ANKO NANIHII AKILA POZI NA SIMBA WA NANIHII...
WAPENDWA WADAU WATUKUFU,
NAAM, NI MIAKA MITANO NA USHEE SASA TOKEA GLOBU YA JAMII IZALIWE HUKO HELSINKI, FINLAND, AGOSTI 8, 2005 CHINI YA USHAURI MWEMA WA BABA WA GLOBU ZA KIMATUMBI, NDESANJO MACHA.
NAMSHUKURU KWA NAMBA YA PEKEE KAKA JEFF MSANGI ANAYEENDESHA www.bongocelebrity.com KWA KUNIPA LAU NAFASI NIJIELEZE KIDOGO KWENYE BONGO CELEBRITY WAKATI HUO GLOBU YA JAMII IKIWA NA UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU TU. BOFYA HAPA UPATE MAHOJIANO HAYO
NAANDIKA HAYA NIKIWA NA FURAHA YA KUFIKA HAPA NILIPO, NA KWAMBA MWEZI WOTE HUU WA AGOSTI NI MWEZI WA SHEREHE KWANGU, KWANI AGOSTI 28 NI SIKU YANGU YA KUZALIWA. HIVYO NIKO KATIKA HEKAHEKA YA KUTAFUTA NAMNA YA KUSHEREHEKEA NA WADAU HEPI BESDEI ZA KUZALIWA KWA GLOBU NA MIMI MWENYEWE KWA MPIGO.
BILA NYINYI, WADAU WAPENDWA WATUKUFU, NISINGEFIKA HAPA NILIPO. NAWAHESHIMU NA KUWAPENDA SANA. YAANI HATA WALE WACHAFUZI WA HALI YA HEWA MIE KWANGU NI SALUTI TU, INGAWA KWA BAHATI MBAYA, NA KUTOKANA NA MADILI YETU, INAKUWA VIGUMU KURUHUSU MAONI YAO YAONE MWANGA WA JUA. LAKINI MCHANGO WENU NAUTHAMINI SANA TU.
UJUMBE WANGU WA LEO NI JUU YA HUU UTATA UNAOZUKA MARA KWA MARA, AMBAO KUNA BAADHI YA WADAU WANAOKERWA KUONA WADAU WENZAO WAKITUMIA KINGÉNG'E KATIKA KUJIELEZA, KUTOA MAONI AMA KUTOA MADA.
BILA KUCHUKUA UPANDE KATIKA HILO, NAOMBA KWA UNYENYEKEVU WA HALI YA JUU, NIWASIHI WADAU WANAOKWERWA NA KIINGLISHI WAWE WAVUMILIVU NA KUFANYA SUBIRA KWANI GLOBU YA JAMII HAIBAGUI LUGHA, JINSIA, ITIKADI WALA IMANI ZA KIDINI. HIVYO MDAU ANAYEANDIKA KWA KIIGISHI HUENDA ANA NIA YA KUWASILIANA NA WADAU WENYE KUWEZA KUIELEWA LUGHA HIYO. HAIMAANISHI VINGINEVYO, NA MIMI SINA NONGWA NAO WALA NYINYI.
VILE VILE SERA YA GLOBU YA JAMII NI YA LUGHA INAYOTAMBULIKA KITAIFA - YAANI KIMATUMBI NA KIINGLISHI. HIVYO SIONI KOSA KWA WANAOTUMIA LUGHA YA KIINGLISHI, INAGAWA NI KWELI WASOMAJI WENGI WENGINE (MIE MMOJA WAO) KINGLISHI IZ NOTI RICHEBO. SAA INGINE HUWA NAACHIA VITU VIENDE HEWANI HUKU NIKIWA SIJUI KILICHASEMWA.
NITOE PIA SHUKRANI KWA WADAU AMBAO WAMEKUWA WAKIENDELEZA LIBENEKE KILA MARA KWA KUTUMA TASWIRA NA HABARI KUPITIA GLOBU YA JAMII, KIASI HATA HIVI SASA GLOBU HII IMEKUWA YA KILA MTU NA SI YANGU PEKE YANGU TENA. NAFURAHIA SANA SWALA HILO NA NAWASIHI WOTE WENYE LIBENEKE WASISITE KUTUMA TASWIRA NA HABARI KUPITIA issamichuzi@gmail.com
NDOTO YANGU KUBWA NI KUONA GLOBU YA JAMII INAKUWA KAMA 'FACEBOOK' AMA YOUTUBE' AMA ''TWITTER' AMBAPO BADALA YA MIE UWEKA TASWIRA NA HABARI, WADAU MCHUKUA NAFASI HIYO KIMOJA. HII NI KWA SABABU YA KUTAMBUA UMUHIMU WA KILA HABARI YA WADAU AMBAYO KWENYE VYOMBO VINGINE VINGI VYA HABARI HAITOWEZA KUOANA MWANGA WA JUA. HIVYO LIBENEKE LA BESDEI, KUMEREMETA NA HATA KUTAFUTA UCHUMBA NA KUELEZA YALE YA MOYONI YATAELNDELEA KUWA RUKSA KATIKA GLOBU YA JAMII.
KWA LUGHA INGINE, WADAU WAPENDWA, GLOBU YA JAMII NI YENU ITUMIENI MNAVYOTAKA NA MAMBO YAKIENDA MSWANO IKO SIKU UTAKUWA HURU KUTUNDIKA HABARI NA TASWIRA BILA KUPITIA KWANGU. INSHAAALLAH MUNGU YUPO. KUMBUKA, UKIWA NA TASWIRA AMA LIBENEKE LA AINA YOYOTE LETE TU KUPITIA
MWISHO NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WAFADHILI WANGU AMBAO WAMEIWEZESHA GLOBU YA JAMII KUWA HAI NA KUTEMEBELEWA NA WADAU TAKRIBAN MILIONI MOJA KWA SIKU. HAO SI WENGINE ILA NÏ:
VODACOM TANZANIA PAMOJA NA TANZANIA BREWERIES LIMITED KWA KWELI BILA WAO INGEKUWA VIGUMU KUENDELEZA LIBEKENE.
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. tunakushukuru sana kutupa habari kwani blog yako imetusaidia kufahamu kila kinachoendelea kwa hiyo hatuna budi kukupongeza kwa kazi nzuri.

    ReplyDelete
  2. Hongera Mishuzi kwa miaka mitano ya blogu ya jamii, na sie tuko nawe mpaka kufaaaaaaaaaaa. Lakini umeona juzi Manu alivyochemsha?, bwawa la maini mtakuwa na ubavu kweli mwaka huu?.

    Mdau Fc Bongo Damu Helsinki.

    ReplyDelete
  3. Naona lakini Simba wenyewe aumi.

    ReplyDelete
  4. MGANGA_NJAAAugust 11, 2009

    August 8, 2005 to August 8, 2009 = 4 years NOT 5 years

    ReplyDelete
  5. Mwachimbolo wa Duga MaforoniAugust 11, 2009

    Ninakupongeza wewe mwanzilishi wetu na wadau wenzangu wote kwa ushirikiano tunaopeana kwenye libeneke hili katika lugha mbalimbali na hasa kimatumbi kwani na mimi hicho kiingilishi sikujaaliwa kukijua hata cha kuombea maji. Hata hivyo nina imani wewe mwenzangu iko siku utaijua hiyo lugha hapo binti Michuzi atakapolamba nondo yake kule Kampala. Nawstakia kila la kheri na mafanikio tele.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Kaka Nanihii kwa mafanikio haya pamoja na besidei ya kuzaliwa kwako.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Mkuu kwa kusherekea siku yako ya kuzaliwa na pia bethidei ya blogu yako.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  8. Ongera Michuzi kwa libeneke lako kutimiza miaka 5. Naona mambo mswano mpaka nani hiii unaingia na kupiga picha sio mchezo. Ungeweka shindano la kutambua huyu mnyama yuko wapi leo ningewaburuza wadau hahahaha. Endeleza libeneke siku moja kweli utawapata watembeleaji wa blog milioni moja kwa siku kama ndoto zako zinavyoona.

    ReplyDelete
  9. Ukishaona mtu mzima anaanza kuandaa besdei bongo, basi ujue vijihela vimeanza kufurika mfukoni kwake. Jamani, hii culture ya baba au mama kusherehekea besdei imeanza lini? Hongera balozi na mkuu wa wilaya ya nanihii.

    ReplyDelete
  10. hongera sana kaka MICHUZI..blog yako ni nzuri na mimi binafsi nafurahi sana kuisoma kwa napata habari mbali mbali za nyumbani na duniani kwa ujumla.sasa kwa kumalizia nasema hivi, Mnyaazi Mungu aendelee kukulinda na kukuongoza katika shughuli zako zote za kila siku.
    MDAU-UK

    ReplyDelete
  11. Wewe Michuzi inaelekea hukuwa mzuri sana wa somo la hesabu shuleni, maana umefikisha miaka miine na si mitano, kama blog ilizaliwa 8, august 2005 mpaka august 8 2009 ni miaka minne tu kaka ambayo si haba vile vile.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Michuzi kwa besdei mbili kwa mpigo. Ubarikiwe na asante sana kwa kutujuza mengi kila kukicha.

    ReplyDelete
  13. Mungu akulinde daima akuongezee maradufu. Michu naona wewe umekuwa kama fisadi, kama huruhusu mada zingine zionekane, wewe si fisadi? Jieleze! Basi mola akupe uwe kama fisadi wengine wa kitanzania!

    ReplyDelete
  14. Bado mwaka mmmoja ifike miaka 5, since 2005 mpaka sasa ni minne tu au siyo, Ila hongera anyway!

    ReplyDelete
  15. Ndugu Balozi Michuzi,

    Happy Birthday. Mungu akupe miaka mingi ya maisha na akulinde na familia yako. Hongera sana.

    Nakushukuru kwa kuweza kutupa jicho la kuona nyumbani tukiwa nje.

    Ila, nasita kusema kuwa unatupa uhuru wa kutoa maoni hapa. Kuna hoja nyingi na maoni mengi ya watu pamoja na yangu binafsi umeyabana kwa sababau ambazo unazielewa mwenyewe. Sijii wenzangu, lakini mimi situmii lugha chafu au kama unavyosema, kuchafua hali ya hewa. Ni miezi kadhaa sasa nimeacha kutoa maoni yangu japokuwa kuna wadau waliandika hapa kuwa mimi ni mmoja wa wale wadau wanaochangamsha blogu hii ya umma. Inatia huruma kuona kuwa bado haki ya mtu kutoa maoni haiheshimiki hapa japokuwa umetangaza kuwa maoni yote ni huru kama yatasaidia maendeleo ya taifa. Ni haki yako kama mwenye blogu hii kuamua kuchapisha au kutochapisha maoni. Lakini itakuwa unadanganya kama uansema kuwa unakaribisha maoni yote yatakayoleta maendeleo ya Tanzania huku ukiyabana maoni ya watu.

    Mimi sio kichaa, nina elimu ya juu ya uchumi Marekani (B.Sci.,MBA). Ninatumia muda wangu kutoa maoni yangu, hasa yanayohusu CCM, serikali na Mwalimu Nyerere. Sioni sababu za kimsingi za kubana maoni zaidi ya kubahatisha kuwa hupendi kuwakasirisha "wakubwa" wanaosoma blogu hii labda kwa kuwa wewe ni mfanyakazi wa serikali.

    Shukurani kwa kutupa fursa ya kuona picha za nyumbani, tunashukuru sana. Ila nimeacha kutumia muda wangu kutoa maoni kwa kuwa huyachapishi, pamoja na maoni ya watu wengi hapa wanaolalamika.

    Kila la heri na shukurani kwa wingi.

    Mdau wa Tokyo, Japan

    ReplyDelete
  16. HONGERA SANA MKUU KWA KTUUNGANISHA."MWENYE CREDIT APEWE"
    ILA UKOME KUTUWEKEA MAMBO YA CHAMA KUSHIKA HATAMU!!

    ReplyDelete
  17. Hongera lakini punguza kubana maoni yanayoisakama CCM na serikali yake.Kama unaiita globu ya jamii basi uwe neutral kwa jamii na si kushabikia upande mmoja tu. Vinginevyo iite globu ya CCM.

    ReplyDelete
  18. Michuzi tuwekee picha ya wewe na fammilia yako, mke na watoto wakikulisha keki ya berthiday, kwani wewe unavyojua kujibamiza na vyeo vya watu, hukawii kuweka picha ukilishwa keki na macelebrity vimwana wa kibongo, duh jamaa hata siku moja hajaweka picha hata ya birthday za watoto wake, hata anivessary basi au huna????

    ReplyDelete
  19. Hongera kaka Michuzi. Mola swt akuongezee baraka na imani. Tunakuombea kila la kheir katika mizunguko ya maisha na familia yako. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  20. Hongera sana mzee wa Libeneke na Happy Besdei nakutakia mafanikio mema na blogu yetu iendelee kukua kwani hivi sasa tayari ni kama gazeti letu tunakutegemea mno kwa habari hasa sisi wa ughaibuni.Mungu akubariki sana.Matunda ya TSJ na Daily News tumayaona hongera sana umetokea mbali kaka Mdau DC.

    ReplyDelete
  21. Hongera sana.Ila jaribu kuwa mwana jamii wa kweli.Acha Mambo ya itikadi ya ccm na serikali.Usiwe unabana maoni yanayowalenga viongozi.

    ReplyDelete
  22. hongera sana Michuzi,blog yako ipo juu sana.imetufanya wengine tuwe maarufu sana. keep it up.

    kila la kheri
    MDAU M6

    ReplyDelete
  23. acha uzushi michuzi. wewe ndio blog pekee inayoongoza katika kubania maoni ya watu hata kama hayana matusi ili mradi tu yawe yanaiponda CCM au IKULU HUYATOI hiyo ni kawaida yako. Mtu akiwa na mada inayoichambua serikali kwa kina inabidi aende JF huko kuna uhuru 100% sababu ni web ya watanzania wanaolilia haki yao. people who cry for eqality in the sharing of the national cake have no CHANCE in your blog but rather in JF hiyo inatukatisha tamaa.
    unaposema unatamani siku moja kila mtu awe huru kupost mwenyewe bila kupitia kwako nakushangaa..labda utaanza kuikana kwanza blog kwamba wewe si mmliki tena kisha ndo utaruhusu huo uhuru!!!!
    VODACOM, TBL wadhamini wako HAWAGUSWI humu bloguni mtu akitoa maoni ya kuwachokonoa Voda au TBL maoni yanatupiliwa mbali lol!!!!!
    kwenye ile hoja aliyoitoa yule dada mla vumbi wa UDSM kuhusu makampuni kudhamini urembo na burudani na si watoto yatima, mimi binafsi nilitoa mchango wangu nikamfafanulia kiundani yule dada sababu hasa za hali halisi, lakini sababu niliigemea zaidi Voda na tbl mzee ukayatupilia mbali bila kujali kuwa wenzio tunatumia muda wetu kuandika!!!
    acha hizo bwana, pia acha danganya totoz! na hii ukipenda ITOSEEE!!
    ahsante
    Mdau, IL.

    ReplyDelete
  24. Michuzi's version of Freedom of Expression:1

    Universal right of freedom of Expression:0

    Aluta continua

    ReplyDelete
  25. Yaani wooote mmeshindwa kumuimbia!

    Haya wote: Hepibesdei tuyuuu, hepibesdei tuyuuu, hepibesdei dia Issa hepidesdei tuyuuu.
    Kata keki tuleee, katakeki tulee, hepibesdei dia issa hepibesdei tuyuu.

    Tunakutakia maisha mema Mungu awe nawe, utimize miaka mingine kama hii ya blog yako.

    ReplyDelete
  26. Duh! Halafu kaka yaelekea wewe ni mmasai na umepitia katika mafunzo ya Umorani. Yaelekea huogopi simba kabisa. Hongera

    ReplyDelete
  27. Happy Anniversary Kaka Michuzi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...