steve kanumba akipokelewa kwa shangwe alipowasili toka sauzi alikoshiriki kwemnye Bog Brother IV kama starmate
wadau na wapenzi kibao walikuwepo eapoti ywa uwanja wa ndege wa dar kumpokea kanumba
kanumba akihojiwa na wana habari
kwenye mnuso ulioandaliwa na wasanii wenzie kwa heshima yake

vincent kigosi a.k.a ray akiongea kwenye mnuso huo. Ray alitoa masikitiko yake kwa jinsi watu walivyokuwa wakimbeza Kanumba kwa madai ya lugha gongana ya kiinglishi na wasanii hao inas
emekana wanaandaa waraka maalumu kupeleka serikalini ili kukomesha mambo kama hayo
anko nanihii akiongea na supa staa steven kanumba muda mfupi uliopita walipofanya intavyuu exclusive juu ya mustakabali wake katika mjengo wa Big Brother Africa IV ambako alialikwa kama star-mate kwa masaa 24. intavyuu hii ambayo imerekodiwa kwa video itarushwa muda si mrefu ujao.
pamoja na mambo mengi Kanumba ametoa masikitiko yake kwa kashfa nzito alizolengwa nazo na baadhi ya wenye roho za korosho kwamba kiinglishi hakipandi, madai ambayo amesema si kweli.
ushahidi wa kukanusha kwa Kanumba utaupata kwa kumuangalia na kumsikia kisha amua endapo kama madai hayo ni ya kweli ama uzushi tu wa baahi ya wadau. utakuta wengine hao wanaokosoa ngeli iko ugokoni ila hodari kuchonga utadhani wao ni malaika wasiotindikiwa na kitu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. naomba nisaidie kumuuliza Bro Kanumba kama ameshalisikia tangazo la Ditective Tibaigana Clouds Fm Radio teh teh teh

    ReplyDelete
  2. Waraka wa nn ss, kama inglisi ziro ni ziro tuu....kwisa kazi....

    ReplyDelete
  3. kwanini wabongo tunakuwa wajinga hivi?kama mtu hujui vizuri lugha ya mkoloni unachekwa!Ni lini tutaamka kutika huu usingizi ambao unaelekea ni wa milele.

    ReplyDelete
  4. Kwa hilo wabongo hawajamtendea HAKI Kanumba..Nimesoma na wachina ,wajapani na wakorea ukisikia kiingereza chao wakati wa presentation unaweza ukalia ,lakini pamoja na hivyo wanaendelea mpaka wanachunkua degree..NI KWAMBA ENGLISH SIO KIPIMO CHA KUJUA AU KUTOKUJUA KITU.
    Kanumba english sio mother tongue yake kwa hilo hamjamtendea haki.SHAME ON U BONGO PEOPLE, haka kanchi kuendelea ni ndoto.
    Mdau wa UK

    ReplyDelete
  5. WATANZANIA WATANZANIA NANI ALITULOGA, LUGHA YA KIINGEREZA NI LUGHA YETU YA PILI, JE KUTOKUWEZA KUONGEA LUGHA HII KWA UFASAA NI DHAMBI AU NI ROHO MBAYA TU NA WIVU, ANGEKWENDA ANAYEWEZA LUGHA HIYO VIZURI WAOSHA VINYWA NAO MSINGEKOSA LA KUSEMA. HEBU WATANZANIA TUONGEE MAMBO YA MSINGI TUACHE KUBWABWAJA KWA MAMBO YASIO NA MAANA.
    HONGERA KANUMBA USIVUNJIKE MOYO CHA MUHIMU NI KUANGALIA MBELE, LUGHA HAUWEZI KUJUA KWA SIKU MOJA.
    TUMEKUWA TUNAFANYA KAZI NA WATU WA NJE YA TANZANIA AMBAO KIINGEREZA NI LUGHA YAO YA PILI, WE! USIOMBE LAKINI HATUWEZI KUWACHEKA KWA VILE NI WAZUNGU. NANI KATULOGA TUNADHARAULIANA HIVI BADALA YA KUTIANA MOYO NA KUREKEBISHANA KWA UPOLE PALE TUNAPOKOSEA.
    WATANZANIA HAWAIWEZI HII LUGHA KWA VILE TUNAOGOPA KUONGEA MBELE ZA WATU TUTACHEKWA, NA HII LUGHA HAIPANDI BILA MAZOEZI.
    TUBADILIKE TAFADHALI

    ReplyDelete
  6. huyu Kanumba na mwenzake Ray ni wajinga kweli wao ndio waliokua wanashabikia eti ili uwe msanii mzuri wa kike hapa bongo ni lazima uwe na mvuto. Kwa upande wa kanumba yeye alikuwa anasema good looking na Ray yeye alikuwa ansema appearance sasa nani aliwaambia mvuto kiiglish mvuto ni hayo waliyokuwa wakiyasema. sasa na yeye ajue kama wale wadada aliowananga hawana good looking basi na yeye akubali kuwa hana good english. mkuki kwa nguruwe eheeee. kazi mapowder tu na malipshine watoto wa kiume inahuuuuu???!!!!

    ReplyDelete
  7. Hawa wajinga kweli dawa ya ki-english kuwa not reachable ni kwenda english course! Kwisha kazi mi sasa nitaacha kununua movie zao maana naona somo wanalolitoa kwenye movie zao na taswira yao ni tofauti! tena Kanumba ashukuru wamemtoa mapema maana PR yake ingeharibika kabisa

    ReplyDelete
  8. mimi sioni tatizo, yeye ameongea alichoweza,watanzania hicho ndio kiingereza chetu, hata ukienda universties zetu utakuta professor wetu wanaongea hivyo hivyo. tusiwe na wivu wa ajabu ajabu. hii sio lugha yetu ya kwanza. Tumpongeze tumpe moyo nafikiri iko siku tutafika. Watanzania tubadilike katika kukosoa mambo ya msingi, tupeane moyo, leo watani wetu(wakenya) wapo maeneo mengi kwa vile hawakatishani tamaa, sisi tumebaki tunakosoana hata kwa mambo ambayo tungeweza kurekebisha. Tunaogopa hata jumuia kwa vile tunahisi watatupita. Watanzania tuamke kwenye huu usingizi, la sivyo tutakuwa tunakwenda hatua moja mbele na tunarudi hatua mbili nyuma.HONGERA KANUMBA UMEJITAHIDI KWA ULIVYOWEZA, MIMI NIMEONA UMEFANYA VIZURI, LUGHA KWANGU NI MUHIMU LAKINI HANIFANYI NIMSHUSHE MTU HADHI YAKE KAMA UJUMBE ULIFIKA.

    ReplyDelete
  9. mara nyingi waTZ tunapenda kuwa kinyume na kila kitu! yaani tuna wivu wa mtu na mke mwenzake! kwamba ataka apate yeye mwenziwe asipate! tuwe na wivu wa maendeleo jamani!! tujiulize kanumba kafikaje kwenye mjengo ule na c tufikeeee!! siyo eti hajui kiinglis!! mzungu akija hapa akashindwa kuongea kiswahili mtamchekaa!! acheni ushamba watanzania

    ReplyDelete
  10. Huyo Ray, bora akae kimya, Kwani kama hujui kitu ni bora kunyamaza kuliko kuonesha watu ulivyo mtupu,
    Toka lini Serikali ikatoa walaka kutuia watu kutoa Maoni, Yeye jana ameona Rais alivyokuwa anapokea Maoni ya Watanzania, si yote yaliyomfurahisha, Kama Rafiki yake hajui Kiingereza amshauri waende wote Kozi ya Kiingereza na wawe watu wa Kujifunza vitu ili wawe waelewa wa mambo mengi,
    Huo Waraka utasaidia nini Wakati hata Kenya na Uganda Wamemponda, Sasa Serikali itawanyamazisha na Wakenya ?
    Ray acha ujinga, Wewe na Kanumba mnalipia gharama za kukimbia Shule, Jipangeni upya na msome

    ReplyDelete
  11. English ndio ni lugha kama zingine. Lakini kama hujui lugha fulani kwa nini ulazimishe kuiongea? Nadhani cha msingi ni kuacha kulazimisha kufanya mambo ambayo hujui hasa mbele za watu.

    Matokeo ya kulazimisha mambo ndiyo haya aibu kibao sasa.

    Tanzania english inafundishwa kuanzia primary na secondary mpaka vyuo vikuu ndiyo lugha kuu ya kufundishia hivyo kama mtu aliyesoma mpaka form four anatakiwa aweze kuongea english bila matatizo kwani utakuwa ametumia english kusoma na kuandika kwa muda wa miaka minne.

    Lakini wabongo wengi wakimaliza form four wanakuwa bado english haipandi. Hili ni kwanza kubwa kwenye mfumo mzima wa Elimu ya Bongo. Kwa maneno mengine ni tatizo la kijamii.

    Kitu muhimu, kujua katika anga za kimataifa kiswahili hakina nguvu, kwani ni lugha ambayo maneno yake hayajitoshilizi. Huwezi kuzungumzia sayansi, uchumi au biashara za kimataifa kwa kutumia kiswahili.

    Kazi ipo kubwa tu ya kuboresha hii lugha.

    Wizara ya elimu vipi hapo?

    ReplyDelete
  12. ankoli nanihii akiongea na supa staa wa bongo steven kanumba aka maimuna...balozi mwambie kanumba kutokujua kiinglishi siyo dhambi coz ataalikwa kwenye usahili na kina sembeyu atatoka nduki,,,ehehheee

    ReplyDelete
  13. waraka wa nini? kukomesha mambo gani? Kwa hiyo serikali itatoa tamko kama lifuatalo " Ni marufuku kwa kanumba na Ray kutegemewa kuongea kiingereza sahihi, ni marufuku kutegemea kumwelewa Kanumba na Ray wakiongea kiingereza, na pia ni marufuku kuwakosoa Kanumba na Ray kuhusu wanavyoongea kiingereza"

    ReplyDelete
  14. Michuzi kama unamjua Kanumba nakupa huu ushauri umfikishie mwenyewe,Kwa kifupi Kanumba asijali watu wanaomsema kiingrishi hakipandi kwani si lugha yake ya kwanza,pili kipaji cha kuigiza anacho na hiyo ndio what matters,Mimi niko UK na uagiza filamu za kanumba jamaa ana kipaji ila akijiendeleza kidogo mfano kama ana hela za kutosha aende akasomee mambo ya filamu na uigizaji nje ya nchi pamoja na lugha na haweze kujimantain vizuri ana uwezo hata wa kupata kazi nje ya nchi wanakoitaji waigizaji weusi wanaotoka Africa,Nakumbuka nilikuwa na rafiki zangu waingereza (wao ni maproducer wa filamu nk)wakasema kuna upungufu wa waigizaji weusi wanaotoka africa hapa uingereza kwenye filamu na dramas au michezo yao ya kuigiza nk,ila ilikuwa kitambo kidogo. Kwahiyo Kanumba aachane na watu walio na fikra za kijinga kuwa english ndio kila kitu but still anaweza kujiendeleza na akaongea lugha vizuri tu atizame mifano ya wana hiphop wa kibongo kama Mwana FA na Mr 2 au Mr Paul wanajiendeleza kimasomo uku wanafanya shughuli zao za kila siku za kimuziki

    ReplyDelete
  15. Wakiandika waraka waandike ili serikali iwasaidie kunoa sanaa yao kuanzia lugha na mengineyo kutokana na yaliyomtokea msanii wetu mkubwa Kanumba. Na wengine wasilale na kuridhika kuwa walipo. Waliomchagua Kanumba wamefanya vizuri ili kuweza kuwafunua macho watu wengine nao wakaze buti.

    ReplyDelete
  16. Stop Ujinga Ray kila kitu Serikali ujinga gani?Think utoto unawasumbua jamani hiv uliangalia siku ya ufunguz alikuwa anajibu tofauti na maswali ,Hatukatai ni Actor ila wako Celebrity kibao Bongo Watangazaji wazuri Ushauri muende British Council mkapate msasa sawa ,South tu walipeka watangazaji ingekuwa Miss Tz nyie kina Ray na Kanumba midomo juuu ooh hajui kizungu leo Ama kweli Nyani Aoni Kunduleeeee.DSTV Wamechemsha si bora wangempeleka Nancy Sumari Miss World Yeye kanumba katuletea nini Toka Kaole na kwenda Nigeria kutaliii anajiona kizungu anajua

    ReplyDelete
  17. Hee makubwa RAY!nadhani mgeomba waraka wa kudai kwanza haki miliki inayowapa kula yenu na watoto wenu kwenda WC kuliko upuuzi huo eti waraka !Hata serikali wameona aibu ya huyo Kanumba eti celebrity!Kama ni mie ningeomba waraka wa sponsor kwenda nje kusomea fani na english kwa ujumla hata mie ningemchangia nauli ya Kanumba!

    ReplyDelete
  18. Wewe Ray ndo uchicheme kabisa!bora Kanumba wa watu lakini kime mtouch duuu!!!!!!!! kuliko hata alivyovunjiwa gari na Wema Sepetu acha Jazba wewe ndio maana ukamuweka ndani Wema wa watu Sero na mlikuwa mwa share one bed!dah!

    ReplyDelete
  19. Wee Ray na kanumba wako rudini class ndo mtakuwa really celebrity kubalini ukweli!oneni movie zilizokwenda shule za wenzenu wa clouds FM!Mie hata sioni movie gani nzuri ya kanumba!tena bora ze comedy wana act kuliko kanumba!

    ReplyDelete
  20. Kiingereza ni Second au Third Language kwa sisi waTanzania. Tunajivunia kwa kuongea Kiswahili fasaha (perfect and proper). Safari nyingine Kanumba aongee Kiswahili halafu waweke sub-titles au awe na mtafsiri. Halafu utaona wimbi la watu wanaotaka kujifunza Kiswahili. Hapo tumekosa nafasi ya kutangaza lugha yetu.

    ReplyDelete
  21. you guys don't know how to think sasa waraka wa nini hammeki sensi kwa kweli hamjakua kiakili bado ubishoo tu hamnakitu.
    mdau
    canada

    ReplyDelete
  22. ningekuwa kanumba nisingejali hata chembe, maana hii ni pure wivu, wanamuonea donge tuu kwa maana wao wanaokijua hicho kiingilishi chenyewe hawakuchaguliwa kwenda mjengoni na wala hawajulikani, kanumba kaka kaza buti achana na waosha vinywa kwa nothing, muhimu big brother alikuelewa na hao wote walikuelewa sema ndiyo hivyo wivuuuu umewajaaa, waambie waende wao sasa wakakiongee waone kama watakaribishwa mjengoni

    ReplyDelete
  23. KM KIINGEREZA NI LUGHA YAKO YA TATU, MBONA HUWA UNAZIPA MAJINA YA KIINGEREZA MOVIE ZAKO? Katika kitu kinachoniboa na movie za kibongo ni kitendo cha kuzipa majina ya kiingereza halafu maudhui yake ndani ni ya kiswahili. Hii ni ukosefu wa utalaamu kabisa (LACK OF PROFFESSIONALISM). Hebu fikiria mtu asiyejua kiswahili ananunua movie ina jina la kiingereza halafu akienda kuangalia watu wanaongea kiswahili, yaani huyu mtu hawezi nunua tena movie zenu hizo. Inabidi mjipange kiukweli katika soko la kimataifa, maana movie zenu zinauzwa hadi nje ya nchi. Kwenye soko la kimataifa mnaonekana matapeli wa kutupwa. Wewe fikiria unanunua movie yenye jina la kiswahili halafu ndani watu wanaongea kihehe. Haileti maana kabisa. Nadhani Kanumba mtajirekebisha, kama hamjui kiingereza zipeni majina ya kiswahili, vinginevyo muwe mnaziwekea subtitle kwa kiingereza.
    Kaka kama ulichemka big brother kanowe kiingereza chako, maisha ni kujifunza na daima tunajifunza kwa makosa.

    ReplyDelete
  24. Eti Africa nzima walimuona yeye ndio celebrity bora ndio maana wakamuita BBA duh!Kanumba acha fix bwana sema nilibahatika sio kwamba Africa nzima wewe uko juu NOPA!Wako Acters and actress kibao wamekupita naona 1000% kwako wewe!So futa usemi eti walikuona wewe tu!Acha kuji proud ndo maana unapata madongo!Hivi ungekuwa kama Sauda Simba Kalumanga sijui ungetambaje?mwenzio aliitwa movie zilizoenda shule plse go back Maimuna school!

    ReplyDelete
  25. Mwanangwa siku nyingine wasemeshage kwa KISUKUMA

    ReplyDelete
  26. Kwani kuna makosa gani mtu asiyejua au kuelewa kiingereza?Wabongo wengine ni wapumbavu sana.Kuna waigizaji kibao wanashinda OSCAR kila mwaka hawajui hata kuandika A,B,C,D... itakuwa huyu.

    ReplyDelete
  27. Mr. Michuzi, I think each and every person adding any comment either against or for this discussion better express his or her views in english. That way we will see who actually can communicate better or worse than Mr. Kanumba even though I'm not supporting Tanzanian representatives not to be the best ones we can offer especially when it comes to communicating properly in english or any other foreign language.
    When you are a representative means that you the best of the best and your opinion has values and you will not take the blame solely but also with whom you are representing. In this case each one of us provided a bad picture as Tanzanian to whomever paid close attention to the broadcasting of the BBA thereto!
    I understand that english and many other languages are our second, third or even fourth languages bearing in mind our mother tongues and any other tribal languages spoken at home if there are any. But that should not be out excuse to not communicate properly. For instance Kenyans and Ugandans speaks very well both in english and their local languages. We will say that we don't learn like them, then let's meet the challenge and be the best we can be.
    Even if we laugh at each other and find ways to put one another down, it won't solve anything as it still remains that, we cannot communicate well in foreign languages especially english in that matter.
    It is time for Tanzanians to wake up and smell the cappuchino, and quit pretending to be great at things while majority are not.
    Whether we like or not, most great jobs in our country will be taken by foreigners if we don't educate ourselves and be proud of each other. Remember, 'to learn is to change, and education is a process that changes the learner' so carry on.
    My advice to Kanumba and the likes, take this as a challenge and accept constructive criticism whenever occurs and take any negative you so far felt out of it and turn it into positive.
    Besides, don't just accept any position just because you can fly for leasure instead of getting the job done, if you can't conquer the task be frank and let the procient person do the job. And this goes from the higher ranking officials tot he lowest ones...
    I guess is how things are done in Tanzania for years!!!!!
    We gotta change!!! and change begins now... carry on my people.

    ReplyDelete
  28. Unajua watu wamekusakama kwa sababu unajifanya bab kubwa, wewe huoni watu kama kina Michuzi ni baadhi ya watu ambao wamefika mbali kitaaluma lakini wako down to earth na ndio sababu ana support kubwa ya watu kwa sababu si mtu wa KUJIINUA MABEGA kama wewe Kanumba, Michuzi lugha inapanda lakini si mpenda misifa kama wewe na anajiweka simple tu, sasa wewe unapokuwa uko kwanye goodtime huna time na watu halafu ati unategemea UKIYAKOROGA watu wawe upande wako, hiyo haipo. Kwa ufupi umetia aibu kubwa tu, usianze kujitetea wewe jaza form za english course mapema tu!

    ReplyDelete
  29. Mimi ni mtanzania na ninaishi ughabuni,baada ya kupata taarifa za ndugu yetu Kanumba jinsi alivyokashifiwa na Watanzania wenzetu "TUNALAANI KWA NGUVU ZOTE" na wote waliohusika kwa kutuma ujumbe wa maandishi ya kashfa juu ya msanii wetu huyo,pili TANALAANI Radio zote zilizohusika na kukashifu juu ya Kanumba ,wabongo wenzetu naomba muelewe kuwa kingereza ni kama lugha nyingine tu,jaribuni kutembea muione dunia kila mtu anajivunia lugha yake duniani,jaribu kufika italy uone kama hicho kingereza chako mtu atakuelewa nini unaongea(USHAHIDI MUULIZENI CHIBIRITI)nenda hispania wanaongea lugha yao nenda ugiriki wanaongea lugha yao,au jaribuni kuangalia mashindano ya mamiss muone kila mtu ajitambulisha kwa lugha yake jamani,mbona bado AKILI zetu za kitumwa hivyo
    USHAURI KWA KANUMBA:Ndugu yangu Kanumba usibabaishwe na hao waganga njaa, mimi naamini hakuna kingine ni "WIVU WA KIKE" unawasumbua,na naamini ni wabaya wako wa kiusanii na naamini kabisa unawajua wasikukatishe tamaa,wasikubabaishe,wala wasikutishe nakwambia Kanumba tunakupenda sanaa na tunajivuna hapa uk juu ya usanii wako,hao wanaopiga MIDOMO ni WAHUNI TU WASIKUSHULISHE,kama ulivyosema kwenye mahojiano yako kuwa NABII HAKUBALIKI NYUMBANI
    KANUMBA KARIBU SANA UK

    ReplyDelete
  30. KANUMBA MY DEAR SIKUTAKA KUCHANGIA ILA NIMEAMUA NIFANYE HIVYO: nimesikitika sana kwa yaliyo jiri. Napenda kukwambia kuwa laiti ungewajua maadui zako kwamba ni wachache na wadogo kama piritoni usingesikitika. Maadui zako ni wale walioshindwa kufurukuta kukuzidi wewe. Napenda kukuhakikishia kuwa wewe ni hazina ya Tanzania na MWENYEZI MUNGU AMEKUJALIA KIPAJI. Nakuamuru sasa amka usiwaze wala kujisumbua kwa sababu ya watu hovyo. Mtu haitaji akili nyingi ili kuelewa kuwa watu wapuuzi wanataka kukudhalilisha. Tuko pamoja nawe na wengine hutujui ila iuna jeshi kubwa saaaaaaaaanaaaaaaa. SIMAMA NA ENDELEA! Kama wao wanajua kiingereza ziko wapi sasa kazi zao za sanaa ili zituburudishe???? Duniani hapa kila mtu na kazi yake...kama wao wanahitaji kiingereza ili wale na waishi wakuache kwani wewe kwa hicho kiingereza ulichosema unakula na kuishi ....ringa kanumba jidai tena peperusha bendera kwa raha zakooooooooo na zetuuuuu....

    ReplyDelete
  31. wote mliomnanga Kanumba hovyoooooo hamna lolote hata mtaani kwenu balozi wenu hawajui maana hamna dira wala sera nyie tena nyie ni no talent mmelaaniwa kazi kuto furahia kazi za wenzenu na hamtatatoka ng'o na viingereza vyenu mtabakia kuongelea majumbani kwenu kwenye puplic hamtoki ng'o. Hamuwezi kushindana na Kanumba nyie hayoooooo yameshindwa mshindwe na mlegeeeeeeee

    ReplyDelete
  32. Ray na Kanumba hawa watu wa hovyo hovyo wasiwababaishe..hawa ni watu wachache sana hata sunami ikiwapiga yaani wala hamtatetereka. Nyinyi mnahitaji watu wachache wenye commitment na kazi zenu.. na ushauri unaokwenda na wakati . Mtu anayevutiwa na kazi zenu kama mimi hivi na wengine wengi anaona hawa wanaowachafua kama kelele za chura tu kwa ng'ombe anayetaka kunywa maji...watu hata wakijiita ma anonymous utajua tu quality zao kwa maneno waliyoyaandika..hawa wote ni hovyo tu hawana constructive critics hawa......

    ReplyDelete
  33. Jamani naomba kuuliza eti, walmuuliza kanumba kwanini hali chakula mchana akajibu "I am Closing because it is Ramadhani"

    ReplyDelete
  34. unamuuliza nani swali si uangalie bofya humo uone we kipofu? ebo

    ReplyDelete
  35. we anon wa Thu Sep 10, 08;22:00 umepata wapi umbea huo kwamba watu wanaona KANUMBA anajifanya bab kubwa hebu kwanza toa definition ya mtu kujifanya bab kubwa unamaanisha nini? na hiyo down to earth maana yake nini wewe mtu hovyo? mbona michuzi na ustaarabu wake wote kashindwa kutoka na wake zake siku ya besidei yake na bado tukamtetea kwamba ni haki yake na familia yake kuona nini wafanye! jifunze wewe kwamba kila binadamu aliyefanikiwa ana mapungufu yake ambayo wewe utayaona inategemea tu unaangalia kupitia angle gani..hovyo sana wewe FIKIRI.....

    ReplyDelete
  36. Nimeangalia simema moja ya kibongo sitaki hata kuitaja jina Subtitles ni hovyo! hovyo! hovyo! ningekuwa mwuingereza ningesema Subtitles were horendous! Very horrible, ugly! Mnataka kutuambia kwamba kwa sababu english is not our mother tounge tunahaki ya kugonganisha lugha kiasi kile! Nilicho jifunza hapa ni kwamba watu hawa niwachoyo wala hawana professional ethics. Jamani tangu lini Director, Editor actor, mpiga picha upande wa sauti, mwanga msimamizi wa mavazi ni mtu mmoja tu! huyu mtu ana uwezo gani! Watu ma genius kama hao hata Hollywood hawapo

    ReplyDelete
  37. Mimi sina ugomvi na hawa mabwana! Ugomvi wangu! ni ushamba wao hasa katika masuala ya movie! Yaani Tangu lini muuaji tena kwa kuchoma kisu akaishia kuwa huru, na mtu asiye na hatia kukamatwa. Na wewe unayekamatwa na polisi huwezi kusema kwamba fulani ndio alua? Polisi gani wasio uwezo wa kuchimba undani na chanzo cha mauaji hayo! Sinema nzuri ni ile inayo reflect uhalisia! Unapoiangalia mtazamaji lazima story ikuchue usahau kwamba unaangalia sinema! Hapa Bongo tunaaangaliaga maigizo wala sio sinema!

    Haya sinema nyingine mtu anapata ajali analetwa na ambulance pamoja na ndugu zake Ndugu na madakitari na manesi wanaingia wote chumba cha operation! what a crap!

    ReplyDelete
  38. mbumbu mmoja go back to school na hao wanaokutetea wanatetea ujinga kama wewe malipo ni hapa hapa duniani ulimuaibisha wema wa watu na wakati mlikuwa mnajifunika shuka moja ukamweka ndani kisa kioo cha gari cha laki moja ulidhani mungu kaenda likizo sio?? leo zamu yako kaa kimya hata yeye alikuwa na ruho ya nyama na aliumia kuzidi wewe ndo ukome ulidhani sifa maimuna wewe? mara mia ungemuomba akufundishe ngeli kuliko ulivyomtenda manake mtoto yule ngeli inapanda uspime kabisa yani ungevumilia ukawa naye miezi sita tuu ungekuwa unashuka ngeli balaa
    miss michuzi ukerewe

    ReplyDelete
  39. Achana na maneno ya watu Kanumbasiku zote watanzania ni watu wa kuponda tu na wengi wao wenye kutoa comment za kijinga wako nje ya Tanzania. Swali ni je wao huko waliko wanafanyaje? bahadhi yao wako shule kila semister ni kufeli at the end wanarudiswa nyumbani,, hapo hapo ndugu yangu achana na maneno ya waswahili. Waliokuchagua kuwakilisha walijua utaweza na umeweza,,

    Mdau,, Malaysia

    ReplyDelete
  40. hata mtu ukikosea kiswahili kiduchu watasema umechapia, wacha waoshe vinywa vyao wewe tengeneza pesa, usijari keep it up usilegeze kamaba utafanikiwa, Billgate aliskuwa sio mzuri Darasani ila sasa ni Tajiri na kampuni yake inategeneza Software nzuri tu, zimetafsiriwa kwa Lugha zote, wewe usijari utafanikiwa ++

    ReplyDelete
  41. Capo di Capi TutiSeptember 11, 2009

    Uncle Michuzi, nadhani sasa tumepata msamiati mpya. Badala ya kusema mtu ni maimuna kwa maana kuwa hajui kiinglishi sasa tutaanza kusema mtu analeta U-Kanumba. Mfano, naweza kusema, "huyu mshikaji ni bonge la Kanumba" ikimaanisha kwamba inglishi haipandi.

    ReplyDelete
  42. kweli ukiwekwa humu ndani haijalishi we ni nani watu haturembi hii ndo blog ya jamii na katika ishu za jamii ni kuwekana sawa kuelimishana sasa kanumba wengi wape kozi ya kiinglish lazima uende ukaungane na mwanawani wa ze comedy pale british counsil usilete urembo hapa hatuangalii sura tunaangalia kichwani kumekaaje hata kiswazz tu umeng'ang'ania namuachia mungu lol ili iweje?? hata kwenye biblia imeandikwa 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa' so nenda skuli atii sio utafute mchawi wakati mchawi ni umaimuna wako mwnyewe
    miss michuzi

    ReplyDelete
  43. MICHUZI TATIZO KUBWA KWA WASANII WETU SHULE NDOGO.WASANII WOTE WAKIISHA ONEKANA KWENYE LUNINGA BASI KOSAAAAAAAA, KESHO WANAJIITA SUPER STAR, KILAKITU KINAHITAJI SHULE,HUKO SHULE UNAPANUA AIKYU YAKO.NDIO MAANA HATA WACHUNGAJI NA MAPANDRI WANASOMA OTHERWISE KILA MTU ANGEJISIKIA KWA MTUMISHI WA MUNGU ANGESHIKA BIBLE NA KUANZA KAZI,SASA BONGO NI TOFAUTI UKIPACHIKWA TU KUIGIZA KIPANDE KIDOGO UKATOKA KWENYE LUNINGA BASI WEWE NI STAR KI UHALISIII KANUMBA SIO STAR.HIVI ALI CHOKI,NI STAR? JEE ANAJULIKANA WITHINNOUR CONTINENT?MI NAFIKIRI WARAKA WA RAY KWA SELIKALI UNGELENGA NI JINSI GANI SERIKALI ITILIE MKAZO FANI YA UIGIZAJI KAMA VILE MPIRA KUWA NA CHAMA CHA WAIGIZAJI UPUUZI WATE HUU HAUTATOKEA

    ReplyDelete
  44. halafu huo mkitambaa unaong'ang'ana nao shingoni kila kukicha ebu sasa ugawe manake ni tuu machi na hayo maviatu ya chui chui sijui cheetah mh! wanavaa wale akina hawavumi wamo vipo kishamba kweli ni vya wale mabishoo wa kijijini nikivionaga mbavu zinauma, ushauri uende kozi ya kiinglish kama noma kwenda shule ati kwa vile we ni denzil kanumba basi tafuta mwalimu mzuuri awe anakuja home kukufunda nakuambia baada ya miezi kadhaa utakuwa unapandisha ngeli iliyonyooka

    ReplyDelete
  45. jamani baadhi ya watanzania mmna wivu wa kupindukia...mwacheni kaka wa watu...wote waliochangia pumba, yakwao yanawashinda ss wanakalia ya kanumba!!!

    ReplyDelete
  46. mdau wa muviSeptember 11, 2009

    kanumba kanumba kanumba mdogo wangu,pole sana lakini usiseme nabii akubaliki kwao koz sie ndio tunaonunua hiyo mikanda yako na u must take it as a challenge my dia,unawajua binadamu mara nyingi mistake ikitokea kidogo tu ndio hukuzwa kuliko mazuri,ni kweli kuna baadhi ya vitu ulichemka mle ndani lakini wewe chukulia kama ni challenge kwako,na usonge mbele tunajua kingereza ni lugha ya kigeni au ya 3 kama ulivyosema lakini ukumbuke na wewe unataka kujiuza kimataifa so kama vipi nenda british pale ukasomee english koz hakuna mtu atakae kucheka bwana,tunajua hii sio lugha yetu lakini mimi nakujua kanumba punguza mashauzi yako pia!KUWA MPOLEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  47. Wew mdau unaesema hata ma professor wetu vyuo vikuu wanaongea kienglish kama cha Kanumba ebu acha masihara bwana...labda icho ni chuo kikuu ulichosoma...mi nimesoma UDSM B.com.nimefundishwa na watu makini na ngeli inapanda sana..Mfano Dr Assad,Prof Mtambalya,Late Prof Haroub Othman,Prof Kaijage na watu wengine makini...napata wasiwasi sana na icho chuo ulichosoma na wasiwasi wangu unazidi kuongezeka kama kweli ulifika uko chuo kikuu maana usiongeandika icho ulichoandika...kufananisha ngeli ya kanumba na Prof wa chuo kikuu??? nakataa

    ReplyDelete
  48. KWENU MASTAA WA BONGO.
    JITIHADA ZENU ZA KIMUZIKI NA KIMAIGIZO ZINAWEZA KUKUTOWENI NJE YA MIPAKA YA TANZANIA.

    HUKO SANAA ZENU ZITAKAPOWAFIKISHA WATU HUWA WANAWASILIANA KWA KUTUMIA LUGHA ZA KIMATAIFA.

    HIVYO KWA WASTAA AMBAO WATATAKA KUJITANGAZA WAO NA KAZI ZAO NJE YA MIPAKA YA BONGO WAACHANE NA UKANUMBA.BADALA YAKE WAJIENDELEZE NA LUGHA ZINAZOWAUNGANISHA WATUKIMATAIFA.

    ACHENU UKANUMBA

    ReplyDelete
  49. watanzania mnaboa sana, tatizo kubwa hapa kwa wote wanaochonga ni elimu na exposure inawasumbua. Guys take some happy pills bana!
    siyo siri that hamko happy na life yenu ndio maana mnasakama watu!

    ReplyDelete
  50. not thats not true tanzania deserve much beter than that bwana. huyo jamaaa bwan isajust so fake even in movies.kwakifupi simzimikii

    ReplyDelete
  51. MNATAKA KUMUOSHA KANUMBA AU, KIJIKO KITABAKI KIJIKO NA KOLEO LITABAKI KOLEO. HUU NI WAKATI WA GLOBALIZATION, HUJUI KIMOMBO KAA CHONJO. KUTETEA UJINGA NDO KUMEFANYA LEO HII MAHOTEL YOTE YA KITALII ARUSHA NA DAR ASLIMIA 90 WAFANYAKAZI NI WAKENYA, MMESHIKILIA TU KISWAHILI LUGHA YETU, WAKUPELEKE WP KIDHUNGU HUJUI. KISWAHILI UJUE NA KIDHUNGU UJUE. HAO WANAOKUTETEA KANUMBA KAZUNGUMZE NA WATOTO WAO UONE KM HAWAHUI KIDHUNGU. WANAOKUTETE WANAKUPOTOSHA. ULAYA UNAENDA SANA, UKIFIKA HUKO 7BU KISWAHILI UNAJUA MUDA MWINGI ONGEA KIDHUNGU WITHIN 3 MONTHS UTAKUWA UKO FLUENT

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...