Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Pindi Chana (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la wodi ya wazazi la hospitali ya Wilaya ya Ludewa, lililojengwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wodi hiyo imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 42.(kushoto) ni Mbunge wa Ludewe Profesa Raphael Mwalyosi (Kulia) Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba wakishuhudia uzinduzi huo.
Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kushoto)Mkuu wa Vodacom nyanda za juu Jackson Kiswaga,Mbunge wa Ludewa Profesa Raphael Mwalyosi na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa pindi Chana wakiangalia moja ya kitanda vitakavyotumiwa na wakina mama wajawazito baada ya Mfuko wa kusaidia jamii wa vodacom(Vodacom Foundation)kuwakabidhi jengo la kusubiria akina mama wajawazito ambalo limegharimu kiasi cha milioni 42.

Kikundi cha ngoma cha umoja cha Wilaya ya Ludewe kinachoundwa na wajawazito wanaosubiri kujifungua wakicheza ngoma ya lindima baada ya kukabidhiwa msaada wa jengo la wazazi na Mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya Simu ya Vodacom,Vodacom Foundation.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Akina mama wanosubiri kujifungua siku hizi hucheza ngoma?????? Asalleee!!

    ReplyDelete
  2. akina mama wajawazito wanatakiwa kufanya mazoezi, kama mazoezi hayo yamekuja katika mfumo wa kucheza ngoma sio mbaya alimradi tu ngoma hiyo haihatarishi afya yao na ya viumbe walivobeba!!

    ReplyDelete
  3. NImefurahi kuona something kimetokea Ludewa
    Ni wilaya iliyo nyuma sana kimaendeleo Tanzania hivyo mashirika mengi zaidi yapige kambi huko kusaidia
    Vodacom mmefanya jambo kubwa sana kuisaidia Wilaya hiyo
    Ndio wilaya niliyoanzia kazi serikalini na niliona real life ya mtanzania na ugumu wake
    Wilaya inahitaji more and more support

    ReplyDelete
  4. Pindi what happened mbona umenenepa hivyo?u had a great body d au ndo uheshimiwa?salimia Norman.

    ReplyDelete
  5. mna akili sana...

    ata mie nna mpango wa kusaidia uko kwetu asa wilaya za makete na ludewa

    asante

    ReplyDelete
  6. Makete haihitaji msaada toka Vodacom. Makete inahitaji sensitization tu ya wenyeji wake waliotapakaa Mwanza, Mbeya, Kariakoo, Songea Makambako na wote hao ni wenye biashara kubwa za kwenda Dubai, China na Japan na vile viel wanamiliki majumba ya uhakika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...