wasamaria wema wakimzong mwanamama na mwanae ambaye aliamua kusaula nguo na kubaki na nanihii tu kwenye geti la ubalozi wa ufaransa mchana huu. haikujulikana mara moja sababu za yeye kufanya hivyo ila walinzi wa ubalozi walisema hawamtambui na wala hakuwa ameenda ubalozini hapo. walinzi walisema walimuona amesimama mbele ya geti akiwa kama anataka kuvuka, ghafla akambwaga mtoto chini na kuanza kusaula huku akisema maneno yasiyoeleweka. askari polisi waliitwa mara moja na kumchukua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ulipaswa ufuatilie ili ubaini cnanzo cha yeye kuvua nguo hapo na si kwingineko. Nini mkimemsibu. na Nimaneno gani hayo yasiyo eleweka.

    ReplyDelete
  2. Ametelekezwa na bwana mlinzi wa kampuni ya sekurite anayefanya kazi maeneo hayo.

    ReplyDelete
  3. anony Sun Sep 06, 01:31:00 PM, kwani wewe ukifuatilia itakuwaje? kwa kuanzia nenda kituo cha polisi cha oysterbay ukaulize kabla ya kwenda kwa kamanda wa polisi wa mkoa.

    ReplyDelete
  4. ugumu wa maisha huu unaosababishwa na watu wa mungu (akina Nkapa, Lowasa, Sumaye na Kikwete) ndiyo unaowafanya watu wawe hivi.

    ReplyDelete
  5. Kufulia kubaya,amefulia huyo

    ReplyDelete
  6. huyu dada maskini tumeishi nae paris huyu hadithi yake ni ndefu na inasikitisha alirudishwa ndani ya masaa 24 bongo,sasa amekuwa kama aliechanganyikiwa vile akisikia umetoka france sijui anajisikiaje sijui

    ReplyDelete
  7. duh au kanyimwa visa huyo!mpeni visa azame kiwanjani manaa njaaa kaali bongo africa

    ReplyDelete
  8. Haya nyie mliotaka mambo ya mswati yahamie bongo. Pole mama kwa yaliokusibu, pengine hapo akili isharuka. Ni matatizo tu na ugumu wa maisha.

    ReplyDelete
  9. Huyu mama ni Kigagula, namfahamu vyema huwa anafanya shughuli za kuwafanyia mazingaombwe watu ili wapate VISA kilichotokea leo ni kuwa mmoja katika walinzi wa Geti ni ''Ustaadh''na vigagula wakija na vituko vyao huadhirika.Huwa nafanikiwa kufanya mambo haya bila kuonekana!Leo imemgeukia baada ya Ustadh Fadhil wa pale ubalozini kuwepo!!

    ReplyDelete
  10. Aisee mdau ICT wa Sun Sep 06, 03:15:00 PM hapo juu uliyetoa
    link ya hilo gazeti la Guardian nimelisoma. Aisee jamaa wametuchafua sana Tanzania Kimataifa na hiyo ishu ya Loliondo. Inabidi afisa Uhusiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii ajipange kuthibitisha au kukanusha shutuma hizo zingali zikiwa zamoto moto...Kwani hapa London ishakuwa GUMZO.

    ReplyDelete
  11. KUCHANGANYIKIWA MAISHA MAGUMU, MNAIMBA MAISHA BORA KWA WOTE KUMBE SI KWELI, HAYA NI YA GEORGE O. MWANDISHI WA U.K. WA ZAMANI KIDOGO KWA WALE WASOMI WATAMKUMBUKA ALIANDIKA KITABU KUHUSU ANIMAL FARM, AKASEMA ALL ANIMALS ARE EQUAL, BUT THERE ARE OTHERS WHO ARE MORE THAN EQUAL, AKINA SIMBA KULA WAZENZAKE, NASI NDO HIVYO TENA MAISHA BORA KWA KILA MTU, LAKINI YA WENGINE NI BORA ZAIDI, KWANI KUNA WATU WANAKULA MILO MINNE KWA SIKU, KWA SIAGI, MKATE, ASALI NA MAZIWA WAKATI WENGINE HAWAJUWI HATA NEXT SECOND WATAKULA NINI. NDO YALE YA AKINA OMARY BONGO KUANCHIA NCHI MTOTO WAKE - ALLY BONGO SOON AFTER HE KICKED THE BUCKET - KABILA TO KABILA DRC - UKISHINDWA UCHAGUZI UNANG'ANG'ANIA NA UNATAKA SERIKALI YA USHIRIKA NA CHAMA PINZANI, HII NI KWELI DEMOKRASIA- KENYA NA ZIMBABWE. MAISHA BORA NI KWAO TU SI MKWA WOTE NA WENGI TUTAVUA NGUO MIAKA INAVYOENDA.

    ReplyDelete
  12. Natanguliza pole kwa huyu dada, Allah ampunguzie yaliyo mfanya awe na dhiki hii ya kuvua nguo hadharani...Ewe Mola twakulilia ndani ya Mwezi mtukufu huu umpe ponyo la kweli huyu dada na mwanawe na umuondoshee kero na shida zake zote na zisijirudie Amiiin
    Shehe jAMAL Muhiyidiin Al-Qadiriy

    ReplyDelete
  13. ACHENI JAMANI ANENIUMA NI HUYO MTOMTO EE MUNGU TUSAIDIE SADIA AFRICA SIJUI LINI HAKI YA MTOTO ITAJALIWA NAUMIA SANAAA! KAMA UNAUJUA UTAMU WA WA MTOTO UNAWEZA KULIA

    ReplyDelete
  14. Eewe Mungu wa Rehemu nakuomba umnusuru dada huyo jamani na mtoto wake, Taabu nyingi za TZ zinafanya watu waonekane vichaa lakini kumbe si vichaa ni taabu tu za maisha zimekuwa nyingi jamani!! Njaa nyingi, Jua kali, kazi hazipatikani, hakuna kipato cha aina yoyote ile watanzania wengi wanateseka sanaa jamani. EE mwenyezi Mungu msaidia mama huyu na wamama woote wanaoteseka sio Tanzania tu ila ulimwenguni pote..Amen,!

    ReplyDelete
  15. Mungu awazidishie na kuwabariki Shehe Jamal Muhiyidiin Al-Quadiriy na Anon wa 07:45 AM - Jamani mwenzako anapotatwa na baya muuombee Mungu amnusuru na sio kumsemea maneno mabaya kwamba kigagula au kafulia, ukiona mtu mzima kavua nguo au analia ujue kuna jambo kubwa sana ambalo hata wewe usipo tegemea ipo siku linaweza kukusibi, hakuna anaefurahia matatizo. Atakae msaidia leo siye atakae kusaidia wewe kesho bali mtu mwingine wa tofauti usiemtegemea,sasa usipojijengea misingi mizuri na Mola wako utapata wapi msaada katika dunia hii. Binadamu tupendani tusaidiane kwa khali na mali ukijaliwa.

    ReplyDelete
  16. Eeeeh Mungu muweza na muumba wa yote.Muepushe mama huyu na mwanae na matatizo yote haya.

    Mkulima-Kijijini Gezaulole

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...