Ndugu Wadau wa Elimu, Rasimu ya Sera Mpya ya Elimu imeshazambazwa kwa Wadau mbalimbali wa Elimu hapa nchini ili waichambue na kutoa mapendekezo yao kabla haijapitishwa rasmi na Wizara husika.
Nasikia, japo sijui kama ni kweli, kuwa hakuna nakala ya Kielektroniki. Kama si kweli basi naomba mdau yoyote ambaye ana nakala ya aina hiyo aitume humu na sisi wananchi tuichambue. Na wale wadau walioniahidi kunipatia nakala ya kawaida naomba wafanye hivyo. Kwa mujibu wa habari hiyo, sera hii 'inadhamiria' kukifanya Kiingereza Lugha ya Kufundishia shule za msingi:
Kusoma habari hii
Mdau Chambi Chachage
Kwanza tuangalie jirani zetu na lugha wanazotumia katika shule zao za awali.
ReplyDeleteKenya (English)
Uganda (English)
Malawi (English)
Zambia (English)
Rwanda (English/French)
Burundi (French)
DR Congo (French)
Mali (French)
Burkina Faso (French)
Madagascar (French)
.
.
.
.etc.
Jee ni kweli nchi zote hizi zimetuzidi kielimu na kimaendeleo?
Tatizo letu lipo sehemu nyingine lakini tunalifumbia macho na kujifanya kwamba "eti tatizo ni kiinglish"
Matangalu,
ReplyDeleteUmesema ukweli. Tatizo letu ni kwenye kitu kingine kabisa, siyo lugha. Watu wa Morisi wanazungumza lugha chotara na Kifaransa lakini wanatushinda kwa maendeleo na hata ubingwa wa kufoka kwa Kiingereza. Morisi ni Mauritiuts washikaji, nisiwaache mbali.
Hata hivyo katika hilo sera lao jipya, Kiingereza kitatumika kwa shule zinazopenda hivyo, ambazo ni za binafsi. Shule zote za serikali inapendekezwa ziendelee na Kiswahili, jambo ambalo litafanya kila mzazi fisadi akimbilie shule za binafsi na watoto wengine kujiona kama wamepotea njia. Kwa kifupi sera hii itaongeza rushwa na wizi nchini kwa sababu mkeo akidai shule za Kiingereza, itabidi uibe au ule rushwa ili msitwangane.
Watanzania sisi tatizo letu lilianza baada ya kuua elimu yetu kwa njia na sera na mipango mbalimbali kama UPE ya 1978, uzembe wetu, ujinga na kuzubaa ambako Mwalimu Nyerere alitutengenezea.
Wakenya leo wanakipenda Kiswahili kuliko sisi Watanzania na wanatoa wataalam wengi wa Kiswahili wanaokubalika kiulimwengu kuliko sisi ingawa ni kweli sisi Kiswahili chetu kinajitahidi kuliko chao, lakini hatuna miaka kumi watatupita. Utaona Mtanzania akiula akaenda Majuu, basi anaachana na Kiswahili kabisa kwa watoto wake wakati Wakenya ikifika likizo wanawapeleka watoto wao Kenya ili wajifunze Kiswahili.
Hivi leo jamii yetu haijui Kiswahili wala Kiingereza, angalia wachangiaji kwenye blogu na magazeti yetu utapata ushahidi, na hayo ni baada ya kuhafanyiwa uhariri. Aibu kubwa.
Nchi yetu haina msimamo na haijui inakwenda wapi. Sisi ni taifa la wajinga.
naomba nikusaidie annony wa kwanza,nchi zote hizo ulizozitaja hawabadilishi lugha kama kinyonga .kama masomo yanafundishwa kwa kiswahili basi tujue moja kiswahili,kama kwa kiingereza basi kwa kiingereza sio kama sasa msingi swahili then english.haileti maana.kama kiswahili tayari kimeshakua enough.mie nawaunga mkono serikali kwani hitasaidia watu wasikimbie shule za kata ila cha muhimu ni kuwa na walimu wazuri ,nina wasi wasi kama walimu kufundisha kwa kiswahili hawawezi kwa english itakuwa inshu sana.jitahidid serikali kuwapa darasa kwanza walimu wengi.
ReplyDeleteSawa kiingereza kifundishwe kwa masomo yote ila kuanzia darasa la nne na kuendelea , miaka mitatu ya mwanzo lugha ya kizalendo (kiswahili)kwanza ,Na kuwepo mitihani ya kufuzu kiswahili , Na somo la kiswahili bila kuachwa .na ilo ndo pendekezo langu.
ReplyDeleteAhsanteni .
Nafikiri kuna wakati kulikuwa na kongamano hili la elimu kwenye hii globu ya jamii na nilitoa wazo nikasema tatizo ni namna ya ufundishaji. Ukitaka mtoto ajue lugha ni kuongea naye. Kam kiingereza kina anaza kufundishwa grade 3 basi mwaka mzima wa grade 3 watoto wajifunze kuongea tu kabla ya kuanza kuandika na kusoma. Wakiisha jua kuongea ndiyo unaanza kuwafundisha kusoma halafu kuandika. na waalimu amabao wanatakiwa kuwafundisha hawa watoto wawe wame specialize mambo ya lugha ya Kiingereza if possible wawe ni graduate (B.Ed). najua hii ningumu katika nchi Kama tanzania kuwapata Graduate kwenda kufundisha elementary lakini kama wanapatiwa mishaha mizuri watu wanafanya kazi tu. Waalimu wengi wa shule za msingi wanajua kiingereza cha kusoma na kuandika tu cha kuongea ni kubahatisha je serikali inategemea hawa watoto watafundishwa kiingereza kweli darasani. Nchi nyingi hasa zilizoendela wanafundisha watoto wao katika lugha zao na lugha ya kiingereza wanajifunza na wengi unakuta wanaelewa ingawaje hata mtu akiiongea na accent lakini bado anaelewa. tatizo ni kwamba serikali imefanya english as a second offcial language wakati majority ya watu wanaongea kiswahili. Ufundishaji kwa kiingereza kuanzia sekondari wala haungekuwa na matatizo kama mwanafunzi alipata msingo bora primary.
ReplyDeleteKitakachotokea ni kwamba wajinga tuu ndiyo watakaoliwa. Fisadi litaiba mihela kisha litapeleka mtoto wake shule ya kimombo. Kutokana na kama alivyosema mdau hapo juu, kwamba hatuna uwezo wa kupata waalimu wenye sifa zinazotakikana; watakuja wakenya na viingereza vyao vya kikikuyu (I eat now my chapoo); na wapopo (You gooogo aba framing me uup!) ndiyo watakaokuwa waalimu wa watoto hawa wa mafisadi. Watamaliza shule, Elimu ziro, English ziro na mihela ishakwenda na Mma,(maji); Mafisadi yashakwiba;
ReplyDeleteMatokeo yake nini?
Mlalahoi kosa kitu, Fisadi pata jivu;
Mpopo/Mkikuyu pata kila kitu.
Kulikuwa na kamtindo hapa cha kupeleka watoto kusoma Uganda/Kenya ili wajue Kiingereza matokeo yake yako wapi? Wamejua kiingereza? Watanzania hamjifunzi tuu? (Sanasana u-choko tuu ndo umeongezeka hapa nchini)
Pumbavu wa akili.
Tuangalie jee elimu yetu inatuandaa kuyakabili mazingira yetu?
Kwanini mechanical Engineer wetu hawezi hata kutengeneza manati?
Kwanini tuna ma-profesa wa "Highway/Motorway" Engineering lakini daraja la urefu wa mita 50 tuu lazima waje wajapan kutujengea?
Tunabakia kung'ang'ania kingereza tuu.
Jambo hili kama lipo hivyo basi itakuwa vyema lakini tuache kukurupuka Watanzania. Ebu tujiulize kama kweli itakuwa hivyo, kiingereza hicho kitafundishwa na waalimu wepi? Kweli waalimu wetu wanaofundisha shule za msingi za Serikali kwa sasa wanao uwezo wakufundisha masomo hayo kwa kiingereza? Ukitafakari kwa kina utaona huu yapasa kuwa mpango wa muda mrefu, kwanza tungejitahidi kupata waalimu wenye uwezo wa kufundisha hayo masomo kwa hiko kiingereza kwa shule za msingi, tukiwa tumejiwekea malengolabda tuseme tutakapofika mwaka 2015 basi tutaanza kutekeleza mfumo huu mpya.
ReplyDeleteNasikitika kusema kama tutafanya mabadiriko haya kwa mtindo huu basi hatutakuwa tumetatua tatizo, tutakuwa tumebadili mfumo tu wa lugha kinadharia.
Imefika wakati tujaribu kufanya mambo kwa manufaa ya Taifa na si kwa kuridhishana,ni ukweli ulio wazi kwamba waalimu hawa wa sasa si wakufundisha hayo masomo kwa kiingereza na pia hata hivyo vitabu hatuna. MTAZAMO MZURI LAKINI YATUPASA KUINGIA KWENYE HUO MFUMO TUKIWA TUMEJIANDAA NA SI KUENDELEA KUTENGENEZA MATATIZO YALE YALE YA BORA ELIMU NA SI ELIMU BORA
Ahasante sana Mh. Matangalu.
ReplyDeleteHii ndio hali halisi na imetokea mjini na wala sio Kijijini - na hao ndio Wakaguzi wa Walimu ambao ndio wanafundisha Kiingereza chenyewe tunachoking'ang'ania kukitumia kama lugha ya kufundishia:
ReplyDeleteMimi bado na nalia na suala la lugha. Hivi ndivyo ripoti ya ukaguzi katika shule fulani ya msingi inavyosema: "all teachers were instructed to stop use of Swahili language during teaching in order to make pupils to practice speaking English frequently". Nani anamkagua mkaguzi - who inspects the inspector!