Mbunge wa Viti Maalum Mh. Al-Sheymar akiongea katika kongamano lililoandaliwa kulaani mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
Msanii Mrisho Mpoto wa Mjomba Band Akimwaga Wosia na kutumbuiza waliohudhuria. Mjomba Aligusa nyoyo za watu

Baadhi ya Wageni Waalikwa katika Halfa ya Tuwajali wenzetu iliyoandaliwa na Mwanaharakati John Mashaka

Msanii Marlow naye Alijitolea katika hii shuguli ya kulaani mauaji ya kikatili ya Ndugu zetu wenye ulemavu wa Ngozi
Mwanaharakati John Mashaka akiwa pamoja na watoto maalbino waliohudhuria kongomano la tuwajali wenzetu

HOTUBA YA JOHN MASHAKA KATIKA
VIWANJA VYA BIAFRA, KINONDONI

Mheshimiwa Profesa David Mwakyusa, Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii,
wadhamini wetu kampuni ya zain, clouds FM na Business Times, wageni waalikwa na watanzania wenzangu.
shukrani za dhati kwa kuukubali huu mwaliko, na kujumika nasi wa siku ya leo kujikumbushia maswala muhimu kuhusu taifa letu hasa maswaa ya haki na usawa. Huu ni uzalendo wa aina yake, ni uzalendo unaotukumbushia uhuru wetu wa mwaka 1961, nchi hii iliposaini hati ya makabidhiano ya uhuru,

Hati ya mwaka 61 iliikabidhi nchi yetu haki yake ya msingi, haki ya maamuzi yaliyo mhakikishia kila raia maisha bora, na usawa. Hati hiyo ya mwaka 1961, ilitoa matumaini kwa kila mmoja. Raia wa Tanzania, walihaidiwa maendeleo makubwa.Watanzana hawakuahidiwa haya yanayojitokeza kwa sasa ; hawakuhaidiwa ahadi zisizotekelezeka, Walipewa ahadi za dhati za kukabiliana na maradhi, ahadi za kuondokana na umasikini na ujinga. Watanzania walipewa ahadi za haki, bila kujali matabaka, walihaidiwa usalama kwa raia wote.

Ahadi za mwaka 1961 hazikuwa za kuleta ufisadi kama huu tunao ushuhudia sasa. Hati ya Uhuru ilikuwa ni ya manufaa kwa raia wote. Kwa hakika katika miaka 48 ya uhuru wetu, yapo mambo kadhaa ya kujivunia.
Kuna mabadiliko makubwa hasa katika jiji la Dar es Salaam na hata kwingineko Ambako Kuna majengo marefu, mazuri ya kisasa, yanayoelekea mawinguni. Miaka 48 imeleta mabadiliko ya kijamii, kuna matabaka ya wasomi wenye maisha ya juu. Kuna makundi ya watawala na wenye mamlaka; Kuna kundi la matajiri wanaoshi katika sayari tofauti na watanzania walio wengi.

Watanzania wenzangu, wakati wapo wenye maisha mazuri, wanaoishi katika raha na utukufu, wapo pia wengi ambao wana maisha ya dhiki, wapo mamillioni wanaoshi katika ukiwa. Wapo wengi wanaoishi kwa kubahatisha na kwa kukata tamaa; wale ambao hawaoni faida waliyoitegemea kutokana na kupatikana kwa uhuru wao. Wapo maalbino wanaoishi kwa ukiwa na wasiwasi mkubwa.
Umbali mfupi tu kutoka hapa tulipo wapo wenzetu ambao wanaishi kwa hofu; wanaume kwa wanawake walio na wasiwasi, siyo tu juu ya maisha yao wenyewe, bali maisha ya umbele ya kiafya, na kielimu kwa watoto wao.
Hawa ni raia wenye hofu kuhusu usalama wao.
Ni raia wenye hofu jinsi watakavyowalisha watoto wao.Ni raia wenye wasiwasi ni jinsi gani watawasomesha watoto wao, siyo katika shule za ng’ambo bali katika shule za humu nchini. Hawa ni raia wenye hofu ya kupata hata mmlo mmoja kwa familia zao nahuu ndio ukweli wa mambo;
Ni ukweli unaouma. Ukweli wa mambo wenye machungu,haupo mbali nasi, ukweli huu upo manzese, upo kigogo na kule Temeke. Hali mbaya zaidi ya ukweli huu upo pale msimbazi center ambapo vitoto vichanga vya miezi mitatu vinaishi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu ili hali nchi yao inayo uwezo wa kuwapa maisha yenye uhakika.
Ukweli unaosononesha tunao hapa kati yetu, ambapo maelfu ya vijana hawana ajira, ni wachovu katika lindi la ufukara. Ukweli huu unaoumiza tunauona kwa vijana wetu ambao, licha ya kuwa wamesoma vya kutosha, wanabakia wakichuuza maji ya kunywa ili kujikidhi kimaisha.

Wengine wanaamua kuchukua silaha na kufikia hatua ya kuyachukua maisha ya wengine ili kujipatia riziki. Huu dio ukweli wa mambo; ni ukweli unaouma.
Natumia nafasi hii kuwasihi wale wote wanaochota raslimali za inchi hii; Wale wote ambao wanahamisha mamilioni ya pesa za walipa kodi na kuyapeleka katika akaunti nje ya nchi, Nawasihi wale wote wenye roho za kifisadi kufikiria mara mbili juu ya maadili na vitendo vyao.

Nawasihi hawa waliopewa dhamani ya kuilinda hii nchi kuvitembelea vyuo vyetu, na tasisi nyingine za elimu ili kuangalia hali halisi ya mahitaji katika taasisi hizo. Nawasihi viongozi wetu kwenda katika vituo vya mabasi, na masokoni na kuwaona vijana na watoto wadogo waliolemewa na ufukara, wanaolala kwenye mabaraza ya majumba na kwenye magenge kwa sababu hawana makazi.
Nawasihi viongozi wetu kutega masikio yao ili kuwasikia, vijana wenye majonzi makubwa , vijana wanozishuhudia ndoto zao za kielimu zikitokomea kutokana na ufukara mkubwa walionao wazazi wao.

Siku ya leo ndugu zangu, tunawaomba viongozi wetu wavisikie sauti za ndugu zetu wanaowindwa kutokana na uumbaji wa Mwenyezi mungu. Tunawaomba wazisikie sauti za ndugu zetu maalbino wanaoishi kwa uwoga na ukiwa .
Tunaomba walindwe, na kupewa haki zao za kimsingi, na za Usalama. Hii siyo tu kwao maalbino, bali kwao watanzania wote wanaotikiswa na wimbi la ujambazi. Hii siyo hati nchi yetu ilisaini kwa ajili ya raia wake, Hii ni hundi batili MAFISADI wa kimaadili wanawalazimisha raia wema kuvichukua.
Tunawasihi viongozi wetu waondoke nje ya ofisi zao ili watafute muhafaka kwa kushirikiana na wananchi wengine juu ya ulinzi wa watoto albino wasio na hatia. Ninawasihi, msikie kilio cha yule Albino, binti wa miaka 10 ambaye hawezi kukilalia kitanda kimoja kila siku kwa sababu tu anawindwa na watu wenye tamaa na imani potofu. Huu ndiyo ukweli wa mambo, ukweli wa miaka 48 ya uhuru wetu!Ni ukweli unaouma !
“Miezi michache iliyopita nilighafirika kwamba kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Kimarekani niliyeongea naye, aliweza kuikumbuka Tanzania kwa mauaji ya albino badala ya mambo mengine mengi mazuri tu yanayoihusu Tanzania”.Jambo hili ni la kifedheha!
Huu ni umaskini wa kifikra na UFISADI wa kimaadili ambao umetukumba sisi watanzania. Kumuwinda binadamu kutokana na umbile lake siyo utanzania, huu ni ushetani.

Tusiitegemee serikali kuwa na miujiza ya kusuluhisha kila tatizo letu la kijamii na kiusalama. Tatizo hili lipo mikononi mwetu. Sisi raia ndio wenye nguvu na uwezo wa kutokomeza haya mauaji ya kinyama. ni lazima tushirikiane ili kuzuia jambo hili la kiovu.
Watanzania wenzangu, wakati wapo wenzetu wanaume kwa wanawake chini ya bahari, angani na kwingineko wakifanya utafiti na shughuli zenye hatari kubwa kwa manufaa yetu, nchini kwetu, wengine wanatafiti namna ya kuwaua maalbino wasiokuwa na hatia. Tuwalindeni maalbino, tuwasaidieni tunapoweza.

Ndugu zangu, tusipojitizama vizuri, basi tunakokwenda ni giza kubwa na majonzi yasiyokuwa na kipimo kwa sababu binadamu ambaye hawezi kuyathamini maisha hana zaidi ya kuthamini.

Tumeumbwa tulindane, si kuwindana. Tumeumbwa kuwa watumishi, siyo watumikiwa,Tumeumbwa kuwatendea haki wanyonge, siyo kuwanyanyasa,Tumeumbwa kujitolea kwa hali na mali kwa manufaa ya wengine.
Hiyo ndiyo maana halisi ya maadili, Hiyo ndiyo maana ya uongozi!
Mwanafalsafa wa Kimarekani , Edmund Burk, alipata kusema kwamba, “ tofauti kubwa kati ya kiongozi wa dhati na yule ajifanyaye kuwa kiongozi ni kwamba; kiongozi wa dhati uangalia mbele, wakati yule bandia uangalia ya leo. Kiongozi bandia anaishi kwa ajili ya leo na anatenda udanganyifu, wakati mwenzake anavumilia machungu ili kuyalinda madili na kutizama maisha ya baadae”.
Viongozi wanaoipenda hii nchi, badala ya kutafuta utajiri wa kitambo, tunawaomba muangalie ni wapi tunaelekea. Tunawaomba mtafakari mustakabali wa nchi na maisha ya mbeleni ya vijukuu vyenu ambavyo havitahitaji mabillioni ya fedha ya wizi iliyolimbikizwa nchi za nje. Bali mazingira mazuri ya kuishi yenye amani .

Ndugu zangu, muda hauna uhadilifu wala subira. Muda hauwezi kubadilisha au kutatua matatizo yetu, Muda hauwezi kuponya vindonda vilivyosababishwa na umasikini. Muda hauwezi kuyarudisha maisha yaliyopotezwa kutokana na tamaa na ulafi wetu. Muda haupo upande wetu, wala maneno matupu hayawezi kuponya maumivu.Muda hauwezi kutuondoa katika masumbuko yetu, bali unaweza kutuacha ili tuendelee kuumia.
Wakati umefika tujitoe mhanga ili kuleta mabadiliko na kuondokana na maumivu yanayotukabili. Wapo wengi ambao wamekuwa wakihoji haya ninayoyafanya katika jamii, wengine wamekuwa wakidhania kwamba nina malengo ya kisiasa !
Ninachoweza kusema ni kwamba mtu yeyote mwenye hutu ambaye analiona wingu la umasikini uliotanda katika taifa letu, anayo jukumu la kimaadili kutoa mchango wake ili kuondoa kukata tamaa kunakowakabili mamilioni ya wanachi wetu, dhamira hii ipo juu ya dhamira nyepesi za kisiasa. Ninalilipa deni langu kwa jamii yangu.
Nalipa fadhila kwa mwenyezi Mungu. Haraka iliyopo katika hitaji la kuwasaidia ndugu zetu wenye matatizo, ni ya kasi zaidi kuliko haraka ya kukimbilia madaraka ya kisiasa. Hitaji la kumsaidia mtoto mwenye kulala na njaa ni kubwa kuliko tamaa za madaraka ya kawaida ya kisiasa.

Kimsingi huo ndio mvuto mkubwa ambao umekuwa ukiusumbua nafsi yangu kwa muda mrefu. Ninachokifanya ni sehemu tu ya utashi wa kiroho ambao umenifunulia wajibu wangu, na jukumu langu kama binadamu mwingine anayetambua kati ya wema na uovu. Huu ni utashi ulionipa changamoto ya kujitazama upya katika taswira ya maadili. Ni utashi unaotusihi wote kujitolea mhanga kwa ajili ya amani katika taifa letu.
Kila mmoja ana ndoto ya kuishi maisha yenye furaha. Wote mliopo hapa mmekuja kwa sababu mnaamini kwamba tunalindwa na bendera moja, na kutumikiwa na rais mmoja. Hivyo, nawasihi mrudi majumbani kwenu na ujumbe mmoja kwamba, maisha yenye matumaini ni muhimu kuliko maisha ya kukata tamaa.

Ni lazima wote tufahamu kwamba upendo ni muhimu kuliko chuki. Lazima mtambue kwamba ushirikiano ni muhimu kuliko utengano. Hizi ni tunu ambazo tunatakiwa kuzilinda; Ni lazima tuwe sehemu ya mabadiliko kueleka katika maendeleo chanya.
Kufika kwenu hapa leo imekuwa kama chanzo cha uharakati wa watanzania, uharakati wa kijamii ya kuwalinda wenye ulemeavu, wenye ukoma, na wasioona. Ni uharakati wa kuwavalisha wanaotembea uchi. Ni uharakati wa kuwalisha wanaoshinda njaa. Ni uharakati wa kuwalinda maalbino wanaoishi kwa wasiwasi na ukiwa

Ni uharakati na maendeleo ambayo yamevuka mipaka ya siasa, dini, hata asili za watu. Ni maendelao yaliyovuka ubaguzi wa rangi, matabaka, na hata kasumba. Ni maendeleo yanayowakutanisha Watanzania wote. Huu ni uharakati na mchakato wa masikini na matajiri. Mchakato wa wenye madaraka na wanyonge, Ni mchakato kuhakikisha kwamba MAFISADI na masikini wanapewa haki sawa mbele ya sheria.

Ni mchakato na uharakati wa kuleta upendo kwa kila mwanadamu. Ni mchakatona ambao umedhamiria kurudisha yale matumaini ambayo watu walikuwa nayo mwaka 1961 wakati nchi yetu ilipopata uhuru. Uharakati wa kuondokana na magonjwa, ujinga, na umasikini. Uharakati wa kuhakikisha usalama kwa kila raia. Uharakati wa kukomeza Ufisadi.

Haya ni mapambano ya kuwalinda watu wote bila kuwabagua,
Ni mapambano ya kuwalinda maalbino.
Ni mapambano yaliyaonza mwaka 1961;
Ni mapambano yenye manufaa kwa kila mmoja wetu.

Mungu Ibariki Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 87 mpaka sasa

  1. Huyu John Mashaka, ana jumbe nzito hivi walengwa wanamsikia kweli, kama wanamsikia wanamuelwa?

    ReplyDelete
  2. Joni Mashaka, nina swali moja tu, mbona haukumpa rafiki yako Kanumba twisheni kabla hajaenda Big Braza? Ni swali tu

    ReplyDelete
  3. Hongera Mashaka kwa kutetea maalbino.

    Shida ni kwenye uandishi sahihi na Kiswahili sanifu. Herufi kubwa na ndogo zina utaratibu wake. Maneno ya Kiswahili yana usahihi wake na muundo wa sentensi una usahihi wake pia, siyo kutwanga tu. Hebu chungulia makosa machache niliyodaka ili siku za usoni urekebishe, mfano ni kuahidiwa, siyo kuhaidiwa; wazisikie sauti, siyo wavisikie; kumwinda siyo kumuwinda; mlo siyo mmlo; masuala siyo maswala. Yako mengi mno. Waosha vinywa msikasirike, kama tunavyowashambulia akina yahe wasiojua Kimombo, na Kiswahili pia lazima kilindwe.....
    Naweka baadhi ya sehemu zenye matatizo makubwa ya herufu kubwa na ndogo na Kiswahili sahihi:

    Mheshimiwa Profesa David Mwakyusa, Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii,
    wadhamini wetu kampuni ya zain, clouds FM na Business Times, wageni waalikwa na watanzania wenzangu.
    shukrani za dhati kwa kuukubali huu mwaliko, na kujumika nasi wa siku ya leo kujikumbushia maswala muhimu kuhusu taifa letu hasa maswaa ya haki na usawa.
    Hati ya mwaka 61 iliikabidhi nchi yetu haki yake ya msingi, haki ya maamuzi yaliyo mhakikishia kila raia maisha bora, na usawa. Raia wa Tanzania, walihaidiwa maendeleo makubwa.; hawakuhaidiwa ahadi zisizotekelezeka, Walipewa ahadi za dhati za kukabiliana na maradhi, walihaidiwa usalama kwa raia wote.

    Ahadi za mwaka 1961 hazikuwa za kuleta ufisadi kama huu tunao ushuhudia sasa.
    Kuna mabadiliko makubwa hasa katika jiji la Dar es Salaam na hata kwingineko Ambako Kuna majengo marefu, mazuri ya kisasa, yanayoelekea mawinguni. Kuna kundi la matajiri wanaoshi katika sayari tofauti na watanzania walio wengi.

    … wanaume kwa wanawake walio na wasiwasi, siyo tu juu ya maisha yao wenyewe, bali maisha ya umbele ya kiafya, na kielimu kwa watoto wao.

    Hawa ni raia wenye hofu ya kupata hata mmlo mmoja kwa familia zao nahuu ndio ukweli wa mambo;
    Ni ukweli unaouma. Ukweli wa mambo wenye machungu,haupo mbali nasi, ukweli huu upo manzese, upo kigogo na kule Temeke. Hali mbaya zaidi ya ukweli huu upo pale msimbazi center ambapo vitoto vichanga vya miezi mitatu vinaishi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu …

    … ili kujikidhi kimaisha.

    Huu dio ukweli wa mambo; … raslimali za inchi hii;

    Nawasihi hawa waliopewa dhamani ya kuilinda hii nchi kuvitembelea vyuo vyetu, na tasisi nyingine za elimu ili kuangalia hali halisi ya mahitaji katika taasisi hizo.

    Siku ya leo ndugu zangu, tunawaomba viongozi wetu wavisikie sauti za ndugu zetu … haki zao za kimsingi, na za Usalama. Hii siyo hati (neno “ambayo” linakosekana) nchi yetu ilisaini kwa ajili ya raia wake, Hii ni hundi batili MAFISADI wa kimaadili wanawalazimisha raia wema kuvichukua.
    Tunawasihi viongozi wetu waondoke nje ya ofisi zao ili watafute muhafaka kwa kushirikiana na wananchi wengine juu ya ulinzi wa watoto albino wasio na hatia.

    “Miezi michache iliyopita nilighafirika kwamba….Jambo hili ni la kifedheha! (fedheha siyo kifedheha)
    . Kumuwinda binadamu kutokana na umbile lake siyo utanzania, huu ni ushetani.

    kiongozi wa dhati uangalia mbele, wakati yule bandia uangalia ya leo.
    Ndugu zangu, muda hauna uhadilifu wala subira. Muda hauwezi kuponya vindonda vilivyosababishwa na umasikini.
    Ninachoweza kusema ni kwamba mtu yeyote mwenye hutu …


    Kimsingi huo ndio mvuto mkubwa ambao umekuwa ukiusumbua nafsi yangu kwa muda mrefu.

    Kufika kwenu hapa leo imekuwa kama chanzo cha uharakati wa watanzania, uharakati (neno sahihi ni harakati) wa kijamii ya kuwalinda wenye ulemeavu,

    ReplyDelete
  4. kidumu Chama Cha Mashaka, kidumu
    adumu mwanaharakati, adumu

    ReplyDelete
  5. Mlioko USA hebu tuambieni, mtu anaweza kupewa likizo kibao hivi kila mwaka, anakuja anakaa miezi kibao? Jamaa huyu siyo anacheza heko akirudi anaonyesha wafadhili kazi alizofanya, anadaka, anasonga mbele?

    Kiongozi gani wa juu wa Marekani alimuona kama siyo kamba? Si ukiombaomba unaonana na wengi tu?

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLELASeptember 12, 2009

    MIMI KAMA PETER NALITOLELA KUTOKA CHUO KIKUU CHA UNIVESITY YA MUZUMBE YA KULE MOLOGOLO, MUDA MWINGINE NAMPONDAGA MTAKATIFU NABII MESIAH YOHANNA MASHAKA, MUDA MWINGINE NAMUUNGA MKONO. HAPA NAMUUNGA NABII MKONO KWA MAANA ANAFANYA VITU VYA MAANA SANA. TULIPOSOMA NAYE PALE MUZUMBE CHUO CHA ECONOMY, ALIKUWA MTU WA BUSARA SARA NA ALIESHIMU WATU SANA. MIMI NINA AMINI YA KWAMBA HUYU BWANA MASHAKA SIKU MOJA ATAKUJA KUWA RAIS WA AFRIKA NZIMA KWA MAANA MADA ZAKE ZIMETULIAGA SANA. SIYO KAMA SWAHIBA WAKE KANUMBA. BWANA MASHAKA KAMA BADO UPO HAPA DARISALAMA BASI NAOMBA TUKUTANE NA YULE MUTOTO WA MUNENE ILI TUBADILISHANE MAWAZO. NI KWA NINI BWANA MASHAKA HAUKUMUALIKA YULE WAZIRI KIJANA MWENYWE WIZARA NYETI ANAYEJIKITAGA KWENYE MASHINDANO YA ULIMBWENDE WAKATI HATA JIBU MOJA KUHUSU MAUAJI YA ALIBNO HAYAJAPATIKANA?
    MASHAKA KAMA UTAKUWA LAIS WA TANZANIA, BASI UTAKUWA MSOMI WA KWANZA KUTOKA MUZUMBE AMBAYE NI MUTU MAKINI SANA HAPA NCHINI NA MBEBA BOXI NAMBA WANI.
    NABII MTAKATIFU YOHANNA MASHAKA, NAOMBA UENDELEE HIVYO HIVYO, ILA JITAYALISHE WIKI IJAYO NITAKUKANDYA KISAWASAWA, LEO BAHATI YAKO SIWEZI KWA MAANA UMEANDIKA HOTUBA YA MAANA SANA. NA MUNGU AKUBALIKI

    ReplyDelete
  7. kusema kweli hii hotuba imetulia sana sana na inagusa sana. bwana michuzi mimi ningekushauri ushikilie sana haya anayoandika bwana mashaka, kwa sababu huyu dogo anaingia kwenye vitabu vya historia, safi sana, keep up the fight mwanawane. habari ndo hiyo.
    huyu mashaka ni sawa na nyerere, ukimpa microphone umekosa, utakesha kumsikiliza ila swafi sana

    ReplyDelete
  8. vita dhidi ya john mashaka vimeanzishwa na
    wanamajungu kule jamii forums.
    wanampaka jamaa kweli kweli ya kanumba cha mtoto.
    kinachowasumbua ni wivu, mashaka wakune vichwa mkuu huko juu

    ReplyDelete
  9. huyu jamaa mwogopeni, kamwaga mihela jimbo la ukonga utadhani hana akili. wewe $350,000 kweli unaweza kutumia kwenye kampeni ya kisiasa? basi yeye ameshafanya hivyo kwenye kura ya maoni kumng'oa makongoro mahanga. mashaka kwa taarifa yako makongoro atoki kabisa kwenye jimbo la ukonga. amezaliwa ili kuliwakilisha jimbo hilo kwa hiyo rudi wall-street ukabebe boxi

    ReplyDelete
  10. Kumbe unajua Kiswahili hivi, Mashaka? Mbona umeeleweka vizuri zaidi leo? Tafadhali endelea hivi hivi. Hongera kwa kuwambuka wanyonge.

    ReplyDelete
  11. mashaka supporterSeptember 12, 2009

    BWANA MASHAKA, MM NAKUSHAURI KITU KIMOJA, HUKO JUU SANA NA TANZANIA NZIMA INAKUHESHIMU. HACHANA NA YULE DADA WA HOUSTON MWENYE MAPEPO; HAFAI, HASA KWA MTU MWENYE HADHI KAMA YAKO. LIMECHANGANYIKIWA LILE, KAFANYA VITUKO KWELI, SIYO CHOONI, SIYO CLUB, SIYO WAPI. SI HUKO DAR, ULIZIA ALIYOYAFANYA ALIPOKUWA HUKO. NJOO H-TOWN UTAAMBIWA HATA CRACK HEADS WAMEPATA SHARE YAO, NUNULIA SIGARA KAZI KWISHNEY

    ReplyDelete
  12. tatizo kwenye hii globu ya jamii ni kwamba ukitundika tu joni mashaka, hali ya hewa ubadilika ghafla, sasa hivi inachafuka. subirini wakina nalitolela wafike na us blogger.

    ReplyDelete
  13. hii hotuba siyo ya joni mashaka, hii ni hotuba ya hayati Shaban Robert

    Mashaka atoe wapi ubavu wa kuandika hotuba kama hii??? yule jamaa hana akili ki hivyo wengine heti wanamuita jinias?

    mimi nilimuona pale PPF towers haonekani mtu mwenye akili

    ReplyDelete
  14. Hi John
    Hotuba hii ni adimu. Inazungumza toka moyoni mwako na inafundisha/ inaonya/ inahamasisha/ inakumbusha wajibu na inatoa mwanga. Ni hotuba inayogusa na ningelifurahi kama wana Blog wakawa na mtazamo wa mrengo wa kujumuisha zaidi ya punguzo. Nimevutiwa sana na imebidi niandike ijapo nitawasiliana na wewe kwa e mail. Sasa nimerudi toka field tutazidi kuwasiliana. ni Brother wa New Hampshire

    ReplyDelete
  15. US-Blogger)

    Barua ya Wazi Kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete:

    Mh. Rais, I highly respect you and know that you are a man of integrity, however, I will be highly dissapointed with you to give Mesiah and false prophet Yohanna Mashaka a post in your cabinet.

    Yes, he is very capable but very contreversial to be a minister. Mr. Mashaka is currently in Tanzania trying to buy voters in Ukonga with Dirty Wall-street money yet the very consituents he is trying to drum support from have no food in their houses.

    He thinks you can give him Foreign Affairs or Finance or Justice Department. please dont blunnder Mr. President. Mesiah yohhana Mashaka is indeed corrupt even though he pretends to be humble and hardworking

    These speeches he is currently giving are copy and paste from Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere. Mashaka has no brain to write a speech of his own. I have asked him many times to come and debate me but he has refused meaning he has no guts to face a real man

    I have offered him $500,000 for a live debate but he has refused. I thought maybe his team of experts such as Dr. Shayo and michuzi would have helped but they are all afraid of me.

    I am an economist from Oxford, and very knowledgeable than the Mesiah Yohanna Mashaka. i fit to be a minister because every time he brings his bogus articles, I crush him

    I hope you dont pay attention to this confused kid Mr. President, even your son Hon: Rizwan is more brigheter than him. John Mashaka and Mashaka are upto no good, ten times Zitto Kabwe and John Mnyika are more brilliant than them

    Dr. US-Blogger
    OXFORD Univesrity Economics Graduate

    ReplyDelete
  16. Field Marshall ESSeptember 12, 2009

    - Ningemshauri tu kwamba aweke mapema tena wazi, background yake na Kenya, maana itakuja kumharibia sana mbele ya safari hii, mafisadi jana nzima walikuwa wanahaha kutafuta historia yake ya maisha.

    - Ni ushauri wa bure tu!

    Respect.

    FMEs!

    ReplyDelete
  17. mimi kiinglish is not richebo ila nawakilisha

    1. Mashaka awe Rais wetu 2015
    2. Kanumba awe Waziri Mkuu 2015

    teteteteteteeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  18. Ujumbe Kwa:

    Nabii Yohanna Mashaka,na Basketball Superstar Hasheem Thabeet:.....

    Najua wote mko juu. Mmoja yuko NBA, mwingine ni Investment Banker wa Wall-Street. Hela bila shaka mnazo lakini mjaribu kuwa makini

    Bongo kuna utapeli, hizo misaada mnazozitoa, mngejilimbikizia wenyewe kwani mtashtukia hata chupi zenu zimeuzwa ili watu wajinunulie PRADO.

    Bongo Tambarare kweli kweli, hizo ndo biashara, na siku mnafilisika, yala marafiki yote yanayowazunguka yatawakimbia wote

    Mimi nilimshangaa huyo joni mashaka kutoa millioni 4 kwa TMH wakati wenzako wameshanunua viwanja Bunju.

    Haya subirini mtakiona, Tanzania watu hutoa elfu 50 ukitoa nyingi ni ahadi ya laki tano ambazo hazitolewi

    ReplyDelete
  19. Kuanza hotuba kwa rejea ya hati iliyokabidhiwa na Mkoloni mwaka 61 ni ufinyu wa uchambuzi wa haki za binadamu ambazo zilikuwepo hata kabla ya mkoloni kufika na kuvamia haki zetu kibao.

    John, nitafute au tafuta watu wenye upeo zaidi na wazuri zaidi katika kukuandaa kupanda majukwaani ukipenda.

    ReplyDelete
  20. Ndugu JM hongera sana kwa kazi hii nzuri. sasa sie ambao hakipandi - kile kile - tunaweza kukuelewa. hata hivyo jaribu kupunguza urefu wa hotuba. nimesoma hii hotuba hadi katikati tu. ni ndefu mno bila sababu kama zile za JK!!! unaweza kuzungumza kwa kifupi na wasomaji au wasikilizaji wakakuelewa vizuri zaidi kuliko kuwa na ngonjera (yaani beti zinajirudiarudia).

    ReplyDelete
  21. Huyu bwana akishirikiana vizuri na Kanumba lazima nchi ipate maendeleo... Kwani wote wana-CONFIDANCE za kutosha kabisa.

    ReplyDelete
  22. Bila kuficha wajameni, huyu kaka anatisha. JOHN MASHAKA mkuu unatisha na hata CCM watakuogopa. Hii Hotuba kali ndugu zanguni, imeandikwa toka moyoni

    ReplyDelete
  23. bwana mashaka, usiinginwe na jeuri, ni dhahiri kwamba utaifikisha bara la afrika mbali. nakuona siku moja ukiibuka kuwa kiongozi wa afrika nzima. upeo wako ni mkubwa kweli hii hotuba nimeikubali kweli ni mwanaharakati

    ReplyDelete
  24. In a NUTSHELL the only standing Tanzania Genius !!!

    Hakuna ubishi tena

    ReplyDelete
  25. hivi hawa wakurya mbona mijasiri sana, wanakula nini?
    ni damu, samaki au nyama? kwa maana huyu jamaani jasiri mno na ni mtu mwenye akili kupita kiasi. anajiamini mno
    kwenye kiingeleza wamo, kiswahili pia wamo... sasa tufanyeje? tumpeni waziri wa Fweza au tusubili 2015 tumpe nyumba kubwa moja kwa moja?
    Rais mtarajiwa wa Africa, vuta subira mkuu. Endelea kutetea haki za wanyonge mungu atakuzawadisha

    ReplyDelete
  26. Mithupu:
    Huyu jamaa bwana mashaka anakipaji fulani inayomfanya awe kivutio fulani kwa watu. Yaani kule Jamii Forums sasa hivi yeye ndo gumzo, na watu wanachangia mada yake ki-kweli kweli. anakuna vichwa
    hapa kwako akitundikwa basi utadhania kumbikumbi. hebu fuata hii linki ukamjue joni mashaka ni nani, aisee jamaa anakuna vichwa siyo kawaida. when i grow up i want to be like john mashaka

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38401-john-mashaka-avamia-ukonga-kwa-kishindo-makongoro-mahanga-hoi.html

    ReplyDelete
  27. jon mashaka naye alikuwaga
    "community organizer"
    hongera rais mtarajiwa kazi nzuri kwa watanzania wanyonge

    ReplyDelete
  28. US BLOGGER WACHA UJINGA WAKO NI WIVU WAKO KWANZA HUJASOMA OXFORD UNIVERSITY UNIYOISEMA WEWE, KWANZA HATA HUJUWI MFUMO WA OXFORD UNIVERSITY, KAMA HUJUWI OXFORD NI MKUSANYIKO WA COLLEGES SASA WEWE UMESOMA COLLEGE GANI YA OXFORD UNIVERSITY, MIMI NIMEFANYA UTAFITI HAKUNA HATA MTANZANIA MMOJA ALIYEwahi FANYA PhD OXFORD UNIVERSITY, HIVI UNAFIKIRI KUSOMA OXFORD UNIVERSITY COLLEGES NI MCHEZO HAPA WAZUNGU WENYEWE WANAKUNYA MAVI KUPATA NAFASI FROM AMONG THE OXFORD COLLEGES, KWA MFANO MWAKA HUU WAZUNGU KIBAO WITH "A" STARS KWENYE MASOMO YOTE WAMEKATALIWA KUININGIA OXFORD COLLEGES NA UTARATIBU WAKE SI KUPATA "A" TU PIA KUNA ENTRY EXAMS UKIFELI UCHUKULIWI HATA KAMA "A" ZAKO ZINA MAPEMBE, SASA WADANGAMYE HAO HAO WAJINGA WASIOJUWA MFUMU WA ELIMU WA OXFORD, I HAVE BEEN THERE SEARCHED FOR ANY TANZANIA UNDERTOOK PhD THERE I FOUND NONE, SO USIDANGANYE WATU KWANZA UWE NA PhD YA OXFORD UNIVERSITY UNGEANDIKA UTUMBO HIVYOOO, MTU MZIMA OVYOOOOOOO

    ReplyDelete
  29. Mashaka, big up urself bro!

    ReplyDelete
  30. Wewe anon wa Sep 13, 12:5100am usidanganye umma hapa.
    Sio kwamba wazungu mwaka huu wamekatiliwa kuingia Oxford sababu ya exams... sababu ni kuwa serikali imetoa pesa (fungu)ndogo for higher education (just under 60%) na ndio maana best universities nyingi zimechukua idadi ndogo sana kutokana na fungu walilopewa na govrnment. Ingawa wanafunzi tunapewa loan... hiyo ni kama top-up tu. University fees hapa yapishana sana kutokana na chuo unachosoma na pia course unayochukua. Mfano kwenye MBA pale London school of commerce ambako MBA haijawa registered na Association of MBA of UK unasoma MBA yako kwa £4,000... lakini ukisema uchukue MBA chuo maarufu duniani kama vile London school of Business andaa £14,000 mapema. 90% ya wazazi waingereza hawajui kulipia watoto elimu kama wazazi kule Africa, wao wanajua kununulia watoto wao zawadi za kijinga kupoteza pesa nyingi lakini panapokuja education hawajui hilo. Ndio maana sasa schools zote pale Oxford iwe school of Law au medicine wageni toka Asia hasa wachina, na sio hapo tu hata colleges za Cambridge, London school of Business, etc. Hizo universities watoa up to 15,000 pounds a year. Mzazi mwingereza alivyo bahiri hawezi toa hiyo pesa...

    ReplyDelete
  31. I read and understood different issues on the speech.I like it and the messages are represented brilliantly and concisely.

    I,as well skimmed through various comments to ensure readers perception on what is addressed.

    I could correlate facts and come up with ideas that depict Mr Mashaka ideologies and career drift.

    Mashaka feels morally obliged to help,enhance and make differences to his society by demonstrating his altruistic personality.ie we see him engaging with disadvantaged,people under attack for being different due to primitive ideologies,he gives short term relief which is ok but I would prefer to be sustainable eg provide enterpreneurship guidance,invest in children education etc

    I would feel to acknowledge his contritutions without attempting to critisize his motives since,I as human being,have to appreciate and implement my responsibilities when is right and capable.

    However,I would prefer to contemplate retrospectively on his circular personality as he lives abroad,different culture and exposed to global issues,have money and feels responsible to his own people in other words philantropy.There is nothing wrong about this,but surely he might have calculated his NPV which is is positive,keep it up,and please whenever appropriate report on your activities progress.

    I would suggest that he should not overstep his political and legal boundaries since there are touchy accusations he writes explicitly which could jeopardise his objectives and hence bad publicity or litigation and in turn demoralization.

    Please be careful to issuing political oriented speeches instead use your constituent MP to reach political figures who might address the house and remind Tanzanians of their patriotism.Focus on social economic changes from our leaders initiatives and critisize convisingly.


    GOD bless you and don't give in.Convey my greetings to Dr Shayo and Kaka Michuzi hapo nyumbani.

    mdau (John) uk

    ReplyDelete
  32. HAHAHAHAHA JOB TRUE TRUE....YAANI I CAN SEE THINGS OF MASHAKA HAVE COTTON FIRE TRUE TRUE! AND I THINK MOST OF MOUTH WASHERS ARE AFTERNOON TORTOISES IN THIS MONTH OF CLOSING....

    ReplyDelete
  33. john mashaka ni sumu ya wabeba boxi na wala vumbi. yaani ni wazi kabisa kwake wakifika hawana la kusema au kufanya lakini wanajilazimisha kuongea tu ili mradi.

    ReplyDelete
  34. OBAMA The communitty organizer!
    Mashaka, The community organizer
    Both share many things in common
    Both Brilliant Luos
    Both Humble men
    Both agents of change
    Both Mesiahs
    Both Lawyers
    Both give superb Speeches
    Both are media sensation
    comom

    ReplyDelete
  35. MHESHIMIWA MASHAKA, BWANA SIKUSEMI KWA UBAYA ILA NASHANGAA HAUKUNISALIMIA WAKATI WATU KIBAO WALIKUSALIMIA PALE BREAKING POINT YA MILLENIUM TOWERS. ULIKUWA NA MAIWAIFU WAKO BOMBA KWELI KWELI,TENA NARUDIA BOMBA KWELI KWELI, SIJUI YULE NI MMAREKANI AU TOTO BOMBA LA KIBONGO.AU YULE NDO SECRETARY WAKO???? NIKAONA WADAU WANAPIGA PICHA NA WEWE ILA TU NILIKAA KI USTAARABU NIKIDHANIA UNGEKUJA HATA KUNISHIKA MKONO MKUU. ILA NAKUBALIANA NA WEWE KWANI MTU WA KUJICHANGANYA SANA. HAUNA MAKUU . MUNGU NA AKUBARIKI KWA KAZI NZURI UNAYOIFANYA KWANI WENYE KIPAJI KAMA YAKO NI WACHAHCE HATA MARAIS WENGI WANALILIA BUSARA NA HEKIMA ULIYO NAYO
    WEWE UKIWA RAIS NA YULE POMBE MAGUFULI, BASI TANZANIA ITAENDELEA KWELI KWELI VIZURI SANA ILA UKIJA NEXT TAIMU, NISALIMIE ANAGALAU NAMI NIJIONE NAFAHAMIANA NA WATU MAARUFU

    ReplyDelete
  36. Anony wa 4:02am, umeshitukia sio waoshwa vinywa ni tortoise wa mchana sio,LMAO! Nimependa kiingereza chako mno, lol! Job true true...........lmao!

    ReplyDelete
  37. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  38. mashaka ubarikiwe kwajuhudi zako

    ReplyDelete
  39. watanzania kusema kweli tungemuiga mashaka kwani ni chachu ya kizazi chetu. huyu mtoto anajituma mno na kuwa mfano mzuri wa kuigwa.

    ReplyDelete
  40. mashaka dili kama kina nanihii, vipi bado single??? naweza kujikita ulingoni, hakuna cha mahari wala nini. mimi bure mzima mzima, toa email nikutumie picha, bonge la mali....

    ReplyDelete
  41. hivi siri ya mashaka ni nini? kwa maana kila anapowekwa watu wanatiririka kama hawana akili vile. mbona ni kijana wa kawaida tu anayejituma sasa hii ndo nini? kijana wana comment kumhusu kuliko Kikwete ambaye ni Rais? au ndo ile tambiko la kondoo mweuzsi aliyefanyiwa inafanya kazi? mimi nashindwa na hata Michuzi mwenyewe nadhani anafurahi sana anavyotembelewa akimuweka mashaka. Jamii Forums pia wameanza na Mashaka siku hizi, kila ukifunua ukurusa jina la joni mashaka lazima liwemo, nadhani wameona mali kumuandika jamii pengine ad sense yao itapanda.

    ReplyDelete
  42. JOHN MASHAKA KISWAHILI CHAKE NI CHA KENYA NA SIO TANZANIA, HIVYO MNASHANGAA NINI!!

    MDAU
    NAKURU.

    ReplyDelete
  43. mashaka nashindwa kabisa busara uliyonayo. wewe ni kijana wa ajabu kweli.vipi tunaweza kukutana ili tubadilishane mawazo? mimi naishi Dallas TEXAS, naomba email yako, kupitia kwa michuzi

    ReplyDelete
  44. mie sitaki harrier au dola 5000 kwa mwezi. mie namtaka huyo mwanaharakati nizae naye. hiyo ni dili tosha akipenda kunioa poa akikataa pia haina noma, nina uhakika huyo mtoto akichukua akili za mashaka atalipa sana.yaani baba yangu hataki maari wala nini, mashaka hata kama ni nyumba mie tayari ninayo wewe ni kuja kukaa na kunizalisha mtoto mwenye ubongo kama wako, vipi hiyo dili??
    ila mimi mnene kidogo sijui unapenda totozyenye minyama nyama ila shepu na makalio pamoja na reception zinalipa sana, haya basi nitafute kupitia tigo 0719-558-0874

    ReplyDelete
  45. OBAMA The communitty organizer!
    Mashaka, The community organizer
    Both share many things in common
    Both Brilliant Luos
    Both Humble men
    Both agents of change
    Both Mesiahs
    Both Lawyers
    Both give superb Speeches
    Both are media sensation
    comom
    POINT ADDITION TO YOUR CONTRIBUTION
    BOTH: were raised by grandmothers after being being abondoned by their fathers

    ReplyDelete
  46. The guys is Tanzanian by birth. Suala la kusoma nje ya nchi au kuwa na ndugu upande mwingine wa mpaka hauwezi kumnyima uraia wake wa kuzaliwa.
    Kwahiyo kama mnatafuta wachawi sio kwake.
    Sio kila mjaluo ni Mkenya.
    Trash this talk.

    ReplyDelete
  47. mheshimiwa mashaka, kwa nini umage dola laki tatu na hamsini, yaani US$350,000 na Land Cruiser Prado 4, wee umerukwa na akili wee mtoto, ubunge wa nini na umri bado unaruhusu? Angalia wakina Zitto Kabwe, njaa tupu !!

    ReplyDelete
  48. ninapandwa na hasira kuwaona watanzania wakikashifu shuguli kama anazozifanya bwana mashaka.

    nani mwingine anayejitolea kama huyu mtoto has akatika umri wake.

    watanzania tuhacheni upumbavu, nchi yetu inaliwa na kubaki mifupa wakina lowassa, rostam wameshachukua kila kitu

    ReplyDelete
  49. napenda huyu bwana anavyojibidiisha.

    ReplyDelete
  50. watanzania walivyowajinga. sasa hivi wameanza kumtafutia mashaka mchawi, hivi hivi walimtafutia Obama Ujinga wa Uraia. mashaka ni mtanzania tena wa kuzaliwa, bahati amesomea nje za nchi. kwa wanaomfahamu, ni kijana wa kuogopwa, mtaratibu, simple lakini kichwani kipaji cha ajabu. mnaozusha Ukenya, huu ni upuuzi mtupu, huyu ni mtanzania. nyumbani kwao ni musoma. Baba yake ni mtanzania aliyesoma Musoma Alliance, Oxford na Baadae Harvard Business School. Marhemeu baba yake amefanya kazi UNDP kwa miaka, baadae na World Bank pale Kenya na hatimaye Aliendsha mradi hapa Tanzania.kwa hiyo swala la uraia ni upuuzi mtupu. hebu jaribuni kujadili mada za mashaka badala ya kusumbuliwa na wivu kama wanawake,

    ReplyDelete
  51. Kitabu ambacho kinawanukuu,
    Mandela
    Martin Luther King Jr.
    Malcom X
    Mahatma Ghandhi
    Nyerere
    Kwame Nkrumah
    kadhalika inaenda kumnukuu huyu kijana wa Afrika
    MESIAH YOHANNA MASHAKA
    Huyu ni mibaraka toka kwa mwenyezi Mungu endelea kutetea haki za wanyonge

    ReplyDelete
  52. LONDON SCHOOL OF COMMERCE, THAT IS JUST A NAME NI COLLEGE KAMA VI-COLLEGE MBUZI VILIVYO MITAANI BONGO, NA MBA YAO NI YA KUTOKA UNIVERSITY INGINE NINA MAANA UKIMALIZA CHETI KITANDIKWA KUWA KOZI YAKO IMEKUWA MODERATED NA HICHO CHUO. PIA KUHUSU WAZUNGU KUKOSA NAFASI SI SABABU YA PESA HASA INAPOKUJA KWA LEADING UNIVERSITY NI KWAMBA HAWACHUKUWI WATU OVYO TU LAZIMA UWE KIPANGA SANA HAO WACHININA NA WAHINDI UNAWOWASEMA SI WALE DODGE NI WALE WENYE AKILI KAMA SAMAKI, NI KWELI WENGI YA WENYEJI WAZUNGU HUO WANASHINDWA KUPASS ENTRY EXAM KWENDA KWENYE HIZI UNI KUBWA KWA VILE HUWA ZINZHITAJI ENTRY EXAM SI KAMA ZINGINE ZISIZO NA MAJINA, WENGI YA WAZUNGU HUPATA MA-"A" LAKINI MENGI NI YA MASOMO MBUZI KAMA MUSIKI, MEDIA, CIVICS AMBAYO HAYASOMWI MARA NYINGI KWENYE HIVI VYO VIKONGWE NA INASEMEKANA MTAALA WA SECONDARY SCHOOL HAPA NI WEAK KIASI KWAMBA HATA WALE WENGI WANAOENDA UNI U-DROP ON THE WAY KWA KUSHINDWA KU-COPE NA MASOMO. NI SAHIHI KABISA WENGI WANASHINDWA KWENDA BIG UNI HAPA KWA VILE HAWAPATI NAFASI YA KUINGIA KUTOKANA NA PAMA PASS ZAO AU KUSHINDA KUPASS ENTRY EXAM SI SWALA LA PESA, FANYA UTAFITI NA HUO NI UKWELI.

    ReplyDelete
  53. hali ya hewa imechafuka mtaa wa pili jamii folum. mashaka anakuna watu vichwa NYANI NGABU aka KUIUS amechachamaa na wivu wake wa kipumbavu na rafiki yake FIDEL80 ambao wote ni wajinga kama wanawake kazi zao ni kusengenya watu. wangekuwa wanaume wangefanya mavituzz kama mashaka badala ya kujificha kwenye mitandao kupazia watu. mashaka ni damu yetu, nyie endeleeni tu mtakiona cha moto kilichomtoa kunguni uvunguni

    ReplyDelete
  54. Leo wengine wanalalama kiswahili cha mashaka sio kizuri, sitashangaa kesho wakilalamika kwa nini asiandike kwa kiswahili?

    ni yale yale ya kijinga yaliyompta kanumba. Mashaka huko juu, endelea kuwatetea na kusaidia masikini wa kitanzania.

    ReplyDelete
  55. JOHN MASHAKA NI KANUMBA MTARAJIWA, TETETETEEEEE.
    NGOJA SIKU MOJA UKOROGE KWENYE KIINGLISHI, US-BLOGGER BASI SIKU HIYO ATAFURAHI HADI BENKI

    ReplyDelete
  56. Rais 2015 ni??????????
    John Mashakaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  57. I am prouding of you Tanzania jinias. Kijana, uliwahi umande na darasa likakubali kazi nzuri kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu tanzania. umekuwa mfano mzuri sana wa kuigwa
    Swahiba wako US-Blogger kaishia wapi, Jehanamu?
    Hana lolote Yule Fixii tuuuu

    ReplyDelete
  58. Shida na hawa wabeba boxi, wakirudi hapa bongo wanajiona wao ndo wao, sehemu za kujirusha hela wanamwaga kama karanga watoto kwa sana.

    Hela zenyewe zimekusanywa kwa miaka,punde wanatokomea kama pedejee Jack Unguja. ukifatilia unakuta nyumba moja wanaishi utadhani kumbikumbi.

    Gari moja wanatumia kwa zamu, kitanda ukitoka ukirudi unalala chini. Ndo maisha, rudini bongo bwana hata bongo watu wana wini, majuu kumewashinda.

    Mashaka hacha kuwaumbua Maisha mnayoyaishi huko ni maisha ya kudhalilisha mno ndo maana wanaona wivu kwa kila anachokifanya mashaka. Mimi na kibanda changu baada ya mzigo wala sifikirii nani atanitupa nje mwisho wa mwezi.

    Nyie badala ya kurudi na mitindo ya nywele, viatu vya lebo, hebu mrudi na maadili. Msibebe boksi iwachanganye vichwa mkasahau kwenu. Mashaka shukrani kwa makala mazuri safi kichaa wangu

    ReplyDelete
  59. US-Blogger)
    I see mashaka supporters in full gear praising some American puppet.
    Tanzanian’s you must wake up and see what is ahead of you instead of being blind flowing Mashaka so irresponsibly.

    You must be people of low IQ’s not to see there is nothing new here. I can write ten times better and high quality material than this.

    Bring him on and you will see how I will crush him in debate
    Mashaka is not a Samaritan he is just an opportunist like any other politician, and being an Investment Banker does not make him a god.

    They are the people who broke the world economics and you are now praising him????????????????????????????

    People, use your brains, don’t give this guy votes because he is not qualified let him remain in the Wall-Street crap he think he is

    Mashaka are you still dodging me, do you want to debate or not?
    Acheni akili kama watoto wadogo watanzania, mashaka siyo ajabu yoyote heri hata mange kimambi kuliko nabii wa uongo yohanna mashaka

    US Blogger.

    ReplyDelete
  60. HAWA WATU WANAOSHA WAZEE HADI AKILI ZINAWARUKA KABISA, HUYU NI CHIZI. HUYU MTU MBUZI KWELI HETI MASHAKA NI MKENYA, WEWE fmes ZIMO KWELI KICHWANI
    MJINGA SIKU ZOTE HUFIKIRI ANAJUA,NA NI RAHISI KWAKE KUKATAA USHAURI. MASHAKA ANACHOONGEA NI UKWELI MNAOUPUUZA LAKINI MIOYONI MKIUMIA, NI UJINGA NA UZEMBE WA KUFIKIRI. SOMA MAONI YA PILI JUU, HUYO JAMAA ANATUTUKANA WASOMAJI WA BLOG YA JAMII ,AKAFIKIRI HAPA NAPO NI ZE UTAMU,NI MJINGA HUYO.
    WATANZANIA WANAOISHI NJE ,WENGI HAWAJASOMA, NA MAISHA YAO YANASIKITISHA, LAKINI BADO WANAPONDA USHAURI. WATZ BONGO, KILA SIKU JUMAPILI, JAMAA ZANGU BAADA YA CHUO,BADO WANAPENDA KAMPANI ZA KITOTO, TUBADIRIKE,HII UCHUMU MPINDO ITATUTOA KAMASI!

    ReplyDelete
  61. Sie watanzania wa kawaida tunakuunga mkono, na kama wadau wengine walivyowahi kutamka, tupo tayari kukutetea hata na damu zetu kwa sababu thamani yako ni kubwa

    Umahiri na kipaji ulichonacho inawagusa wengi, juhudi zako zitazaa matunda mazuri kwa hii nchi iliyozingwa na ufisadi. Usikate tamaa, kwani asilimia kubwa ya watanzania 95% wanakukubali na kukutetea

    Hachana na hawa 5% ambao wameshindwa maisha na wamebaki makopo matupu zilizojaa kelele. Vijana aina yako wanaojituma ni wachache sana kwa hiyo endeleza libeneke

    Usishangae hawa wanaokuonea wivu ndo wale watakaokuja kujikomba kwako kuomba uasidizi. Wivu wao unatokana na U-Celebrity wako ambao unakua kila kukicha

    Hongera jwa lugha yako iliyoenda shule na shule ikakubali. I wish I culd only be able to have a quarter of your rhetoric and langeage might

    ILA KUMBUKA KWAMBA MAFISADI DAIMA WATAKUPINGA TU, NDIO HIYO MIFISADI KWENYE MITANDAO YA JAMII FORUM (CHADEMA) NA WABEBA BOXI NA WAOSHA VINYWA KWA MICHUZI

    ReplyDelete
  62. I recommend the use english language in addressing issues that could be of relavance to the entire population of readers. I am worried if all the readers of this blog are conversant with SWAHILI.
    english is a global language, used from China to Britain, and since this blog is frequntly visted by people of all races, I am sure then will benefit when u use English

    ReplyDelete
  63. Nyerere who was one of the biggest brains of Africa was never a Tanzanian, he was a Tutsi, theferore Mashaka is not a Tanzania but a Kenyan. and so is Hasheem Thabeet.

    I realized this after reading your article regarding EA community Debate; you nailed it and were shocked that a Tanzanian had such brilliant mind.

    But then realized that you had your educational foundation from Kenya , that gave you an opportunity to reign intellectually unopposed, therefore we see a parallel between you and our Obama, both of you have Kenyan roots.

    We as the land where you received your education (Kenya) we are proud of you as we are proud of our existential son, B. H. Obama who is a day away to be inaugurated as the 44th President of the United States of America.

    I am sure you are soon going to hold the candle for your countrymen (Tanzanians) just like our Obama did to Kenyans

    Mr. Hasheem Thabeet, Please keep on the torch for us Kenyan's. We are proud of you like we are proud of John Mashaka. Please carry high the Kenyan flag

    It is clear that, even though you are not in the leadership, we see you as one of brilliant young men with Kenyan roots who have leadership might.

    As a Kenyan and an East African, I must salute you for the article well written. All the best in your future endeavor

    Mjomba: Mr. Waweru Githinji
    Nairobi.

    WATANZANIA HAWANA AKILI NDO MAANA WANAANDIKA UJINGA KILA SEHEMU BADALA YA POINTS. SISI KENYA ATUANDIKI USHUZI KAMA WENU

    ReplyDelete
  64. mie naomba mjadala kuhusu mashaka na Kanumba. Je nani zaidi kati yao

    Mashaka Vote 1
    Kanumba Vote 2

    tutahesabu kura humu humu,

    ReplyDelete
  65. MIE NI SHIDA MOJA TU, HUYU US-BLOGGER ANANIKERAGA SANA NA MAJIVUNO YAKE HATA PASIPO STAHILI. MTU BWEGE SANA

    ReplyDelete
  66. NIMEMFATILIA KIJANA MASHAKA KWA UKARIBU KUHUSU IDEOLOGY YAKE NA MIMI KAMA MTANZANIA NINAEONA KWAMBA NCHI YETU HAIJAPIGA HATUA YEYOTE TANGU TUPATE UHURU NA VIONGOZI WETU WAMEKUWA WAKIENDA IKULU KUTALII KWA MIAKA 10 NA KUIACHA NCHI IKIWA IMEDORARA KULIKO WALIVYOACHIWA.

    MAONI YANGU NAMSHAURI BWANA MASHAKA NA DR. SHAYO WAANZE MIKAKATI YA KUGOMBEA URASI KWA SABABU ZIFUATAZO:

    1.HUYU KIJANA ANA HURUMA KWA MTANZANIA WA KAWAIDA,WATANZANIA KAMA 80% WANAISHI MAISHA DUNI KTK DIMBWI LA UMASIKINI,SASA MASHAKA TAYARI KISHAONYESHA KUJALI WANYONGE NA NIMATUMAINI YANGU HUYU BWANA ATAWASAIDIA SANA WANYONGE WALOTELEKEZWA KWA MIAKA HII YOTE TANGU TUPATE UHURU.

    2.BWANA JOHN MASHAKA NI MCHUMI AMBAYE ANAELEWA CURRENT ECONOMIC ISSUES AND HOW TO SOLVE THE CRISIS,HUYU JAMAA NI MWELEWA NA NI MSOMI MAKINI.NI MATUMAINI YETU ATATUSAIDIA SANA KUJENGA UCHUMI WA NCHI YETU.REJEA ARTICLE YAKE HAPO JUU.AMEWEZA KU-FORESEE WHAT OUR COUNTRY NEEDS,SIO VIONGOZI WETU WANATUDANGANYA TU HAWANA DIRA YOYOTE KUKWAMUA NCHI YETU TOKA KWENYE UMASKINI WAKATI RASILIMALI TUNAZO NYINGI TU.

    3.JOHN MASHAKA NI MNYENYEKEVU ASIE NA MAKUU NA HII NI SIFA KUBWA SANA KWA KIONGOZI WA TAIFA.

    4.JOHN MASHAKA NI KIJANA AMBAYE AKILI,FIKRA ZAKE NI ZA KILEO HIVYO HE WILL DRAMATICALLY OVERHAUL THE CRISIS OUR COUNTRY FACING RIGHT NOW.

    5.JOHN MASHAKA HANA HARUFU YA UFISADI NA ITAKUWA RAHISI KUSAFISHA MAOVU NDANI YA MFUMO WA UTAWALA.

    BWANA MASHAKA MIMI NAKUPA 5 NA NIPO TAYARI KUKUPIGIA KURA RIGHT NOW.....HUYU KIJANA NI GENIOUS TUMPE SUPPORT AWEZE KUTULETEA MAENDELEO YA KWELI.

    JOHN, I GOT TRUST IN YOU MAN NA NINAOMBA WASOMI WOTE VIJANA TUSIMAME KUMSUPPORT HUYU NDUGU YETU NA MATUNDA MTAYAONA,MAY B TUJADILI NI VIPI ANAWEZA KUPATA HII CHANCE YA KUGOMBEA URAIS.

    ReplyDelete
  67. MIZUPU SWALI KWAKO, HIVI VODACOM WANAWEZA KUANZISHA JOHN MASHAKA CHALLENGE CUP AU PROMOSHENI YA AINA YOYOTE YENYE ZAWADI JUU YAKE KWA SABABU JAMAA ANAVUTIA SANA KWENYE GLOBU YAKO NA MSHIKAJI WAKE KANUMBA???? MIE NAONA HII NI IDEA NZURI YA KUWEZA KUONGEZA WASOMAJI WA GLOBU, HUYU DOGO NI KIBOKO ANAJUA SANA KUCHOKOZA MADA NA WADAU WANAITIKA KWELI KWELI

    ReplyDelete
  68. Sioni alternative zaidi ya kizazi cha mashaka kushikia usukani wa uongozi Tanzania. Tukihacha mambo ya wivu, ukweli unajulikana bayana sana. Wengi tunakubali kwamba huyu mtoto anakipaji cha aina yake lakini hatutaki kukubali kwa sababu tunaamini kwamba anatushinda, na nina amini huyu na hizi hotuba zake na maandishi yake ana kikubwa kuliko tunavyofikiria sisi. Watu kama hawa ni adimu kweli ni wale wanaotokea baada ya karne.

    ReplyDelete
  69. spichi imetulia kweli kweli, safi sana mkuu.... inabidi tuchapishe nakala tuwapelekee viongozi wetu na mawaziri wote

    ReplyDelete
  70. kazi nzuri sana mashaka, usikate tamaa dunia inawahitaji wengi kama wewe siyo ile full kujiachia

    ReplyDelete
  71. NYIE WABONGO HACHENI UZUSHI. MASHAKA NI MTU WA MALAWI, TENA WALIKUJAGA TANZANIA MWAKA 1995

    ReplyDelete
  72. JAMANI YULE NYANI NGABU aka JULIUS NI BINADAMU AU SHETANI, JAMAA ANA WIVU UTDADHANIA NYANG'AU. HABARI NDIYO HIYO. WANA JAMII FORUM MNAMUONA NYANI NGABU

    ReplyDelete
  73. watanzania, ni kweli mashaka anagombea ubunge?

    kwa maana kama ingekuwa ni kweli, basi kule Rorya hata kampeni isingehitajika. Yaani angembwaga Sarungi kama mtoto mdogo

    Huyu kijana nakubalika Rorya kweli kweli, ndo maana Sarungi kakimbia kupiga kambi. Ametishika kweli. lakini kama ni hivyo basi yeye ni Mbunge wa jimbo mbili

    Ukonga na Rorya ambayo itakuwa ni historia Tanzania

    ReplyDelete
  74. wakina mashaka ni watu wachache sana duniani, tusemi kweli tuache wivu

    ReplyDelete
  75. jamani watanzania, hebu someni wosia wa bwana mashaka, ana mambo mazito kwa watanzania, someni mambo yake na maneno yake hacheni uzushi kuhusu ubunge, yaani tutakuwa butu hadi lini? tuamke wajameni

    ReplyDelete
  76. jon, ungekuwa karibu nami ningekubusu mpenzi, hii hotuba nzuri sana nashangaa wengine badal ya kuchangia wanaweka upup wao

    ReplyDelete
  77. angaau tuna mtu mmoja a mbaye ni serious, siyo ile mijinga ya kujirusha kila kikicha. mashaka mie nakufagilia, na hata ukigombea ubunge au urais nitakupigia kura tu, waseme watachoka. mashaka hoyeee

    ReplyDelete
  78. hii siyo kazi ya mashaka peke yake kulaani mauaji ya albino, inbidi tushirikiane watanzania wote kulaani hii tabia. yule waziri kijana anayetembelea mashindano ya ma miss wakati maalbino wanauwawa anaitwa nani?

    ReplyDelete
  79. Breaking News

    thread ya John Mashaka yaangusha jamii forums.........

    ReplyDelete
  80. AMA kweli binadamubwote hawaumbwi sawa mwenzeru ameumbwa tofauti kabisa. Huyu kaumbwa kivyake kabisa

    ReplyDelete
  81. I suspect that the same mashaka who is against gjadaffi will come up with gjadaffi policies. Boy you must listern to US blogger who is Oxford genius not you. Even ridhwani is the only genius from kikwetes family can beat you in English he is not lime you and kanumba who don't know English

    ReplyDelete
  82. Ukichunguza kwa undani ni kwamba wengi wenu mnamkubali mashaka na idiology yake Ila tu mnaosha vinya kwa kuulana ukweli wa mambo. Nadhani mtazamo wa mashaka kamwe jaujaegemea ufisadi hata kidogo kwa wanaobwabwaja endeleeni kubwabwaja lakini ukweli mtakuja kuukubali muda siyo mrefu

    ReplyDelete
  83. mweee kumbe MASHAKA uko ivi???

    asante

    ReplyDelete
  84. mungu na akulinde jamani kwa kuwajali hawa viumbe masikini wanaonyanyasika

    ReplyDelete
  85. wanduguzanguni, tupendeni maendeleo ya wwengine. mashaka anatumia rasilimali zake kusaidia masikini tanzania, wewe unafanya kazi gani

    ReplyDelete
  86. $350,000.00 ni karibu milioni mia tano za madafu ($500,000,000.00) kama unazitupa katika kampeni ya ubunge basi business model yako ni mbovu, utazirudishaji hizo, ili zirudi unatakiwa kupata mshahara siyo chini ya milioni mia moja kwa mwaka (Ths 100,000,000.00)
    miaka mitano ni 100,000,000.00x5 = Ths 500,000,000.00 sinahuhakika kama wanapata hivyo kwa mwaka labda waibe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...