Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja anawashukuru wadau wa Stockholm na kujiunga kuombea dua futari ya mwisho kwa mwaka huu wakiongozwa na mwenyekiti wa Watanzania Sweden Bw. Khalifa Zam. Wa pili shoto ni kaimu balozi Mh. Victoria Mwakasege Mheshimiwa Ngeleja anapozi na wadau baada ya kufutari jijini Stockholm. Chini ni wadau waliohudhuria futari hiyo ubalozini na chini ya hii ni Mh. Ngeleja akiwa na Mwenyekiti wa Watanzania Sweden Khalifa Zam
wadau wakifutari
wadau wakifutari
Wadau wa Sweden wakijumuika kupakua futari








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Duh wadau wa Stockhnyoko kweli wanafuturu futali ya mwisho
    tupeni email zao mwakani tuwaalike Tensta

    ReplyDelete
  2. Inashangaza sana. Nimeishi Finland miaka miwili tayari na nimeanza wa tatu, toka nifike hapa Finland sijawahi kusikia mheshimiwa balozi akitutembelea watanzania tuishio Ufini.

    Kinadharia nchi za Sweden, Finland na Norway (sina hakika kuhusu Denmark) huwakilishwa na balozi mmoja na ofisi za ubalozi zipo Uswidi (Sweden). Lakini kiuhalisia huyu anaonekana ni balozi wa Tanzania Uswidi!

    Anyway, pengine huyu atakuja one day. Lets see. Tafadhali muheshimiwa tutembelee siku moja, tunahitaji kukkutana nawe.

    ReplyDelete
  3. Lakini hii miguu ya kuku yamechinjwa kihalali???na sikia kule ughaibuni hakuna mabucha wa ki 'halali'...bugia tuuu!!!

    ReplyDelete
  4. hao wadau mbona wanaikodorea hivyo camera au ni mara ya kwanza kuiona?
    haya tena mtanisamehe kama ni mewakwaza

    ReplyDelete
  5. Waafrika tunapenda sana kula vyakula visivyokuwa vya mbogamboga. Ukichunguza minuso yetu utakuwa nyama, mchele, ngano vimetawala.
    Tofauti kubwa ya ulaya na ughaibuni ni kwamba ughaibuni matajiri wanaishi maisha marefu kuliko masikini na hii inatokana na tofauti ya lishe zao. Lakini Afrika ni tofauti sana, matajiri wanaishi maisha mafupi sana kwa sababu ya kula vyakula vibovu.

    ReplyDelete
  6. hawa wadauzi wametoa macho kihivyo kulikoni?au hamkuwatarifu

    ReplyDelete
  7. Mdau uliyesema huko ughibuni hakuna mabucha ya halali umekosea kuna maduka yanauza Halali food na nk. so usifikiri ukiwa ghaibu hakuna waislam wanaofata sheria ya dini, na ukitaka kula vibudu na visivyo halali ni khiyari ya mtu tu
    au kutojua maduka ya chakula halali.

    ReplyDelete
  8. Mdau,
    Sat Sep 19, 07:55:00 Anonymous

    Unaishi Finland ipi? Balozi Ben Moses ambaye aliondoka mwaka jana 2008 alikuwa anakuja kututembelea mara kwa mara. Tulikuwa tunakuwa naye katika shughuli za kiofisi na kibinafsi. Namba yake ya simu na email yake karibuni watu wote hapa Finland tulikuwa nazo. Tangu aondoke Balozi Ben Moses hajateuliwa balozi mpya na huyo anayemkaimu ndiye ambaye hajafika Finland kuja kujitambulisha wala kutujulia hali.

    ReplyDelete
  9. Balozi wa wilaya ya nanii,naomba niulize swali moja ni hivi kila ukifungua michuzi blog,unakuta picha za wadau mbalimbali wakifuturu ,lakini swali langu ni je wanafunga kweli??au kufuturu imekuwa kama mtindo tu?hasa mwezi huu wa Ramadhani ambao tunaumaliza leo?Eid Njema

    ReplyDelete
  10. nawaona wadau hapo wanavyoinjoy pamoja na sister zangu na mashemeji zangu
    kila la kheri
    mdau m6

    ReplyDelete
  11. asante sana mtoa maoni wa tarehe 19.09.09 saa 07:55. ni kweli yawezekana kabisa kwamba muheshimiwa balozi Ben alikuwa anakuja Finland na namba na email yake ''karibu wote'' mlikuwa nazo - NOT ME!

    Tena sijawahi kusikia ujio wake toka nije ufini mwaka 2007 sept, yawezekana nilikuwa sina connections bado, let say for the first three months. But since then, sijawahi kusikia yet - kwani ujio wake ulikuwa mkitangaziwa wapi? AMA THROUGH YLE TV? Maana kwa blog hii ya jamii sijawahi kuona taarifa kama hizo.

    yawezekana alikuwa anakuja kwenye shughuli zenu binafsi kama ulivyosema, is ok na hakukuwa na haja ya kutangazia uma ujio huo.

    Usiwatetee hawa watu, they have to work because they are getting tax payers' money. Huyu balozi mpya alikuja around April/May this year kwa taarifa yako. Since then, hajatia mguu ufini, ama amekwisha kuja kwa shughuli zenu binafsi pia? HUYO NI BALOZI WETU SISI SOTE. miezi minne sasa, lets see.....!

    ReplyDelete
  12. Labda kama unataka kuleta zogo tu humu.
    ....umeshawahi kutumia muda wako kila alfajiri pale vingunguti ukajionea mambo yanavyoenda? ngombe wa wizi wanachunwa nje ya machinjio , hakuna daktari kuthibitisha wala nini, sembuse hiyo habari ya Halal ???

    ReplyDelete
  13. Acheni kunyanyapaa wenzenu hivyo. Kwani mwenzio akichinja kwa nini usile? Sasa kila mtu hapa duniani ale alichochinja mwenyewe itawezekana kweli? Kumbuka tuko zaidi ya bilioni 6. Logic ya arguments nyingine km hizo sijui iko wapi?

    ReplyDelete
  14. Sun Sep 20, 09:02:00 PM

    Asante kwa majibu yako. Naomba nikushauri ili kwamba uwe unapata taarifa za matukio mbali mbali yanayowahusu Watanzania hapa Finland tafadhali wapatie contacts zako Ndugu Humphrey Kalanje, Dennis Londo, Dj Eza, au Dk Eduard Mtafungwa. Pia ukijiunga na Chama cha Urafiki kati ya Tanzania na Finland (Suomi-Tanzania Seura)au Jumuiya ya Watanzania Finland(Association of Tanzanians in Finland TAF)Utakuwa unapata taarifa zote za matukio mbali mbali hapa Finland.

    Siku ya sikukuu ya uhuru Dec 2007 iliyofanyika Helsinki Balozi Ben Moses alikuwa mgeni wa heshima. Katika mabalozi tangu enzi ya kina balozi Mloka, Mhina, Fatuma Tatu Nuru, Marehemu Tibaijuka, Katega hadi Ben Moses naweza kusema na Watanzania wa Scandinavia watakubaliana na mimi mabalozi wote niliowataja walikuwa karibu sana na jumuiya ya Watanzania isipokuwa balozi mmoja tu kati ya hao na siyo Marehemu Tibaijuka au Ben Moses. Maofisa wetu wa ubalozini mjini Stockholm kuanzia kina Mama Mwakasege, Nginila, Sanga hadi Mwaipaja walikuwa wachapakazi haswa. Tena huyu Ndugu Mwaipaja sijui alienda wapi jamaa alikuwa ni 100% super efficient.

    Siwezi kusema najua kila kitu na ninakushukuru sana kwa kunifahamisha kwamba tayari tuna Balozi mpya mjini Stockholm. Naomba unipatie jina lake. Asante.

    ReplyDelete
  15. Jamani mie nataka nitoke kidogo nje ya mada....aiseee dada mwenye nguo nyeusi na nyeupi wa pili toka kushoto (JINA KAPUNI) naomba tuwasiliane kupitia kwa kaka ISSA MICHUZI...Nimeshamuachia contact yangu...MIMI NDUGU YAKO BABY S.

    ReplyDelete
  16. we unayehoji uhalali wa nyama ulaya kumbuka, "baniani mbaya lakini kiatu chake dawa". wengi walienda ulaya kwa emirates, gulf air, nk lakini hawakukubali kushuka transit yaani nchi za uarabuni kunakosifika kwa uhalali. na hizo nchi zinazosifika kwa uhalali wa nyama, zina ubaguzi kuliko hizo wanazozilaani lakini kuondoka hawataki. jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. mzungu angalau ni mwema lakini muislam mwenzangu muarabu ...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...