKUSHAURI JITAHIDI SANA KUWA MPOLE KATIKA KUTAFUTA UFUMBUZI, USIPANDISHE HASIRA, pia sali sana kwani huyo shetani ana ngumu. Ushauri wa Anonymous wa 1 ni mzuri kwa kiasi ila PIGANIA NDOA YAKO, maisha ya single parent ni sikitiko la moyo "(SHIDA SIYO PESA ILA UMPENDAYE NI MAJONZI)"

    ReplyDelete
  3. POLE SANA DADA YANGU. USHAURI WANGU NI KAMA IFUATAVYO; KAMA IMEFIKIA MPAKA MNALALA KITANDA TOFAUTI SIDHANI KAMA HATA UKIMUWEKA CHINI NA KUZUNGUMZA NAE MTAELEWANA MAANA ANAVYOONEKANA AMESHAPAGAWA TUNAITA KISHAMBA NA SIKUZOTE MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI. ITA WASHENGA WENU KWANZA ONANA NAO WAELEZE YOTE YALIYOTOKEA WANAWEZA KUWAWEKA CHINI MKASULUHISHA VIZURI KABISA INGAWA SOMETIMES ANAWEZA HATA AKADHARAU YA WASHENGA MAANA KESHA PAGAWA KWA MADAI YAKE HAELEWI CHOCHOTE. IKISHINDIKA PLEASE NENDA KAWAONE WAZAZI WAKE KAMA WAPO WAELEZEE YOTE NADHANI MUAFAKA UTAPATIKANO. NAKUOMBA KITU KIMOJA KAMA MTAAFIKIANA NAOMBA KABLA HAMJAKUTANA KIMWILI MKAPIME AFYA ZENU MAANA SIKU HIZI DK 1 NI KUBWA SANA KUPATA MAAMBUKIZI KISA CHA KUFA KABLA YA SIKU ZAKO SIKIONI KWA TABIA YAKE MBAYA. NI HAYO TU DADA ANGU. HUNA HAJA YAKULUMBANA NAE MAADAM UMESHAJUA NINI KINACHOENDELEA NAJUA UNAUMIA KIASI GANI BUT KUWA MWANAMKE JASIRI ALWAYS. BYE.

    ReplyDelete
  4. ameamua kulala kivyake? pole dada..nakushauri kwanza kuwa mwangalifu....gonjwa linapiga hodi..usimpe naniliu plzzzzzzzzz....tumia kondomu nae kama siku akiomba gemu...pili ilo tatizo bora uanzie kanisani au msikitini moja kwa moja, washenga hapo hawana nguvu kabisaaaaaaaaaaaa....kila la heri...

    Mdau wa ndoa....

    ReplyDelete
  5. pole sana dada ila mdau namba moja ametoa point sana naungana naye asilimia mia moja shughuli ipo kwenye suala la ngoma! mama wee hapo hapachimbiki ni kiama tu ishu hii sio ya kufanyia mzaha ipeleke fasta kabla presha haijapanda na kushuka
    mdau, canada

    ReplyDelete
  6. POLE SANA DADA YANGU!!NACHOPENDA KUKWAMBIA KUWA HUYO MUMEO KITENDO CHAKE CHA KUKATAA KULALA NAWEWE NIKAMA KAKUPUNGUZIA MZIGO WA KUKULETEA MARADHI.
    INABIDI USHUKURU SANA HICHO KITENDO INAWEZEKANA ANAJUA KUWA WWE NI INOCENT KWAHIYO HATAKI MGAWANE MARADHI.
    VUMILA UKISHINDWA DAI TARAKA NA UMPATE AKUPENDAE MAANA HUYO MUMEO ANAFANYA KUSUDI NA SIO BAHATI MBAYA!!NA MTU ANAEFANYA KUSUDI HAKUNA SURUHISHO HAPO UTATWANGA MAJI KWENYE KINU YAWEZEKANA HAKUTAKI TENA AMA ANAKUTINGISHIA KIBIRITI KWA KUUJUA UDHAIFU WAKO,SASA AKIJUA KUWA HAKITINGISHIKI ATAOGOPA KUKUPOTEZA KAMA ANAKUTAKA BADO NA KAMA HAKUTAKI NI KHERI URUDI KWENU MAANA HAKUNA MAPENZI TENA.

    ReplyDelete
  7. Duh..noma. Huyo mwanamme anastahili kucharazwa viboko hadharani. Mambo gani haya ya kumfanyia Mama wa watoto wake..!!!

    Pole sana Bi. Mkubwa, wadau hapo juu wamekupa ushauri mzuri sana. Kuwa jasiri, yatapita haya.

    ReplyDelete
  8. LOVE IS AN EMOTION, MARRIAGE A CONTRACT AND RELATIONSHIP IS WORK. Deal with the problem spiritually, philosophically and sociologically. Jipe Moyo dada.

    ReplyDelete
  9. Akirudi tu usiku anzisha mada ya watoto atakapojibu tu, mvue surually au pajama au bukta au chochote na mbake. Ni mwili wenu. na ni haki yako. CHAKE CHAKO NA CHAKO CHAKE.MLA JANA KALA JANA MLA LEO KALA NINI???

    ReplyDelete
  10. Dada pole sana.....
    Maisha ya ndoa kweli ndoana... wanaume wanavyokuwa na maneno ya busara wakati wa kuchumbia wangekuwa wanazeeka na maneno yao ya busara basi ndoa zingekuwa na maana kweli kweli!

    Pili nawapongeza wadau waliochangia kwenye hii hoja kwani wameonyesha ukomavu na ubinadamu kwa yanayomsibu huyu dada...kama wote tungekuwa hivi then nahisi blog hii ingepata nguvu za ajabu!!

    Dada wote wametoa ushauri mzuri tu ..ila mimi nashauri anzia kwa wakwe zako, waone washenga kama itabidi ...kanisani au msikitini ni pahala nyeti sana kwa kugusia agano la ndoa!! Nina imani Mungu atasikiliza kilio chako!! You have been too honest!!
    Mungu na akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu katika safari yako ndefu ya ndo!!!

    ReplyDelete
  11. Kaza roho dada yangu, huyo hakupendi mwache ahangaike na dunia na akunyimae kunde......!!!!.lea watoto wako ogopa hili gonjwa la ukimwi.

    ReplyDelete
  12. kwani wewe unangoja nini sasa na wewe tafuta mwenyewe anaona ama kweli sasa labda mwenzangu anafaidi ataomba msaamaa na isitoshe wanaume huwa wanaumiwa zaidi wakijua wake zao wanamahusiono nje maana watamcheka na unampakazia kuwa ulikuwa unangoja hii nafasi kwanza mwambie alikuwa hakufikishiiii..

    ReplyDelete
  13. NENDA KWA WAZEE UKASHITAKI. ATAITWA NA KUONYWA. KISHA ATAJIREKEBISHA

    ReplyDelete
  14. dada pole sana ila jamani hawa kina dada nao pia wengine wanakuwa wana gubu sana sasa mambo yakishakuwa mazito wanatakaga ushauri kwa kutoa maelezo nusu nusu ili mradi tu waonekane kuwa wao ndio wanaoonewa(innocent)mimi kuna mwanamke nimezaa nae kisa anajua naishi nje basi anadhani nina kisima cha kuchimbia pesa huku.Kilichonisikitisha ni jinsi alivyoenda kuyageuza maneno kuwa pesa simtumii na nikimtumia ni ndogo kwa bahati nzuri ninazo risiti zote kutoka western union nilizotuma pesa ndani ya miezi 14 amepokea shilingi milioni 3.Na pia ikumbukwe kuwa yeye kwasasa ni mama wa mtoto wng tu anaishi na bwana mwengine na hizo pesa za mtoto wanabunya wao tu na huyo bwanaake jobless.INANIUMA SANA KISA ALITAKA PESA NIKAMWAMBIA PESA NINAZOTUMA NADHANI ZINATOSHA SANA AKALETA JEURI NIKAMWAMBIA ATAKUWA AKIPOKEA PESA KUPITIA KWA WAZEE WNG KWAHIO AORODHESHE MATUMIZI YOOTE YA WATOTO KISHA WAZEE WAONE KAMA PESA ILE HAITOSHI AU INATOSHA.KWA AIBU ZAKE SASA ANATAKA MM NDIO NIONEKANE MBAYA NA YEYE NI INNOCENT.kwahio jamani tuangalie au tusikilize pande zote mbili

    ReplyDelete
  15. Pole mwanamke mwenzangu,kama walivyosema waliotangulia, tafuta muda mzuri uongee naye ujue sababu kubwa ya kuwa hivyo maana mapenzi yapoisha hapo anakuona kama mdudu tu. Kama hataki, hata wewe umezaliwa kama yeye, anza mbele, maisha ni popote, pengine hakuwa wa ubavu wako.

    ReplyDelete
  16. Pole sana dada yangu kwa hilo linalokusibu.Lakini ushauri wangu ni mmoja tu PIGANIA NDOA YAKO usikubali kumuacha mumeo kwa hilo, try your level best kwa BUSARA nying ,UPOLE usio kifani na UVUMILIVU wa hali ya juu umnasue mumeo huko mikononi mwa wanyang'anyi.
    Nakuahidi haijalishi ni kiasi gani amebadilika atarudi ktk mstari sahihi.
    CHUKUA HII:
    What is more painful?When a person whom u trust,hurts u?
    OR
    The person whom u hurt,still trust u?
    PLZ still trust in him U will get him back. But ukimwi hapo sina cha kusema eeeeh Mungu Muepushe mume wa huyu dada na Mnyang'any huyo na pia eeeh Mungu gonjwa hatari limpitie mbali.
    I wish all the best my lovly sista.

    ReplyDelete
  17. Kwanza pole kwa yaliyokukuta, usijione mwenye mikosi kuliko, maana mi najua hayo ni mapito tu ya dunia, na pengine Mungu anataka akuokoe na dhahama, ninachoweza kukushauri ni kwamba, kama una kazi yako basi LIVE YOUR LIFE, maana inavyoonekana huyo mumeo amekuchoka kwakuwa ANGEKUWA ANAKUPENDA ASINGEJIBU HIVYO, NI KAMA ALIKUWA ANANGOJA UMUULIZE TU ILI AMALIZANE NAWE, muombe Mungu akupe subira na uvumilivu ilhali unatafuta hatma yako, kama walivyosema wadau hapo juu, USIKUBALI BILA KUPIMA UKIMWI! Asitumie udhaifu wako wa kumpenda akakuambukiza maradhi (kama anayo), wakati mwingine U NEED TO HURT UR HEART TO SAVE UR SOUL!

    MANUTD-DIE-HARD-FAN

    ReplyDelete
  18. NI HIVI SISTA USHAURI WANGU, KWANZA WEWE MWAMBIE MME WAKO HIVI MME WANGU NAKUPENDA SANA, UMENISAIDIA SANA KUNIEPUSHA NA MARADHI, WEWE NI MME WA PEKEE, HATA HUYO MDADA ANAJUA HILO. THANK YOU SO MUCH.
    TUENDELEE KUDUMISHA STYLE YETU MPYA.
    WAKATI UNAONGEA NAE UWE NA TABASAMU NA FURAHA ISIYO KIFANI, UKIMALIZA KAMA NI MCHANA BAADA YA CHAKULA WEEKEND ONDOKA NA WATOTO NENDA KATEMBELEE NDUGU KAMA WAZAZI PAMOJA WATOTO KILA WEEKEND USIWEKE MAWAZONI MATATIZO YA NYUMBANI,
    BAADA YA HAPO RUDI HOME NA WATOTO USIMBUGHUDHI MME HOME,WALISHE WATOTO KALALE FANYA HIVYO KWA MIEZI KAMA MINNE, VILE VILE KUMBUKA AKIRUDI AMECHELEWA FUNGULIE MLANGO UKIWA UNATABASAMU USIMWULIZE UMETOKA WAPI,KAMA ANAHITAJI CHAKULA MWANDALIE VIZURI UKIMALIZA OSHA VYOMBO MWAGE KWA TABASAMU MWAMBIE GOOD NIGHT KALALE CHUMBANI KWAKO. UTAONA KUNA MABADILIKO YA AJABU.
    ILA USIMWAMBIE MMEO NAEMDA KUMTEMBELEA MZAZI MWAMBIE KWA UPOLE NATOKA KUWATEMBEZA WATOTO.
    AKIJA JUU MSIKILIZE KWA MAKINI AKIMALIZA MJIBU KWA UPOLE MME WANGU, NAKUPENDA, WATOTO WANAHITAJI KUBADILI MAZINGIRA KUREFRESH THEIR MIND.
    JITAHIDI USIONGEZE MANENO MENGINE HATA KIDOGO YA KUMLETEA HASIRA.
    HATASAHAU MAISHANI ITABAKIA HISTORIA KICHWANI MWAKE. KAMA ANAKUPENDA UTAONA NI MTU WA UCHUNGUZI UCHUNGUZI.
    IKISHINDIKANA HAPO OMBA USHAURI KWA WAZAZI.

    ReplyDelete
  19. INANIUMA SANA KUPATAGA HABARI KAMA HIZI POLE SANA DADA.TOKA UTOTONI MWANGU MPAKA SASA NAKARIBIA MIAKA 30 WAZAZI WANGU WAMEKUA WAKIGOMBANA KISA DINGI ANA WANAWAKE NJE. MAMA ALIAMUA KUPIGANIA NDOA YAKE SHE ENDED UP BEING HIV POSITIVE AND SHE IZ THE ONE WHO IS SICK EVERY THERE AND THEN, DINGI YEYE ANADUNDA NA NGOMA YAKE NA ANAENDELEA KUSAMBAZA. HII KITU IMENIATHIRI SANA NACHUKIA WANAUME KUPINDUKIA I DONT EVEN WANT TO GET MARRIED COS MTU AKINI-CHEAT I MIGHT JUST KILL HIM.

    DADA MAAMUZI YAKO MIKONONI MWAKO KUNYOA AU KUSUKA, UKITAKA JARIBU KUPIGANIA NDOA YAKO HUKU UKILINDA AFYA YAKO COS WATOTO WAKO WANAKUHITAJI. NA KAMA VP ANZA NA MOTO WAKO.

    IF I WERE YOU NINGEMUULIZA HUYO MY HUSBAND WAKO ACHAGUE ANAMTAKA NANI HUYO MWIZI AU WEWE, AKICHAGUA HUYO MWIZI BASI UNAMWAMBIA AANZE NA MOTO NA MUWASILIANE KWA MAMBO YA WATOTO TU AS HE SUGESTED

    ReplyDelete
  20. Shukuru hata kakwambi mlale vitanda tofauti, cha msingi ni nend kapime kwanza wala usisubiri akuombe wala suhulu kama ni mzima kapime tena mara ya pili baada ya miezi mitatu, ukijikuta salama anza bibi wee, yakimkuta ya kumkuta utamuuguza tu huko mbele ya safari. Maisha ni wewe kwanza na watoto wako wenye damu yako, yeye hamjachangia damu. Kama damu imeshaharibika itabidi ujipange kuanza kupambana nao usife mapema kwa hofu utadunda tu kuna watu huu mwaka wa 25 bado wanaishi hapo hapo bongo

    ReplyDelete
  21. POLE SANA DADA.

    USHAURI WANGU MIMI ENDELEA KULALA MWENYEWE MDHARAU AKIKUSALIMIA MSALIMIE LAKINI USIONDOKE KABISA AKIKUAMBIA UONDOKE MWAMBIE AONDOKE YEYE.

    KAMA UNAFANYA KAZI ENDELEA NA KAZI ZAKO, KAMA UNAENDA KANISANI NENDA SALI. LAKINI UKIONDOKA NDO UMEMPA UHURU. YEYE ANATAKA UONDOKE MAANA AMESHAFANYIWA DAWA.

    ReplyDelete
  22. Matayo 5:31-32

    31``Pia mliambiwa kwamba, `Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.' 32Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.''

    Mama nakushauri mwache haraka sana huyo mumeo, Ameshatenda dhambi kuendelea kulia lia unampenda unashiriki dhambi mwache mara moja, Kimbia Jiokoe wewe na Roho

    ReplyDelete
  23. Mama usichelewe kula kona, tafuta atakayekupenda pia. Muhimu si kumpenda mtu, bali yeye akupende wewe. Usijidanganye kusema mtatatua hili tatizo wakati yeye anampenda mtu mwingine. Maisha yako yatakuwa ya tabu sana kama utaendelea kuwa na huyo jamaa. Usidanganyike na mambo ya kuomba Mungu, haisaidii chochote, kama hupendwi hupendwi tu. Tafuta mtu akupendaye nawe mpende huyo utasahau haya yote.

    ReplyDelete
  24. mi niko tayari kupima nitafute kupitia namba 0787***700 misupu atakupa hidden numbers natafuta mwenza huyo achana nae kishakupiga chini ukiendelea kumpenda utateseka for 77 X 7 years kwa nini usimove on ?hilo kosa halisameheki kama mtu hajakiri nitafute mama maisha popote ,usijali tutaanza kwa secret

    ReplyDelete
  25. HAPA DADA UMEFIKA KWA WATAALAMU WA MAPENZI...USHAULI ULIOPO NA UMESEMA UNAMPENDA SUBILI AKULETEE NGOMA AU KASWENDE NDIYO UTAMPENDA ZAIDI....
    MDAU CASHMONEY..001.832

    ReplyDelete
  26. Pole na maswaibu yanayokukuta. Kwa hali ya magonjwa mengi, bila kipira usimpe kitu jamaa.
    1. Wahusishe washenga kujaribu kuwakalisha kupata ufumbuzi.
    2. Wahusishe wazazi wa pande zote mbili.
    3. Yote yakishindikana ni vema kila mmoja aendelee na maisha yake peke yake. Haisaidii kuwa umeoa au kuolewa wakati unashinda na huzuni kila saa.
    Mkipata usuluhishi kabla hamjafanya pekupeku nendeni mkapime halafu mrudie tena baada ya miezi mitatu.

    ReplyDelete
  27. Jamani inatia imani sana, wewe dada ni mvumilivu sana , na kwa hilo nakusifu!!!ila mimi ushauri wangu ni kwamba!!mungu anakuandikia wako wa milele kama siye huyo ulokuwa nae mwengine atakuletea akuridhishe moyo wako. siamini haya mambo wanayosema watu kuwa eti mvumilie au muende kwa wazazi, ila kumbuka wakati wewe unamvumulia na unaenda kushtaki kwa wazazi mwenzako anakula uroda kwa mwanammke mwengine , kwa nini ujitese??? maisha ni mafupi na ukimwi upooo!!kama ni mimi naondoka kwa huyo bwana siku hiyo aliyokuniambia tulale vitanda tofauti life is too short to beg a man.I only beg God

    ReplyDelete
  28. DADA WEWE BANANA NAE TU HUYO MBAYA WAKO!!!HAPO MJINI HAMNA MMOJA MMOJA.. CHOKOA CHOKOA UTAKUJA KUCHOKA PWEZA!!! NDIYO HAYOOOO!! POLE SANA...

    ReplyDelete
  29. Siku zote unaambiwa kwamba toa love inayotakiwa ndani ya nyumba...Hata kama mimi hunipi ninachotaka lazima nitoke nje nikae ndani tufanye nini????Kazi kwako mama kama unataka njoo kwangu nitakusaidia shida yako!!

    ReplyDelete
  30. wote wamesema mie nahitimisha kama mwanaume mwenye ndoa. shemeji ndoa haisikilizwi upande mmoja hata siku moja. sema ukweli ishu ilianzia nini hadi mshikaji akaanza mbele, kwanini alianza uhusiano nje ya ndoa na wewe ukiwepo? kuna mahali ulicheza mwingine akafungua uwanja na anampelekea mzigo wa akili. tatizo lenu mnajisahau mnadhani mkishazaa basi huyo kafika wanaume wengi hatuko hivyo tunahitaji faraja na upendo. kama jamaa alikuwa akirudi home unamnyongea mdomo unakuwa mchafumchafu unategemea nini? kama yote hayo hukufanya basi jamaa ni mtu wa fasheni itakuwa wewe fasheni yako imepita so kiufupi tulia usimpe mambo hata alie vipi labda mkapime tena mara tatu. na siku zingine zijazo jamaa akirejea kaza buti wanaume wanadekezwa sana. vei sori kwa hadi advice

    ReplyDelete
  31. HEH, DADA YANGU TUKIA NIKUOE USHAURI
    HUYO MUME WAKO ANATAKIWA KIZINGULIWA, HUKO KWA BI MDOGO AMEFUNGWA MACHO, MDOMO NA MASIKIO NDIYO MAANA HAMUELEWANI.
    MIMI MUMU WANGU ALIFANYIWA KAMA HIVYO NIKAMWENDEA KWA MTAALAM AKAMZINGUA.
    SASA HIVI ANACHOKIFANYA NI KILE NINACHOSEMA MIMI. AKITOKA KAZINI BAADA YA KAZI NDANI. NIMEMTOA HAMU YA KUPENDA MAHAWARA.
    SASA ITABIDI TUWASILIANE TUMSHUGHULIKIE KISAWASAWA, HAO WANAUME HAWANA UJANJA.

    ReplyDelete
  32. dada, pole sana!..mimi mtazamo wangu ni tofauti kidogo..ENDAPO YAWEZEKANA, wewe kuwa mpole na kubali yaishe - muhimize jamaa amuoe mwenzio huyo mara moja!..we utabaki daima kuwa mke mkubwa, na haki zake..na utakuwa umethibiti haki zako vema..

    ReplyDelete
  33. Bull shit!
    sijui mimi akili yangu mbovu au vipi?
    mtu hawezi kuniambia tulale kila mtu kitanda chake halafu nitegemee kurudi kulala nae, hiyo ni dharau ya mwisho kukuonyesha, wewe ni mke wake na si hawara au hawara umeficha? maana heshima ya mke na hawara tofauti kuna vitu unajeuri ya kumwambia hawara lakini mwanamme kweli hathubutu kumfanyia mke wa ndoa.
    ushauri wangu hapo mi ndo kwaheri tutagawana mpaka mabati ya nyumba, niradhi nikafe njaa kuliko kuishi na mwanaume mwenye dharau. NEVER!

    ReplyDelete
  34. sijui kama hi nistory ya kutunga tu ili kuona watu watajibu nini au ni yakweli,kama ni ya kweli basi kwanza nisikitike na ba baadhi ya watu wengine wanao ongea UTUMBO hapa wakati kuna tatatizo kubwa.
    kuvunjika kwa ndoa kunaleta madhara makubwa kwa mtoto/watoto!! maana wana athirika kisaikolojia na kiumla mwisho wa maisha yao unakuwa mbovu tu hata kama watafanikiwa kifedha!nazungumza ninacho kifahamu sio kuwa nababaisha. kwa hivyo wanao shauri kuvunja ndoa MKOME KABISA maana you don't know what a hell you are creating for innocent children who don't know nothing about your problems in marriage iwe ni kuto ridhika na tendo la ndoa kwa mume au mke au anything,wao wanachoona ni baba na mama wanaingia chumbani and that is all. hivyo wazazi wana wajibu wala sio hiari ya kulinda na kutoa haki wanayostahili watoto kuipata hadi watakapo kuwa watu wazima kama ni kuachana ndipo muachane.
    tambueni kwamba wengi wa watu ni wahanga na wameathirika na jinsi ya malezi waliyo lelewa,mnacho kiona jujuu ni lele tu za tatizo kubwa ambalo mizizi yake iko rooted deep down in sub-conscious level.na wengi wanahitaji ushauri nasaha ili waweze kutoka ktk dimbwi zito na kuathirika waliko kwisha athirika tayari.
    wengi wamekulia ktk ndoa mbazo baba wa nyumba akiingia ndani watoto wanafyata mkia,na wengine wamekulia ktk ndoa zilizo vunjika, so they end up with children with broken hearts,broken life with a broken future(hapa sizungumzii fedha)!!mnaona matatizo yanayo zikumba jamii mnadhania ni matatizo yanayotokea bahati mbaya,yana mizizi yake mbali sana!si mashuleni,si ktk siasa mnaona watu wa ajabu ajabu wasio jali wasi na utu wala huruma kwa maisha ya wengine mnadhani ni mambo ya bahati mbaya tu?hicho ni kivuli cha uvundo uliokuzwa ndani kusiko fikika kirahisi,na hata wao hawajitambui pia kuwa wanashida.
    mwisho nikushauri tu utambue kwamba una deal na monster sasa! unapaswa uwe na busara kwa kila hatua utakayo chukua,ila lengo liwe moja,nalo ni kuhakikisha ndoa inaendelea.

    mdau-ughaibuni masomoni

    ReplyDelete
  35. NASHUKURU WADAU!
    point zimenigusa sana tena sana na nimesoma kwa makini ushauri wenu nimerudia mara mbilimbili. Nitajaribu kufuata ushauri mlonipa ule ambao naona unafaa.
    siwezi kuelezea kiurefu kiasi gani mmenisaidia ila kwa ufupi ahsanteni sana na kuna bahadhi ya ushauri umenigusa zaidi nilikuwa gizani sasa naona nuru inakuja na mmenipa moyo
    ahsanteni sana na mungu awazidishie.
    ni mimi ninayeteseka na mume wangu aliye nipenda sana miaka 5 iliyopita thanks

    ReplyDelete
  36. Nami nachukua nafasi kumpa pole huyu dada na pia kuungana na wanablog wengine kutoa ushauri wangu.Kwa kiasi fulani naungana na ushauri wa anony wa Aug 27 saa 02:04 pm na saa 02:54 pm. Dawa ya mwanaume kama huyo ni ndogo japo ni ngumu na yahitaji uvumilivu,mwanaume kama huyo haitaji vikao, vikao vitakuwa ni tiba ya muda tu lakini hataacha kabisa. Namshauri huyo dada ajifanye hana muda na hababaiki na huyo mumewe, ajitahidi kuwa smart(msafi) muda wote, avae nguo nzuri zinazompendeza kila siku, na ajitahidi kutoka kila mara ikiwezekana kila siku, ajitahidi kujifanya ana furaha sana kila siku,kama ana simu ajitahidi mara kwa mara kufanya mawasiliano ya sms mumewe akiwepo akijifanya kuficha mawasiliano anayoyafanya na zaidi ya hapo amtafute ndugu yake au mtu yeyote na mtu huyo awe anampigia simu dada huyu mumewe akiwepo na dada huyu ajifanye kumkwepa mumewe wakati anaongea na hiyo simu na maongezi yawe marefu kidogo.Ajaribu kufanya hivyo kwa muda wa mwezi moja tu kama kweli mumewe bado ana mapenzi naye ataona matokeo yake, nina uhakika mumewe atarudi kwa spidi ya ajabu ila asimkubalie akomae kabisa kana kwamba hana haja naye, akiona jamaa yuko serious ndipo amuitie watu hususan ni ndugu wa pande zote mbili na kutafuta suluhu.Kama njia hiyo haitafanikiwa tafadhali namshauri huyo dada aanze kuangalia maisha mapya bila ya huyo mume hapo MAPENZI yameisha na huwezi kulazimisha ndoa pasipo na PENZI,na kama hakuna wivu jua PENZI limeisha.

    ReplyDelete
  37. DADA NINAPENDA KUKUAMBIA UMEAMBIWA MENGI SANA LAKINI ZINGATIA SANA YALE YANAYOSEMA USIONDOKE.

    NAPENDA KUKUPAUSHAURI MMOJA.
    NILIKUWA NA DADA YANGU, MUME WAKE ALIPATA MTOTO MDOGO AKAWA KILA SIKU ANAMWOYESHEA DADA KWA MAKUSUDI VITU MBALI MBALI MARA PICHA ANAJIFANYA AMESAHAU KWENYE GARI, LAKINI DADA ALISIMAMA KIDETE HAKUONDOKA KABISA YULE BABA ALIONDOKA YEYE KWA MIAKA KATAA LAKINI BAADAYE ALIMKUMBUKA MKE WAKE NA WATOTO AKARUDI. DADA WEWE MDHARAU USIMUHULIZE WALA USI MWAMBIE MCHUNGAJI WALA MSHENGA. NDOA NYINGI ZINAZOAMULIWA AMULIWA NA WATU SIO NZURI. USIMWANGALIE KWA DHARAU WEWE MSALIMIE KAMA KAWAIDA ILA UCHI WAKO STOPISHA KIDOGO MPAKA HAOMBE MSAMAHAA. USIPOMWAMBIA CHOCHOTE UKAWA UNAMSALIMIA KAMA KAWAIDA YEYE MWENYEWE TUU ATAKUOMBA MSAMAHAA KAMA UNATABIA YA KUMWEKEA CHAKULA WEWE MWEKEE TUU LAKINI ENDELEA KULALA KULE KULE. USHAURI WANGU NIDO HUO. MWOMBEE AMKA SAA KUMI AU 8.00 SALI. ACHANA NA WASHAURI WANAKUAMBIA UONDOKE. PIA ACHANA NA SIMU ZAKE.

    ReplyDelete
  38. DAH POLE SANA DADA,
    TATIZO NA NYINYI DADA ZETU SOMETIMES MNATUROGA ILI TUWAPENDE SANA, INAWEZEKANA HUYO MUMEO ALIJARIBU KUONJA MALA MMOJA TU BASI DADA AKAENDA KWA SHEKHE YAHAYA KUMUWEKA SAWA.KISHA VILEVILE HATA HAYA MATATIZO YANAPOHADITHIWA NA UPANDE MMOJA UNAKUWA HAUYAPATI SAWASAWA MANAKE CD INAKUWA INARUKA RUKA, KWASABABU KUNA MDAU MMOJA HAPO JUU KAELEZEA KISA CHA MSICHANA ALIEYEZAA NAE. TATIZO NA NYINYI DADA ZETU HUWA MNAJISAHAU SANA PINDI MKIPENDWA, HUWA MNAJINA NDIO KILA KITU, SASA UNAKUTA HATA MAMBO MUHIMU ULIYOKUWA UNAMPATIA BABA WATOTO UNASITISHA, SASA AKITOKA NJE NA KUKUTANA NA WADADA WENYE MALEZI YA KITANGA KAMWE HARUDI NDANI, NA UKIONGEZA DAWA ZA KARUMANZILA NDIO KABISA.
    sO USHAURI WANGU NI KUPIGA BONGE YA MAOMBI TENA UTUO SADAKA KWA MAYATIMA WADOGO KWA MUDA WA SIKU 7 MFULULIZO KISHA RUDI KWENY GLOBAL YA JAMII KAMA M/MUNGU ASIPOMREJEA NIJULISHE.MANAKE M/MUNGU HANA SIFA HIZO.

    ReplyDelete
  39. Pole sana kwa yaliyokupata, najua utakuwa unaumia moyo lakini usiache moyo ukavunjika.
    Napenda kukujulisha kuwa mume anayerudi nyumbani ni wako, kwani ni wangapi waliokuwa wazi na mahusiano yao ya nje na wakatokomea huko bila hata kujali watoto?
    Huyu anadiriki kukuambia tujadiliane juu ya watoto!!!!!!!???? Huyo bado ni wako.
    SASA, jaribu kuangalia wakati ule mna maelewano alikuwa anakulalamikia nini? kama ni kitu unachofikiri unaweza kurekebisha taratibu na kimyakimya wewe fanya hivyo, binadamu wengine tumeumbwa na visirani vya kila aina na ukiona jambo lako halitimizwi basi unazira na kufanya mambo kinyume. Hisia zangu ni kuwa huyo bwana amezira tu lakini anakupenda.
    Kwa ushauri zaidi mdogo wangu tuwasiliane kupitia ambwene65@yahoo.com

    ReplyDelete
  40. kweli ndoa ni ngumu sana mi naona siku ya kuimbiwa anameremeta ndo tamu kuliko zote ila fukuto likianza humo ndani dunia unaiona haina maana dada pole sana hiyo kitu haivumiliki maumivu ya pendo ni tofauti na kidonda manake unaumia ndani sana na madhara yake ni makubwa hapo penzi lishachuja kama tui la mwisho jiondokee tu na huyo miss aje ndani tuone kama wataishi milele siku moja atakuja kukukangukia tu ingawa wanaume wengine ni wagumu mno sasa huyo wakwako kumuuliza tu kwa upole kama ana mahusiano kafyumu lala chumba chako ukimuuliza tena ishu nyingine utaambiwa uame kabisa shosti songa mbele achana na huyo mwewe wewe unakonda yeye ananenepa juu ya nini maisha mafupi mama chukua na wanao kabisa bila kusahau kwenda ustawi wa jamii ili atunze wanae

    ReplyDelete
  41. mini ninaona huyo bwana lazima akapimwe ukimwi before asamehewe. pole sana bibie mume wako pendo lake kwako limekwisha toweka. hata kama mtapatanishwa huyo mume wako ataendelea kuwa na mapenzi na wanawake wengine. just imagine alivyo mjeuri ati alikuuliza unataka nini na kuamua kwamba mlale vitanda tofauti. huyo bwana amekuona kuwa ni mjinga sana ndio sababu ulikubali. mimi ninakushauri ni afadhali uondoke kabla ujapata ukimwi. kubali kumeza machungu sasa kuliko kupoteza maisha yako.

    ReplyDelete
  42. narudia tena,kwamba watu wanaokupa ushauri wa kuondoka ni watu wenye mawazo finyu,na wengi watakuwa hatakama wamekwenda shule shule haija wasaidia na hawaja eleimika. maana wao wanacho tizama ni faida tu za hapo kwa papo lakini wanasahau kwamba hiyo ni familia yenu,yaani wewe,mumeo,na watoto! sasa wanapo kwambia ondoka urudi kwa wazazi wanategemea wewe bado ni mtoto mdogo? wanatambua kwamba watoto sio tu wanahitaji mahitaji ya kawaida kama nguo,elimu,afya mavazi bali pia wanahitaji mahitaji muhimu ktk makuzi yao kama vile upendo wa baba na mama,mfano bora wa maisha,malezi ya kiroho n.k vitu ambavyo vitawafanya wakue ktk muelekeo bora wa kibinadamu.
    huenda watu hawa wanaoshauri kuachana wengi ni watu waliojaa uswahili(sio kwa maana ya utanzania)yani tabia za kutenda kwa mikumbo bila reasoning na kupima matokeo ya madhara kwa kuangalia vigezo vingi!
    historia inanionyesha watoto walio lelewa bila upendo wa wazazi wengi wao wamekuwa wa ajabu na wakatili,mfano ni adolf hitler.shaka zulu n.k
    sasa nakuomba upuuze ushauri wa watu wanaokwambia beba watoto uondoke,hapo utakuwa huja tatua tatizo ila umeliahirisha na kuanzisha jingine kubwa zaidi kwa wanao.
    chakufanya kuna njia mbili za kuushinda ubaya wa binadamu,nazo ni:-
    1.kuushinda kisheria,njia ambayo sikushauri kuitumia kwa sasa.
    2.kuushinda kwa kutenda wema! hii ndiyo njia ninayo kushauri kuitumia. japo inaweza kuchukua muda mrefu kuona matokeo yake lakini matokeo yake ni mazuri na bora zaidi kuliko unavyoweza kufikiri.
    cha nyongeza tu ni kuwa makini ktk kushiriki naye tendo la ndoa kama atahitaji,hakikisha unajikinga na kumshauri mkapimwe afya kabla ya kuendelea bila kinga.
    kama utaona anakuwa agrssive na kutishia usalama wako basi hapo itabidi utumie njia ya kwanza,hadi atakapo acha kuhatarisha usalama wako ndipo unaweza kurejea njia ya pili.
    ila ushauri wa kuondoka au kufanya vitimbi ili apate wivu ni ushauri potofu ambao unaweza kupelekea ktk matatizo makubwa zaidi kwa baadaye.uwe mpole na mwerevu ukizingatia usafi na kupendeza,muombee mema na mafanikio hata akiwepo pia!zungumza na watoto kwa upole kuhusu jinsi baba yao anavyoipenda familia yake na jinsi alivyokuwa mtu mzuri wakati akiwepo na anasikia. hayo ni mambo ambayo yatakuwa yana mkumbusha awali na kumuumiza kila anapoyasikia yakizungumzwa kwa upendo na uplole.
    lakini kumbuka kwamba kama hayaleti matoeo usikasirike bali uwe mvumilivu. maana kama nilivyosema watu wana background za ajabu ajabu,ndio maana utaona hata wengine wanazaa na kutelekeza watoto si wanaume si wanawake!!kwa kuwa sio wazima,hivyo wewe uliye mzima usifuate njia zao!

    mdau-ughaibuni masomoni

    ReplyDelete
  43. Yaani nilicomment lakini imebidi ni rudie tena!!kwa sababu comment za watu zinachefua !!!hivi kwa nini wanawake tunakuwa tunaonekana kama tuna akili za watoto, eti mtu anashauri kuwa uwe mtulivu ,upendezee blah blah blah!!!halafu mpime afya zenu!!hivi realisticly mtu keshakwambia ana mwaname halafu wewe mkewe ujipambe kwa ajili yake??na yeye anaondoka anaenda kwa bibi yake???umuneshe mapenzi??wakati yeye anaenda kuyaonesha kwengine???nadhani hapo juu kuna dada amesema mama yake alivumilia na akaletewa ukimwi kwa ushauri wa aina hii hii ukimwi hautoisha tz !!! utamaduni wa mtanzania unamuongezea mwanamke matatizo eti ukiachika ni aibu!!kwa hivo hata kama mwaname ,mumeo anabehave like jerk inabidi umgh'ang'anie ujirembe usiwe jeuri ili abadilike!!!kwa kweli hii hata mtoto wa miaka kumi hawezi kuikubali ukimuambia!!cha muhimu mwanamke hasa mke anastahiki heshima kama mwanamme, kwa nini nijirembe ,nijipendekeze na penzi langu mume analiweka rehani!!!???wake up people!!especially kina mama, tusikubali kunyanyaswa kwa ajili ya kasumba!!!jirembe akirudi kwa bibi yake akuletee ukimwi!!

    ReplyDelete
  44. anon wa aug 30 saa12:47pm nakushangaa kwa sababu wewe unataka kulazimisha vitu ambavyo wakati mwingine havipaswi kulazimisha. kwa maana ungetaka kila kitu kiwe kama unavyotaka nadhani basi hata masikini wasingekuwepo duniani pia na wanaishi miongoni mwa matajiri hata kama ni ndani ya new york marekani.
    hebu jaribu kuangalia hata nchi zilizoendele na zenye utawala mzuri wa sheria kwa mfano marekani,unadhani matatizo ya kindoa hawayapati?na kwa wale wenye jeuri kama unayomshauri huyu dada kuifanya unajua matokeo ya ndoa zao? sasa ona jamii ile ambayo ilipaswa kuwa civilised watu wake walivyo,ni watu ambao kila mtu anajali life yake tu na hana time na mtu mwingine!sasa hayo ndiyo matokeo ya jamii inayotokea baada ya thamani ya kutunza ndoa inapotoweka ktk jamii yeyote dumiani. zile jamii ambazo bado zinaheshimu ndoa kama india,china,hebu angalia jamii zao kisha ulinganishe na jamii zenye jeuri ya kila mtu ana haki sawa kama marekani utaona tofauti kubwa.
    kumbuka kwamba kuishi hakutegemei nguvu na jeuri ya pesa tu!!angalia kwa haraka wanawake wa ki afrika ambao wakisha soma kisha wakawa malimbukeni wakadhani ndoa inaendeshwa kama chama cha siasa wengi wao wanavyoishia,ama atachelewa kuolewa hadi jeuri ikiisha anaolewa akiwa mzee wakati amesha gundua kuwa ni ubatili mtupu,au anaolewa kisha anaachika na matokeo ndiyo kutengeneza jamii za ajabu ajabu.
    kumbuka kwamba ndoa ni institution iliyowekwa na mungu na siyo mwanadamu,na hiyo ndiyo tofauti kati ya institution zilizo anzishwa na mwanadamu kama vyama na zilizo anzishwa na mwenyezi mungu kama ndoa, it is a HOLLY thing.sasa kama linatokea tatizo lazima mmoja akubali kujishusha ili kuilinda kwa garama zote. that is when when you take the marriage vow you say FOR BETTER OR FOR WORSE!kwa hivyo kama sasa imetokea kwa huyu dada kwa situation yake yeye ndiye anakabiliwa na tatizo na ndiyo maana anashauriwa yeye atumie busara zote kuilinda ndoa na siyo swala la unavyoliona wewe la win win thing! sijui kama umeolewa/umeowa lakini hili wapaswa kulitambua.
    hakuna anaye shabikia wanawake kunyanyaswa,lakini unapokuwa umesha ingia ktk ndoa na mume anataka kukunyanyasa basi kunanjia mbili za kutatua migogoro,ama za kisheria ama za kidini sasa hapo unapaswa kutumia busara ni wakati gani utumie njia ipi. na kuvunja ndoa inakuwa ni hatua ya mwisho kabisa kama imeshindikana na kuona kwamba mmoja anahatarisha maisha ya mwenzie,hata kama ni mama anahatarisha maisha ya mwanawe basi hao wanalazimika kutenganishwa kama last solution.
    basi na uwe mwenye busara usiwashauri wengine kuingia ktk matatizo ambayo wakati yatakapo tokea wewe hutakuwepo,na hata watakapo hitaji msaada wako utwacheka pia na kuwafumbia macho!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...