Brother Michuzi,
Tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Katibu mkuu wa Daruso (2000/2201) Kamaradi Gervas Mkili aliyefariki jana.
Mkili atakumbukwa na wana DARUSO kama mpiganaji makini na mahiri kabisa aliyesimama kidete kutetea haki za wanajumuia ya chuo kikuu na jamii kwa jumla.Mungu amlaze mahali pema peponi
Amin.
Eng. Juma Hussein Msonge
Former DARUSO Cabinet Memeber and
Acting Secretary General (2000/2001)
----------------------------------------------------------------
KAMARADE MKILI GERVAS AMETUTOKA
Kwa niaba ya wenzangu wote tuliokuwa pamoja katika harakati za siasa za wanafunzi UDSM miaka ya mwishoni mwa 1990's mwanzoni mwa 2000's, tunasikitika kutangaza kuondokewa na ndugu, rafiki na kiongozi wetu mpendwa Mkili Gervas aliyefariki alfajiri ya jana Jumapili.
Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Salasala pembezoni mwa kanisa la TAG. Mwili wa marehemu utasafirishwa leo jioni kuelekea kijijini kwao wilayani Kahama, Shinyanga.

Kwa taarifa zaidi na michango yenu
tafadhali wasiliana na
Goodluck 0713 322058
au
Galani 0713 505941

Omar S Ilyas,
UDSM 1999 - 2003

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. RIP kaka Mkili, tunakukumbuka enzi za mgomo Nkurumah tulipokuwa tunakuimbia tunaimani na Mkili Oya oya oya.

    ReplyDelete
  2. Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. RIP Mkili

    ReplyDelete
  3. RIP Mkili, ulikuwa kiongozi shupavu hasa katika kutetea maslahi ya wanafunzi.

    Hukuweka mbele ubinafsi na kuwa tayari kufanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya wanafunzi, hasa pale uliposimamishwa masomo mpaka uwataje waliohusika kwenye mgomo. Lakini ulikua tayari kupoteza muda wako kuliko kusaliti hata member mmoja wa DARUSO.

    We will miss you Brother

    ReplyDelete
  4. ooh RIP kaka Mkili na utakumbukwa kwa ujasiri wako enzi za mgomo udsm ukihangaika kupigania haki za wanafunzi.ulifanya kazi kaka.wote tu safarini upumzike salama.

    ReplyDelete
  5. UUUUHh Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, ninamkubuka sana Mkili kwa ujasiri wake wa siasa za Daruso hasa siku moja alipokimbizwa akidadaiwa kukutwa na mabango ya Punch. Hakuna na moyo mwepesi ama kweli chema hakidumu.

    ReplyDelete
  6. Rest in Peace!
    mtoa habari si vibaya kutupa japo kwa ufupi sababu za kifo kwani wale tuliokuwa chini yake enzi za daruso..tuna majonzi mno kwa taarifa hii ya ghafla!

    ReplyDelete
  7. HE WAS ONE OF THE BEST SOLDER I EVER WORKED. BEING A MEMBER OF USRC( UNIVERSITY STUDENT REPRESENTATIVE COUNCIL) HE WAS A SOLDER LIKE GASPER OTIENO, JOHN KENGELE, SELEMANI WAZIRI, SEMALI WE WORK HARD TO MAKE CHANGES IT IS SAD FOR HOM TO BE ONE OF THE FALLEN.I MY SELF I AM STILL WORKING ON THE THE CHANGES JUST BRIEFINGS THE PEOPLE OF FOE NOW CALLED CET THAT FREEDOM IS COMING TOMMOROW. MSONGE THANKS FOR LET US KNOW WE ARE CORDIAL WAITING FOR THE DAILY BRIEFINGS OF THIS SAD NEWS.
    ACADEMIA TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete
  8. This is really sad news! May the Almighty God rest his soul in eternal Peace.

    ReplyDelete
  9. Wadau naomba msaada kidogo maana mimi nimapitwa wakati.Niliondoka nyumbani baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 1995.Lakini kumbukumbu zangu nilipokuwa kidato cha nne mwaka 1992 Ujiji seminari alikuwepo kijana mmoja anayeitwa Gelard ama Gervas Mkili.Sina taarifa nyingine baada ya hapo.Nawaomba wadau mnielimishe kama marehemu anahusiana na mazingira niliyoyataja.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Natoa pole sana kwa familia yake na ex-Udsm wote mliomfahamu kama mpiganaji.
    Mdau-USA

    ReplyDelete
  10. Michuzi hebu saidia kutafuta habari zaidi, amekufa kwa ajali au ugonjwa? Mkili alikuwa anafanya nini kwa sasa baada ya UD? Familia yake? Tumeachana siku nyingi ni mate wangu Mazengo!

    Pumzika Mkili! Mdau wa Mazengo High school 1994-1996

    ReplyDelete
  11. HUZUNIIIIIIIII JAMANI,BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE,NAMPA POLE SANA RAFIKI YANGU KIPENZI(MKEWE)NA MTT,JIPE MOYO BWANA YESU NI MUME WA WAJANE NA BABA WA YATIMA,TUPO PAMOJA KTK KIPINDI HIKI KIGUMU,MUNGU AKUTIE NGUVU.MWANGA WA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE.GIJO

    ReplyDelete
  12. MUNGU AILAZE MAHALI MEMA ROHO YA MPIGANAJI MKILI. NAKUKUMBUKA TOKA ENZI ZA MAZENGO SECONDARY MPAKA UDSM. TUTAKUKUMBUKA DAIMA

    ReplyDelete
  13. Mkili amefariki kwa ugonjwa wa moyo. Alikuwa mzima kabisa jioni ambapo alienda uwanja wa Taifa kuangalia mechi na rafiki zake. Usiku ndipo alipoanza kujisikia vibaya na kupelekwa hospital kabla ya kufariki dunia. Alipoondoka MLIMANI alijiunga na Green Acres schools ambapo aliendelea kuwepo huko hadi kufarki kwake kama Mkuu wa Shule hiyo. Mwili wake umesafirishwa jana jioni kuelekea Kahama, Shinyanga.

    Marafiki zake wanaangalia uwezekano wa kuwa na mjumuiko wa kumkumbuka hapa Dar mara waliokwenda Kahama kurudi.

    ReplyDelete
  14. NIMEPOKEA KWA MAJONZI MAZITO NA MOYO WANGU UME UGUA SANA KWA TAARIFA ZA MSIBA WA Bagheshi GERVAS MKILI.

    MKILI ALIKUWA RAFIKI WA KARIBU NA MPIGANAJI MWENZA NDANI YA BUNGE LA CHUO KIKUU.

    NIKIWA KATIBU MKUU WA DARUSO NILIMPENDEKEZA KWA RAIS NA ALITEULIWA NAIBU WAZIRI ELIMU. UTENDAJI WAKE WA KAZI NA UWAZI WAKE ULIKUWA NADHIFU.

    MKILI HAKUSITA KUWA MSHAURI MWENYE FIKRA TENDAJI.

    NAKUMBUKA USIKU WA MANANE NILIPOMWITA NA KUMSHAURI AENDELEZE MAPAMBANO YA KUDAI HAKI ZA WANA DARUSO NA INAPOBIDI WATANZANIA KWA UJUMLA. NILIFURAHI ALIPOKUBALI.

    ALITENDA WEMA AKAENDA ZAKE LAKINI LEO AMETUTOKA.

    BWANA ALITOA NAYE AMETWAA.MPAKA TUTAKAPO ONANA TENA SIKU ILE...

    MAINA ANG'IELA OWINO

    ReplyDelete
  15. kwa niaba ya wanafunzi wenzangu wa green acres high school mwaka 2004/2005 natoa salam zangu za rambi rambi kwa wanafamilia wote na wanjumuia wote wa green acres katika kipindi hiki kigumu.

    mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi! amin!

    solo6k

    ReplyDelete
  16. Doh! Nimepokea habari hizi kwa masikitiko na mshituko mkubwa sana. MUNGU AWAPE NGUVU NA AMANI FAMILIA YAKE. UTAKUMBUKWA SANA KAKA KWA UCHESHI NA BUSARA ZAKO NA JITIHADA KATIKA KUTETEA HAKI ZA WANACHUO KIPINDI CHETU 1997 - 2001. MUNGU AUPUMZISHE MWILI WAKO KATIKA NYUMBA YA MILELE mpaka siku utakaponyakuliwa kwa neema yake MUNGU. Amen.

    Msafiri. M Calgary, AB - Canada)

    ReplyDelete
  17. HABARI ZA KUSIKITISHA HIZI, LAKINI NI MAPENZI YAKE MOLA. MKILI TUNAMKUMBUKA SANA JUMUIYA CHUO UDSM HASA ENZI ZA MGOMO WA 2000 JINSI ALIVYOSIMAMA KIPIGINAJI AKASUMBULIWA HADI KUWEKWA NDANI LAKINI HAKUBADILISHA MSIMAMO WAKE.
    NATOA POLE KWA FAMILIA YAKE NA WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU WA KAMANDA
    MUNGU AMPUMUZISHE PEMA

    ReplyDelete
  18. Habari za kushtusha sana hizi.
    Mkili pumzika kwa amani.
    Ulituongoza vema kwenye mapambano ya wanaharakati wa UDSM, ulisimama kidete ukiwa Katibu hata Rais alipokimbia mapambano na kwenda mafichoni.
    Pole kwa mkewe, mtoto/watoto, familia,ndugu na marafiki.

    WS
    MDAU UDSM 1997-2001.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pumzika kwa amani Mkili katibu Mkuu Daruso 2000/2001. Tutakukumbuka daima hata ulipokuwa mahabusu tulikuja kukuona. Nilikuwa najiuliza sana, wapi Mkili, kwa nini sikuoni kwenye siasa za Tanzania? Nimekutana na R.I.P. Hakika Mungu akupumzishe. Vizuri havidumu. Bye bye Mkili mapamabanaji.

      Delete
  19. Form 4/ 2004October 21, 2010

    rest in peace Mr Mkili..u will alway be in our heart...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...