Mcheza filam ya Bbay Powder na rapper Justellh akiwa na Sunday Simba Shomary, mtangazaji wa VOA idhaa ya kiswahili katika mnuso wa Labour Day weekend Washington DC ikiwa ni katika pilika pilika za kutangaza filam hii mashuhuri itakayoanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza huko Atlanta Georgia mwezi Novemba mwaka huu.
Fundi Ima akiwa amezungukwa na wacheza filam wa Baby Powder kushoto kwake Justellh na kulia kwake Tuni na Wada ambao ni mashoga katika filamu ya Baby Powder.

Hawa ni baadhi ya wasanii waliocheza filamu ya Baby Powder walipovamia jiji la Washington Dc katika kutangaza filam yao na kusheherekea Labour Day weekend. Kutoka kushoto Sajo,Babu Sikari-rapper na mcheza filam,Tuni muigizaji mwandamizi wa kike,Lambert a.k.a LBT muigizaji mkuu na Justellh muigizaji na rapper machachari wa ATL.

Kundi la baadhi Waigizaji wa Baby Powder na maprodyuza wao.
Picha zote kwa hisani ya Sunday Shomary


MWANDANI WA BABY POWDER
PHILIP NKASA (Lambert "LBT" Tibaigana) ni kijana wa kitanzani anakwenda marekani kwa matumaini ya kupata elimu ili kuweza kuboresha maisha yake na ya familia yake nyumbani. Philip ananzaa maisha yake ndani ya marekani katika mji mdogo wa Wichita,KS na baada ya kumaliza shule na kushindwa kupata kazi ,Philip anakata shauri kwenda kujaribu bahati yake katika jiji la Atlanta, GA.
Mambo hayawi kama Philip alivyo tegemea upatikanaji wa kazi Atlanta unakua wa shida,ili kuendesha maisha Philip anachukua kazi ya malipo kidogo pamoja na kuaa ana degree...hali ya maisha ya wazee wake inaendela kua mbaya kutokana na mapato yake kidogo anashindwa kuwasaidia,Baada ya kugundua mfanyakazi mwenzake Mamdo (Albert Levasseur) anafanya biashara haramu, Philip anona nafasi ya kutatua matatizo yake...

Lakini baada ya kuonja asali anachonga mzinga na kuingia katika biashara haramu kwa nguvu zote. kutokana na kukua kwa biashara yake Philip anaoneza msaada kutoka kwa vijana wenzake Tizo ( Carlos Mwaibulla) Chuma (Ulimboka GWAII Mwanjabala) Wesi (Hadji saidia) kwenye wengi hapa haribiki jambo lakini kundi hili linaubadilisha msemo huo....( mengi yana haribika)Philip anaingia mapenzi na mrembo kuoka Kenya WARIDI (Tuni Ngigi) ambaye anashindwa kumuambia ukweli kuhusu biashara zake,lakini za mwizi arobaini,Waridi anakuja kugundua...utamu unafikia kilele hapo.....
Majina ya waigizaji
Lambert Tibaigana- PHILIP NKASA
Tuni Ngigi WARIDI
Carlos Mwaibulla TIZO
Ulimboka Mwanjabala CHUMA
Hadji Saidea WESI
Lydia Mbuah JOSELYNE
Warda Hassan JACKEY
Dynamic DULAH
Albert Levasser MAMADO
Babu sikare KAI
na wengine wengi....

BABY POWDER ni filamu inayo elimisha, sikitisha ,furahisha,na kutia moyo...na ni mkasa wa kuburudisha...Filamu hii haita toka kwenye DVD mpaka mkatikati ya mwaka 2010 nafasi pekee ya kuiona filamu hii ni wakati wa uzinduzi rasimi katika sehemu mbali mbal.

Kwanza kabisa BABY POWDER itazinduliwa rasmi:
*ATLANTA,GA November 14th 2009,
*HOUSTON,TX ( November 26th 2009)
*WASHINGTON DC ( December 5th 2009)
*MINNESOTA ( December 19th 2009)
tour ya AFRICA/EUROPE kuanzia DECEMBER 25th 2009

tembelea
www.jake-productions.com
au angalia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Eh bwana jamaa inaonekana wametulia na kazi zao! Mi naona Kanumba sasa akae mkao wa kula labda jamaa na wao Kiiglish kiwe kinagonga ugoko! Lakini nawaaminia babaake! Sasa miji mingine lini tunaomba tujulishwe mapema! Kazi nzuri bandugu !

    ReplyDelete
  2. mtoto katulia, jicho jicho, mtoto we hata uki-act movie mwaah.

    Sawa Man City mmetufunga ila tutawafunga Bwawa la maini.
    Arsenal oyee.

    wanaume kama panya wanakimbia kimbia wakitafuta mashimo wajifiche.

    ReplyDelete
  3. kamwulize jackie chain kama kufanikiwa kwake kumetokana na kujua sana English,kwanza vile vile tuelezee English subject ulipata Grade gani?
    You are a stupid man, unajifanya kimbelembele ati kanumba cannot speak english, kama unajua sana Lugha inapanda sana tuandikie Essay.
    outline:
    explain about yourself, where are you from?,what grade did you get in English exam?

    ReplyDelete
  4. LBT.Houston tupo kukufagilia, tunaubiri baby powder, we got ur back Hongera na Kila la kheri.Gud Job!

    ReplyDelete
  5. Tuni,tunu kwelikweli!! mtoto mzuri kama vile kafinyangwa!! jichojicho

    Mdau wa Juu

    ReplyDelete
  6. Fundi Imma kama nakuona vile henzi zetu za ufundi AFOL, mzeeyaa hapo husije ukafanya ufundi wa watu maana hizo konozii na hayo maua itakuwa tabu bdae...

    ReplyDelete
  7. hUYO MBONGO ANAJIFANYA MJAMAIKA ANABOA SANA. ACCENT YA KIJAMAIKA WAPI NA WAPI?? WEWE NI MBONGO TULIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...