Bwana Michuzi pole na kazi.
Mimi ni mdau wako mkubwa. Naomba wadau wako wengine nao wanisaidie katika shida yangu hii.Nimeolewa na nimedumu kwenye ndoa yangu kwa miaka 11 sasa, Lakini miaka nane ya ndoa hii imekuwa ya mateso makubwa sana.
Mume wangu hanijali kabisa na hulala nje bila taarifa. Pamoja na kwamba yeye ni muajiriwa anayepata mshahara mzuri tuu lakini hatoi huduma ya chakula na mahitaji mengine nyumbani, ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya watoto wetu wanaosoma english medium school. Juzi sikukuu ya Idd hata hakuwanunulia watoto nguo na ilibidi mimi mwenyewe niwanunulie. nimeajiriwa kama mtoza kodi TRA.
Napenda kusema kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa yangu kwa miaka nane ambao huyu mume wangu amekuwa akini-mistreat kama mnyama. Anakataa kunipa haki yangu ya ndoa, pamoja na kwamba nina viwango vyote muhimu vya kusheherekea haki hii.
Swali ni kwamba kuna bwana kaanza kunipenda na nami nimempenda na nataka sasa kuanza naye uhusiano wa kimapenzi, japo nasita kwa sababu ya ahadi niliyotoai siku ya ndoa yetu. Je wadau niendelee kuteseka, au potelea mbali nianze uhusiano wa kimapenzi na huyu anayekuja katika maisha yangu ambaye kwa uchunguzi wa miaka miwili naona kuwa ananipenda?
Dada!! wanaume wote are all the same, hata huyo wa sasa kwasababu anakutaka ndio maana anakuonyesha anakupenda, akishachoka na wewe nae atakufanyia vituko. Wewe sasa hivi jijali wewe na watoto wako. kama unaona huyo mpya anakufurahisha sasa wewe endelea tu!! Lakini usifikiri yeye ni better than mumeo!! Make "you" and your happiness comes first, kwani watoto wako wanaona unavyotesaka na hiyo sio nzuri kwa watoto.... Good luck
ReplyDeletepole dada dadayangu mimi kama mwanamke mwenzako nakupa ushauri wangu uliwahii kuwaita wazee wote wapande mbili kusema na wewe na mume wako kila mtu aseme shida yake kama kuna suluhu ya nyinyi kusikilizana basi muwe pamoja mulee watoto wenu na kama hakutaki tena basi akupe njia yako usiwe na mafikiria ya kimaradhi maana hii dunia tulokuwa nayo kisasa maradhi yame kuwa mengi kisha pia juwa una watoto leo upo macho hawashuhulikii je kesho kama haupo duniani nani atawatizama ukiona ametowa sababu isiyo fahamika basi kheri kila mtu ende na zake kumi huyo mwana mume uliye naye sasa kwanza muwangalie anavyo kuwa na watoto wako ukimuona ndani ya heart yake anawapenda basi mchukuwe haraka.thanks mdau toronto.
ReplyDeleteKwanza pole sana na misuko suko ya maisha na hongera kwa kuweza kujilinda bila kutumbukia katika uhusiano usio wa kihalali. Ushauri wangu ni vyema ukapitia hatua hizi.
ReplyDelete1. Kwanza kama familia mbili ya kwako na huyo mume hazijakutana kujadili jambo hilo ni vyema ugalianza na hatua hiyo. Huenda mukafikia makubaliano na kuondoa tatizo hilo liliojitokeza.
2. Kama la kwanza halikuwezekana hatua inayofuata ni kudai talaka katika vyombo vya sheria. Hii itakupa wewe uhuru wa kufungamana na huyo mwengine. Si jambo la busara hata kidogo kuingia katika mapenzi na mtu mwengine wakati bado ni mke wa mtu.
3. Huyo unayehisi ana kupenda ni kufunga ndoa ya halali baada ya kwisha kuondoka kwa ndoa hiyo uliyonayo hivi sasa.
Kila la kheri katika safari hii ngumu.
Yazid M.
Dada yangu kwanza pole sana. Ila usikate tamaa Ila Kama unaweza , kula raja yako ukishapima naye. Tafuna hadi kichwa, huyo mbuzi fisadi atajiju. Yalinipata hayo hayo lakini nimemega nje hadi jamaa kaamua kutumia. Mwanzoni alijaribu sana kunipiga
ReplyDeletedada kama anakunyima unyumba basi wewe una bahati sana, kwani atakupa lingwasuma huyo. Achana naye haraka sana, kaa singo kwa muda mrefu kidogo acha mwanaume anayekupenda akutongoze muda mrefu sana bila ya mafanikio, huku ukimpa matumaini kama na wewe unampenda. Akithibitisha kuwa anakupenda kweli pimeni ngwasuma kisha anza naye mapenzi mapya.
ReplyDeleteYOU MUST BE STUPID!!!!!
ReplyDeleteWewe acha papara kwanini usimnase vibao huyo mumeo na atulia? Kama hakuli basi nenda kwingine ni Rukhusaa kabisa hata dini zinasema hivyo. Wewe jikite tu, na wewe uanze kulala nje tuone atasemaje. Akileta za kuleta mshtaki kwa mjumbe
ReplyDeleteAcha kugawa kama pipi kwanza, jaribu kununua dildo ikupoze kiu.
ReplyDeleteMdau Moro
We dada huna haya na huna adabu hata kidogo umesahau kuwa ndoa ni ustahamilivu na na uaminifu kama ulikuwa unataka kuisaliti ndoa yako ulikubali vp kuolewa mwanzoni. Fatilia kwanza tatizo alilonalo mumeo yawezekana ana misiba imemkuta but anaogopa kukwambia, pengine ana ugonjwa ndio maana hatoi huduma kwako yote hutokea ndani ya ndoa la msingi fatilia kwanza tatizo la mumeo na sio kukimbilia njia ya mkato. mara nyingi njia ya mkato huishia majuto kiufupi ukimwi maana uaminifu hupotea.
ReplyDeleteKwa kifupi unaonekana kwamba una hela ya kujitosheleza wewe na wanao. Nasema hivi kwa sababu kwanza umeonekana umeweza kuitunza familia yako kwa miaka minane toka huyo mtu wako alivyoanza ku misbehave, pili unafanya kazi TRA kwa hiyo hapo huwezi kuwa maskini.
ReplyDeleteKwa huwa huyo jamaa hatunzi familia yake na pia hakupi haki yako, then nakushauri umwache, kabla hujaanza kupata chachandu pembeni, mfukuze humo ndani, au ondoka wewe - vunja hiyo ndoa, halafu nenda kapata chachandu yako. Hiyo ni haki ya kila mtu, achana na jinga hilo. Mimi ningekuwa nimemtimua miaka 7 iliyopita.
Samahani kama haya yatamkweza yeyote yule(wadau), lakini haswa lengo ni mlengwa wa swali hili,kama wewe dadaangu ni muislamu na uko na ndoa yako,Na huyo mumeo "URODA" hakupatii Ikiwa hiyo ni haki yako.
ReplyDeleteBasi mimi ninakushauri uombe talaka yako na hapo ndio unaweza kumwambia huyo jamaa kama kweli anakupenda akuoe.
Na jamaa kama kweli anakupenda wala hatojiuliza mara mbili ,he will marry you ,bila kujali kingine ,ila kama ni mtu wa kuchezea chezea basi angalia saana dadaangu usije ukaula wa chuya,maana inawezekana anakupenda tu kwa sababu uko kwa mtu na pengine umeishamuhadithia kila kitu ,hivyo anajkua situation yako na ndio anatumia hiyo nafasi kukuhadaa ila abanjue amri ya sita na wewe.
Ninakutakia kila la kheri katika hili ,kwani hali hii sio mchezo ninakuonea huruma maana ndoa bila hako ka mchezo ni kazii kweli kweli ,ilhali unajua kabisa kuwa jamaa yuko vyema na wewe uko vyema.
Goodluck.
Mimi nakushauri ufanye kitu roho inapenda kama amekuchapa kibao shavu la kushoto usimgeuzie shavu la kulia, ni yesu kristo tu aliweza kufanya hivyo.Good luck
ReplyDeleteNAKUPA USHAURI WANGU WA BUSARA KWA AJILI YA WATOTO TU SIO WEWE NA HUYO MMEO
ReplyDelete1. USIJIINGIZE KWENYE MAPENZI KWANI YAKIKOLEA UTASAHAU WATOTO AMBAO NDIYO KITU CHA MUHIMU KULIKO CHOCHOTE
2.HUYO ANAYEKUTONGOZA MCHUKULIE KAMA BUZI TU WA KUKUTOA HAMU IKIKUZIDI NA NI LAZIMA ATUMIE SALAMA MBILI
3. IWE SIRI KALI KAMA MNAVYOFISADI HUKO TRA
4.MSALIMIE OTTO AU OTU KAMA BADO ANAFANYA KAZI NILIMUACHA PALE MAGOMENI
5.HUYO MMEO MUACHE AKULINDIE HESHIMA YA KUWA WEWE NI MKE WA MTU NA HUKU UKIFANYA UFISADI KWA SIRI ILA KWANZIA HIVI SASA NAE INABIDI UMVALISHE SALAMA MBILI USIMWAMINI MTU USAWA HUU SITANII NAKUPENDA NA WANAO
Ushauri wa bure.
ReplyDeleteJaribu kuhusisha wazee kuweka mambo sawa. Ikishindikana mkubaliane kila mmoja achukue uelekeo wake. Nina uhakika huyo jamaa anayekutaka ukishaachana na huyo mwanaume uliye naye sasa hivi naye atakuwa hakutaki.
Anza maisha mapya, kama ukiamua kula tunda sehemu nyingine baada ya kuachana kula tu kwa amani, ila usisahau kutumia kinga.
dada kwa kuwa una watoto mimi nakuomba utulie kabisa kwani biblia inasema kama unashindwa kumsamehe huyo mumeo basi usiolewe tena kwani utakuwa unazini
ReplyDeleteUNA-POINT LAKINI DADA UKIMWI JEEEEEEE, MIMI NAONA MPE ULTIMATUM HUYU MKWARE WAKO MWAMBIA WEWE NA YEYE NA ACHANE NA UKWARE WAKE AMA ZAKE AU ZAKO UTAONDOKA NA KUACHANA UNAHAKI ZOTE ZA KUVUNJA MKATABA WA NDOA, NA KAMA IKIFIKIA MAHALI PA KUVUNJA NDOA BASI ATAKAYEFUATA SISITIZA KWENDA KUPIMAMA UKIMWI NA MUKAE CHINI MUELEZAZA KWAMBA KAMA TUTAANZA NI MIMI NA WEWE MACHO MIA MIA MIMI SITAKI IKOTOKEA NDO ITAKUWA MWISHO WETU, NASEMA HIVYO NI KWA SABABU YA UKIMWI, UNAYO HAKI ZOTE ZA KUPATA URODA IT IS A NATURAL THING AND A FACT OF LIFE PROVIDED YOU A FIT
ReplyDeletekitu kimoja utakumbuka maishani ni hiki, we mwanamke mpe penzi huyo mwanaume unayefikiri anakupenda bado uko ndani ya ndoa na utakuja kulia baadaye.
ReplyDeletekama ulimwelezea matatizo yako ujuwe ndio chanzo cha udenda kumtoka kujaribu kutupa ndoana ale urojo ati ukadhani anakupenda.
KAMA UNAFIKIRI ANAKUPENDA MWAMBIE HIVI NATAKA NIVUNJE NDOA YANGU KISHA TUOANE NA WEWE USIKILIZIE LA SIVYO UTAKOSA VYOTE MWANAWANI, HAPA UGHAIBUNI NI KUNA SISTER MOJA ALIKUWA NA TATIZO KAMA LAKO AKATOKA NJE YA NDOA BWANA AKABWAGA MANYANGA, MWANAMKEA AKALIA AKAJARIBU KURUKIA KILA BWANA, NA KILA BWANA AKAWA ANAONJA KISHA ANAKULA KONA KUOA MWINGINE MWISHOWE DEMU HUYO AKAAMUA KULEWA NA BABU WA KIZUNGU NA KUZAA NAYE, ILA ANALIA KILA LEO KUMKUMBUKA MME WAKE, NI HAYO TU MWANAWANI KARIBU KWENYE MATATIZO YA KUJITAKIA NENDA NJE YA NDOA UPATE MATATIZO 100%.
ReplyDeletepole sana na situation yako lakini naomba nikushauri yafuatayo, kwani nadhani katika miaka yote hiyo tangu ameanza kutoka nje na kukumistreat wewe hukumkosea chochote na umekaa naye kwa vile ni ndoa
ReplyDelete1. Kwanza kabisa naomba uhame kwa huyo mwanaume, ( mumeo ) kwani unasomesha watoto na unajishughulisha kivyako, hama kaa kwako na watoto usitake kuwabadilishia lifestlye ( school etc )
2. Jaribu kutafuta course yoyote usome jioni ikupunguzie mawazo, huko pia utapanua mawazo na wanafunzi wenzako na hutakuwa na muda mwingi wa kumfikiria huyo mwanaume
3. Huyo mwingine mliyeanza naye mapenzi , naomba sana asiwe mume wa mtu, kwani pia mkewe akijua unaweza kupata zahama pande zote, kama yuko single na umeshatoka kwa mumeo, unaweza kuendelea lakini hakikisha humlazi nyumbani ( respect to kids !! ) unless hawako pale
4. Kama ni mkristo jiunge na vikundi vya kanisani , fellowship na kadhalika ili pia umuombe Mungu wako na ubaki ktk mstari ulionyooka, kama muislam vivyo hivyo
5. kama ni uroda, wala sikukatazi miaka 7 anadhani wewe kisiwa kisichotembelewa ? it is your right to enjoy and indulge..but cautiously, the more it is cautious the sweeter it gets...
6. have fun ! take care of yourself and your children
Matatizo kama hayo ya ndoa yapo mengi,wengi wanavumilia na wengine wanashindwa. Na sidhani kama huyo utakayempata una uhakika kuwa atakutimizia kila kitu.
ReplyDeleteChamuhimu tafuta usuluhisho kupitia kwa mshenga wake, ikishindikana wahusishe wazazi wake,ikishindikana wahusishe wazazi wapande mbili, na ikiwezekana muombe kiongozi wa dini akutane naye.
Nasemahivikwasababu huwezi jua jamaa kapagawa na nini, unaweza ukamtelekeza na kumwangamiza moja kwa moja. Ni bora kwanza ujitolee kwa ajili yake mpaka uone sasa huyu basi ndipo uchukue uamuzi wa kuomba talaka.
Kumbuka kuna watoto, na watoto ni baba na mama, kama mmoja ataondoka duniani hilo tunamuachia mungu, lakini mkiachana hivihivi wakati watoto wanajua baba yao yupo mahali fulani, na umeshawaeleza ubaya wa baba yao, utawajengea taswira mbaya maishani mwao. Kwahiyo kwahatua yoyote utakayochukua ufikirie watoto wenu.
Mshukuru mungu kuwa una uwezo wa kuwasaida watoto wako, wapo wenye mateso kama hayo na hawana kazi maalumu. Mungu awasaidie nyote mliokutana na mitihani hii.
Mwisho kabisa usinje ukadanaganyika na kuanza kuzini, hilo litakuwa balaa kwako na familia yako, hakikisha unavumilia mpaka utakapopata ufumbuzi wa kudumu, kwani mvumilivu hula mbivu.
M3
Dada pole kwa mkasa ulionao. Ila kwa mimi nakushauri uite wazee muongelee suala hilo. Au kama ukiona wazee wameliongelea suala hili wameshindwa basi nenda mahakamani. Ila sikushauri kwa saaaana uondoke kwa mumeo kasha eti huyo mwanaume wa nje amekuambia anakupenda. Huyo mwanaume anakupenda coz upo kwa mumeo na haupata ule mzigo wa kukulea wewe na watoto na pia anakuona unafanya kazi nzuri. Laiti ukijaacha kazi, au ukijaachwa na mumeo anaweza akakubwaga ukumbuke maisha ya sasa ni magumu sidhani kama huyo mwanaume wa nje atakubali mzigo wa watoto wa manaume mwingine.
ReplyDeleteHivyo dada usiende pupa kama unampenda mumeo bora uvumilie kuliko kuja kujutia baadae, utajamtamani mumeo usimpate tena. Bora uibe tuu nje usijulikane, ule uroda kwa huyo anayedai anakupenda ila kuwa makini Ukimwi upo haujaisha, tumia kinga au muende kupima muwe salama.
Note: Watoto wanafurahisaana wakiwa wanapata mapenzi ya pande zote mbili yaani baba na mama. Muwekee huyo mwanaume limbwata atulie ikiwezekana.
Mamaa pole. Mimi ni mwanaume. Ushauri wangu IKIMBIE ZINAA. Huna haki kwenda nje ya ndoa. Nenda kwa wachungaji wa kiroho wakusaidie. Au tafuta watu waliookoka. Nenda kwenye website ya Christopher Mwakasege anao usahuri mzuri. Hata mim kanisaidia. Narudia IKIMBIE ZINAA mamaa.
ReplyDeleteBila shaka umepokea mawazo mengi kutoka kwa watu mbali mbali lakini nikwambie bayana hivi.
ReplyDeleteNdoa iko moyoni.
Jamaa wako huenda hataki kukuambukiza UKIMWI ndo maana halali nawe.
Huyo mshikaji wa nje-Pima naye. After 3 months mpime tena kisha ule naye maraha ya maisha kwa siri ili watoto wasiathirike kisaikolojia.
Usimfikirie sana mume wako kwani yeye anakufikiria akiwa na huyo dem mwingine?
As a woman nami nimepitia huko. Nimejifunza ndoa iko moyoni siyo katika karatasi wala katika kuita wajumbe wawasuluhishe. Kama mtu ameamua love imeisha, imeisha! usipoteze muda chasing the wind!
Epuka sana kuita vikao na kuelezea shida unayoipata ndani ya ndoa yako. Mwisho wa yote utachekwa na hakuna kati yao atakayekupa mapenzi badala yake jina lako na sifa zako nzuri zitakuwa misinterpreted.
Mama B
Nakubaliana sana na wewe mama mwenye ndoa safi. Ningepata contakti zako ingekuwa poa sana.
ReplyDeleteI like the part "kisima kisichotembelewa" kweli kisima kimejaa maji lazma yachotwe kwa caution.
Mama B
HAYA MAMBO HAYAHITAJI MASHAURI YA JAMII NZIMA.
ReplyDeleteWEWE KAMA UMECHOKA, AMUA LA KUFANYA.
USIWE NA KIGEUGEU.
KWANZA INAVYOELEKEA UNATAFUTA UHALALI KWENYE BLOG YA KUTEMBEA NA HUYO UNAYEMNADI KUWA ANAKUJALI; KWANI YEYE MUMEO ALIANDIKA KWENYE MA BLOG KABLA HAJATOKA KUTAFUNA??
HAYA MAMBO NO MAZITO, NA NI PERSONAL ZAIDI; HATA KAMA UKIWA ANNONYMOUS, BADO NI PERSONAL; NA MAWAZO YOYOTE UTAKAYOPEWA NI PERSONAL KWA MUJIBU WA ATAKAEKUPA HAYO MAWAZO.
WEWE NI MTU MZIMA, MZAZI, MWENYE KAZI, TENA HILI LISIKUSHINDE; AMUA MWENYEWE; KWANI HAYO NI MAISHA YAKO. HAKUNA MSHAURI HATA MOJA HUMU ATAKUWA NA WEWE BAADA YA MAAMUZI UTAKAYOFANYA.
KILA LA KHERI
Ahadi ya ndoa isikufanye uwe mtumwa wa ndoa! kama huna raha ndani ya ndoa, make it official! mwambie its not working, and you need to have life and enjoy haki ya ndoa!!!! unangoja nini!! kuiba iba kumepitwa na wakati, utaambulia magonjwa bure, but kama wengine walivyosema, wanaume wote ni sawa, sije ukaruka mkojo ukakanyago uharo! go with ur insticts, ok!
ReplyDeletePole kwa yalokukuta. Ila hapo suala la kumuingiza mnyama ndani ya hii kesi utakuwa hujamtendea haki mnyama kwa sababu wanyama wanataratibu zao katika suala la kufanya mapenzi, dume hawezi kumuingilia jike bila kuwa tayari.
ReplyDeleteTabia za kibinadamu katika suala la mapenzi hata sijui nifanaishe na kitu gani hapa duniani, ila wanyama wala hawana tabia hiyo..
wewe mwanamke angalia 100% wanaokushauli uende nje ya ndoa hawajaolewa au ni malaya, na ukipata matatizo watakucheka na kusema wewe ni malaya mkubwa na hufai nje ya jamii, ila jambo moja mamaa nakushauli kama unataka jema uonane na wazee uwaelezee kisha udai talaka baada ya hapo, uoane na mwingine.
ReplyDeleteIla kama ni TRA ujue kuna wanaume wakware sana hapo wengine wana HIV ni hayo tu ila ukienda vibaya utalia sana ni hayo tu.
Dada yangu kwanza pole, lakini muhimu muogope mungu na uisthubutu kwenda nje ya ndoa.
ReplyDeleteNi bora utumie njia za ushauri kwa kuzishirikisha pande mbili yaani wazazi wako na wa mumuo. Huyo nayekupenda nje na kukutongoza ni kama wanaume wengine tu, hana la zaidi, lakini kwa kuwa unamatatizo ndani ya ndao ndio maana unamuona mwuokozi.
Kabla ya mengine ni bora pia kuhakikisha usalama wa afya yako, kwani mumeo kama tabia yake ni kulala nje, unaweza ukawa katika hatari.
Jichunge ndugu yangu kwani magonjwa ni mengi siku hizi na jiepushe na tamaa. La muhimu ni kutatua matatizo ya ndoa yenu na kama ukiona mwenzako bado anaendelea na tabia hiyo ni bora kuchukua talaka yako, na kutafuta anayekupenda kikweli na uolewe.
duh!kwanza pole sana dada yangu!!
ReplyDeletehii kali!!
ninachoweza kukushauri ni kwanza achana na huyo baba watoto wako kumkomalia akupe haki yako ya ndoa it must be a strong reason for him to denied,huwezijua!!kuna lingwasuma na mna watoto!!what if wote wawili mkitumbukia huko mtoni?!!watoto mama!!!achana nae usimuanze na akianza yeye mwambie kupima kwanza tena asikupeleke yeye kituoni mpeleke wewe unapopajua!!wanahonga siku hizi cheti kinakuja safiii!
na pia najiuliza unakuaje na mzuka nae mtu aliyekutenda kwa kiasi hicho!!,au kuna mahali ulimkosea so he punish u for what u did?!!maana wakati mwingine inatokea katika mahusiano,unalipia kwa ulichokifanya!!ila hata kama ndo hivyo jamaa anakisirani gani cha miaka saba?!!he must be stupid!unaweza kumtisha tishia mwenzio nyau kwa kipindi flani,na akikaa sawa mambo yanarudi kwenye mstari mnalea watoto,siwezi kusema sana coz tunakosea kujugde kwa kutazama upande mmoja yani upande wako tu!!jamaa pia huenda angekuwa na lakusema!!!simsemeii!!
kuhusu huyo jamaa aneyekupenda penda u must b very careful,sim'banii jamaaa ila najua sana wanaume tulivyo!!,siku zote wanaume tunapotongoza tunarudi matawi ya chini sana,wakati mwingine u cant even imaging,unaweza ukajifanya unaililia kabisa na chozi linatoka na akajifanya matatizo yako ni yake,si tunajua wenzetu mmeumbwa na huruma??!!swali jingine najiuliza huyu jamaa miaka yote hiyo miwili aliyekuwa anakutongoza anaishi maisha ya peke yake au yuko katika mahusiano?!!,take a notice!!kwa sababu kuna probability ya kuwa na future iliokuwa blind!!,asikwambie mtu,wanaume niwashenzi kinoma anaweza kukula mara ya kwanza mara ya pili!!..mara ya tatu akajiuliza whats so new into her?akarudi faster kwenye mahusiano yake ya awali!!,na akakudiscourage kwa namna flani flani,zinaweza zikawa si za moja kwa moja ila ndo akufukuzae..!!.coz hana future na wewe!!wewe ni mke wa mtu bado,na pia una watoto tayari!!ijapokuwa inaweza kuwa si sababu ya msingi sana!!ila ina click kwa kiwango fulani pia!!take a notice!!,nakueleza hivyo coz kuna watu wanachukulia advantages kwenye matatizo ya wengine!!hasa wanaume katika angle kama yako anajua kabisa mwisho wa siku lazima uhitaji mwanaume wa kukuliwaza!!,na wanaume huwa hatuachiani hata siku moja bora uwe nao hata mia tano ila kumpa mwenzako hata mmoja ni issue!!waulize washkaji hapo ofisini watakwambia,its true
pole sana dada kwa kiasi flani nahisi maumivu yako coz somhow somwhere nina kamtima ka kupenda pia!!so I can feel it!,pia nakupongeza sana kwa kuwa mvumilivu miaka yote hiyo umemtunzia huyo bwana na temptition za dunia hii,maaana zinahitaji moyo wa chuma,ningependa kukufahamu personal sidhani wewe ni mtoto wa kizazi hiki ambacho mwanamke anatoka nje ya ndoa bila hata tatizo lolote!!,anaamua tu kula uroda hovyo tu!,Mwenyezi Mungu akupe moyo zaidi coz siku moja yote haya yatakuwa historia!!Im telling you!!Nisalimie watoto!!!hiyo ndo nguzo yako.
Unakitazama kibanzi kilichoko ndani ya jicho la mwenzako wakati ndani yako kuna Boliti. Mara ngapi umemkosea heshima mme wako na kumwonyesha kuwa si chochote kipato chake duni na mambo kama hayo! Kiasili wanaume wameumbwa kuwa washika hatamu ndani ya nyumba unapomyima haki hiyo lazima aende kule anakopowe hiyo heshima! Sidhani kama mke wangu is down to earth naweza kumsaliti na kumfanyia usaliti mkubwa kama huu. There must a reason! Jipeleleze kwanza mwenyewe ujirekebishe and then ongea nae! Mwambie umhimu wa watoto wenu na maisha yao ya badae! Wazazi ambao hawakuwalea watoto wao vizuri watapata adhabu kubwa sana!
ReplyDeleteMama mmoja alimwendea mchungaji wake akamweleza nia yake ya kutaka kuachana na mme wake! Baada ya kusimulia matatizo anayoyapata na jinsi gani mme wake wake anavyomtendea Mchungaji alimwambia kabla hajaachana nae kwa kipindi cha mwezi mmoja ajifanye kuwa anampenda sana mme wake amfanyie wema na amwonyeshe upendo wake wote. Mama huyu alifanya kama alivyokuwa ameagizwa na mchungaji, akamtendea uzuri wote, mwezi ulipoisha mchungaji akamwuliza kama bado anayo nia ya kuachana na mme wake, cha kushangaza Mama huyu alikataa katu na kwamba wazo lake hilo huenda ni shetani tu alimpitia!
ReplyDeleteWanadamu tuko wepesi sana kuangalia upande mmoja wa sh. Principal ni moja tu PENDA ILI UPENDWE! Unaposhindwa kufanya sehemu yako mambo hayatajiendesha automatically! Mimi kama mwanaume siwezi kuendelea kujipendekeza tena mke wangu kama hanithamini na kuniheshimu!
PENDA ILI UPENDWE!!!!!!!
Wewe dada kama namna gani vipi mroge tuu halafu ukishampiga limbwata mpe mkuyati au viagra mzee kichwa wazi lazima aamke then you take control of him and that's it nitolee.
ReplyDeleteSasa mshikaji wangu michuzi,mbona mimi nimetoa maoni mazuri tu na sijatukana lakini umeyatupa kapuni?sikuelewi unatumia kigezo gani ktk hilo maana mwisho wa siku watu tutakutukana wewe kumalizia hasira za maboxi kwako.. wewe hata ukiniminya hii messegi powa tu lakini that is how i feel and u r hurting my feeling so beware mchusi
ReplyDeleteSioni kama kuhusisha wazazi wa pande mbili kutasaidia kitu, kwani wazazi wamewafunza na sasa ni kazi yenu kuendeleza libeneke. Ni jambo la aibu kuingiza wazazi katika ndoa haswa mmekuwa kwa muda mrefu. Mimi ushauri wangu ni kama annon hapo awali alisema kaa na mume wako akulindie heshima na kama unataka kukunwa ndio unaenda kwa huyo jamaa, ila chunga magonjwa na wala usionyeshe kama unampenda kwani atakutumia na kukunyanyasa akijua unaogopa.
ReplyDeletemama B naungana na wewe pia kabisa,
ReplyDeleteninarudia tena hao wanaokushauri sijui muite wa wazee, makuhani etc, jamani ndoa is more of heart than mind..kuna mmoja pia kasema hilo, mtaita wataongea yataingilia huku yatatokea huku, na sidhani kwa hiyo miaka 8 hujawaita bado, siwezi kukubali mwanamke mwenzangu akae miaka 7 bila uroda na dume linafaidi nje, hata kama lina ngwasuma, mama wewe kwakweli raha jipe mwenyewe, ni nini kumlilia mtu eti kulinda'hadhi' ya ndoa kina late princess DI na prince Charles ilikuwaje? si alikuwa bikra wa miaka 19 lakini dume alikuwa bado anampenda someone a whole lot older! such a taboo in sacred royal family, kwahiyo wewe ni nani useme uvumilie?? na kwanini usipate sexual satisfaction ?? after all sisi tunashauri kama nanonymous at teh end of the day uamuzi ni wako, nahisi unajua unataka nini, mimi binafsi kama ninavyojinadi ndoa ni imara sana na tunapendana sana ( for today ) ya mbeleni namwachia Mungu ila siwezi kuvumilia yote hayo kwakweli mama fikiria sana na uamuzi utakaoufanya uwe kwa manufaa yako na watoto wako, mwenye ndoa yake akikuhitaji basi wewe mpe ToR, terms of Reference kwenye kurudiana, mimi nimesimamia zaidi ya ndoa 9 na kati ya hizo imara ni 3 tu, hizo nyingine tumesuluhisha mpaka tumechoka, jamani usijizeeshe bure bileshi...
mama B ningetoa contact sema hapa watanirukia watu wengi sana kunishambulia kwani email za kazini na ofisini zina majina yangu..
pole sana dada, mimi kama mke na mama wa watoto ninakushauri uwe mvumilivu. Usiwaeleze watu wa kazini kwako matatizo uliyonayo, maana wapo wasiopenda kukuona una raha utajuaje huyo unayesema anakupenda kama katumwa ili akuharibie maisha? na ujue hakuna siri dunia hii dadangu. Kinachofanyikia gizani kitawekwa nuruni tu tena mumeo akijua ndiyo atapata point yakukuacha na yale aliyokufanyia wewe yatasahaulika na wewe ndiyo utaonekana umevunja ndoa kwa uzinzi wako. Nakupa ushauri: jishushe sana kwa mumeo, nyenyekea dadangu, mtakuwa mmetoka mbali achana na huyo ambaye anakushawishi umtimizie haja zake. Angekuwa ameoa na mtu akawa anamtake mkewe angefurahi? hata kama unakazi nyingi ofisini jitahidi urudi nyumbani mapema, uwe mke mwema hata kama unamsaidizi wa kazi (housegirl) wewe fanya kazi zote ambazo mama anatakiwa afanye, mumeo akirudi mpokee kwa upendo, hata kama hataki kuongea na wewe jitahidi uwe mdogo kwake, usiangalie kipato ulichonacho kuwa ni kikubwa zaidi ya chake, au usiangalie cheo ulichonacho kazini ndiyo vikupe dharau au kiburi. Unapokuwa nyumbani wewe uwe mke mwema na utaona hata watoto watakufurahia na mumeo atabadilika. Kama ulikuwa unaona karaha kuwa nyumbani jitahidi uwe unarudi nyumbani mapema. Mwisho wa siku mkishapataka mwenyewe utafurahia kwa kutomsaliti mumeo na hata watu wakitaka ushauri kwako utawapa ushauri wa kuwa wavumilivu, hujaanza wewe kupendwa dadangu ukiwa na raha hawaji lakini ukuwa kwenye matatizo na kipato kizuri ndio utawaona wanaume watajipendekeza. Siku zote kumbuka wewe ni mke wa mtu na kumbuka kila siku ahadi ya ndoa yenu na kama mumeo hakuoni, MUNGU ANAKUONA HUWEZI KUJIFICHA. Baadaye usije ukajutia kuwa ningejua nisinge..
ReplyDeleteDadangu hakuna ndoa zisizokuwa na matatizo, waone mume na mke wako pamoja kwenye sherehe au kwenye gari utatamani ingekuwa ni wewe na mumeo lakini ndani ya mioyo yao ndio wanajua siri ya ndoa yao. Mwombe Mungu asuluhishe ndoa yenu. Jipe moyo utashinda haya ni mapito yana mwisho. Ubarikiwe na Mungu.MimiMama D.
Wewe dada huna akili. Hilo ni swali la kuuliza watu. Eti nitoke nje ya ndoa. Hata wanaokushauri utoke nje ya ndoa hawana akili.
ReplyDeleteMimi ni kijana mdogo wa miaka 25 ninatafuta FATAKI wa kike naona hii kazi inakufaa wewe kwanza upo TRA na inaonyesha pamoja na ufisadi mshahara wako ni mkubwa hivyo natuma application kwako tafazali naomba unikubali.
ReplyDeleteMama/dada, naungana na anayesema uogope zinaa. Kama imeshindika kabisa kabisa kabisa kabisa......, basi tafuta talaka. Baada ya kupata talaka funga ndoa na huyo "anayekupenda" sasa.
ReplyDeleteMengi yamesemwa. Naomba kusisitiza. Watu wengi wenye UKIMWI hawa-disclose kwa patner(s) wao. Kwa hiyo kuna uwezeekano kwamba ana UKIMWI na anashindwa kukwambia.
Pia yawezekana hawezi tena kufanya tendo la ndoa. Uhanithi unaweza kumpata mwanaume baadae (baada hata ya kupata watoto). Wanaume wengine huona aibu kubwa ku-disclose hicho kitu. Na hata huo nje akokaa na kuchelewa kurudi nyumbani inawezekana hakuna ngono yoyote anayofanya.
Take home message: Chunguza kwanza upate sababu halisi. Pili, kuwa mwangalifu na hatua yoyote utakayochukuwa.
Mdau: Is this You?
ReplyDeleteA client I'll call Sharon knew that something was missing in her marriage. She and Robert used to be passionate about each other, she said, but after 12 years and two children, she felt removed. Robert never asked her about work or what she was worried about or felt like doing. She was no longer attracted to him, and they rarely spent time alone together. Instead, she threw her energy into raising the children and her job as a paralegal. Life had become bland.
Then there was Todd. He'd been at the law firm longer than Sharon and showed her the ropes. They would discuss complicated cases, and Sharon found his enthusiasm engaging. They'd grab coffee together, and soon coffee became lunch, and lunch led to phone calls and e-mails as their conversations went from professional to deeply personal.
Sharon thought about Todd all the time, and told me she hadn't felt this alive since she and Robert had started dating. While she recognized a crush — her excitement about seeing him, her pleasure in his jokes, her relief in confiding in someone who got her — she told herself there was nothing wrong with what she was doing because they weren't having sex.
Robert, however, started to notice his wife's coming home later. She was on her cell phone a lot on the weekends, and when he asked who she was talking to, she became evasive. At one point, he complained that they never had sex anymore, that he felt lonely in the marriage, and that he wondered if there was someone else.
Sharon assured Robert — and herself — that she wasn't having an affair. While she felt a little guilty, the thought of giving up Todd, the way he made her feel beautiful and funny and fantastic, was unbearable.
Emotional cheating (with an "office husband," a chat room lover, or a newly appealing ex) steers clear of physical intimacy, but it does involve secrecy, deception, and therefore betrayal.
Mdau
Gail Saltz O: The Oprah Magazine
Yaani umeushika mkia wa mbuzi halafu unatuuliza wadau mkundu uko wapi....unataka jibu gani?
ReplyDelete