WAZIRI Mkuu Mh. Mizengo Pinda ametoa salamu za rambirambi na pole kwawazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi 12 wa shule ya Sekondari ya Idodi mkoani Iringa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na ajali yamoto iliyotokea shuleni hapo usiku wa kuamkia leo (Jumapili Agosti 23,2009).
Katika salamu hizo, Waziri Mkuu amesema, kwa niaba ya Serikali nakwa niaba ya yeye mwenyewe binafsi, amesikitishwa na kuhuzunishwa sana natukio hilo na vifo hivyo na kuwaomba wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wamarehemu kuwa wavumilivu na wavute subira katika kipindi hiki kigumu chamajonzi.
Alitaka waliojeruhiwa katika tukio hilo watibiwe vizuri nao wapate ahueni haraka.
Chanzo cha moto huo hakijathibitishwa rasmi, lakini kuna habarikuwa huenda kikawa ni mshumaa uliowaka na kusahauliwa na mwanafunzialiyekuwa anajisomea usiku.
Katika tukio hilo la moto, wanafunzi 12 wamefariki dunia na 23wamejeruhiwa. Kati ya majeruhi hao, 14 walikimbizwa na kulazwa hospitaliIringa na wengine 9 walikuwa wakitibiwa katika kituo cha afya cha Idodi.
Maiti wamepelekwa hospitali Iringa kwa ajili ya kutambuliwa rasmikabla ya taratibu za mazishi.
Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.
Amin.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAA
Jumapili, Agosti 23, 2009


Jamani Mola we taifa la kesho hilo.Poleni sana wazazi mlio poteza watoto na wanandugu wote.Mungu wa rehema awatie nguvu.
ReplyDeleteSERIKALI WEKENI UMEME KWENYE MAHOSPITALI NA SHULE ZOTE ZA BWENI. NI LINI NYIE MTAONA AIBU
ReplyDeleteInasikitisha sana na kutukumbusha yaliyotoke kule shauritanga. Kwa kweli poleni sana. Mungu mwenyewe ndiye atakayewapa ujasiri na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha kuomboleza. Mungu awape nguvu na ujasiri, Japo mliwapenda lakini Mungu aliwapenda zaidi na jina lake libarikiwe. Amina
ReplyDeleteni wakati umefika kwa serikali kuwa serious na vitu kama smoke detector, fire alarm, fire exit, fire exitungishers na fire safety training kwa wahudumu na wahusika katika sehemu zote za public. hii ina maana ya shule, hospitali,mahakama, clubs, hoteli na sehemu nyingine zote zenye mikusanyiko ya watu. ajali huwa na kinga wakati mwingine.
ReplyDeleteinaniuma sana juu ya hivyo vifo vya hao watoto tatizo serikali inajenga majego ya kizamani mno (old stone age)
ReplyDeleteMwenyezi Mungu (S.W.) awalaze Pema Peponi.
ReplyDeleteKitu ambacho kinacho kinatatiza ni hizo tetesi kuwa walikuwa wanataka kujiokoa kukawa kuna mtu anazuia mlango amevaa koti limefunika uso akisema leo mtafia wote ndani, na kuwa wanafunzi walisikia harufu ya petroli. (KUTOKA KATIKA VYANZO VYA HABARI MBALI MBALI MFANO GAZETI MWANANCHI LA LEO tar: 24 / Aug. na CHANNEL TEN JANA) Je ni nani huyu mtu? na kwanini waliokuwemo nje kuokoa wasimkamate ? Inamaana kwamba hili bweni liliwashwa na mtu sio mshumaa ?
Wadau hebu tusaidieni kujibu mnaojua zaidi inashtusha sana !!???
**********************************
Mdau unaeilaumu serikali na kuishauri iweke Magari ya zima moto zote za public: shule, hospitali,mahakama, clubs, hoteli na sehemu nyingine zote zenye mikusanyiko ya watu.
Kumbuka kuwa nchi yetu pia bado ni changa kifedha, sidhani kuwa serikali itaweza kununua magari yote hayo na kuyaweka sehemu zote hizo, hebu fikiri tumia upeo wako woote Shule ngapi Tanzania tunazo za binafsi na za serikali kwa kila mkoa, naimani ni nyingi sana, hapo hapo cheki Mahoteli tuliyo nayo, Sehemu za starehe vile vile kama hotels a.k.a. Guest houses ni nyingi sana.
Mikakati hii ningependa kuwashauri kwa wale wenye uwezo pia na hao wenye kujenga mashule wafanye fanye utaalamu wa kuwezesha pia kununua magari ya zima moto na kuweka katika shule wanazojenga. Wenye mahoteli pia wanunue gari la zima moto na kuweka katika hotels zao kwaajili ya janga kama hili. Kwani naamini hasa hawa wenye mahoteli kununua gari ni jambo dogo tuu kwao. Uwezo wanao.
Hospitali za serikali wanunue serikali, Hospitali kubwa mfano Agakhan wanunue wenye hospitali. Mizigo mingine tunaitwisha serikali jamani tufikirieni.
We mdau unaesema kuwa Serikali iweke Umeme mashuleni. Kumbuka kuwa hiyo shule ilikuwa na umeme ila kama ilivyo taratibu za shule za bweni Baada ya Prepo (Muda wa kusoma) ile saa 2:30 hadi saa 4 au 5 ukiisha huwa wanafunzi wanatakiwa walale na wazime taa za bwenini. Si ruhusa kuwasha taa za bwenini baada ya hapo kama ilivyo taratibu za shule nyingi ndio maana baadhi ya wanafunzi wanaotaka kusoma huchukua hata simu au mshumaa na kujisomea ili asiwasumbue wenzie wanaotaka kulala kwa kuwawashia taa.
Hivyo hili sio kosa la serikali, ila ni kosa la taratibu za shule pia..
Jamani Serikali pia ni watu kama nyinyi pia nyinyi mnastahili kuisaidia Lini mtaacha kuilaumu serikali???
ReplyDeleteKaeni fikirieni na nyinyi mnaojenga Mfano Mahoteli, Mashule hakuna milango ya dharura mnafikiria nini?
We anon unasema Serikali iweke umeme kumbuka kuwa hiyo shule ilikuwa na umeme pia. Na hata kama haikuwa na umeme jua kuna shoti za umeme. Ingekuwa umeme vile hapo pia Mngeilaumu Serikali.
Fikirieni, nyinyi mnaopewa dhamana ya ujenzi wekeni milango ya dharura, na pia mnaojenga kumbukeni kuweka njia za walemavu sio majengo yoote kuwa na ngazi hakuna mahali mlemavu mfano wa baiskeli anaweza kupita.
Sipendi mnavyoitupia serikali lawama kwa baadhi ya vitu.
Mdau Mzalendo
Kwako kaka MICHUZI,
ReplyDeleteKwa kweli jpo blog ni yakwako lakini naamini kuwa blog hii umeifungua kwaajili ya jamii. Mimi unaniboa sana sana na sio mimi tuu ila pia baadhi ya watu wengine. Comments nyingine huziweki. Tunatuma comments hii ni moja ya kuonyesha nasi tunamchango wetu upi kwa jamii lakini hauweki maoni yetu.
Naimani hata mtoto anaweza changia ikiwa tuu maoni yake yasiwe yakuchafua hali yahewa yani ya matusi. Maoni ni maoni hata yawe yakijinga mwache mtu atoe maoni atakosolewa na wengine wanaotoa maoni.
Tunaomba maoni yetu uyaweke yote, usibague ya kuweka na yasiyo ya kuweka.
Labda mtu akitukana ndio usiweke.
Na pia mtu akiuliza kitu hata kiwe cha kijinga ujue kuwa yeye kinamtatiza ndio maana ameamua kuuliza. Kuuliza si ujinga.
Mwache anayeuliza atajibiwa na wanaojibu, japo upeo wake utapanuka. Tunategemea blog hii ni maarufu na kila mmoja anauwezo wa kutoa yake kwaajili ya kuelimisha, kufurahisha.
Wapo watu wanaotuma maswali kuuliza sio kama wanakosa majibu ila ni kuwa wanahitaji mtizamo zaidi kutoka kwa wengine labda mtizamo alionao yeye haujitoshelezi Eg. Mtu aweza uliza 3 - 4 = ? Mimi najua 3 - 4 haiwezekani ni 0, lakini mwingine atasema inawezekana jibu ni -1. (Huu ni mfano tuu sio kama ndio swali linalotakiwa kuulizwa) Hiyo ni mitizamo tofauti ya watu katika kupanua upeo wa watu.. Napia ni njia moja ya kushtua watu ambao wameshaanza jisahau katika jambo fulani.
Natumai utasikia kilio changu. Blog hii ni ya jamii ifanye iwe ya jamii kweli kweli..
Mimi Mdau kipenzi cha blog hii.
mdau unayesemema kwamba nimeshauri serikali inunue magari ya kuzimia moto kila sehemu ya public naona hujasoma maoni yangu vizuri, HAKUNA sehemu niliyozungumzia magari ya kuzimia moto. Pia naomba unielewe kwamba ushauri wangu kwa serikali siyo kwamba wao ndio wawe wananunua, NO bali iwe mojawapo ya requirements wanazohitaji ili kutoa lesini ktk hizi sehemu kujiendesha kibiashara. Kama sehemu hizo hazina vitu nilivyovitaja i.e at least one fire/emergence exit, fire exitinguisher(si maanishi magari), fire alarm, smoke detector na kama managements ya hizo sehemu hawawezi kutoa fire sasety training kwa wahudumu wake leseni isitolewe kwa hizo sehemu whether is hospital, shule, clubs na kadhalika. na serikari pia inaweza kuplay its role ya kuzidisha fire departments na emergence calls japo kuanzia kwa kila wilaya then kila tarafa. waanze na sehemu ambazo ni highly populated.
ReplyDelete