Mwenge wa uhuru ukiwasili katika kata ya Kawe,viwanja vya Tanganyika Packers jana jioni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Jordan Lugimbana akizungumza na wakazi wa kata ya Kawe waliofika kuupokea Mwenge wa Uhuru jana jioni

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Jordan Lugimbana akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru jana jioni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, kata ya Kawe, Kinondoni jijini Dar. Mwenge huo ulilala katika viwanja hivyo na kuondoka leo asubuhi.
Mwenge wa uhuru ukilindwa kwa heshima zote



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Sisi,
    Tunataka,
    Kuwasha mwenge,
    Tunataka kuwasha mwenge,
    na kuuweka
    juu ya mlima
    mlimaaaaaaaaaaaaa
    kilimanjarooooo
    kuwasha mwenge
    kuwasha mwenge
    nakuuuuweeeeekkk
    kilimanjarooooooo....

    ReplyDelete
  2. ...Umulike hata nje ya mipaka yetu,
    Uleteeeeeeeeeeeeeeeee tumaini.
    Pale ambapo hakuna matumaini,
    Upendo mahali ambapo pana chuki,
    Na heshimaaaa ambapo, pamejaa dharau

    ReplyDelete
  3. Umulike nje ya mipaka yetu uteletee Tumaini,
    Pale ambapo hakuna matumaini,
    Upendo mahali ambapo pana chuki,
    Na heshima ambapo pamejaa dharau

    ReplyDelete
  4. hivi huu upuuzi wa mambo ya mwenge bado upo,
    ni moja ya ujinga wa watanganyika.

    ReplyDelete
  5. Kaka nakumbuka mika ya 80 nikiwa pale mshiri(marangu) tuliamka saa 11 alfajiri tunaelekea marangu mtoni kuuona mwenge, cha ajabu jamaa walipita kimyakimya mida ya saa12unusu, wakatuacha tunakodao macho tunasubiri mwenge,akatokea mshikaji akasema jamaa wameonekana himo,tukarudi zetu migombani kwa upole, toka siku hiyo sina hapetaiti ya kuuona mwenge tena

    ReplyDelete
  6. Mwenge wa Uhuru maana yake nini kama hauwezi kuyamulika mafisadi sugu hapo bongo! Kama mambo yataendelea ya kuibiwa wachache basi huu mwenge uzimwe na nchi isipoteze pesa zaidi ktk mbio hizo.

    ReplyDelete
  7. Alas!! huu mzimu wa nyerere bado unagubiaka Tanzania. acheni mambo ya Kishirikina hayooooooo!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. I miss CHIPUKIZI activities jamani. Enzi hizo wimbo hapo juu kama sala ya asubuhi. Na ule Naapa naahidi mbele ya chama mapinduzi nitakulinda mpaka kufa.. Natoa hii ahadi kwa moyo mkunjufu nitalinda mipaka yote ya nchi yanguu............ Viwanja vya Kaitaba Bukoba...

    ReplyDelete
  9. Wadau, bila kutania wala nini naomba niulize.
    Hivi mwenge kweli sasa hivi ni wa nini? I mean una message ipi? Unaitwa mwenge wa uhuru..na almost miaka 50 tangu uhuru upatikane.
    Naomba kuna mtu anajua ni nini hawa watu wanazongusha mwenge wanatoa message ipi?

    ReplyDelete
  10. Mwenye huo mwenge, mbio mbio.Mwenge tunaukimbiza, mbio mbio.Mbaka makao makuuuuuuuuuuuuu mbio mbiooooooooooo.

    It is just part of good tradition.Watu tusijifanye huu ni upuuzi it is what makes us.It will be a sin to ditch our good old tradition of mwenge pps.

    ReplyDelete
  11. mwenge huohuo mwenge mbio mbio mwenge tunaukimbiza mbio mbio....kwa upande fulani ni kijifani fulani nakumbuka mwenge ulikuwa ukitangaziwa kuwa utapita kijijini kwetu basi shuleni tunajiandaa wiki nzima kwajili ya kuupokea mwenge kwa nyimbo mbali mbali...lakini kwa upande mwingine hizo hela za kukimbizia mwenge zingetumika kwenye matatizo mbali mbali hakuna faida kukimbiza mwenge na ujumbe ni ule ule kila siku na ujumbe wenyewe hauleti maana mafisadi kila kona mwenge haumuliki mafisadi unamulika wenye njaa tu ....mdau uholanzi

    ReplyDelete
  12. Mambo mengine inabidi yawekwe pembeni jamani!! Mpaka sasa Mwenge unapitishwa mikoa yote aiiiiiiii!Badala ya hizo pesa za mafuta ya mwenye kujengea barabara au kuboresha huduma nyingine za wanachi.....tunajua kuwa mafuta yamepanda bei kwanini lakini hii serikali yetu jamani....

    ReplyDelete
  13. Inasikitisha kuona maelfu ya watanganyika wakiwa wanakabiliwa na njaa,wakiwa hawana kazi na makaazi,watanganyika hadi hii leo wanafika baadhi yao kulala sakafuni walazwapo mahospitali.Watanganyika walio wengi hawana uwezo wakula mlo zaidi ya mmoja kwa siku.Viongozi wa Tanganyika hawalali majumbani mwao kutwa kucha wako ughaibuni kubembeleza na kuomba wapatiwe misaada.

    Lakini cha kushangaza watanganyika hao hao wanapoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuurandisha mwenge nchi nzima.huu ni ujinga ulioje.

    Cha kusikitisha ni kuwa hadi saa bado watanganyika wengi tu wangali wakiwa na kasumba kuwa mwenge utangarisha mipaka yao,pia mwenge huo utaondosha chuki.

    Watanganyika hakika mnasikitisha sana.hii ni karne ya 21 amkeni nyinyiiiiii..mtalala mpaka lini??????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...