Mambo vipi michuzi,
tangia asubuhi ya leo najaribu kucheki globu ya jamii lkn sijaona habari za wanariadha wetu walioenda Berlin. Mm sipo Berlin, Ujerumani nipo Bratislava, Slovakia, Nimekuwa nikifuatilia Michezo hiyo ambayo imnaonyeshwa moja kwa moja na kituo kimoja cha Eurosport cha hapa Slovakia.
Jana Usiku majira ya saa mbili usiku hv, Kwetu saa tatu usiku niliona wanariadha wawili kwenye mashindano ya mita 10,000 wakiwakilisha Tanzania na wanevalia jezi nzuria na viatu vizuri sana (Walipendeza). Anyway nisiandike maneno mengi sana, Matokeo ni kwamba. Mtu wa kwanza ni M-Ethiopia , wa pili Eritherea na watatu ni mtani wa jadi (Mkenya).
Jamaa wa Tanzania kweli walizungukwa mara moja kwenye mbio hizo za 10,000m na mtanzania amechukua nafasi ya kumi na mbili kama sikosei na mwingine nafasi kama ya ishirini. Watanzania tufanyeje katika michezo ili tufanye vizuri? Tatizo ni nini? Unaweza kutoa matokeo haya ya fainali za riadha ktk globu yako ukipenda.
Mdau wa Brastislava
----------------
Mdau wa Brastislava
asante kwa ujumbe. tatizo hakuna, ila mtandao ulipata kwikwi kwa jamu na isitoshe alfajiri hii nimeruka kuja mwanza kwenye kajivekesheni kidooooogo. hapa ndo kwanza napata mtandao. asante kwa habari na Globu ya Jamii ni ya kila mtu, habari sio lazima alete anko nanihii. we tumwagie tu kama ulivyofanya.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Namshru sana ndugu yetu kutoka Slovakia, hata mimi nilishangazwa sana na matokeo ya jana. Najua nimchezo kuna wa kwanza na wa mwisho ila kwa kweli kuhusu riadha ebu tuikimbuke jamani kama tulivyofanya kwenye Mpira wa miguu-si munaona matokeo sasa. kwani faida yake ni kwa taifa Zima,
    kwani nchi yetu itajitangaza vizuri kupitia mchezo huu. Vijana tunao wengi ila wanahitaji maandalizi mapema,kambi za kudumu na walimu mahsusi. Inasikitisha kuona hao majirani zetu wanatuzunguka hivyo. Ebu tufanye kitu basi- MWAKANI AU SIYO

    ReplyDelete
  2. Pole na kazi mkuu wetu, naam! vekesheni muhimu sana ili kurudisha nguvu. Asante sana kwa kutoa na kutupa fursa na mwanya wadau wako kuweza kupost habari na makala. Hata hivo kumekuwa na malalamiko yanajitokeza hapa na pale kwenye comments eti unabania posts za wadau na maoni kwa ujumla, wengine pia wanalalamikia post nyengine unazotoa hazistahili kuwemo humu, kwa mfano ile ya mdau wa marangu ya shuka moja na mashuzi! Wako wanaoargue uhuru wa habari, hivyo aachiwe kila mtu ajifarague, kadhalika wengine wanasema blog ni yako hivyo una mamlaka ya kuamua kile unaona sawa na kama kuna mtu anakuwa offended aende kwengine, lakini binafsi umekuwa ukisisitiza blog ni ya jamii. Sasa, kwa kuzingatia hilo si vibaya kuachia watu wajirushe na posts za vichekesho, naamini sote tuna a sense of humour mradi hizo jokes na utani hazi transcend sika na hulka zetu na zaidi hazidhalilishi mtu.

    Kwa sisi tunakutumia posts ili tuweze kukusaidia na kufanya censoring iwe nyepesi kwako, naomba utuwekee na utueleze kanuni gani tunatakiwa kutumia tunapoandika makala zetu, kwa mfano lugha gani tutumie, makala zenyewe ziweje, kama kuna limit za urefu, binafsi sijui kuandika makala fupi. Hali kadhalika, tuambie ni vigezo gani unatumia katika kufavor post moja na kuacha nyengine, unaweza kutuwekea limit kwa mfano mdau ukishamtolea makala yake ndani ya week basi utueleze kama asibodhe kukutumia email ukizingatia kuna wengine nao wanahitaji nafasi. Mimi binafsi nimekutumia post mbili ndani ya siku 2 umenitolea moja, nashkuru na siwezi kulalamika sana, infact nilijua nilipo post hiyo makala ya pili I was asking too much of you ukizingatia ushanipa nafasi jana yake na bila shaka kuna wengine uliwanyima nafasi. Ila nadhani hata nyinyi waandishi wa habari mnaelewa how it feels editor akibania kutoa habari yako, naamini wengine mnavunjika moyo hata mkikoseshwa front page tu.

    Jengine, naamini wewe kama mwanahabari una nafasi kubwa ya kudirect wasomaji kwenye makala unazohisi zitakuwa na manufaa sana kwa jamii basi ni vizuri uachie comments zaidi, kwani kuna wengine wakiingia humu kwenye blog wanajali sana kuona nini wengine wamesema juu ya post fulani, hivyo naamini makala zinazopata comments nyingi ndio zinapata attention kubwa hata kama ni juu ya mashuzi. Naomba nisieleweke vibaya, nimetumia hiyo post ya shuka moja na mashuzi kama mfano tu, binafsi sina opinion yeyote juu ya hiyo post wala sikulaumu, simply nimeeleza kutokana na mtazamo wa wengine kulingana na comments zilizotolewa. By the way, mbona nahisi kuna post za zamani kama picha hazionekani kwenye kumbukumbu au umeziondoa? nakumbuka siku zile za mwanzo wa blog yetu mwaka 2005, ulikuwa umepost picha ya mtoto wako anaitwa Hassan ukawa umeweka caption like father like son, au ni mimi tu ndio naota hakukuwahi kuwa na post kama hiyo?

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Mmoja alishika namer ya 13. Na huyo mtanzania mwengine alishika namba ya mwisho na ndiye aliyekuwa wa mwisho. Michosho tu, sijui hawawandai vizuri, na kama mandalizi hakuna, kwanini? waende kule na kushika namba za mwisho kila siku sisi ndio washika mkia.

    ReplyDelete
  4. Ukweli ni kwamba hawakufanya vizuri maana wote walizungukwa mara moja, lakini hakuna mtanzania aliekuwa wa mwisho. Waliomaliza mbio walikuwa 25 na watanzania walishika namba 13,16 na 21. Bado tunasafari ndefu katika michezo!!
    Hata hivyo inaonekana hata watangazaji wa mbio hizo hawakuwa na habari kuwa kuna Watanzania katika mbio hizo au tuseme ulimi iliwateleza, maana walisema wanariadha wa East Africa ndio wananyanyasa, lakini wakataja, Ethiopia, Eritrea, Kenya na Uganda, wakati kumbukumbu yangu
    haikuwa na Mganda alieshiriki mbio za mita 10000.

    MDAU USA.

    ReplyDelete
  5. SISI TULIOYAONA MASHINDANO LAIVU TUMESIKITISHWA SANA NA MATOKEO HASA YA FAINALI ZA MITA 10,000 WANAUME, LAKINI PAMOJA NA HIVYO TUMEPATA FARAJA KUWA TZ IMEWEZA KUINGIZA ZAIDI YA MKIMBIAJI MMOJA KATIKA FAINALI. KUNA NCHI NYINGI TU MAARUFU ZILIISHIA KUINGIZA MWANARIADHA MMOJA TU.
    KWANGU BINAFSI IT DIDNT MATTER KWAMBA TUMESHINDWA VIBAYA. HILO KWA KWELI LISINGEWEZA KUEPUKIKA, HASA UKITILIA MAANANI KUWA RIADHA HAIPEWI TENA KIPAUMBELE HUKO NYUMBANI, LABDA KWA KUWA HAIWANUFAISHI VIONGOZI BINAFSI.
    SASA SANA SANA UTAONA VIONGOZI WAMESHUGHUKLISHWA NA MISS TZ, MISS UNIVERSE, MISS MIKOA, MISS WILAYA,NK MAANA HUKO NDIKO WANAKOPATA KUWAKODOLEA MACHO NA HATIMAYE KUWANYATIA BINTI ZETU.
    TAMAA ZA KIMWILI!!
    KWENYE RIADHA KUMEKUWA KAMA HUDUMA ZA ZIMAMOTO TU, UPIGE SIMU, MAGARI YAJE KUZIMA, MENGINE HATA HAYANA MAJI!!
    MIMI NAWAPONGEZA SANA SANA VIJANA WETU WALIOTUFIKISHA KATIKA FAINALI HUKO BERLIN.
    WANASTAHILI SIFA KUBWA JAPO HAWAKUPATA MEDALI.
    HONGERENI, NAAMINI NI KWA JUHUDI ZENU BINAFSI MMEWEZA KUFIKA MLIPOFIKA.
    ILA MUELEWE KUWA INAWEZEKANA SANA MSICHAGULIWA KUWEMO KATIKA MASHINDANO MENGINE MAKUBWA KAMA HAYA, KWANI HILO WABONGO TUSHALIZOEA. MAMBO NI KWA NAIZI. VIONGOZI WETU WA MICHEZO NI WABINAFSI KULIKO KITU GANI, HAWANA UZALENDO HATA CHEMBE, SI AJABU WAKAWAPACHIKA WANAOWATAKA BILA HATA KUZINGATIA UWEZO NA REKODI ZAO.
    VIJANA WETU HONGERENI SANA.MMEIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA NCHI YETU.
    Ahsante
    Mdau, Ukerewe

    ReplyDelete
  6. Yani huyu mdau wa 02;11;00 umenichekeesha mno! yani wa mwiiisho kabisa ni mbongo?? Baaasi ndio maana jamaa Hasheem mpaka na rais anakuja kumpokea,,anastaili sifa. Kubulula mkia duniani!!! oh la ,la ,la.

    ReplyDelete
  7. Kwa maoni yangu nadhani si haki kabisa kuwatupia lawama wanariadha washiriki.Spoti(sports) ni chuo(academy). Sidhani tunayo Tanzania.Mtu kuwa mwana spoti inabidi uanze utotoni pia sio kila mtu aweza kuwa mwana spoti.Mwanaspoti anatakiwa kula vizuri, kufanya mazoezi na hiyo iwe ndio kazi yake pia anatakiwa kuwa na wataalamu wa uhakika.Kama Tanzania tunataka tuwe na wanaspoti wetu watakaoshinda michuano basi hatuna budi kuwa na hayo niliyoyataja hapo juu. HONGEAR WANASPOTI WETU KWA KUSHIRIKI
    KILI
    BG

    ReplyDelete
  8. mimi si walaumu hao jamaa zetu waliotuwakilisha, bali nawapa pongezi, nyie mnaolalamika nendeni mkakimbie nyie tuone mtafika wapi. hayo ni mashindano kuna kushinda na kushindwa, mdau hapa. morroco

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...