Vodacom Tanzania leo imechezesha droo yake ya mwezi ya Tuzo Droo na kumnyakua Fitina Mohammed Mbamba, mkazi wa Kigogo DSM kama mshindi wa droo hiyo ambaye amejishindia Tsh 40 Milioni PESA TASLIMU.
Vilevile, Tuzo Droo ya wiki ilichezeshwa leo hii na kuwapata washindi SABA ambao wamejishindia Tsh 1 Milioni PESA TASLIMU KILA MMOJA ambao ni Ibrahim Ally, Mfanyabiashara wa Tanga, George Minja, Mwanafunzi wa Chuo Arusha, Demitria Sagumo, Mwalimu wa Mbagala Kuu DSM, na Freddy Elias, Mfanyabiashara wa Kisarawe.
Wengine ni Kulwa Abdallah, Mwalimu wa DSM, Raju Manase, Fundi Magari wa Mbeya, Rajabu Maulid, Muuza Samaki wa Lindi, Pamoja na washindi wengine 100 waliojishindia Tsh 50,000 za muda maongezi KILA MMOJA.
Endelea kutumia mtandao unaojali wateja wake wa Vodacom KILA SIKU na ubahatike kuwa mmoja wa washindi hawa. Pamoja daimaVodacom Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. USAWAIA WA KIPATO MAZOEA NA KIPATO CHA GHAFLA(THE EQUILIBRIUM OF AVERAGE INCOME AND A SUPRISE INCOME(FORTUNE).
    HALI YAKO YA KIFEDHA HUWA HAIBADILISHWI NA KIPATO CHAKO CHA GHAFLA. KIPATO CHA GHAFLA KITALAZIMISHA MATUMIZI YA GHAFLA ILI HALIYAKO KIFEDHAMAZOEA IRUDI KWENYE USAWIA WAKE(EQUILIBRIUM) MTU AMBAYE HAJAPATA FEDHA ZA GHAFLA KAMA HIZI KATIKA MAISHA YAKE ANAKUWA IMARA ZAIDI KIMAWAZO KULIKO MTU ALIYEPATA PESA KAMA HIZI HALAFU HAJUI ZIMEISHAJE HUWA ANAATHIRIKA KIMAWAZO.KATIKA MATUMIZI MTU HULAZIMIKA KUELEKEA KUISHI KWA UCHACHE AU WINGI WA MTUMIZI KULINGANA NA MAZOEA YAKE. MTU TAJIRU SANA NI RAHISI KUWA MASIKINI WA KUTUPWA KULIKO MTU WA WASTANI KUWA MASKINI WA KUTUPWA. UKIWA TAJIRI MFILISIKA UNA NAFASI YA KUJIDENISHA KWA KIASI KIKUBWA MAANA WATU WANAJUA UNAZO ( KUMBE KISIRI UKO KWENYE MPOROMOKO {FREE FALL} WA KIUCHUMI) UMASIKINI PIA UNA UBORA WAKE KIAFYA

    ReplyDelete
  2. Hongera Mh. Jk

    ReplyDelete
  3. Hivi unaingia vipi katika draw??? mbona mimi sijashinda wala nini na nipo online muda wote au mpanga niwe fundi magari au muuza samaki ndiyo nishinde???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...