Wandugu nawatangulizia movie nyingine hiyo ambayo iko jikoni inapikwa "Fair Decision" itatoka soon baada ya "Divorce" ambayo itakuwa madukani kuanzia tarehe 29/9/2009. sina mengi saana itakapotoka pata nakala yako. Mdau Ray.
kwa picha na habari kibao
za tasnia ya filamu bongo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. wee haya wee...! na hayo mambo yenu ya "the greatest". Muangalie mwenzako Steven Maimuna, u-greatest wote hautaki sasa hivi.

    ReplyDelete
  2. Hivi Viingereza vyenu vina mambo, tangu lini FAIR DECISION ikatafsirika Maamuzi sahihi?

    ReplyDelete
  3. Kwenye hizo Movie hakuna shida.. Maumivu ya kichwa huanzia kwenye KIINGEREZA. Mwenzako KANYOLEWA, sasa wewe anza kutia MAJI.

    ReplyDelete
  4. Mtoto wa CoastSeptember 13, 2009

    Ray tunashukuru kwa kazi nzuri kweli mnajitahidi.

    Hata hivyo kama mdau mmoja alivyoshauri hapa kwa Kanumba tafadhali tafuteni wataalamu wa kuwa wanasahihisha na kusanifu kazi zenu za usanii kabla hamjaziweka kwenye maonesho au mauzo.

    Ni aibu sana na hakika ni kuchemsha kama sio kufulia kitaaluma ukikosea mwenyewe(katika sarufi (umoja na wingi - 'UAMUZI' NA 'MAAMUZI') na maana ('CORRECT/RIGHT' isn't synonymous to FAIR) kutafsiri kichwa cha habari au jina la sinema au onesho lako.
    Kama jina hilo mlilitunga kwa Kiswahili basi kwa Kiingereza lingesomeka,

    'THE RIGHT DECISIONS'


    Kaka Michuzi mimi nawakubali kuwa hawa ni Magwiji wa Bongo katika hiyo fani lakini pia wawe wanakubali kusahihishwa vinginevyo itakuwa kama aibu tuliyoipata leo wakati Gwiji Serena Williams ananyea taranta yake hadharani kwa kutokubali kosa alilolitenda!

    ReplyDelete
  5. SWALI,KUELEWA KWANGU ENGLISH NISINGE TAFSIRI 'FAIR DECISON' KWA KISWAHILI 'MAAMUZI SAHIHI' WALIOSOMEA LUGHA NAOMBA MTAZAMO WENU.

    ReplyDelete
  6. TARATIBU TUNATOKA BY 2045 TUNAWEZA KUWA ZAIDI YA HOLLYWOOD MAANA SASA HUKO KUNACHOMEKA KILA SIKU.

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu Ray nimefurahishwa sana na moyo wako wa kupenda maendeleo, nimefurahishwa na kitendo chako cha kusikiliza maoni ya watu na kuchukua ushauri wao na kubadilisha title ya blog yako sasa inasomeka vizuri, huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine pengine rafiki yako Kanumba ataiga mfano wako na kuchukua ushauri wa watu badala ya kulialia na kuona ameonewa, nakupa pongezi sana kwa hilo, ukifuata mtindo huu utafika mbali Ray, sio kila mtu anawaonea wivu kama wachache wanavyofikiri. Nakutakia kila la heri.
    Mdau Mnoko

    ReplyDelete
  8. UKANUMBA MWENGINE NDIO HUU SASA.
    VIPI MTATAYARISHA DVD COVER YA KITOTO KIASI HICHO.

    JAMAA NAONA AMEWEKEWA MIKONO YA BANDIA KAMA MUNGU WA KIHINDI.

    PLEASE!FANYENI MAMBO YANAYOINGIA AKILINI.

    NAAMINI UWEZO HUO MNAO SASA KWA NINI MNALETA UCHAFUU HUU .

    ReplyDelete
  9. huyo jamsi bondi wa kibongo mbona pozi kama mungu wa kibaniani???

    ReplyDelete
  10. Fair decision = Uamzi wa haki

    Right/correct decision = Uamzi sahihi

    Hii unaweza kumuuliza hata mtoto wa sekondari akakusaidia kabla hujaweka kazi yako sokoni. Tusiwe wavivu kwa mambo hata haya madogo.

    ReplyDelete
  11. Ebawana mdau wa 10:12pm u made my day to day!!yaani nimecheka sana sana, yaani wewe ni kichwa fulani, poa mshikaji tuletee vingine vya kututo vistres!!!
    ndimbo Indonesia!!!

    ReplyDelete
  12. Ndiyo kawaida yenu kutumia maneno ya English halafu hamjui hata kiswahili chake ni kipi. Fair maana yake "haki" na decision maana yake "uamuzi". Hence fair decision ni "maamuzi ya haki" na siyo "haki maamuzi". Umeelewa???

    Ninawashauri muwe na kamati au board ya kufanya editing. Lakini najua hata hizo bodi nazo zimejaa vihiyo vitupu. Nchi yetu elimu kwa kweli ni ya kimaimuna jamani. Aaagh!!!

    ReplyDelete
  13. hawa WANACHOKIKOSEA UMOMBO WAO MWINGI WANAJIFUNZIA KWA WANIGERIA SASA NDIO MADHARA YAKE HAYA WENZAO WANIGERIA WAO WANA-MIX UMOMBO,IGBO NA PIGIN ENGLISH HUKU ULAYA SIE TUNAOTOKA EAST/SOUTHERN AFRICA TUNAONEKANA TUNAJUA UMOMBO KUWAZIDI HAO WAJAMAA MAANA YAKE WANA BIG DIALECT

    ReplyDelete
  14. Ugomvi wangu na nyie Amitabh Bachchan wa bongo ni filamu ya kiswahili kuipa jina la kiingereza...ina maana kiingereza mwakijua sana au ndo ulimbukeni? Kwani mgeipa jina la kiswahili kisha jina la kiingereza likawa kwenye mabano isingekuwa sahihi?

    ReplyDelete
  15. POOR COVER DESIGN..! U can do better than this.

    ReplyDelete
  16. NYIE WABONGO KWENU LIPI JEMA? NAONA HAMNA KAZI ZA KUFANYA MAANA KILA KUKICHA MNASEMA WATU, JARIBUNI KUWA POSITIVE JAMANI. NA HAWA WANAOSEMA WENZAO NI WAJINGA WACHACE TU!

    ReplyDelete
  17. Kwani lazima muandike kingereza jamani, kumbukeni wengi hamkusomea sanaa wala hamkwenda shule kiasi cha kuwa fit kwenye gramma, na tatizo kubwa MNATAKA KUFANYA KILA KAZI, YAANI ETI MMEKUWA MPAKA MADIRECTOR!, WAKALIMANI! FAIR DECISION SIO UAMUZI SAHIHIM, SI KILA KILICHO FAIR NI SAHIHI, Nimeangalia Movie nyingi za kibongo ambazo zina SUBTITLE ZA KINGEREZA, NI VITUKO TU!

    Mwana toka TMK

    ReplyDelete
  18. sasa bila mikono bandia mnafikiri hicho kitambi kingefikiwaje?

    ReplyDelete
  19. blog hii ukifungua ni lazima ucheke tu mbavu zangu wee kwi kwi kwiiii umeniacha hoi mdau uliyesema kaweka mikono kama mungu wa kihindi duh sina mbavu
    miss michuzi ukerewe

    ReplyDelete
  20. Ah nyie watu mnaokosoa lugha bora muache tu!manake naona huyu ndugu yangu Ndimbo wa Indonesia ameiandika today as if it is a preposition.Tafadhali kaka.....................!

    ReplyDelete
  21. Nshimimana aka DumisaneSeptember 14, 2009

    Uamuzi wa Haki ni : RIGHT DECISION:

    FAIR DECISION ni Uamuzi YAKINIFU.

    Wabongo mnakuja kasi!?

    = = =
    Buffalo (huku hatuongei kiswahili ki ivo?),
    New York

    ReplyDelete
  22. Kwa kweli kina Govinda wa bongo bado kazi mnayo. Inaonekana kama vile mnakurupuka hivi.
    FAIR DECISION ni UAMUZI WA HAKI
    CORRECT DECISION ni UAMUZI SAHIHI
    Na hiyo picha imeiga picha ya sinema ya Bond, James Bond iitwayo Octopussy. Kwa nini msipate mawazo kutoka kwa wenye vipaji vya masuala ya taswira kama Michuzi? Au maswala ya michoro kama "Kipanya"? Msione ubahili kugawana na wengine kabla ya kutoa sinema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...