Polisi wakiwa sehemu ya tukio

Baadhi ya abiria wakiwa wamebaki na butwaa mara baada ya basi lao kuwaka moto



BASI LA SINGIDA AIR LINES likiwaka moto leo mchana


NDUGU HABARI YA LEO.
NIKIWA NJIANI KUTOKA MWANZA NIMEKUTANA NA AJALI INGINE YA MOTO BASI LA ABILIA KUTOKA SINGIDA KWENDA DAR LILIPATA HITILAFU YA UMEME NA TAIRI HIVYO KUSABABISHA MOTO HUO.

KWA BAHATI NJEMA ABILIA WALIKUWA CHINI WAKICHIMBA DAWA LAKINI DEREVA ALIKUWA AKICHUNGULIA CHANZO CHA MOTO NDIPO TAIRI LILIPOPASUKA NA KUMJERUHI MACHONI AKAKIMBIZWA MANYONI KWA MATIBABU.


POLISI WALIFIKA KWA KUCHELEWA INGAWA SIMU ZILIPIGWA MAPEMA MNO. NA HATA POLISI WALIPOFIKA WALIKUWA WAMESHEHENI SILAHA KALI BILA HATA NDOO YA KUSAIDIA KUZIMIA MOTO HUO.HAPA SASA NIKO DODOMA NJINI KUJA DAR ES SALAAM
"EMMANUELEY MGONGO"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. barabara ya lami i wapi!

    ReplyDelete
  2. Thanks God abiria wengi wamenusurika. Hii ilikuwa ajali mbaya sana ukiona jinsi basi lilivyoteketea. Mungu ni mwema sana. Poleni abiria wote mliosalimika na hiyo ajali.

    ReplyDelete
  3. Thanks God abiria wengi wamenusurika. Hii ilikuwa ajali mbaya sana ukiona jinsi basi lilivyoteketea. Mungu ni mwema sana. Poleni abiria wote mliosalimika na hiyo ajali.

    ReplyDelete
  4. poleni abiria mlioathirika, hao polisi walitakiwa kuja na fire napo najua wasingefanya kitu maana tayari basi lilishaanza kuteketea.
    hivi hicho kipande cha barabara toka singida mpaka manyoni hakijaisha tu du namkumbuka magufuli

    ReplyDelete
  5. Poleni abiria na msukosuko huo, hivi kwanini polisi wasiwe na identity ya rangi ya magari yao? Kuandika Polisi tu haitoshi.

    ReplyDelete
  6. Nasikitika basi hilo kuungua moto ila nashukuru pia hakuna abiria aliyepoteza maisha yake.

    Asante reporter wa habari hii kwa kazi nzuri. Lakini unakosea haswa paragraph ya mwisho unapokimbilia na kuanza kunyooshea polisi lawama. Polisi wamechelewa kufika, sidhani kama ni sahihi kuanza kuwalaumu sababu hujui walikuwa wakifanya kazi gani huko walipokuwa. Hujui kama walikuwa na usafiri na kama huo usafiri ulikuwa na mafuta ya kutosha kufika eneo la tukio.

    Polisi hata kama wangekuja na ndoo ya kuzimia maji, unadhani ingesaidia? Ndoo ya maji na mkoa kama wa Singida, wangetoa wapi maji ya kuzimia hilo gari kaka? Tujaribu kuwa realistic na tutupe lawama kunapofaa, siyo kila sehemu ya kulaumu watanzania wenzangu. Siku hizi wabongo tunaongoza kwa kutoa lawama zisizostahili.

    Polisi walipaswa kuja na silaha sababu ndiyo kazi yao kulinda usalama wa raia na mali zao.

    Steve Dollongo, DSM

    ReplyDelete
  7. Si nilisikia mchanga hutumika kuzima moto na watu wanashauriwa kuwa na ndoo ya mchanga kama njia moja ya kujikinga na moto. Mbona hapa sioni ikitumiwa?

    ReplyDelete
  8. Steve Dolondo, hasira za nini kaka??...ahsante sana Emanuelley Mgongo, itabidi usomee uandishi wa habari, kazi nzuri sana

    ReplyDelete
  9. Wewe unayejiita Steve Dollongo umenikera sana na points zako zisizoeleweka, sina haja ya kuzirudia. Ushauri kwa Polisi mnapopewa taarifa ya moto, licha ya kwenda na silaha pia mnatakiwa kuongozana na wataalamu wa kuzima moto(Fire Dep).
    Emmanueley tunakushukuru sana kwa kutuletea picha hizi na habari ambayo imeeleweka vizuri kabisa. Asante sana.

    ReplyDelete
  10. Hahahahaaaa toka lini basi likawa air lines!?

    ziko airbus lakini hii ya basi la singida airlines imekuwa kubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  11. Huwezi kutumia maji kuzima moto wa mafut kwa sababau mafuta huelea juu ya maji.

    Huwezi kuzima moto wa kemikali kwa maji!

    Unatumia mchanga

    ReplyDelete
  12. ..poleni sana 'wahanga'..jamaa 'wameNUMBIsha' ilo jina: ati, Singida Airlines! ndo yale yaleee ya 'the most great', 'the most', 'the very very', 'the much much', the too much..nk nk..majina makuuubwa, vingine karibu ya 'zero' ni ka 'ukubwa wa pua'..

    ReplyDelete
  13. HII ILIKUWA NOMA. MIAKA HIYO MZEE MOJA KWA JINA KAMWALA . BAADA YA UCHUMI KUYUMBA ALITEGEMEA BIMA YA BASI LAKE MARA LIKAWAKA MOTO SIJUI KAMA WALIMLIPA. BAHATI MBAYA LILIUNGUA BILA ABIRIA. KWA WALE TULIOSOMA SAME SEC NA SHULE ZA JIRANI TUNAKUMBUKA JINSI HUYU MZEE ALIVYOKUWA ANATUPATIA MAHITAJI YETU DUKANI KWAKE TULIKUWA HATUKOSI KITU PESA ZETU TUU.

    ReplyDelete
  14. Poleni sana abiria wa basi hili mungu kawanusuru ilikua mchana lakini ingekua usiku ni vibaya zaidi, Na mimi pia nilisikia kua nyia sasa hivi imekua lami naona katika picha ni tupu kama kawaida yake, Sasa hii inatakiwa mabasi yote yawe na kizima moto kidogo ndani yake na hao wahusika wa basi wangeweza kutumia hata mchanga at least kuzima kuzima kidogo.

    ReplyDelete
  15. Isingekuwa busara kwa abiria kujaribu kwa namna yoyote kuzima huo moto.....hatari ya mlipuko wa tenki la mafuta na mifumo mingine ya kimakenika ingeweza kusababisha maafa makubwa....first thing to do whenever you are in that kind of situation is to "RUN" and try to stay far away as possible....unless you can figure out a 'safe' way to tackle the fire!

    ReplyDelete
  16. hayo mabasi singida yanaruka hewani? maana naona singida airline duhh... bongo tuko nyuma....

    ReplyDelete
  17. yan nimecheka karibia kuvunja mbavu nyie annons

    Mungu yupo na anaratibu kila hatua ya mwanadamu..ndivo ivokua hii ajali sipati picha mshtuko wa abiria mnachimba dawa mara puuuuh!!

    ofkoz annon iyo road wala haijaisha wala nn cjui itaisha lini pabaya sana apo..ndo mana watu wanafisadisha wapande ndege tu kanda ya ziwa ilhali nauli karibia na DUBAI air tickets mweee

    ReplyDelete
  18. mzee steve D, nimefurahi sana kuona comment yako kaka hapo juu.
    tuwasiliane mzee. ni mimi flamboyant. mahundi yuko wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...