wanafunzi wakiangalia digital billboards
leo viwanja vya biafra jijini dar
magari ya digital billboards yakipata
wese leo sheli ya camelcom bamaga, dar

digital billboards maeneo ya coco beach, dar. kila yanapopita magari yaliyobeba digital billboard huvutia macho na hisia za kila mtu, kudhihirisha kwamba hii ni njia bora na ya kisasa kwa matangazo
digital billboard likikatiza manzese

Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Afisa Mauzo wa Milestone International kwa number
0787339488
au
sales@milestoneinter.com
Unaweza pia kuona bidha nyingine nyingi kwenye tovuti yao www.milestoneinter.com






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Inanikumbusha enzi za sinema za bure za magari ya sabuni ya OMO Biafra DSM.

    Mdau
    Kijeba

    ReplyDelete
  2. Hahaha this is too funny..wabongo wanafikiri ni sinema!! LOL waangalie watoto wa shule wametoroka darasani kwenda kuangalia "sinema"..lol

    ReplyDelete
  3. Si ajabu kushangaa, hata hawa walioendelea wanashangaa wanapooona kitu kwa mara ya kwanza.
    ni sehemu ya ubinadamu .
    ni ishara nzuri ya kwenda na wakati bongo .

    ReplyDelete
  4. Nina wasiwasi ajali za barabarani zitaongezeka...

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kabisa "Tarehe Thu Sep 03, 12:11:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous" Ajali zitaongezeka. Hizi Billboards kwanini wasiziweke kama mabango mengine? Au watu watakomba hizo Billboards??

    ReplyDelete
  6. tatizo la bongo watu hawana shughuli zakufanya ndiyo maana kushangaa kwingi,kazi kupanga foleni kwenye ATM.

    ReplyDelete
  7. Ndugu wa Milestone,

    Hizi product zenu mna data za kusupport hiyo effectiveness yake?

    Mfano pale Posta mmeweka ile big screen. Lakini kwa eneo la wasomi na wajanja kama Posta kuna tatizo moja.

    Watu hawapendi kuonekana wanashangaa TV.

    Siku moja kaeni upande wa pili (pale chini ya BWM Towers) na muangalie ni watu wangapi wanatoa macho kushangaa livideo lenu.

    Pili kideo cha bila sauti hakina flavour. Unajua mtu anaelekeza macho kutazama ... anaona moving pictures ... lakini hasikii sauti ... Inakuwa sio natural kabisa.

    Mtu akiona moving pictures anategemea asikie na sauti pia ndio apate flavour.

    Kuna hawa jamaa wengine wanafunga viscreen kwenye sehemu za kupandia lift. Angalau wameweka sauti japo iko chini.

    Na pia ni natural kwa mtu kukodolea macho eneo la juu ya lift kwa sababu huwa wanatazama pia lift iko ghorofa ya ngapi.

    Lakini kukodolea macho juu ya mgorofa kama ule wa BWM sio natural kabisa.

    Ni dalili fulani ya ushamba, hivyo wajanja wa Posta wanakwepa kutazama kile kideo.

    ReplyDelete
  8. annon 9.33am...una akili mbovu sana

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  9. Hizi ndiyo zingetumika badala ya ule uchafu wa mabango uliojaa sehemu mbalimbali jijini DSM. Ninaamini manisapaa zingepata hela nyingi. Lakini kwa ujinga wao pengine hizi digital zinatumika lakini manispaa imelala.

    ReplyDelete
  10. anon 9:33 kama ni umbumbu basi huo wako umepitiliza full madenge, ni hayo tu lol kaaazii kwelikweli

    ReplyDelete
  11. anon wa 9:33 inaelekea wewe ni msomi maana uchambuzi wako japo ni fasta fasta umetulia kweli na una mifano ambayo hata mimi imenigusa.

    binafsi huwa hata sipotezi muda kushangaa shangaa haya madude.

    ReplyDelete
  12. nimetembelea nchi kadhaa,within and outside the african continent.And i saw quite a lot of things for the first time.Digital billboards zinawekwa sehemu ambapo ziko stagnant.it is very dangerous kuweka hizi billboards kwenye moving vehicles.Mheshmiwa aliyezungumzia suala la ajali ana point kubwa.PIli zinabidi ziwe regulated na the commercial community na manispaa.hii ni kupunguza uchafu na kuhakikisha advertisement hazivuki mipaka.Hizi boards zilizoletwa bongop zinakuwa introduced kiholela,lakini kama manispaa zetu haziwezi kuondoa mabango ya miaka ya eighties barabarani,whos to blame??
    The way i understand it wafanyabiz wanaoweka mabango wanabidi walipe manispaa na manispaa in turn ihakikishe mabango hayaprotude sehemu yasipotakiwa na kwamba yanakuwa removed pindi yanapopitwa na wakati.Our municipal services do none of the above services.Ndio maana entrepreneurs kama hawa wana un regulated ideas.
    DK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...