SERIKALI YAKANUSHA MADAI YA TBC KUUZWA
Na Aron Msigwa- MAElezo
Serikali imekanusha madai ya kwamba shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuuzwa kinyemela kama ilivyoonyeshwa katika taarifa iliyotolewa na chombo kimoja cha habari hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar esa Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyochukuliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuunda kampuni mpya iitwayo Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na mwekezaji.
Amesema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kama shirika la umma halijauzwa na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zozote zinazotolewa kuhusu kuuzwa kwa namna yoyote kwa shirika hilo.
“ Nawathibitishieni leo kuwa shirika la Utangazaji (TBC) halijauzwa ,bado ni la wananchi na kamwe halitauzwa” amesisitiza. Ameongeza kuwa TBC ni mali ya umma na itaendelea kuwa hivyo kama shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na kuongeza kuwa Star Media Tanzania Limited ni Kampuni tanzu ya TBC.
Amefafanua kuwa TBC imeunda kampuni hiyo mpya kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ili kutekeleza mabadiliko ya Digitali na kuendesha mitambo ya kurushia matangazo yake nchi nzima kazi ambayo itakamilika mwaka 2012 kwa gharama ambazo TBC isingeweza kuzimudu yenyewe kutokana na jukumu hilo kuhitaji utaalam mkubwa wa kiufundi ili kukamilisha ufanisi.
Waziri Mkuchika ameendelea kufafanua kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha inaiwezesha TBC kutekeleza wajibu wake wa kufikisha matangazo yake nchi nzima na kuongeza kuwa ililiruhusu Shirika hilo kutafuta mwekezaji ili kutekeleza mradi wa mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda digitali na kukuza mtandao wake kuenea nchi nzima jambo ambalo limefanyika na kutekelezwa kwa kufuata taratibu zote zinazostahili.
“ Kampuni hii si ya matapeli ,uteuzi wake hii ulifuata taratibu uwekezaji , taratibu za manunuzi ya umma kutoka mamlaka husika kwa maandishi (Public Procurement Regulatory Authority) na pia ushauri wa wataalam wa mamlaka mbalimbali husika” , alisema.
Akizungumza kuhusu mradi huo amesema kuwa utaiwezesh TBC kubadilisha mfumo mzima wa utangazaji wa televisheni kuwa wa digitali na kusamabaza matangazo yake na ya watangazaji wengine kufika maeneo yote nchini.
Amesema kuwa ifikapo mwaka 2012 matangazo ya televisheni ya digitali yatafika kote nchini yakiwemo maeneo yote ambako matangazo hayafiki kwa sasa.
Kuhusu uteuzi wa mbia waziri Mkuchika amesema ulifanywa na Bodi ya wakurugenzi ya TBC baada ya tathmini ya kina iliyowashrikisha wataalam kutoka Wizara ya Habari , Utamaduni na Michezo, Wizara ya Mwasiliano, Sayansi na Teknolojia , COSTECH, TCRA na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) kuchambua na kupendekeza mbia anayefaa .
Ameendelea kufafanua kuwa makampuni 5 ya kimataifa yalionyesha nia ya kushirikiana na TBC katika kutekeleza mradi huo wa digitali na kuombwa kuwasilisha michanganuo yao ya utekelezaji na baadye kampuni ya Star Communication Network Technology Co. Ltd ya China iliteuliwa kwa kufuata taratibu.
Aidha tathmini na uwezo halisi wa mwekezaji ulifanywa na ujumbe wa wataalam kutoka TBC wakiongozwa na katibu mkuu Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini China waliitembelea kampuni hiyo iliyoko Beijing China ili kuhakiki uwezo wake kabla ya kusaini mkataba.
Waziri Mkuchika amevitaka vyombo vya habari nchini kuzingatia weledi katika taaluma ya uandishi wa habari na kusisitiza kuwa mchakato mzima ulikuwa wazi na mkataba wa ubia uliandaliwa kwa pamoja kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kumshirikisha mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kusainiwa.
Inatia kinyaa na aibu. Inabidi tufikie mahali tusimame na kufikiria nini tunacho kifanya. This is too much.
ReplyDeleteHebu angalia hizi scenarios: Uganda wameamua kututia vidole vya macho kama walivyo fanya hapo awali. Safari hii mchina ndie alie watuma ili wavune samaki wetu ziwa Victoria. Wachina wanaamua kubania TV zetu zisionyeshe kile kinacho tokea. Je Mkuchika au Tido atasalimika? Kama mheshimiwa waziri alivyo nukuliwa akisema kua TV vijijini hazifiki, na wala magazeti hayasomeki' mjini Tuna TV, Intaneti, Magazeti na shule za kiukweli zinazo tufungua Macho. 65% sio 50% taka usitake mwenye share nyingi ndie anae faidika.
Maustaadhi mkiibania ibanieni tu, Lakini this is too much! hayo ndio matatito ya certificate za machinga, tutazijuta mwaka huu! Langu jicho na naahidi kulifumba kabla halija tobolewa! mwee!
Nivigumu kuiamini taarifa ya serekali aliyoitoa Waziri wa habari,utamaduni na michezo George Mkuchika.Ninasababu nyingi za kutoamimini hivyo hapa nazitaja mbili.Kwanza kwanini taarifa tuzipate katika vyombo vya habari kwanza ambapo waziri anajitokeza kukanusha au kutoa ufafanuzi?Na serikali au TBC haikufanya hivyo kabla?Kunanini cha kuficha?Pili Tunamikataba mingi ya ubia au uuzaji na ununuaji mitambo au vitu n.k aliyowahi kufanya na serikali yote hiyo ilifanyiwa tathimini ya kutosha,wataalamu walisafiri na kufanya na kujiridhisha na makampuni husika na kusimamiwa na mwanasheria mkuuu nini matokeo yake/mifano ni mingi kuitaja michache ATC,TANESCO,Richmund,TRC,Buzwagi n.k.NASHINDWA KUIAMINI TAARIFA YA SERIKALI.MWANZO WA MOTO NI MOSHI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteMHE. MKUCHIKA TUNAHITAJI MCHANGANUO, WANGAPI WALIOJITOKEZA BAADA YA TENDA KUTANGAZWA KAMA ILITANGAZWA, NA LINI. SERIKALI HUWA INAKAWAIDA YA KUKANUSHA HATA KAMA NI KWELI.
ReplyDeleteMbona waziri unajichanganya? Mwekezaji atafaidika vipi kama hana hisa au share zake? Waziri kaa ukijua unaongea na wataalam na mbumbumbu. Unapowekeza lazima ufaidike hata kama ni biashara ya maandazi. TBC watalipa vipi basi hizo gharama? Na kwa nini serikali isilipe yenyewe kama mmiliki wa 100% za TBC? Na hiyo tenda ilitangazwa lini na upi ulikuwa mchanganuo wake. Kina nani waliomba kupewa nafasi ya uwekezaji na vigezo vipi vilitumika kuchuja yupi anafaa kuwa mwekezaji? Waziri ukae ukijua wazi kabisa kuwa hatuwezi kukubali chombo cha habari cha taifa kuingia mikononi mwa wageni. Huu nao utakuwa ni ufisadi babu kubwa. Mabadiliko ya kutoka analogy kwenda digital yanaweza kufanyika bila mwekezaji. Tunayemuhitaji ni mtaalamu wa kuja kuifunga hiyo mitambo ya digital na si mwekezaji. Tuanaomba ufafanuzi zaidi na si huu ubabaishaji. Tuanaelekea kubaya zaidi kama mambo ndiyo haya. Waziri weka mambo wazi.
ReplyDeleteHapo mimi bado sijaelewa vizuri, yaani TBC haijabinafsishwa ila mali zooote za TBC zimeingizwa kama mtaji kwenye kampuni mpya ya Star Media ambapo TBC hio hio ina asilimia 35?
ReplyDeleteMh Mkuchika historia huwa haifutiki kumbuka maneno kama hayo tuliwahi kuyasikia kutoka kwa Mh waziri mwenye dhamana kama wewe wakati wa kuanzishwa kampuni ya CELTEL eti ni kampuni tanzu ya TTCL je leo kiko wapi? au mnadhani wananchi wamesahau? Kumbukeni watanzania hawa wa leo sio wale ambao mnaodhani wako hivyo mnavyo dhania SOMENI ALAMA ZA NYAKATI
ReplyDeleteUzeni tu, wala huna haja ya kutetea jinsi ulivyopata mbia. Kwani hata ongezako la gharama za umeme zilitangazwa kesho yake mkakanusha wk iliyofuata kuna ongezako kuchangia umeme vijijini. Kwa hiyo hata hili ni kweli.
ReplyDeleteMwenda Pole
"Amefafanua kuwa TBC imeunda kampuni hiyo mpya kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ili kutekeleza mabadiliko ya Digitali na kuendesha mitambo ya kurushia matangazo yake nchi nzima kazi ambayo itakamilika mwaka 2012 kwa gharama ambazo TBC isingeweza kuzimudu yenyewe kutokana na jukumu hilo kuhitaji utaalam mkubwa wa kiufundi ili kukamilisha ufanisi."
ReplyDeleteNimenakili kauli hii kuonyesha msisitizo. Waziri anaongea bila kuwa na technical facts, hivyo kuonekana chenga la macho: Watanzania lazima tujiulize mamba makuu katika uundwaji wa kampuni:
1.Je starmedia imeundwa kama public company or private company.
2. Kutokana na maelezo ya waziri, tutaundaje Kampuni tanzu kuendesha shughuli za Tbc, huku Tbc yenyewe ikiwa na share35%
3. Kutokana na kitendawili hiki inaonyesha wazi kuwa star media ni private company, ambayo shares are entitled to individuals, serikali ituweke wazi nani yuko entitled to Tbc share within the frame work of the new company.
Serikali pia ituonyeshe ni shughuli gani TBC itakuwa inafanya.
Tusipokuwa makini kutegua kitendawili hiki tutajikuta tbc inakufa na Star media inawaka, tiari watu wachache wanafaidika na kufilisi shirika letu.
Kuna harufu ya wizi, katika shirika hili watanzania kuweni macho, yasitoke yaliyotokea kwa makaburu, na Tanzania air line. Inahuzunisha sana.
Mdau.
Kuna usemi ambao unasema ukitaka kumnyima Mtanzania habari muwekee kwenye maandishi hiyo ndiyo tatizo lilitokea hizi taarifa zilikuwa zinatolewa kwenye magazeti lakini kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kusoma ndiyo maana tunazishangaa hizi taarifa na kwa hakika wengi wamejua baada ya serikali kuamua kutoa taarifa kwenye Tv ndiyo watu wanashituka lini imeuzwa? Hata aliyetoa taarifa kwenye MWANAHALISI ni mbabaishaji au amefanya maksudi kuitoa kama ilivyo.Haiwezekani uandike story wakati hujapata other side ili uweze kubalance story.Hili ni tatizo kubwa la vyombo vyetu vingi hapa Tanzania,sasa mhariri anapata aibu kwa sabaBu hakutaka kuishughulisha akili yake ili awze kuandika story ambayo iko balance nadhani ni wakati muafaka Baraza la Habari kuvichukulia hatua vyombo vya habari ambavyo vinatoa stori za upande mmoja bila kufanya uchunguzi wa kina KAMA AMETUMWA AFANYE ALIVYOFANYA BASI TANZANIA TUNA HASARA KUBWA SANA.NAWASIHI WATANZANIA TUPENDE KUSOMA HABARI MAKINI TUACHE KUSOMA HABARI ZA UDAKU,HIVI SASA UNAWEZA KUMKUTA MTU MKUBWA NA PERSONALITY YAKE ANAKWENDA KUNUNUA GAZETI LA UDAKU SASA TUNAJIFUNZA NINI KWENYE MAGAZETI HAYO AMBAYO NYINGI YA HABARI ZAKE ZINAISHIA KWENYE MAISHA YA WATU BINAFSI.NAJUA KUNA WATU WATANISHAMBULIA LAKINI HABARI NDIYO HIYO
ReplyDeleteMh.Waziri Mkuchika, nimepata mstuko mkubwa kuwa itakapofika 2012 TBC watakuwa wanarusha matangazo kwa mfumo wa DIGITAL.
ReplyDeleteSasa sie wenye seti za TV zetu ni analogue/terrestrial, maswali yangu:
1.Je serikali inaratibu TV zinazouzwa dukani lazima ziwe digital?
2. Je tulio na TV set zisizo digital tuzitupe?
3. Serikali inauwezo wa kutupatia 'freeview digital box' tubandike na TV seti zetu za zamani tuweze ona vipindi vya kwenyw matangazo?
4. Je serikali imeshatoa somo kwa wananchi juu ya mabadiliko haya ya kwenda digital, na hii digital itawakwaza vipi au wafanye nini ili kwenda digital(wauzaji TV na waangaliaji TV)
Ahsante, nitashukuru kama tukieleweshwa hii DIGITAL.
Mdau
Chakumwenda.
lakini Kubenea kaandika habari za uongo. Kubene na Mengi mindumila kuwili hii, mara yajifanya sisiemu mara wapinzani, kweli kwenye vita ya mamba na kenge wamo!!!!
ReplyDeleteMkuchika usibembeleze hawa wajinga wanaoendesha magazeti yao kutafuta umaarufu kwa gharama za kugonganisha watu!!!
LETIPIPI
wanawane punguzeni munkari ati. Japo yote hayo mliyoandika yanaonyesha kuwa kumbe bado kuna watu waliokataa kata kata kufanywa ndondocha. Iliyo nifurahisha ni hiyo kauli eti "kampuni hii ni halali kabisa" akisahau kuwa hata RICHMOND walituambia hivyo hivyo. Kwa ujumla nji ilisauzwa tatizo hawataki kumgawia kila mtu kilicho stahili yake.
ReplyDeleteHuo ndio usasa katika mawasiliano ya umma ya chombo kinachoendeshwa na kumilikiwa na serikali? Hivi kodi tunalipa za nini? Hivi umewahi kuona bbc, dw, sabc, kbc, abc, cbc, voa nk vikiunda kampuni na kuingia ubia?
ReplyDeletehaya ndiyo matunda ya kuwapa watu vyeo kwa kwa urafiki.
ReplyDeleteNamshangaa Mkuchika kutudanganya kwamba TBC imebinafsishwa what is kubinafsishwa?
ReplyDeleteKUBINAFSISHWA=KUUZA ,kwa hiyo TBC imeuzwa
Watanzania tumekwenda shule sasa sio rahisi kutudanganya hivyo.
hivi viongozi wa serikali na tbc wanajua maana na nguvu ya vyombo vya habari? sasa watabinafsije hii tbc? siwaelewi. yaani kila kitu ni kubinafsisha bila kufikiria? Huwezi kubinafsisha njia kuu za mawasiliano na usafirishaji. huwezi kubinafsisha tv na redio ya taifa. huku ni kukosa mwelekeo. Tunaelekea wapi? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Watabinafsisha mpaka hewa." Naona tunaelekea huko. Hii si sera nzuri hata kidogo. JK na Bunge ingilieni kati kuzuia hii aibu inayolikumba taifa.
ReplyDeleteNawashangaa ambao wanamlaumu kubene na gazeti la mwanahalisi nafikiri wengi hawakusoma habari hiyo hivyo ni bora kuisoma kwanza kabla ya kukurupuka kuchangia soma hapa
ReplyDeletehttp://www.mwanahalisi.co.tz/index.php?id=622
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/37175-tido-mhando-na-ubinafsishaji-wa-tbc.html
Jamani hili swala inabidi kupata majibu ya kina toka katika serikali na vyombo vyote vinavyohusika na sio majibu ya jujuu.Majibu hayo tumewahi kuyasiki kwa TANESCO,Richmud,shirika la ndege,simu n.k.Mwisho wake uko wapi?Imefikia wakati kwa viongozi kuwajibika kwa kauli zao.MUNGU IBARIKI TANZANIA.