Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na balozi wa Jamhuri ya Korea ya kusini nchini, Young-jin Kim kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka nchini kwenda Jamhuri ya Korea kusini kwa ziara ya kikazi.
WAZIRI Mkuu Mh. Mizengo Pinda ameondoka Dar es Salaam Ijumaa Septemba 4, 2009 kwenda Jamhuri ya Korea, Indonesia na India, kwa ziara ya kikazi ya kiserikali kutokana na mwaliko wa nchi hizo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu atajifunza zaidi maendeleo ya kilimo yaliyofikiwa katika nchi hizo, hasa utumiaji wa zana za kisasa nateknolojia.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu anafuatana na Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira na Waziri wa Kilimo, Mifugo naMazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Burhan Sadat.
Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa, Balozi Seif Iddi; Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Luteni-Kanali MstaafuIssa Machibya na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Daniel Ole Njoolay. Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Septemba 18, mwakahuu.
Tanzania sasa imo katika utekelezaji wa mpango mkubwa wauendelezaji kilimo, chini ya azma ya “Kilimo Kwanza”, ili kuongeza kasi yakuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
Mpango huo wa “Kilimo Kwanza”, unaoweka mkazo zaidi katika kilimo,ulizinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Dodoma mapema Agosti, mwaka huu wakati wa Maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane.
Nguzo kuu ya mpango huo ni kukuza kilimo cha kisasa na chakibiashara, kuanzia kwa wakulima wadogo hadi wakubwa, kuendeleza viwanda,miundombinu ya kilimo na matumizi ya teknolojia ya kisasa.
Azma ya “Kilimo Kwanza, ilibuniwa chini ya Baraza la Taifa laBiashara ambalo ni mfumo wa mashauriano kati ya sekta ya umma na sektabinafsi. Rais Kikwete ni mwenyekiti wa baraza hilo.
WAZIRI ANAOMBA MKWANJA NINI?
ReplyDeleteMheshimiwa WM tunakutakia safari njema na yenye mafanikio.
ReplyDeleteHii picha noma. Mizengo anaonekana kama anakinga bakuli.
ReplyDeleteje ni kweli mtoto wa mkulima atabaki kuwa mtoto wa mkulima?
ReplyDeletehapo anamwambia hebu geuza kwa upande huu hiyo noti, lakini ina pendeza style.
ReplyDelete