Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar kuhusu ziara ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Novemba 19 mwaka huu. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca Cola, Afrika Mashariki na Kati, Rita Tsehai.
kombe la dunia ambalo litafanya ziara ya nchini novemba 19 mwaka huu kwa hisani ya kampuni ya coca cola. litaanikwa neshno jipya wadau walione na kupiga nalo picha. ziara yake hiyo pia itatumika kunadi wanja jipya kuvutia timu zije kula tizi hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Bro Michuzi asante sana kutubandikia hii kitu na Mdau Rwebangira anatoka kunitonya kwa kilugha chao eti senene zimeangukia mahali pasipo na walaji

    ReplyDelete
  2. ulinzi wa kutosha JNIA siku hiyo

    ReplyDelete
  3. ONYO USIWEKE KOMBE NDANI YA BEGI, KWANI UTAKUTA LIMEYEYUKA JNIA, ULINZI MKALI PLEASE.

    ReplyDelete
  4. Wanja jipya= Nganda la muwa la jana,chungu kala kivuno ndivyo wahenga walivyosema. Wenzetu wana viwanja kama hivi zaidi ya kumi sisi chetu kimoja kinatutoa roho.Kila siku uwanja mpya,uwanja mpya kama vile sisi tu ndio tulio na uwanja kama huu duniani kote.

    ReplyDelete
  5. kombe la dunia kwenye hand laguage, please.

    ReplyDelete
  6. Heyyyyyyy waambie wakae macho kwani linaweza likatoweka kwa njia za miujiza wakailalamikia tanzania kwamba kombe la Dunia limeibiwa. Unajua thamani yake ni dollar milioni mia sita (US $ 600,000,000.00) That's a lot of money!

    ReplyDelete
  7. Nendeni Angola muone viwanja...sio jijini Luanda! Vimetawanywa nchini pole ...viwanja ninne: Luanda, Cabinda, Banguela na Hulla yatari kwa Africa Cup!

    ReplyDelete
  8. Kombe tumeliona sana. Lini tutalitwaa?????

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi.

    Inasikitisha sana kwa serikali ya Tanzania kutofanya kitu chochote kuhusu kombe la dunia South Africa. Ilitupasa kutumia muda huu kujinadi kwenye jukwaa la kimataifa juu ya mali asili tuliyonayo nyumbani na kuwa karibisha watu toka nchi za nje kuja kututembea, tutaweza kuingiza kipato na kuajiri watu wachache kwa muda. Ila siajona hiyo initiave ikifanywa na serikali yetu.

    hakuna mtu yeyote atakaye kuja kututembelea ikiwa hajui kitu chochote kuhusuana na maliasili zetu. Hivi vyombo vya serikali vinabidi vianze kushirikiana na kufanya mambo ya maana zaidi kuingizia kipato nchi na si kula jasho la wananchi. TUMECHOKA KUITUMIKIA SERIKALI INAPASWA WAANZE KUTUTUMIKIA SISI WANANCHI.

    ReplyDelete
  10. Wapewe Machinga walipitishe hapa kwetu Manzese kwa mfuga mbwa na uwanja wa fisi

    ReplyDelete
  11. kombe hili litakuwa ni mara ya pili kutua bongo mara ya kwanza tulienda kulionea moven peak nakumbuka tuliambiwa dress code iwe black tuvae tupendeze haswaaa na kweli watu walipiga pamba kishenzi ikawa tunapiga nalo picha kwa magroup kufika kwetu si nijidai kulishika na kulibusu mithili ya ronaldo? hee mzungu acha aje juu kwa kiinglish "utatoka nje huruhuiwi kulishika!! nikamjibu tu okaaay i didnt knooooow!!! basi akalifuta mwenyewe alikuwa amevaa gloves nyeupe tukapiga picha haoo wadau mkienda pigeni nalo picha tu kushika marufuku!!
    miss michuzi

    ReplyDelete
  12. wewe mdau hakikisha unatuma Ivoice orginal ya hilo kombe kwa TRA ya US ($ 600,000,000.00),ili tuone kama halilipiwi kodi. la sivyo tutali-value utalipa kodi yetu na chajuu.

    ReplyDelete
  13. KOMBE LINAKUJA TUHAKIKISHE HALIRUDI JAMANI..LA BURE BURE HILO..WAKILIFISADI TUTAPATA SIFA KIMATAIFA..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...