Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakiwa kikaoni jana ambapo Mwenyekiti wake Mh. Freeman Mbowe aliendelea kupeta kama kinara wa chama huku Dk. Wilbroad Slaa akirejea kwenye kiti chake cha Katibu Mkuu huku Mh. Zitto Kabwe akiteuliwa na mwenyekiti wake kuwa Naibu Katibu Mkuu bara wakati Naibu katibu mkuu wa chama hicho visiwani ni Mh. Issa Yusuf.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. chama la ukweli. nimesoma mwananchi leo huyu zitto nimeanza kupoteza imani nae kabisa naanza kuhisi kama sio mwenzetu vile au kuwekwa karibu na viongozi wa serikali kulikuwa na maana. Ananisikitisha sana na muda si mrefu atapotea kisiasa.
    Maamuzi ya wazee yalikuwa ni mazuri sana KAMANDA amekitoa chama mbali sana kwa muda mfupi tunahitaji aendelee kukijenga ushindi upo haki ikiwepo hata zitto angegombea hiyo nafasi angeshindwa yeye bado mchanga sana tena sana kisiasa

    MUNGU KIBARIKI CHAMA CHETU

    ReplyDelete
  2. Shameless tribalist party; a poison and cancer to our body-politic.

    ReplyDelete
  3. Zito naona anatafuta gia ya kutokea CHADEMA,tunamkumbuka Dk Kaburu...ilikuwa kama ivi

    ReplyDelete
  4. Mbona viongozi wote wa juu wa bara ni wa dini moja tu? huu ni ubaguzi wa kidini.

    ReplyDelete
  5. Uchaguzi? Give me a break! Utachaguaje wakati kuna mgombea mmoja...hapo ni kupitisha jina si uchaguzi. Chadema haina tofauti na enzi za Mwalimu tulipokuwa tunapiga kura kuchagua kati ya kivuli na JKN. Demokrasia imesiginwa katika hicho (Chadema) walichoita uchaguzi.

    ReplyDelete
  6. Namuona Bob Nyanga Makani pale, mtaalam.

    ReplyDelete
  7. Chama cha 'Demokrasia' na Maendeleo ni Chadema?

    ReplyDelete
  8. HIKI CHAMA KIMENISIKITISHA KWA KUONA HAWAZINGATII UHURU WA MTU NA DEMOKRASIA KWA UJUMLA. SIKUONA HAJA YA MWANACHAMA AAMBIWE KUJITOA KWENYE MCHAKATO WA KUGOMBANIA UENYEKITI WAKATI NI HAKI YAKE. KWELI TANZANIA SAFARI BADO NI NDEFU MNOOOOOOO...!HII NINAIONA NI KAMA TU MTU KUPENDA NA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA KATIKA NGAZI YA JUU NA KUONYESHA UOGA WA KUPAMBANA NA WATU NDANI YA CHAMA CHAKE.UONGOZI KWELI NI RAHA JAMANI, SASA HAWA WAKICHUKUA NCHI SI WATAUA KABISA NA KUNG'OANA MACHO!?!? NDO MAANA KILA SIKU NASEMA UPINZANI UWEPO TU KWA KUWAREKEBISHA CCM NA SI KUCHUKUA NCHI, MAANA WATALETA MAAFA TU YA KUJITAKIA.

    ReplyDelete
  9. Haingii akilini kabisa kwa Chadema kuendelea na sera ambazo hata CCM wamezitupilia mbali.
    Eti wanadumisha Fikra za Mwenyekiti Mbowe na Mkwewe Mzee Mtei? Yaani kweli hiki ni Chama makini?
    Kulikuwa na haja gani ya kutunga katiba inayosema kila mwanachama ana haki ya kugombea nafasi yeyote?
    Hivi kweli ingekuwa Lucy Owenya (Binti ya Ndesamburo) ndiyo anataka kum-challenge Mbowe, wazee wangemtaka aondoe jina lake?
    Ni kweli Chadema ina mwenyewe na mwenyewe ndiye Mtei, Mwenyekiti wa Chama ni mkwe wake kwahiyo Mbowe hapindui kwa Mzee. Mbowe amemtaka baba mkwe wake amzuie Zitto asigombee na kweli hakupewa nafasi ya kugombea.
    Mmeiua CHADEMA,sasa zile fununu kuwa CHADEMA ni chama cha mabwanyenye ni kweli.

    ReplyDelete
  10. Wewe mtoa maoni unayezungumzia dini za viongozi wa juu wa chadema una lako jambo, kwani umeambiwa wamechaguliwa ili kusalisha? hapo mtu anachaguliwa kwa uwezo wake na wala si wa dini yake. unataka awekwe mtu wa dini flani ili mradi tu? hata kama hana sifa ya kuwa kiongozi!!!!
    Aipendezi kuona baadhi ya watanzania wenzetu kila mara mawazo yao yanalalia katika dini.

    ReplyDelete
  11. chadema si chama,mdau unayosema mbowe kakitoa chadema mbali una mana gani,chadema ilikuwa hoi,imejengwa bungeni na marehemu chacha wangwe,dr slaa na zito kabwe,na wote wameona weakness ya mbowe ndo maana wanataka atoke,marehemu wangwe alisema sana wakasema anatumiwa,sasa zito vile vile,mbowe anataka chama kibaki kwa wanandugu tuu.chadema ni CHaga DEvelopment MAnifesto.ngo hiyo

    ReplyDelete
  12. Chadema bado ni Imara kama simba dume, wazee walitumia busara kumzuia Zito asigombee, kuna watu waliokuwa nje ya chama walikuwa wanataka Zito agombee ili wakipasue chama kwa kutengeneza ugomvi. Haya yalionekana, Zito aidha alikuwa anajua au hajui kwamba anatumika, lakini kuna vijana kama kina Msafiri Mtemelwa akiwa kama mkurugenzi wa uchaguzi(CHADEMA) alimchukulia Zito fomu pamoja na kumsaidia kuirejesha, wenye akili walione hili, sio kwamba Mbowe aliogopa atashindwa ila ilionekana kwamba mgogoro baada ya uchaguzi huo ungekuwa mkubwa sana, kuna magazeti yalishaandaliwa kuchochea mgogoro. Kwa akili ya kawaida tu unaweza kuona hata kitabu kilichokuwa kinamwelezea uhusiano wake na Mbowe kilitolewa kipindi hiki, hata mwenye akili ya kuku anaweza kuliona hili wazi, Ni ukweli usiopingika kwamba Mbowe anaogopwa na CCM, hawapati usingizi, Mbowe ndiye aliyekijenga chama kwa kuwaweka vijana wasomi kama huyo Zito, Myika na wengineo, aliona mbali sana kwamba chama lazima kijengwe na wasomi tena vijana. Haya juzi hapa mmemsilkia wenyewe akizindua uanachma pamaoja na michango kwa kupitia SMS, Chadema ni chama cha kwanza Africa kutumia mpango huu, unaweza kuona hata CCM wenyewe wamekubali kwamba Chadema kinatisha na watapata fedha nyingi sana. Kumbuka pia ile operesheni sangara inavyoitreka nchi, mpaka na wengine wameiga, Yako mengi mazuri yakueleza kuhusu chadema chini ya kamanda Mbowe, najua mnayajua lakini kwa sababu tu yakutokuwa mzalendo manamponda. Hata Yesu Walimmdhihaki na kumsulubisha bila kosa lolote sembuse Mbowe mtoto Wa Aikaeli. cHADEMA MSIRUDI NYUMA ENDELEZENI MAPAMBANO YA KUIKOMBOA NCHI.From MICHAEL LAISER,

    ReplyDelete
  13. Chadema bado ni Imara kama simba dume, wazee walitumia busara kumzuia Zito asigombee, kuna watu waliokuwa nje ya chama walikuwa wanataka Zito agombee ili wakipasue chama kwa kutengeneza ugomvi. Haya yalionekana, Zito aidha alikuwa anajua au hajui kwamba anatumika, lakini kuna vijana kama kina Msafiri Mtemelwa akiwa kama mkurugenzi wa uchaguzi(CHADEMA) alimchukulia Zito fomu pamoja na kumsaidia kuirejesha, wenye akili walione hili, sio kwamba Mbowe aliogopa atashindwa ila ilionekana kwamba mgogoro baada ya uchaguzi huo ungekuwa mkubwa sana, kuna magazeti yalishaandaliwa kuchochea mgogoro. Kwa akili ya kawaida tu unaweza kuona hata kitabu kilichokuwa kinamwelezea Chacha Wangwe uhusiano wake na Mbowe kilitolewa kipindi hiki, hata mwenye akili ya kuku anaweza kuliona hili wazi, Ni ukweli usiopingika kwamba Mbowe anaogopwa na CCM, hawapati usingizi, Mbowe ndiye aliyekijenga chama kwa kuwaweka vijana wasomi kama huyo Zito, Myika na wengineo, aliona mbali sana kwamba chama lazima kijengwe na wasomi tena vijana. Haya juzi hapa mmemsilkia wenyewe akizindua uanachma pamaoja na michango kwa kupitia SMS, Chadema ni chama cha kwanza Africa kutumia mpango huu, unaweza kuona hata CCM wenyewe wamekubali kwamba Chadema kinatisha na watapata fedha nyingi sana. Kumbuka pia ile operesheni sangara inavyoitreka nchi, mpaka na wengine wameiga, Yako mengi mazuri yakueleza kuhusu chadema chini ya kamanda Mbowe, najua mnayajua lakini kwa sababu tu yakutokuwa mzalendo manamponda. Hata Yesu Walimmdhihaki na kumsulubisha bila kosa lolote sembuse Mbowe mtoto Wa Aikaeli. cHADEMA MSIRUDI NYUMA ENDELEZENI MAPAMBANO YA KUIKOMBOA NCHI.From MICHAEL LAISER,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...