Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe University kilichopo Morogoro Profesa Faustin R. Kamuzora akisoma kitabu kipya cha Ngugi wa Thiongó kilichozinduliwa usiku huu RE na Profesa Issa Shivji katika ukumbu wa Nkrumah Hall wa Chuo Kikuuu cha University of Dar ambapo mgeni wa heshima alikuwa yeye mwenyewe Ngugi wa Thiongó ambaye yupo nchini kuhudhuria tamasha la kujisomea vitabu linaloendelea hapo Nkrumah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nimekuwa nikifahamu kuwa profesa Ngugi aliacha zamani kuandika vitabu kwa lugha ya "kikoloni" na alikuwa kaapa kuandika kwa Kiswahili na Kikikuyu tu. Kuna mabadiliko ya itikadi? Tafadhali mwenye maelezo naomba anipatie.

    ReplyDelete
  2. Kama ilivyo mazoea ya vitabu vinavyochapishwa na Ngugi Wathiongo mfano: This time Tomorrow etc hutumika sana katika Masomo ya elimu ya Sekondary English Literature. Je kitabu hiki kitakuwa pia katika moja ya vitabu vitakavyotumika shuleni??

    Naomba mwenye kufahamu atueleweshi tafadhali.

    Sababu imekuwa vitabu vingi vikitoka vinakuwa vinahitajika kufundishwa mashuleni lkn baadhi ya shule sijui ni kushindwa kununua basi hawafundishwi na wanafunzi unakuta hawavijui hivyo wao wanakuja jikuta swali linatoka katika mitihani kuhusiana na vitabu hivyo na kushindwa kujibu.

    Tukijua kama na hiki kitatumika itakuwa rahisi kwa wanafunzi kujua na kuanza hata kujinunulia wenyewe kuliko kusubiri walimu wao wanunue jambo ambalo ni zero.

    Ahsante.

    ReplyDelete
  3. Prof. Ngugi hongera sana kwa uwezo ulionao. Sidhani kama vizazi vya sasa vitakuja kuwa na uwezo wa uandishi na utungaji kama wako. Hakika vitabu vyako mfano PLAYs tunavitumia leo hadi hesho na nivizuri sana.

    Mungu akupe uzima.

    ReplyDelete
  4. The River Between is 1 of my all time favorite books. Waiyaki,Nyambura, Muthoni, Joshua, Kabonyi, Mugo wa Kibiro,. Ngugi is the best and very sory to what happened to him and his wife when they returned to Kenya which caused them to leave again and i wont blame him for not ever coming back to live in Africa after that.I would leave too.

    ReplyDelete
  5. hiyo picha uliyoiweka huyo jamaa sijui wa mzumbe anaesoma kitabu ni msanii kupita maelezo hana lolote!!!

    ReplyDelete
  6. Anony 05:15:00 PM...una ugomvi binafsi na Prof. Kamuzora? Vinginevyo tujuze huo "usanii kupita maelezo" unaouzungumzia

    ReplyDelete
  7. Kuhusu kitabu kama kitatumika kwa shule za upili.

    Sidhani kama kitabu hiki kitafaa katika level hii. Ila kitakua kizuri kwa wanafunzi wanauchukua degree za kwanza katika chuo kikuu. Kiko na theoretical and argumentative points kibao so it may be a little to advance for our secondary school students. Ila walimu wa shule wanawezaa pia kunufaika nalo.

    Paulo Kamau

    PS: Kuhusu lugha, Ngugi hajabadii msimamo. Riwaya yake mpya (ambaye ndio mojawapo ya riwaya ndefu zaidi Afrika mzima...700pgs) kiliandikwa kwa kikuyu kama MUROGI WA KAGOGO kabla ya kutafsiriwa kwa kizungu na ngugi mwenyewe kikaitwa WIZARD OF THE CROW. Ni kazi zake za kihakiki tuu ndizo yeye huandika direct kwa ugha ya kiingereza. Nadhani kwa sababu kazi zenyewe huwa ni diwani ya mada ambazo amewahi kuwasilisha katika kongamano tofauti tofauti duniani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...