Globu ya jamii imebarikiwa kuwa na washauri wa hiari kibao wanaoisaidia sana kwa mawazo na mawaidha ili kuendeleza libeneke. mmoja wao ni Mh. Patrick Tsere (pichani akiingia kwenye mnuso mmoja na mai waifu wake), ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala mstaafu.

Globu ya jamii inatoa shukrani sana kwa Mh. Tsere na washauri wa hiari kama yeye kwani mchango wao katika kuendeleza libeneke si haba.
Wapo washauri wa hiari wengi kiasi na si rahisi kuwataja wote, ila kwa uchache ni kama Mwenyekiti wa Wazee Club ya A-Taun Danford Mpumilwa pamoja na Suk Chat, Beda Msimbe wa TSN, Charles Hillary wa BBC London, Mwamoyo Hamza na Khadija Riyami wa VOA na Dr. Licky Abdallah.
Wengine ni Tony Barreto, Blandina Kilama, Narendra Gajjar wa Canada, Matina Nkurlu na Rukia Mtingwa wa Vodacom, Jackson Mbando wa Tigo, Kelvin Twissa wa Zain, David Kyungu, DJ Luke, Aboubakar Faraji, Aboubakr Liongo wa DW, Asia Idarous, Auntie Dotnata, Michuzi Jnr na bila kumsahau mdau wa nanihii Freddy Maro.
Kama nilivyosema washauri wa hiari ni wengi mno kiasi hata kuwataja wote si rahisi. Hivyo nisiowataja naomba wajihisi nimefanya hivyo kwani natambua mchango wao na nitaendelea kuwataja kadri nafasi itapojitokeza.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Duuuuuh!! Hata mimi hujanitaja??? mimi natakiwa ningekuwa mtu wa pili au wa tatu kutajwa....

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi,, Hiyo taswira imekaaje huyo mueshimiwa ndo alivyo au,,

    Mdau,, Malaysia

    ReplyDelete
  3. Ndugu mdau wa Malaysia nahisi ni angle ya mpiga picha ni kama vile kaipiga ile picha kutokea juu. Kwa nini hakuipiga kivinginevyo atajua yeye mwenyewe mpigaji.

    ReplyDelete
  4. Brother Michuzi hivi huyu mheshimiwa siku hizi yuko wapi na anafanya shughuli zipi. Maana namkumbuka jinsi walivyokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kandoro, timu yao ilikuwa nzuri sana. Migogoro iliyokuwa inajitokeza Ilala huyu bwana na Kandoro walifanya kazi nzuri ya kulishughulikia. Kwa mfano wamachinga katikati ya jiji la Dar, mtaa wa Nyamwezi, Congo, Tandamti kuzungukia eneo la Soko la Kariakoo wakuu hao waliweza kuwabana manispaa ya Ilala wakatekeleza wajibu kisawasawa.Wamachinga walitoweka. Hali ilivyo sasa? Kama vile hakuna uongozi. Aidha mgogoro wa Tabata Dampo waliibana Halmashauri mpaka Mkurugenzi wake Bw. Lubuva akaondolewa. Hizo ndizo zilikuwa enzi za Kandoro.

    ReplyDelete
  5. Mzee mwanakijiji, kama ni wewe kweli. Kandoro alikuwa mchapa kazi hasa. Na alijenga jina kwa kasi sana nafikiri kuna baadhi ya watu walikuwa karibu na mkulu wakampa yellow kadi, kuwa jamaa anakuja kasi.

    Ila siasa ndiyo zilivyo, kuwa mkuu wa mkoa wa Dar ni rank ya juu sana kwa uongozi wa Taifa maana wewe ni rais wa mkoa ambao hata rais wa nchi anaishi, hivyo basi kila maamuzi unayofanya yanatakiwa kuwa makini maana "you are closely wathched" Ila tuache longolongo Kandoro aliliweza jiji hasa. Sasa kilichomfanya mkulu akamuhamisha anakijua yeye mwenyewe ila kwa sisi wananchi wapenda wawajibaki bado hatuja pata jibu. Kwa kuwa yeye ndite aliye mteua basi sisi wengine tusihoji sana, ila ukiteua mchapa kazi sifa zinakuja kwa mteuzi kwa kuwa makini.

    Ila huenda Mwanza napo kuna kama yaliyokuwa Dar sasa huenda kupelekwa kule ni katika kuboresha baada ya kusafisha njia Dar.

    Nakumbuka wakati nipo Kazima secondary alikuwepo headmaster mmoja alikuwa naitwa Wilson Mbanga, huyu bwana alikuwa ni kiongozi mzuri sana, shule akiishika hata kama ili ovyo ovyo ni mwaka mmoja tu utasikia Division one sabini. Kilichokuwa kinafanyika ni kuhamishwa hamishwa kupelekwa shule zilizoshindikana kama Tosamaganga, etc.

    ReplyDelete
  6. Mzee Wa Zeze, New Albany, OHIOAugust 24, 2009

    Bila kunisahau mshauri mwandamizi wa mambo ya mafisadi na ulaji ovyo wa mali za wananchi wanyonge, MZEE WA ZEZE nawakilisha.

    ReplyDelete
  7. Huyo jamaa wamemharibia reception yake. Mashavu yameshuka down kwa sababu ya upigaji picha mbovu. Vipi Mzee Michuzi kwa nini hukuchukua tender hiyo??

    Mdau Cassablanca, Morocco

    ReplyDelete
  8. michuzi unanikumbusha hadithi fupi ya 'ndoto ya amerika' ambapo mhusika mmoja badala ya kusema 'marekani' anang'ang'ania makerani'.
    Sasa sijui kama 'blogu ya jamii' siku hizi imekuwa 'globu ya jamii'. mbona hukututangazia rasmi mabadiliko hayo!

    ReplyDelete
  9. Ndio maana Luciano Mfupi! Watu wenye akili na hekima zao..hongera Michuzi!

    ReplyDelete
  10. hahahahahaha, sikuwa hata nahitaji ku-coment kwenye hili lakini imenibidi.
    Nimefurahishwa sana na mchangia mada wa 03:50:00pm, kweli nimekukubali uko smart sana, sizani kama kuna mtu mwingine alishtukia hilo.

    Uncle misupu tupe jibu la mabadiriko ya jina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...