Msanii nyota wa kizazi kipya ambwene yesaya a.k.a AY (pichani) sasa atatumbuiza katika jiji la johannesburg kwenye hafla ya Big Brother siku ya Jumapili ya Oktoba 4, 2009 na sio kesho jumapili kama ilivyotangazwa awali, kutokana na sababu ambazo hazizuiliki. Ataongozana na Snare wa east coast.

AY kaiambia globu ya jamii kwa njia ya twitter sasa hivi kwamba yeye kama kawaida yake hana show kubwa wala ndogo na kwamba show zote kwake ni muhimu hivyo anajiandaa kwa makamuzi ya nguvu. Amesema huenda kwa vile kesho wanaingia vimwana katika mjengo wa BBA ndio sababu zilizosogeza mbele shoo yake

hata hivyo kasema baada ya sauzi ziara yake ya Malaysia ambako atakuwa na show jijini Kuala lumpur September 24, mwaka huu ndani ya klabu cha Titunium ipo pale pale . Pia ataporejea anatarajiwa kutoa singo ingine mpya iitwayo 'Bed & Breakfast' ambayo imetayarishwa na Hermy B wa B. Hitz Studios.

Wakati huo huo AY anawakumbusha wadau wote popote walipo hapa bongo kumpa taffu kwa kumpigia kura katika tuzo za Mtv Africa. Kumpigia kura andika 'BHH AY' kisha tuma sms kwenda namba 0789 777 333

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Habari au Tangazo hili kaandika mzungu nini?? Mbona Kiswahili kibovu sana, halafu AFTER nyiingi, au mwandishi vidole vilikuwa na kwikwi?? Sitaki kuamini kuwa Tangazo hili kaandika, Michuzi, HammieB wala AY mwenyewe.

    Kila la kheri mzee wa Commercial.

    ReplyDelete
  2. Bro Michu, September 4 imeshapita

    ReplyDelete
  3. wabaya wapo huku nje wala sio tanzani walioko nje ndio wana kosoa mambo ya wabongo wenzao wanajiona wao hku ulayawana jua kila kitu.

    ReplyDelete
  4. mbona hatumuoni kwenye twitter, jina lake nani humo.

    ReplyDelete
  5. Huyu AY ameahirisha kwenda huko South ili kujinoa na kidhungu au kuna sababu nyingine. Nahisi haitakuwa tofauti sana na kanumba maana wabongo wengi kiinglishi ni matatizo.

    ReplyDelete
  6. We hapo juu nini kujishaua ati wabongo wengi english hawajui...angekuwa mchina hapo intepreter wold have been in board..na asingeongea english yao..why not kwa Kanumba??? Its true hakuwa anaelewa maswali since hajui kingereza ...wangetafuta mkarimani....usifikiri kila mzungu ni padriii...wapo wazungu pia hawajui kingereza tena ni wengi tuuuuuuuuuuu.Acha ushamba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...