Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea taarifa kutoka kwa Mdhibiti naMkagu Mkuu wa Serikali (CAG), Bw. Ludovick Uyouh kuhusu tuhuma za ukusanyaji wahovyo wa mapato katika soko kuu la Kariakoo , ofisini kwake jijini Dar leo.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo (Jumanne Agosti 25, 2005) amekabidhiwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyoiagiza kuhusu tuhuma za ukusanyaji ovyo na ubadhirifu wa mapato ya Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Bw. Ludovick Utoh alikabidhi ripoti hiyo kwa Mhe. Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam mbele ya Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Siasa), Mhe. Philip Marmo na (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Mhe. Celina Kombani.
Ripoti hiyo inafuatia nyingine ya aina hiyo iliyotolewa na Bw. Utoh kuhusu Kituo cha Mabasi cha Ubungo aliyokabidhiwa Waziri Mkuu mjini Dodoma mwezi mmoja uliopita (Julai 28).
Akipokea ripoti kuhusu Soko la Kariakoo, Mhe. Pinda alimpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi aliyoifanya na kuahidi kuwa kilichomo ndani yake kitafanyiwa kazi na serikali haraka iwezekanavyo.
Katika ripoti zote mbili, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliainisha matatizo na kutoa mapendekezo ya kurekebisha hali ilivyo ili kuiboresha.
Waziri mkuu aliagiza ufanywe uchunguzi (Kwa Kiingereza: Performance Audit) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu mapato na matumizi ya makusanyo ya Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko Kuu la Kariakoo ili kuboresha mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Pinda alitoa maagizo hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akiwahutubia viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake ya siku nne ya mkoa huo Machi 15, mwaka huu ya kukagua usafi na mazingira ya Jiji.
Waziri Mkuu alibaini, pamoja na mambo mengine, kuwa Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko Kuu la Kariakoo ni maeneo mawili ambayo yangeingiza mapato makubwa kwa Jiji, lakini ukusanyaji wake ni wa ovyo na kuna tuhuma za ubadhirifu.


CCM waache longolongo mbona ripoti ya Kkoo imetka kabla ya standi ya mabasi Ubungo wakati maagizo ya ripoti ya Ubungo yalitolewa kabla ya Kkoo?
ReplyDeleteNajua utabana hii
Na huyu Mkuu anatupotezea wakati,Ripot anazoomba nizanini? Mbona atuoni utekerezaji.
ReplyDeleteKudai performance audit ni muhimu, hasa kwenye maeneo yanayoshutumiwa, lakini kutekeleza,kuwa na uamuzi,uthubutu na kuchukua hatua ya yale yaliyopendekezwa au mapungufu yaliyogunduliwa ni muhimu zaidi, tena sana.
ReplyDeleteJamani, ni karibu miezi imepita tangia ripoti ya Ubungo itoke,tena kwa mbwembwe na tahaluki,kimya kimetanda diii,hakuna chochote kilichofanyika,hata kauli tu,sasa hii ya kaliakoo,mbwembwe kibao,ripoti ndani ya kitambaa cha blue utafikiri birthday.Jamani!
Nafikiri sababu zilizoleteleza kufanyika kwa auditing hii ni ubadhilifu,ni kero,ni kilio cha wanyonge,kama publicity ni lazima,basi ripoti ingefungwa kitambaa cheusi kuashiria machungu,badala yake kitambaa kinaashiria shangwe, nderemo na vifijo.
Performance auditing,evaluation of program's effectiveness and outcomes ,performance appraisal etc,reflect different forms of operational research.Effective Operational research should be translational.
How these costly auditing findings have been translated into operation,to putting those who mishandled the tax-payers money into justice, to improve the working environment and productivity of these organs is still at large if not questionable.
We better do nothing, than spending millions of citizen money for something we know for sure we are going not to use it.
Dont put it kapuni Mr Michuzi. The comment is intended to enlighten us the importance of translating what we discover in our research to better improve our working situation and public services.
Anon. wa kwanza, Ripoti ya Ubungo kwa kumbukumbu zangu (butu) nadhani ilishatolewa siku za nyuma. Ila tu sijasikiwa ikiongelewa ina nini na nini, hilo ndo lakusubiria pamoja na hii pia.
ReplyDeleteAnony was Aug 25 11:46PM
ReplyDeleteMbona ripoti ya Ubungo ilishatoka?? Naona kwenye serikali ya Kikwete, huyu CAG ni nomaaa. Ripoti zinatoka kwa muda unaotakiwa. Kabla ya Utouh kuingia kwenye hiyo nafasi, mimi hata sikujua kulikua ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali. Hao waliopita walikua hawafanyi kitu naona. Kuddos CAG!!
Wewe Anon wa 11:46 vipi? Sikuelewi. Kwa hiyo ulitakeje? Kwa sababu amri ya kufanya audit for Ubungo na Kariakoo zilitolewa wakati mmoja. Kwa hiyo ulitaka siku ile anaitoa ya Kariakoo na ya Ubungo itoke? Au? Tatizo nini si hiyo imetoka? Acheni hofu jamani. Kila kitu mna politicise aagh. Halindwi mtu hapa kama hiyo ndiyo shuku lako.
ReplyDeleteHicho kigugumizi cha Waziri Mkuu kitamtokea puani, kwani hata mwenzie aliyetangulia alianza na dalili hizihizi. Waziri Mkuu tafadhali usiogope mkwara wa Kinguge huko NEC Dodoma, wananchi tuna hasira naye kampeni zake za kutaka kuwaweka jandoni na unyagoni kuwahubiria hadithi za kale, akumbuke kuwa zama hizo zimeshapita na sasa tupo katika mfumo mwingine. Angekuwa na akili kama Mwl. basi angekaa kimya na hiyo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi iwekwe hazarani kwa manufaa ya umma. Tumenyonywa sana! Tumedhulumiwa sana! Tumekaripiwa sana! Tume...... sana!
ReplyDeleteKUMBUKENI MTAYACHELEWESHA WEEEEH LAKINI YANAMWISHO WAKE UTAFIKA TUUU!!
ninachozipendeee hizi reports za CAG Bwana UTOOOOOOOOO hi hiz GIFT paper na RIbbon, yaani zinanikumbusha zawadi za harusi na birthday.
ReplyDeletekweli report ya kiofisi nilitegemea ningewaona wamekaa chini Utoo ana mbrifu PM, kwa stail hiyo inaenda kuchanganywa na suvenia anazopewaga PM na ndo mwisho wake ndo maana ile ya UBUNGO imepotelea huko. Twendeni kwa kagame tukajifunze kuacha utani
Ni hakika sasa muda umefika tunataka kwanza tuone ile ripoti ya ubungo bus terminal kwani nina uhakika ina harufu ya UFISADI ndani yake na ndio maana inacheleweshwa kutolewa.
ReplyDeleteNina uhakika repoti ya ubungo ikitoka utakuwa ni mwisho wa fisadi KINGUNGE na hapo ndio tutajua pumba ni zipi na mchele safi ni upi,vinginevyo tutashindwa kumwelewa Mhs Pinda.
Au tuseme na Pinda ameanza KUPINDA?
Ni Tanzania tu ambapo ripoti ya kikazi hufungwa kama zawadi ya harusi au bethidei....kweli bongo tambarare!
ReplyDeleteJamani sasa hii kazi au besidei...Ripoti ya kazi inafungwa kama zawadi ya Bedidei??? Jamani?? hii mambo gani haya!!
ReplyDeleteInaonekana jinsi tunavyochezea hela za walipa kodi wa nyumbani na wanje.
Mzawa