Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hivi ndio Mnachochea sasa Muhimu Msichague Walevi na wapenda wanawake Yani Malaya inshallah mwenyezimungu atatufungulia.
ReplyDeleteNDUGU KIPANYA, HII MAANA YAKE NINI?
ReplyDeleteKWANI WEWE KIPANYA UNAFUATA ITIKADI GANI?
UKRISTO?
UISLAMU?
UPAGANI?
AU ITIKADI GANI?
SINA HAJA YA KUJIELEZA MIMI NAFUATA GANI, LAKINI KIGEZO CHANGU NI KWAMBA KWANZA NAFUATA ITIKADI YANGU, KISHA NDIO MAMBO MENGINE.
ITIKADI YANGU INANIELEKEZA HIVYO, NA NAAMINI KWA MTAJI HUO NDPO KITAELEWEKA.
NIKIMPIGIA KURA ASIYE WA ITIKADI YANGU, ETI KWA KASUMBA YA "UTANZANIA TU", NIKIKWAMA SITAWEZA KUMSUTA.
MGOMBEA NITAEMCHAGUA KWANZA NI SHARTI AWE MWENYE KUFUATA ITIKADI YANGU KISAWASAWA, MWADILIFU, MKWELI, MUUNGWANA NA MPENDA NCHI. NA HIVYO NDIVYO VIGEZO KWA MUJIBU WA ITIKADI YANGU.
NIKIJIDAI KUCHAGUA TU KWA KUZINGATIA UZALENDO, ITIKADI YANGU ITANISUTA PALE ATAPOKIUKA MAADILI.
NA HUU NI UKWELI KILA MWENYE ITIKADI YA KIDINI YA KWELI ANAYOIFUATA.
SIDANGANYIKI KWA KUENDEKEZA UMOJA USIOJENGWA KWA MISINGI YA ITIKADI. NA KAMA WEWE KIPANYA NI MTU WA ITIKADI YANGU UTAKUBALIANA NAMI. TANZANIA YA LEO IMEOZA KUTOKANA NA VIONGOZI WENGI KUTOFUATA MAADILI YA DINI ZAO. SIASA TU BILA KUFUNGAMANA NA ITIKADI SAHIHI KWANGU MIMI NI MUHALI.
HII NI KWA MUJIBU WA ITIKADI YANGU, NA KAMA WENGINE WANA MIONGOZO TOFAUTI SI TATIZO, NAHESHIMU MAONI YAO.
KIPANYA WAACHE VIONGOZI WA DINI WAELEZEE HISIA ZAO, NA WEWE KAMA ITIKADI YAKO INAKUFUNZA UTANGULIZE "UTANZANIA" MBELE YA ITIKADI, UNA HAKI KAMILI YA KUIPIGIA DEBE.
DEMOKRASI KWA NINI IWANYANYASE VIONGOZI WA DINI?
I WAPI HESHIMA KWA MAPADRE NA MASHEKHE WETU?
SABABU KAMA KITABU NINACHOKIFUATA KINANAMBIA "MPIGIE KURA MCHA MUNGU WAKO" NI VIPI UAMUZI WANGU WA KUFUATA MAAGIZO HAYO USIHESHIMIWE?
I WAPI BASI MAANA YA DEMOKRASIA?
Ahsante
Mndengereko, Ukerewe
Mi naona huko tumefika kabla hata ya miaka 100.
ReplyDeleteTunachosubiri ni uwazi tuu sasa hivi tuna usiri.
Hii demokrasia ya kisekyula huwa inadanganya kundi moja la kidini na kundi lingine ambalo hupuuza kisiri hufaidika.
Mi naona watu watumie dini zao tuu ili yenye watu wengi ishinde halafu tuone UONGO husaidia nini?
Kwa wale viongozi wa dini mnaotafuta chaguo la Mungu, waambieni wafuasi wenu hivi " UKIMCHAGUA ASIYE MCHA MUNGU AKAKOSEA MTAENDA NAE JEHANAMU"
kipanya hayo unayosema mbona tayari yameishatangazwa katika hizo nyaraka mojawapo?tusijifanye vipofu!ILA NAWAPENDA WATANZANIA KWANI NI MABINGWA WA KUSHABIKIA MAMBO ILA IKIFIKA WAKATI WA KUPIGA KURA HUWA NI SIRI YA MTU BINAFSI HAKUNA CHA SHEHE WALA MCHUNGAJI OK!nawasilisha mdau finland
ReplyDeleteJe, vipi kama wagombea wote wawili wa ubunge katika wilaya fulani ni wakristo, je mnataka waislamu ndio tugomee uchaguzi au vipi? Je vipi kama wakristo wangegomea uchaguzi wa Raisi wa mwaka 2005 kwa hoja ya kuwa mngombea wa tiketi ya CCM (JK) na yule wa CUF (Lipumba) wote ni waislamu, tungefika? Je, vipi kama waislamu enzi zile kabla ya vyama vingi wangesema mgombea pekee wa uraisi (Mwalimu Nyerere) ni mkristo basi waislamu wagomee uchaguzi, tungefika kweli?
ReplyDeleteAcheni kuchochea udini nyinyi. Tanzania ni nchi ya amani. Au mvipofu? Angalieni nchi zinazochochea ubaguzi kwa misingi ya dini kote duniani zinavyosambaritika. Acheni siasa za kinafiki hizi. Hatuzitaki Tanzania.
Mdau, Australia
Hawa viongozi wetu wa dini naona wameingiliwa na kamdudu kabaya tangu lini dini ikawa kama chama cha siasa. Nawashauri waanzishe vyama vya siasa tujue moja badala kutaka kututumia kondoo wa bwana.
ReplyDeleteUrais ni utumishi wa nchi.
ReplyDeleteNchi yetu haina DINI, CCM haina DINI, MWANANCHI yeyote anayo haki ya Utumishi wa kitongoji hadi kitaifa.
DINI siyo sifa katika uchaguzi wa RAIS wala utumishi wowote bali maarifa na juhudi ya KAZI.Nyang'au wa SIASA msitugawe kwa SERA dhaifu.
MUNGU NI MMOJA. Wakristu na Waislamu wa kweli wote wana SUJUDU mbele ya Mwenye ENZI zote MUNGU.
MAINA OWINO
NJAA HAINA DINI. USAFI HAUNA DINI
ReplyDeletewewe wa ukerewe, aliekwambia kuwa bongo kuna kiongozi mwenye kufuata dini ni nani? peleka huko udini wako! Kiongozi bongo anaangalia tumbo lake na wala usitegemee eti kwa kuwa ulimpa kura wa dini yako atakusaidia, sahau! kwanza serekali haina dini! Nyie ningeweze ningewaambia msirudi nchi hii maana mnaleta utamaduni wenu wa kuiga!
ReplyDeleteHaya yanayotokea sasa si ajabu sana.Kiongozi wa siasa nchini CCM,analegalega.
ReplyDeleteMimi ni mwana CCM niliyekubuhu lakini sipendi ninachokiona.
Inabidi CCM icshike tena hatamu za kisiasa.Hii itawezekana tu kama itikadi ya chama itawekwa sawa ili wananchi waielewe.Ilani ni mwelekeo temporary wa utekelezaji lakini itikadi ni vision ya kuaminika zaidi.
Tukiendelea na siasa bila itikadi inayoeleweka matokeo yake ndiyo tunayoyaona kama miongozo ya Wakatoliki na Waislamu.
Siasa hazitaki ombwe(vaacum), na ikitokea interest groups tofauti zitajitokeza kutetea maslahi/maono yao.
CCM ina kazi kubwa ya kuwaunganisha waTanzani katika kupata itikadi sahihi na ikishindwa kufanya hivyo basi vision ya kule tuendako hakujulikani
nakubaliana na askofu kakobe mia kwa mia hatuchague maaskofu wala masheikh tunachagua wiongozi wa serikali.....wao waendeleee kueneza neno la bwana tuu na wahimizee amani na upendo duniani
ReplyDeleteAcha udini rudia kusoma waraka wa wakatoliki na wa ponda uone upi ni wa udini
ReplyDeletewaraka wa wakatoliki ni kama kusafisha kanisa kwa waliyoyafanya 2005 ya kumkaribisha kikwete special area(jina limenitoka)huku wakimnadi kuwa ndiye mteule(chaguo la mungu)na sasa kweli mteule anaonekana
MREMA ALIPONDA SANA HII ISSUE YA KANISA 2005
KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INASEMA WAZI WAZI KUWA SERIKALI HAINA DINI ILA KUNA WATU WANAJIFANYA VIPOFU KUWA DINI YAO NA IMANI YAO LAZIMA ICHANGANYIKE NA SERIKALI ILI SARA ZAO ZIWE KAMILI
ReplyDeletetanzania kura hazipigwi misikitini wala makanisani na kura ni siri ya mtu mtajijua ninyi mashehe na maaskofu mnaotoa miongozo kwa sasa waumini wanawashabikia ila KURA NI SIRI YA YA MIOYONI OK
ReplyDeleteMtoa Maoni Sat Sep 05 01:14:00 PM Uko makini sana. Nimependa sana uliposema kanisa linajisafisha.Lakini si lingeungama tu kwa wananchi waziwazi kwamba jamani ee 2005 tulikosea? Au vipi? Mbona linahamasisha waumini wake kuungama na kuombana misamaha wakikosea? Sasa basi viongozi wa Kanisa wangekuwa mstari wa mbele kuonyesha mfano wa kuomba msmaha na kutubu.Tena makanisa yote tu siyo Katoliki peke yao, na waluteri na wegine.Au vipi?
ReplyDeleteHalafu kina Kingunge walikuwa wapi 2005 wakati Makanisa yalikuwa yakipiga debe waziwazi kabisa.Tena waraka wa sasa ni safi tu manana yake hautaji mtu unasema tu sifa za kiongozi bora ni zipi na waumini wazingatie hizo sifa wanapochagua.2005 viongozi wa kanisa walitaja jina moja hasa mpaka wngine kusema nanhiii ndo chaguo la mungu. Sasa Kingunge- kwa jinsi alivyozeeka na kuchoka na kushindwa kufikiri- masikini eti anang'aaka sasa na 2005 hakung'aaka!! Si maajabu haya!!!
hivi waraka ukisema kwa waumini wake kuwa wakapige kura kwa kikundi una maana gani?mimi nionavyo ni sawa na kusema tukamchague fulani wa dini yetu
ReplyDeleteHongera ndugu Kipanya kwa kutupatioa changamoto, kwa mtu mwenye akili atamchangua kiongozi kwa sifazake za uadilifu sio itikadi fulani. inasikitisha sana kuona tangu waraka wa wakatoloki utoke ndio kwanza viongozi wa madhehebu hayo wamezidi kuutetea bila kufahamu athari zake, sasa matokeo yake ndio hayo kila dhehebu linataka kutoa waraka wake , niaibu sana ktk taifa letu. lakini mwisho wa siku chama ta wala kitarudi madarakani, ni kelele zisizanaokua na tija yoyote.
ReplyDeleteBaadhi y viongozi wa dini wanataka umaarufu kwa kuwagawa wananchi,lakin mwisho wa siku watashindwa kwa uwezo wa Mungu.