Jana tarehe 4 Septemba 2009 Jumuiya ya Watanzania UAE ilifanya karamu ya kufuturu pamoja Watanzania wanaoishi, kufanyakazi na waliokuwa matembezini UAE.
Watanzania toka Emirates za Abu Dhabi, Ajman, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah na Umm Al Quwain walijumuika kwenye kwenye karamu hiyo iliyofanyika Ofisi za Ubalozi Mdogo uliopo Dubai.
Pamoja na mahunjumati ya kumwaga pia kulikuwepo na tombola ya tiketi ya ndege ya Dubai – Dar – Dubai iliyotolewa kwa hisani kubwa ya shirika la ndege la watani wa jadi Kenya Airways ambao walishiriki kwenye udhamini wa karamu hiyo.
Mshindi wa tiketi hiyo alikuwa Bibi Naima R. Nassor.
weee! ubwabwa huo! ndo futari kuu huku. sioni mahanjumati hapo!
ReplyDeleteNaomba kuuliza.
ReplyDeleteKatika miezi mingine(Si ramadhani)wanawake na wanaume wanakaa meza/jamvi moja kula chakula.Sasa inakuwaje wakati wa mfungo wanaume na wanawake hawakai (mezani/jamvini) pamoja kufuturu?
Assalaam to Sharrif Hussein
ReplyDeleteUislamu na Tombola (bahati nasibu) wapi na wapi jamani...tena mwezi mtukufu wa Ramadhani??....tena katika tendo adhwiim la Iftari? Inna-Lillah Wainna- Illaihi Rajiuun!
ReplyDeleteMie sijasoma sana dini lakini "TOMBOLA" ni bahati nasibu ama kamari, je si dhambi hii kucheza bahati nasibu wakati mnafunga na huu ni mwezi mtukufu, sasa hii si ndio ile ya kuoga kisha ukajipaka matope..wanazuoni nikosoeni kama nimekosea..
ReplyDeletesasa hao wanakula biriani mwezi wa ramadhani, siku ya idi watakula nini?
ReplyDeletehizo picha hazionyeshi mahanjumati bkoz watu walikuwa washafanya mambo yao(wakati izo picha zilivyopigwa) lakini ubwabwa muhogo sambusa na mengine mengi 2 yalikuwepo!mahanjumati FULL!niamini mimi niliyehudhuria
ReplyDeletemdau ndi ujuwe ramadhan ni mwezi mwingine sio mwezi wa kawaida!
ReplyDeletehukulitambuwa hilo?
aliyepotea anarudi, mwenye roho mbaya yawa safi, ... hio ndo ramadhan..
kwa nini miezi mengine wanakaa pamoja sijui ila ni vizuri ukifika huu mwezi watu wanaupa heshima yake!
Anko Michuzi,
ReplyDeletePicha za Bango la Air Tanzania Liko wapi!? Au Hai-exist!?
Mdau B anahoji.