mnenguaji nyota wa twanga pepeta, aisha madinda, amesharudi kwenye fomu na anatesa vilivyo katika safu ya ushambuliaji wa african stars band ambayo imerudi billicanas club kila jumatano katika usiku wa mwafrika. hapo ni katika shoo ya iddi pili usiku huu mango garden, kinondoni, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. MMM..naye fuska tu. HANA CHA UNENGUAJI WALA NN.ANATUTEGA TU ATUINGIZE MATATIZONI.

    ReplyDelete
  2. nampenda sana huyu dada ,hata nikisika anaumwa roho inaniuma sana,anajua kucheza mno wala hatumii nguvu ,yeye pamoja na internet

    ReplyDelete
  3. yote 9 ila machozi band iko juu!

    ReplyDelete
  4. Kwani alikwenda wapi???

    ReplyDelete
  5. Mzee Wa Zeze, Columbus, OhioSeptember 22, 2009

    Jamani huu mpini sio mchezo, kama unakutana nae faragha lazima uwe umejiandaa vya kutosha la sivyo unaweza kuadhirika mzee mzima.

    ReplyDelete
  6. Duh bora karudi tulimmiss sana huyu dada.

    ReplyDelete
  7. Huyu dada mkali namfagilia ile mbaya
    Mdau UK

    ReplyDelete
  8. Tuache unazi wala nini. Twanga pepeta ya sasa inatisha. I mean baada ya kutoa album yao mpya ya mwana dar es salaam iko juu sana. Kama unabisha nenda siku za jumapili leaders na TCC Club
    uone wanavyojaza umati na usikilize wadau wanavyoizungumzia na kuburdika nayo

    ReplyDelete
  9. Mimi nadhani uongozi wa TwANGAPEPETA UKO IMARA KULINGANSHA NA BENDI ZOTE, NA NDIYO MAANA IMEWEZA KUHIMILI USHINDANI MKUBWA ULIOKUWA UMEJITOKEZA KUTOKA BENDI ZA WAKONGO YAANI FM ACADEMIA NA ACUDO. KAMA SI UONGOZI MAKINI WALIKUWA WAMEPIGWA BAO, LAKINI WANAONEKANA NGANGARI NA KUWA JUU ZAIDI. NI HUO UBORA WAO WA KUTOTETEREKA NDIYO MAANA WAMERUDISWA TENA KUPIGA CLUB BILICANA BADALA YA AKUDO NA FM ACADEMIA WALIOKUWEPO AWALI

    ReplyDelete
  10. Hayo maneno safu ya AISHA MADINDA, Lilian Internet na Super Nyamwela si mchezo wanapoamua kulshambulia jukwaa. Wananikumbusha enzi za Bilbums hapo hapo BILICANAS. I think it is worth going tommorrow wednesday

    ReplyDelete
  11. kaka michuzi naomba mawasiliano ya aisha madinda plizzzz.
    Mdau-Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  12. Mdau juu kauliza alikuwa wapi?. JIBUI. Aisha alikuwa mgonjwa kipindi fulani, so hakuwepo ulingoni kwa muda, na hata aliporejea alionekana kuwa mnene sana na akawa mzito kwenye unenguaji. Sasa ile shape yake ya mvuto ya umodo modo imemrejea na amekuwa mwepesi sana wa kunengua kama zama hizo. Ni tishio kwa kweli kwa wanenguaji wa kike

    ReplyDelete
  13. GOOD SIDE OF TWANGA PEPETA YA SIKU HIZI INAJIUZA YENYEWE KAMA TWANAGA PEPETA NA SIYO MAJINA TENA KAMA VILE ENZI ZA KINA ALLY CHOKI. SIKU HIZI AILYE STAR NA ANAYEKUBALIKA NI TWANGA PEPETA YENYEWE AS A GROUP NA HAKUNA CHA CHOKO,BANZA SIJUI THABIT ABDUL. WANAONEKANA, THEY WORK AS A TEAM. BRAVO

    ReplyDelete
  14. ukweli ni kwamba wamejiimarisha zaidi,bado wako juu,na hapa tanzania hamna bendi yenye wanenguaji tishio kama hii,

    mimi napenda sana muziki wa dansi especially hizi hizi bendi zetu za tanzania,ninaingia mara nyingi bendi zote,

    FM ACADEMIA,huwa wana kelele sauti za juu sana,na vyombo vyao VINALIA KAMA VINA KELELE

    ACUDO NI WAZURI SANA KATIKA SAUTI NA MIDUNDO,ILA WACHEZA SHOO WAO WA KIKE NI WAGUMU HAWAKATIKI VIZURI

    TWANGA NI WAKALI IDARA ZOTE
    TATIZO I DOGO TU MAMA LWIZA AKIIMBA ASIPANDISHE SAUTI YAKE NI YA JUU NZURI LAKINI ASIIPANDISHE SANA INAKUA INAZIDI

    nawasilisha

    ReplyDelete
  15. Naambiwa shoo ya Twanga Pepeta ya Juzi Jumatano Bilicanas ilikuwa ni hatari, kwani kulifurika watu kutoka kila pembe na warika zote. Nasikia Management ya Bilicanas imekiri kuwa tokea Bilicana ifunguliwe upya baada ya ukarabati wa sasa hakuna bendi kabla iliyowahi kuingiza watu wengi kama Twanga walivyoingiza ile juzi. G0 GO TWANGA zidi kutupa raha wabongo tujisikie. Ila msije mkabweteka kama mlivyowahi kufanya huko nyuma. NINAWAASA SANA SANA, manake mgema ukimsifia huzidisha maji kwenye mnazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...