Mwana FA na AY

Msanii maarufu wa kizazi kipya mwana Fa a.k.a Binamu ni mmoja kati ya wanamuziki mahiri wa kughani Tanzania ambaye video yake "Naongea na wewe"ambayo ameshirikiana na AY imeteuliwa na Channel O Afrika Kusini kati ya Video bora ya kikundi na pia katika kipengele cha Video yenye kipaji cha juu kutoka Afrika Mashariki na amewaomba wapenzi wa Bongo Flava na muziki kwa ujumla kumpigia kura. Shughuli hiyo itafanyika October 29.
Mwana Fa, ambaye hivi sasa yuko vekesheni huko Marekani ni mmoja wa wasanii wachache wasomi ambapo hivi sasa ameamua kujiendeleza zaidi katika elimu na anaendelea na Masters yake katika Fedha(Finance) huko Uingreza katika chuo kikuu cha Conventry.
Akizungumza na Globu ya Jamii ameelezea kuwa suala la elimu lina umuhimu mkubwa katika maisha na hataacha kughani wala kuwa msanii kwasababu ya elimu kubwa lakini amedai sikuzote elimu itakusaidia na hasa ukizingatia masuala ya fedha na wasanii kwani watu wengi maarufu hapa Marekani mfano Mike Tyson hadi Michael Jackson wamejikuta wakitumiwa na watu na kutokuweza kudhibiti mamilioni ya fedha za mapato yao.
Binamu hivi sasa anapika albam na rapper mkongwe mwenzake wa Tanzania huko New York MR II a.k.a 2Proud a.k.a Sugu iitwayo VETO.
Ukitaka kumpigia kura Mwana Fa na AY ni kama ifuatavyo:
Most Gifted or DUO sms 4E to +278 392 08 400
The Gifted East African Video SMS 13B to +278 392 08 400
(International rates Apply)
unaweza kupiga kura mara nyingi utakavyo.
Mdau Sunday Shomary

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HAWA JAMAA NILIWAENZI TANGU ZAMANI MISTARI YAO NI YA NGUVU HUWEZI KUIKUTA KWA PROFESA YEYOTE HAPO MLIMANI HAPO BADO HUJAMSIKIA PROFESA MWEYEWE J WA NDIO MZEE HUPITE KWA WOTE MR POLITICIAN SUMARI KAAYA NA SOMO WANGU DUDU BAYA (tumaini g). HII NDIO SHULE YETU KUU.

    ReplyDelete
  2. longo longo lipochanganyika na fix...conventry ipo wapo wadau?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...