
MH. BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR
Ndugu Watanzania wenzangu,
Ninayo furaha kubwa kuwatumia Mkono wa Idd El-fitri, mwaka huu wa 2009.
Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Nawatakieni nyote kila la kheri wakati huu wa sikukuuu.
Idd Mubarak
Ninayo furaha kubwa kuwatumia Mkono wa Idd El-fitri, mwaka huu wa 2009.
Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Nawatakieni nyote kila la kheri wakati huu wa sikukuuu.
Idd Mubarak
Idd si jumapili au jumatatu au London wameuona mwezi jana nini, Huku Scotland sisi bado tunafunga.
ReplyDeleteAhsante mama ila wanao tunaumia na life huku, salamu bila chochote kitu inakua shida kidogo, mama nitumie angalau pound 40 mwanao niifidi eid. am serious kabisa maana wanajamvi wengine wanaweza kufikiria natania hapa.
ReplyDeleteNashukuru sana mama
Wadau Kwanza kabisa nimshukuru Mh.balozi kwa salamu zake.Lakini kwa wataalamu wa lugha yetu ya Kiswahili na wadau wote kwa ujumla:Hapo karibu na mwisho wa salamu zake kuna maneno(namnukuu:)...na kwa niaba yangu binafsi..!Hapa hii imekaaje wadau?Nielewavyo mimi neno"niaba" hutumika pale ambapo mhusika hayupo eneo husika,hivyo nafasi yake "huwakilishwa"au taarifa zake "huwasilishwa" na mtu mwingine badala yake,..Haya wadau endeleeni...!
ReplyDeletenyie watanzania mnajiletea aibu sana ulimwenguni hii blog inaangaliwa na watu wengi sana duniani, swala la kuongea english limewa affect sana kisaikolijia mtu akikosea kidogo mnamshambulia kama kaua. sio vizuri kuvunjana confidence kiasi hicho kama mtu amekosea unmsahihisha kistaarabu omba ata email yake kwa michuzi au tafuta njia mbadala watanzania mnabaki mkilalamika ooh hatuthaminiwi na mataifa mengine mtathaminiwa vipi kwa tabia kama hizi mnazoonyesha. tuache kudhalilishana jamani.
ReplyDeleteAhsante kwa salaam, nawe pia mama yetu. I so much admire this lady, Eid Mubarak to you!!
ReplyDeleteI have just received this e mail from someone. Thought that I should post it here. Is there anyone with a similar story or experience?
ReplyDeleteFriends,
Please be careful when going to Dar-es-salaam.
There is new scam just started to steal passports in the last few days. After Visa and Immigration when you go through to customs they ask to see you passport. When you hand them your passport they give it to a person near them who takes it and runs straight out of the building. This is planted so you cannot even run behind them and catch them.
Suggest you hold your own passport and just show it to them, refuse to hand over your passport to customs- ... also make few photo copies too !
Please forward this email to anyone who is likely to be going to DAR soon
We Anon wa 08:39. Hii si kweli hata kidogo. Baada ya Immigration check unaenda kuchukua mizigo yako. Baada ya hapo customs. Sasa unataka kusema mtu wa customs ndiye anchukua pasipoti hala fu anamkabidhi mtu mwingine ambayo anakimbia nayo!! Hebu acha hilo haliwezekani wakati tunayo serikali bwana. Hebu acheni kuichafua nchi yetu. Hivi nyinyi ambao mnaishi nje ya nchi mbona baadhi yenu mnajidai hivyo na mmejaa uzushi. I dare challenge you hilo haliwezi kutokea Tanzania. Hebu acheni.
ReplyDeleteMdau wa habari ya wizi wa Passport umepewa uzushi na watu wenye nia mbaya na nchi yetu. Embu nambie mbele ya watu kibao hapo eapoti umempa mtu wa kazitamu pasipoti halafu anampa mtu mwingine anatoka nayo benzi nje ya jengo. Hao mashahidi wooote wamelipwa nini na kipasipoti chako? Na hilo wazo la kumkimbiza umelitoa wapi? Utaanza vipi kumkimbiza wakati hujapewa ruhusa rasmi kuingia nchini? Mdau yeyote akipata e-mail ya hivyo aifutilie mbali. Bongo wanaiba ki-EPA EPA bwana.
ReplyDelete"...na kwa niaba yangu binafsi.." ni kosa la kawaida, na hili sio kwa mama Mwanaidi tu, au kwa wazungumzaji wa Kiswahili pekee, bali kwa wengi na hata wazungumzaji wa Kiingereza.
ReplyDeleteMara nyingi nimewashikia viongozi wetu (akiwemo Mh. Rais) akisema '...na kwa niaba yangu binafsi...' anapohutubia. Na hata viongozi wengine wa nchi zinazozungumza kiingereza nimewahi kuwasikia wakisema "...and on my (own) behalf..."
Ni imani yangu kuwa mama yetu Mh. Balozi Mwanaidi na wale wote waliokuwa wanakusea kwenye hili, basi watatambua kuwa kusema "kwa niaba yangu binafsi" au kusema "on my own behalf" ni kosa!
Kidumu Kiswahili... asanteni kwa mchakato wa kuanza kufundisha shule za Msingi kwa Kiingereza
Sevedo
MINAL FAIDHINA MAMA MWANAIDI.JEE WEWE UTASWALI WAPI? CENTRAL MOSQUE PARK ROAD?
ReplyDeleteNAKUTAKIA IDDI NJEMA NA WAFANYAKAZI WOTE WA UBALOZI.
mmama Balozi tunaomba msaada wako tumenyanyaswa sana na ndugu yetu AMBUKILE afisa wa uwamiji tumechoka sasa.
ReplyDelete