mkuu wa vodacom foundation mwamvita makama (shoto) na CEO wa ttp://8020fashions.blogspot.com shamim zeze wanawatakia wadau wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais wa Marekani Barak Obama naye ametuma salamu za heri ya Mfungo kupitia Youtube. Bofya hapa umuone na kumsikiliza Obama

RISALA YA RAIS BARACK OBAMA
KATIKA KUUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHAN

Kwa niaba ya watu wa Marekani – ikiwa ni pamoja na jumuiya za Waislamu katika majimbo yote hamsini ya Marekani – ninapenda kuwatakia kheri Waislamu wote wa Marekani na duniani kote. Ramadhan Kareem.
Ramadhan ndio mwezi ambao Waislamu wanaamini kuwa Korani ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad, ikianzia na neno rahisi – iqra.

Hivyo huu ni wakati ambao Waislamu hutafakari kwa kina kuhusu hekima, miongozo na mafundisho ya imani yao na wajibu ambao wanadamu wanao kwa wanadamu wenzao na kwa Mungu.

Kama ilivyo kwa watu wengi wa imani tofauti ambao wameshuhudia Ramadhani katika jamii na familia zetu, ninafahamu kuwa huu ni wakati wa furaha – wakati ambapo familia hukusanyika na kula pamoja. Lakini ninajua pia kuwa Ramadhan ni wakati wa ibada, tafakari na maombi ya kina – ni wakati ambao Waislamu hufunga wakati wa mchana na usiku wakisali tarawih, wakisoma na kusikiliza Korani yote katika kipindi chote cha mwezi huu mtukufu.

Ibada hizi zinatukumbusha misingi inayotuunganisha pamoja na nafasi muhimu ya Uislamu katika kujenga na kuimarisha haki, maendeleo, hali ya kuvumiliana na heshima kwa wanadamu wote.

Mathalani, dhana ya kufunga inapatikana katika imani nyingi – ikiwa ni pamoja na imani yangu ya Kikristo – ikitambuliwa kama njia ya kuwaweka karibu waja na Mola wao na kuwakumbuka wale miongoni mwetu wenye njaa. Aidha, msaada ambao Waislamu wanautoa kwa wengine katika kipindi hiki, unatukumbusha wajibu wetu katika kutoa fursa na kuwezesha ustawi wa watu wengine mahali pote. Kwani ni muhumu kwetu kukumbuka kuwa dunia tunayotaka kuijenga – na mabadiliko tunayotaka kuyafanya – ni lazima yaanzie ndani ya mioyo yetu na katika jamii zetu wenyewe.


Katika kipindi hiki cha majira ya joto, watu wengi hapa Marekani wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kusaidia jamii zao – ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watoto, kuhudumia wagonjwa, na kuwasaidia wale wenye shida mbalimbali. Taasisi za kidini, ikiwa ni pamoja na taasisi za Kiislamu, zimekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma hizi za kijamii. Katika kipindi hiki ambapo tunakabiliwa na changamoto nyingi, ni lazima tuuendeleza moyo huu wa kujitolea na kuwahudumia wengine, si katika mwezi huu tu bali pia katika miezi na miaka ijayo.

Ni azma yetu kutekeleza kwa dhati wajibu wetu wa kujenga dunia yenye amani na usalama zaidi sio tu ndani bali hata nje ya mipaka ya Marekani. Ni kwa sababu hiyo ndiyo tunahitimisha vita nchini Irak kwa namna nzuri inayohakikisha uwajibikaji. Ni kwa sababu hiyo ndiyo tunayatenga makundi yenye msimamo mkali na ya kigaidi huku tukijenga uwezo wa watu katika maeneo kama Afghanistan na Pakistan. Hii ndiyo sababu tunaunga mkono kwa dhati haki ya Waisraeli na Wapalestina kuishi kwa amani na usalama.

Na ni kwa sababu hiyo ndipo wakati wote tutasimama kidete kulinda na kutetea haki ya watu wote kutoa maoni yao, kuabudu na kutekeleza mafundisho ya dini yao, kuchangia kikamilifu katika jamii zao na kuwa na imani katika utawala wa sheria.
Jitihada zote hizi ni sehemu ya dhamira ya dhati ya Marekani ya kushirikiana na Waislamu na nchi za Kiislamu kwa misingi ya kuheshimiana na kujali maslahi ya pande zote. Katika kipindi hiki muhimu cha ibada na kujiimarisha kiimani, ninapenda kusisitizia dhamira yangu ya dhati ya kuwa na mwanzo mpya kati ya Marekani na Waislamu duniani kote.
Kama nilivyosema katika hotuba yangu ya Cairo, ni lazima mwanzo mpya utokane na jitihada za kudumu za kila upande kusikiliza na kujifunza kutoka kwa upande mwingine. Aidha, ni lazima mwanzo huu ujengwe katika misingi ya kuheshimiana na kutafuta mambo yanayotuunganisha. Ninaamini kuwa kusikiliza ni sehemu muhimu ya jitihada hizi. Katika miezi miwili iliyopita Balozi za Marekani duniani kote zimekuwa zikikutana sio to na serikali bali pia moja kwa moja na wananchi katika nchi za Kiislamu ili kupata maoni yao. Na kutoka duniani kote, tumepata maoni mengi kuhusu namna ambavyo Marekani inaweza kushirikiana na nchi hizo kwa kuzingatia matarajio ya watu.
Tumesikiliza. Na kama ilivyo kwenu, tunaelekeza jitihada zetu katika kuanza kuchukua hatua mahsusi - kuhusu masuala ya kisiasa na kiusalama niliyoyaelezea hapo awali, na katika maeneo ambayo mmetuambia yataleta mabadiliko yenye manufaa zaidi katika maisha ya watu. Tunaamini kuwa baada ya muda jitihada hizi zitaanza kuleta mabadiliko.
Mashauriano haya yanatusaidia kutekeleza ubia ambao niliupendekeza mjini Cairo – ili kupanua program za mabadilishano ya kielimu; kuimarisha ujasiriamali na kukuza ajira; na kuongeza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia huku tukisaidia mafunzo ya ufundi. Tunaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na nchi wanachama wa OIC ili kutokomeza polio. Aidha, tunashirikiana kwa karibu na jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na changamoto za pamoja kuhusu masuala ya afya kama vile Mafua ya Nguruwe – ambayo najua ni kitisho kwa Waislamu wengi wanaojiandaa kwenda kushiriki ibada ya hija.
Jitihada zote hizi zinalenga katika kutimiza matarajio yetu ya pamoja ambayo ni pamoja na kuishi kwa amani na usalama; kupata elimu na kazi zenye heshima, kupenda familia, jamii na imani zetu. Haya yote yatahitaji muda, jitihada na subira kubwa. Hatuwezi kubadilisha mambo kwa siku moja, lakini tunaweza kuazimia kwa dhati kufanya yale yanayotupasa kufanya, wakati tukijielekeza katika mwelekeo mpya – tukielea kule ambako tungependa kuelekea sisi na watoto wetu. Hii ni safari ambayo ni lazima tusafiri pamoja.
Ninatarajia kuendelea na mjadala huu muhimu na kuubadilisha kuwa hatua mahsusi za utekelezaji. Na leo ninapenda kuwatakia Waislamu wote wa Marekani na duniani kote mwezi wenye Baraka mnapoupokea mwezi mtukufu wa Ramadhan. Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. he huyu dada mwingine mbona antisha na hayo mawani du kama kobe, kama ni fashion lol kachemsha, ufashenista hauwezi...wink ;) lol didnt like it wink..........
    hahaaaa, michuzi usinibanie comment yangu. ni vizuri tukaambiana ukweli hasa ktk mfungo huu wa ramadhani mubarak.

    ReplyDelete
  2. watu hadi wasikie Ramadhan imefika ndio wakumbuka kujifunika vichwa vyao na kuvaa kiheshima. Ramadhan ikiisha tu utaona vichwa waziwazi na vimini. Tujaribu kumkumbuka ALLAH S.W siku zote sio Ramadhan tu InshaAllah.

    ReplyDelete
  3. Tuache unafik Waislam kwa kujifanya eti mwezi wa ramadhani ndio tunamjua Mola.
    Tuacheni hizo,tukumbuke sheria za dini yetu inasemaje,sio tu kwa mwezi huu waramadhani.Nawatakia kila la kheri,pia kwa sote tujitahidi kuepuka kuichezea dini kwa matakwa yetu tu,tuifuate vile inavyosema sheria zake.

    ReplyDelete
  4. Mmependeza wadada zangu, natamani muwe hivi hivi hata baada ya mfungo. Anony wa kwanza, hiyo miwani ndio fashion sasa. Hata mie ndio naitinga hiyo na ki round face changu, wee utakimbia. Haitwi mtu kobe hapo ... Da Shamim upo juu ... WINK kwa saana ... lol!!!

    ReplyDelete
  5. they look fabulous!!! stop hating!!!!

    ReplyDelete
  6. Hebu basi na ww vaa tuone unavyojua kupendeza. Kuliko kumtukana dada wa watu na maisha yake. Amependeza ama hajapendeza ww inakuhusu nini? Kama huna cha kuandika kwa manufaa ya wengine si uache tuu? ustaarabu kitu cha bure mtanzania. Na hekima ya mtu huonekana kwa matendo yake.

    ReplyDelete
  7. Da Mwamvita umependeza, Da Shamim, mmmm,don mean to diss you, I know you alwayz do it right, but may be next time before you step outside with those big miwaniz, you might wanna take a second look and think, not for you honey, they are stylish but not fit for you, again we all have bad fashion days, nimezoea kukuona umependeza always, happy ramadhani,

    ReplyDelete
  8. jamani mimi ndio kwanza nimetoka kufturu na huyu mwamvita anataka kuniharibia ramashani yangu basi yee kila wakati lazima awe fashionable?

    lakini al muhimu je keshaolewa? maana sie wengine wabovu wabovu na hatutaki kuwachezea watoto wa watu..sie bwana ni ndoa tuu na nina imani atakuwa ajua pika

    Basi michuzi inshaalah naomba unipe khabari zaidi na mwambie huyo bibie next time avae ninja nimwone maana nataka nimwone dizaini zote

    Huyo mwingine naskia mke wa mtu na mie vya watu kwangu haram

    ReplyDelete
  9. Kwa mara ya kwanza nasikia rais wa marekani akiwish waislam duniani ramadhani njema, with proper pronounciation of arabic words. Huyu jamaa kweli aliwatesa huko Harvard maana ni interlectual aliyebobea!

    ReplyDelete
  10. MICHUZI WEKA VIZURI HABARI YA OBAMA KASEMA MANENO MAZURI SANA.HAIJAWAHI KUTOKEA MIMI NAONA OBAMA NI MUISLAM.

    ReplyDelete
  11. fashionist amechemsha leo. hizo miwani zipo kwenye fashion lakini kwa face yake naona ni too big.

    ReplyDelete
  12. jamani mie ni kijana wa kiislam ambaye ni rijali, nishachoka kusomewa speeches na wazee na watu ninaoheshimiana nao kutaka nioe...naam, bila kusahau kuwa ni msomi vile vile...sasa kwa mtaji huo naamini kuwa bi Mwanvita angenifaa sana...naaminikuwa anajua kupika na kadhalika...

    Michuzi hebu fanya hima unifahamishe je huyo binti keshapata nusra au bado na kama bado basi si mbaya sana naweza kutumbukiza mkono gizani then tutajua mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  13. we hapo juu unayejiita rijali uwe na adabu ati utumbukize mkono gizani! tumbukiza usipong'wata na nyoka kila siku mnauliza maswali yenu ya kebehi huyo binti kaolewa?? kwanai si mnasoma blog ya jamii kila leo mnauliza mnajibiwa mnarudia subirini tu one day mtawekewa picha yake na mumewe muwe na adabu kipindi hiki cha mwezi wa toba na kuendelea alah!! jibu ni NDIYO KAOLEWA NA MZUNGU TAJIRIIIIIII NA ANA WATOTO WAWALI

    ReplyDelete
  14. kwanza nashkuru kwa comment yako

    mie kuuliza kama kaolewa au la nilikuwa na nia nzuri tuuu sasa haya mambo ya kuambiwa nishike adabu yangu sijui nini imetokea wapi?

    Umesema kaolewa na mzungu sasa hiyo yote imetokea wapi lakini sasa ushanipa sababu ya kuuliza swali lingine...je huyo mumewe mzungu muislam au gala?

    Halafu nimedokezwa kuwa akina Makamba ni makadiani je kuna ukweli gani kwenye hilo?

    wabillahi Taufiq na naona salat Laasir ndio hiyoooo

    ReplyDelete
  15. We rijali, acha kuuliza maswali yasio kuhusu. Unapata dhambi, shughulika na vyako. Tupo mfungoni sasa, chuma mema, tafuta fadhila za mola wako. Wee vipi?

    ReplyDelete
  16. Naam nimerejea baada ya kupata taraweh na naona upo tuu

    Je kuna ubaya gani kwa kijana wa kiislam kuwa na nia ya kumpa stara binti wa kiislam?

    Je wewe mbona umeudhika sana mimi kuuliza kama huyo bibie kuolewa?

    Je ni nani anaaamua kuwa maswali yepi yanani husu na yepi hayanihusu?


    Je huoni kuchuma mema ni pamoja na wale ambao wanafanya akdi au wewe unataka watu wafanye zinaa tuuu?

    Kuwepo kwenye mfungo ni sahih kabisa lakini usisahau kuwa kuelemishana mema na kukatazana mabaya ndio wajib wetu au hilo nalo hulijui?

    Fadhila twazitafuta na moja wapo kati ya hizo fadhila ni kuwapa nusra ma binti kama Bi Mwamvita sasa hapo kuna ubaya gani?

    wabillahi Taudfi na kesho taraweih msikiti wa SINZA inshaalah

    ReplyDelete
  17. nasty hr ladyAugust 24, 2009

    heheheh kijana rijali umefunga kweli au all u think about is getting some?
    anyways its nice that during this holy month peeps are pimpin their stlye and manage to look good, i second one of the honeyz who said ms zeze's glasses are not proper for her face, its true, its just a comment and advice so when you sprint out next time you do away with big glasses, you rock always, there is no hatin.. but truth gat to be told
    kijana rijali mwenzio kashaoelwa incase you want to be a second husband??

    ReplyDelete
  18. ASALAAM ALEYKUM

    nimewapata sasa nauliza je, huyo Mwamvita hana mdogo wake maana naona wenginwanasema tayari keshapata nusra lakini si vibaya akam atakuwa na mdogo wake ambaye tayari yuko kwenye umri wa kuolewa

    The best thing about Mwamvita ni kuwa ana kazi,mzuri,si golkipa,si gobore and last but not least ni binti wa kiislam


    sina makuu mie


    haya tena adhuhuri ishafika maneno NGAZIJA inshaalah tukishafturi ntarejea kama kutakuwa na maoni zaidi

    ReplyDelete
  19. Huyu raisi huzungumza maneno ambayo watu fulani huwa hawayapendi lakini hupiga makofi kinafiki.

    Kama ni kweli mbona hatutekelezi? Na mbona watu wanaamini kinyume? (Watu wanaamini kukandamiza imani nyengine kisiasa, kiuchumi, nk.k)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...